Simba walikua na faida ya refa na wachezaji wao wa zamani

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Kwa wasiofahamu mchezo wa jana simba walipata ushindi wa penalti kwa faida ya vitu viwili mosi refa alikua upande wao kwa aasilimia kubwa na pia wachezaji wake wa zamani wanaotumika kama maafisa vipenyo pale Singida.

Simba wao wanahisi Singida utd na Yanga ni ndugu basi kutambua hilo wakapenyeza watu wao kwa kutumia wachezaji wake walioko kwa mkopo na kigezo cha kujifanya wamewaacha na hakika kwa hilo wameweza kufanikiwa kuanzia ile gemu ya kwanza na gemu ya pili jana dhidi ya Singida Fountain gate.

Ukitizama zile penalti za Gadiel na Mzee wa umepigaje hapo Kagere ni penalti za maelekezo ni penalti za kujikoshesha makusudi kabisa ila Simba waweze kupita na wachezaji hao wawili maafisa vipenyo hakika walifanikiwa hongereni sana kwa kuifanya kazi yenu vizuri.

Simba pia walifanikiwa na faida ya marefa kama tunavyotambua michuano ya mapinduzi ipo kibiashara zaidi kumbe basi ilitakiwa simba ishinde by any means na refa alijua Simba watachomoa goli kipindi cha pili mapema anakuja kushtuka dakika za lala salama Simba bado hawajachomoa goli hapo ndipo akatumia kanuni za magazijuto za CUBA na kuhakikisha simba wanapata goli kama simba wasingepata lile goli ngoma ingeendelea ile mpaka Simba wapate goli sio ajabu tungeshuhudia Dakika 150 jana.

Kwa kifupi Simba wana Quantity na sio quality silaha yao kubwa imebaki kucheza na nje ya uwanja hasa na marefa sijawahi kuona simba ambayo inatafuta ushindi isibebwe na marefa.

EWE KAGERE UMEPIGAJE HAPO

ROMA IKISEMA IMESEMA.
 
Kwa wasiofahamu mchezo wa jana simba walipata ushindi wa penalti kwa faida ya vitu viwili mosi refa alikua upande wao kwa aasilimia kubwa na pia wachezaji wake wa zamani wanaotumika kama maafisa vipenyo pale Singida.
Leo mnaanzisha nyuzi nyingi nyingi za maudhui yale yale. Kunyweni maji hasira zishuke kidogo!
 
Kwa wasiofahamu mchezo wa jana simba walipata ushindi wa penalti kwa faida ya vitu viwili mosi refa alikua upande wao kwa aasilimia kubwa na pia wachezaji wake wa zamani wanaotumika kama maafisa vipenyo pale Singida.
Kuna mchezaji aunawa mpira ndani ya box mpria ambao ulikuwa nakwenda kumkuta striker wa Simba, refa alipeta - hapo napo je unaongeaje ndugu mtoa mada.
 
Unafahamu vema kuwa Kennedy Wilson Juma ni mchezaji wa zamani wa Singida??Kwahiyo ile "assist" yake kwa Rupia,tena bila presha yoyote,akiwa kwenye boksi lake la 18 iliuwa ni kwasababu ni mchezajiwa zamani wa Singida??Nchi ina watu wana akili chache kweli hii
 
Back
Top Bottom