Simu kumi "10" bora zaidi kwa sasa

Reuben Challe

JF-Expert Member
Dec 10, 2021
2,761
5,039
Leo nimeona nilete list ya simu kumi bora kwa sasa. Simu nyingine zimetoka mwaka Jana na nyingine zimetoka mwaka huu na kwenye hii list zote hizi ni flagship. Sitaelezea sana nitaweka tu jina la simu na picha.
Kabla hujaendelea, jua hii list nimeirank according to me kwa hiyo ukiona kuna sehemu haipo sawa unaweza kunirekebisha

1. Samsung Galaxy S23 Ultra
Hii ni simu ya mwaka huu na nimeona ndio simu bora zaidi kwa sasa. Katika Samsung Galaxy S23 series hii ndio ina mwonekano premium, lakini S23 plain na S23 plus zina mwonekano cheap kwa mtazamo wangu.
images%20(3).jpg

2. Apple iPhone 14 Pro Max
Kwenye list yangu hii ndio simu pekee isiyotumia Android.
Screenshot_20230212-195534~2.jpg

3. Vivo X90 Pro Plus
Kuna uwezekano kwa sasa hii ndio most premium Chinese flagship lakini kwa bahati mbaya ni Chinese version. Global release yake haijajulikana kama itakuwepo. Vivo X90 Pro inaweza kuwa released globally lakini hii Vivo X90 Pro Plus Ina probability ndogo. Bei ni around TSh 2.3M AliExpress, very fair price [emoji847
Screenshot_20230212-200644~2.jpg

4. One Plus 11
Hii ina Chinese version na Global version yake. Bei ni around TSh 1.8M AliExpress
Screenshot_20230212-200744~2.jpg

5. Xiaomi 13 Pro
Hii ni flagship ya mwaka jana kutoka kwa kampuni ya Xiaomi a.k.a "Chinese Apple". Kuna Chinese version kwa sasa ila Global version inaweza kutoka mwaka huu. Bei ni around 2.2M AliExpress, very fair price . Mwaka huu Xiaomi hajatoa flagship bado
Screenshot_20230212-200712~2.jpg

6. Samsung Galaxy S22 Ultra
Hii ni flagship ya Samsung ya mwaka jana. Bei ni around TSh 1.7M AliExpress. Very fair price
Screenshot_20230212-200805~2.jpg

7. Xiaomi 12S Ultra
Hii ni flagship ya Xiaomi ya mwaka jana ambayo kwa mara ya kwanza ilionesha nia thabiti ya Xiaomi kwenye kutoa simu zenye kamera kali. Hata mwonekano wake unajidhihirisha. Bahati mbaya ni Chinese version tu ingawa unaweza kuiflash ikawa Global version. Kupata Google apps ni rahisi. Pia kuna app ya Xiaomi GetApp ambayo inafunction kama Playstore, inapatikana kwenye simu za Xiaomi. Uzuri wa app hii ni kwamba unaweza kutumia bila hata kuwa na account, yaani unadownload tu app hamna haja ya kujiregister kama ilivyo PlayStore. Bei ya Xiaomi 12S Ultra ni around TSh 2.1M AliExpress
Screenshot_20230212-200825~2.jpg

8. Google Pixel 7 Pro
Hii ndio simu yenye weakest chipset kwenye list hii lakini nimeiweka hapa kwa sababu ya unyama wake kwenye kamera na software. Bei yake ni around TSh 1.8M AliExpress
Screenshot_20230212-200847~2.jpg

9. Motorola Edge 30 Ultra (a.k.a Motorola Moto X30 Pro in China)
Hii ndio simu yenye bei fair sana kwa bei yake maana ni 1.3M tu lakini inashindana na simu za 2M.
images%20(4).jpg

10. Xiaomi 12T Pro
Miongoni mwa Xiaomi zilizopendwa ni hii kwa sababu ipo straight focused on display na kamera, tena kwa bei ya 1.2M lakini bado inashindana na simu za 2M. Bila shaka ndio simu bora zaidi kwa bei hii (TSh 1.2M). Global version pia ipo
Screenshot_20230212-200914~2.jpg

Mimi hata ukiniroga ukiniambia nichague simu hapo nitachagua Xiaomi 13 Pro hata kama najua kuna simu zaidi yake
NB: Hii list ni kwa mtazamo wangu kwa hiyo kama kuna sehemu unaona haipo sawa unaweza kuniambia
 
Back
Top Bottom