RPC Simiyu asema wanafanya uchunguzi aliyefariki akiwa chini ya ulinzi, ndugu wapeleka mwili Bugando

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi zaidi kuhusu tukio la kifo cha Limbu Kazilo, Mkazi wa Mtaa wa Kilulu, Wilaya ya Bariadi ambaye inadaiwa amepoteza maisha akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi hilo ambapo ndugu wa marehemu wanadai kifo hicho kimesababishwa na kipigo alichokipata kutoka kwa Askari Polisi wakati walipoenda kumkamata.

Kutokana na tukio hilo ndugu wameamua kutouzika mwili hadi waambiwe chanzo cha kifo cha ndugu yao.

KAIMU RPC ALISEMA MAREHEMU ALIUMWA HOMA
Ikumbukwe kuwa awali, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Maulidi Shaban alinukuliwa na JamiiForums akisema kuwa marehemu alipata homa akiwa kituo cha Polisi ndipo akapelekwa hospitali na huko ndipo alipofariki Dunia.



RPC ASEMA WANACHUNGUZA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe amesema:

Tunaendelea na uchunguzi wa kifo cha Limbu Kazilo, Mkazi wa Mtaa wa Kilulu, Wilaya ya Bariadi ambaye alifariki Dunia Januari 2, 2024 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi.

“Ikumbukwe mtu huyo alikamatwa usiku wa Desemba 29, 2023 na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Masanja Kidana.

“Alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu baada ya kutekeleza mauaji, wataalam wa maiti wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo na hatua nyingine zifuate.”

Januari 5, 2024, tulienda kuuangalia mwili wa marehemu tukiwa na madaktari wa Hospitali ya Bariadi, tukakuta una majeraha ya mgongoni, kifuani, kwenye makalia na sehemu alionekana amechomwa na kitu chenye ncha kali na ulikuwa na damu puani na mdomoni.

Tamko la Familia
Kiongozi wa Familia, anaitwa Gambuna Masalu Lukuba amesema "Madaktari wakasema majeraha hayo hayawezi kusababisha kifo na wao hawana uwezo wa kufanya uchunguzi zaidi, wakashauri twende Bugando na sisi kama Familia tumekubaliana mwili upelekwe Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi."

Mama: Walimpiga sana mwanangu na kumwambia ‘leo utakufa’
Upande wa mama mzazi wa marehemu, Bi. Nyahoga Nandi amesema “Nilichungulia dirishani nikaona mwanangu anapigwa na askari, alipigwa hadi akazimia, walikuwa wanatumia mpini wa shoka, wakawa wanasema ‘leo utakufa’ huku wanaendelea kumpiga.”

Anaendelea kusema kuwa walikamatwa kisha kufungwa pingu na kuanza kupigwa, anasema Kazilo alipigwa sana na Askari hao kwa kutumia mpini wa shoka licha ya kuwa alitoa ushirikiano walipofika Kwa ajili ya kumkamata.


Pia soma
- Simiyu: Askari Polisi Bariadi watuhumiwa kumpiga mtuhumiwa na kusababisha kifo chake
- Simiyu: Askari wawili wadaiwa kumshushia kipigo kijana na kumsababishia kifo wakimtuhumu kuiba baiskeli
 
Tamko la Familia
Kiongozi wa Familia, anaitwa Gambuna Masalu Lukuba amesema "Madaktari wakasema majeraha hayo hayawezi kusababisha kifo na wao hawana uwezo wa kufanya uchunguzi zaidi, wakashauri twende Bugando na sisi kama Familia tumekubaliana mwili upelekwe Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi."
Simu ya maelekezo itakuwa imeshapigwa Bugando
 
Ifikie wakati serikali ibadilishe muundo wa hili jeshi! Hivi litaendelea kuwa na muundo kama ule wa jeshi la Kikoloni mpaka lini?
 
mnachunguza ili mgundue nini wakati mnajua Polisi wamemuua ?

mnadhani huo uchunguzi mtapata majibu sahihi ?

kifupi Polisi wa laana mimi nilishasema nikikuta Polisi anapigana na Nyoka namsaidia Nyoka
 
mnachunguza ili mgundue nini wakati mnajua Polisi wamemuua ?

mnadhani huo uchunguzi mtapata majibu sahihi ?

kifupi Polisi wa laana mimi nilishasema nikikuta Polisi anapigana na Nyoka namsaidia Nyoka
 
Back
Top Bottom