Simbachawene: Muda wowote kutoka sasa Serikali itatangaza nafasi za kazi kwenye utumishi wa umma

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,108
49,809
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema serikali imepanga kutangaza ajira mpya zaidi ya 47,000 ili kupunguza uhaba wa watumishi.

Waziri Simbachawene ametoa taarita hiyo wakati akizungumuza na watumishi wa umma wilayani Chato mkoani Geita na kueleza uhaba wa watumishi unatokana na ujenzi wa miundombinu unaoendelea.

Simbachawene ameeleza, katika kuendelea kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada tofauti kwenye ofisi za umma hadi mwezi Agosti 2023 serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kutoa ajira kwa watumishi 129,074.

Amesema serikali pia imepandisha vyeo watumishi 455,497 tangu ilipoingia madarakani mwezi Februari mwaka 2021 hadi Agosti 2023 na kufanya gharama za serikali kufikia Sh bilioni 84.3 kwa mwezi.

Amebainisha kwa mwaka 2022 pekee watumishi 145,225 walipandishwa madaraja kati ya watumishi wa serikali 544,714 waliopo kwenye mfumo pasipo kujumuisha watumishi wa mikataba na vyombo vya ulinzi.
===

My Take
Kwa Upendo huu ambao Mama anazidi kumwaga, aisee msipopata kazi awamu hii ndio nitolee. Watakuja wale wakunja ndita mtaona moto wake.

View: https://www.instagram.com/p/CxQh3v0NRR_/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema serikali imepanga kutangaza ajira mpya takribani 47,000 ili kupunguza uhaba wa watumishi.

Waziri Simbachawene ametoa taarita hiyo wakati akizungumuza na watumishi wa umma wilayani Chato mkoani Geita na kueleza uhaba wa watumishi unatokana na ujenzi wa miundombinu unaoendelea.

Simbachawene ameeleza, katika kuendelea kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada tofauti kwenye ofisi za umma hadi mwezi Agosti 2023 serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kutoa ajira kwa watumishi 129,074.

Amesema serikali pia imepandisha vyeo watumishi 455,497 tangu ilipoingia madarakani mwezi Februari mwaka 2021 hadi Agosti 2023 na kufanya gharama za serikali kufikia Sh bilioni 84.3 kwa mwezi.

Amebainisha kwa mwaka 2022 pekee watumishi 145,225 walipandishwa madaraja kati ya watumishi wa serikali 544,714 waliopo kwenye mfumo pasipo kujumuisha watumishi wa mikataba na vyombo vya ulinzi.
===

My Take
Kwa Upendo huu ambao Mama Anazidi kumwaga,aisee Msipopata kazi awamu hii ndio nitolee.Watakuja wale wakunja ndita mtaona moto wake.
Kazi ni maisha, ukiona upo hai jua una ajira
 
Wewe chawa mbobevu kupata kazi ni haki ya vijana wote waliosoma sio suala la upendo mtu flani kutoa kazi. Sasa vijana
Pamoja na hiyo haki awamu ya 5 iliwanyima ,endelea kusubiria Haki bila kujali bipaombele vya Serikali.

Nakusisitiza isipopata kazi awamu ya 6 imekukata,utaisubiria sana Haki we endelea kuongea na kukaza ujinga kichwani kwako
 
Back
Top Bottom