Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Klabu ya Simba leo Jumapili February 13 inashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na ASEC Mimosas kutoka Ivory coast, kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi Kombe la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC.

Hautakuwa mchezo mwepesi, bali utakuwa mgumu na wa kusisimua hasa ukizingatia timu zote mbili zina mbinu zinazofanana uwanjani.

Ubora wa Simba SC kwenye uwanja wa Mkapa ni Mentality nzuri kwa wachezaji kucheza kwa kupambana kwa soka lao la kuburudiasha kwa pasi nyingi na ndefu wakianzia chini mpaka kusogea mstari wa kati huku wakisogea pembeni na mashambulizi ya kasi kupitia kati ama pembeni kutoka kwa mabeki Hussein na Kapombe, ambao ni wazuri kwa 'Crossing'

Kwa upande wa ASEC Mimosas ni wana uwezo mkubwa kama timu na kasi yao ni 'dynamic' wanakimbia kwa kasi kwa mashambulizi ya pembeni kutoka kwa wachezaji wao Athohoula na Coulibally.

Nani kuibuka na ushindi? Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Jioni Usikose Ukaambiwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


=====

00' Naaam mpira umeanza uwanja wa Benjamin Mkapa.. Simba SC vs ASEC Mimosas.

05' Simba SC 0-0 ASEC Mimosas

Mpira ni mkali huku mashambulizi yakielekezwa kwa pande zote mbili hata hivyo bado milango ni migumu.

10' ASEC Mimosas wakijaribu lango la Simba SC, lakini mabeki wanakaa imara.

13' Sakho Goooooooooooooaaal gooal

Pape Sakho anawatanguliza Simba SC bao la kwanza kwa tikitaka murua kabisa | Simba SC 1-0 ASEC Mimosas

15' ASEC wanakosa utulivu, shambulizi lao linashindwa kuzaa matunda.

Pape Sakho yupo chini, baada ya kupata rabsha, anaomba kuingia ameingia sasa.

22' Kagereeee loooooo mpira unaginga mlingoti, almanusura Simba SC waandike bao la pili, ilikuwa hatari sana.

26' Kona kuelekea ASEC, inapigwa kona lakini inaokolewa, mpira uko kati na wamiliki ni Simba SC sasa.

30' ASEC wanatumia sana kujilinda kuliko kushambulia, huku Simba SC wakijaribu kuongeza bao la pili, ngoja tuone.

32' wanao mpira ASEC mbele kulee anapiga shuti, lakini Aishi Manula anadaka, ni shambulizi la On Target.

37' ASEC wanajenga kibanda lango la Simba SC, huko Sakho akiwa chini kwa mara nyingine tena

40' Ametoka Pape Sakho na ameingia Mzamur Yassin upande wa Simba SC, mabadikio yasiyokuwa ya ufundi.

44' Peter Banda anakosa nafasi ya kuiandikia Simba SC bao la pili, ilikuwa nafasi nzuri kufunga...Dooooh

45+3' Kuelekea kuwa mapumziko kwenye mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.


Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanatoka wakiwa mbele ya bao moja kwa bila dhidi ya ASEC Mimosas.

HT: CAFCC; Simba SC 1-0 ASEC Mimosas

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Benjamin Mkapa.

47' ASEC Mimosas wameingia kwa kasi kujaribu kusawazisha.. Lakini Simba wapo imara kulinda lango

53' Kagere anashindwa kuunganisha wavuni Krosi ya Banda, ilikuwa nafasi nzuri kwa Simba SC, Umiliki ni wa Simba SC

ASEC wanajenga kibanda tena lango la Simba, Jaribio lao la kufunga linashindikana hapa.

60' Goooooooooooooaaal, ASEC Mimosas wanasawazisha kupitia kwa Aziz Stephanie kwa shuti kali, shughuli ni pevu sasa ni makosa ya mabeki. Simba SC 1-1 ASEC Mimosas.

64' Kona kuelekea ASEC Mimosas inapigwa konaaa inaokolewa na mabeki wa ASEC.

70' ASEC wanamjaribu golikipa Manula, lakini anadaka shuti lile, ilikuwa hatari lango la Simba SC.

71' Kanoute ametolewa nje kwa matibabu baada ya kupata rabsha

74' Ametoka Kagere na ameingia Jonh Bocco, huku Mhilu akichukua nafasi ya Kanoute..Simba SC 1-1 ASEC Mimosas.

Simba SC wanapata mkwaju wa penalty baada ya Mhilu kuchezewa rafu, Kapombe anakwenda kupiga mkwaju wa penalty

80' Kapombe Goooooooooooooaaal gooal, Kapombe anaandika bao la pili.. Simba SC 2-1 ASEC Mimosas

81' Goooooooooooooaaal gooal
Peter Banda anapiga bao la tatu upande wa Simba baada ya kazi nzuri ya Bocco

Simba SC 3-1 ASEC Mimosas

86' Simba SC wanafanya mabadikio. Ametoka Bwalya na Banda na wameingia Nyoni na Patrick mpira unaendelea.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa CAFCC, Umiliki wa mpira ni wa Simba SC

Almanusura Simba SC waandike bao la nne, baada ya Krosi ya Bocco kutolewa nje na beki wa ASEC

Ni mpira wa adhabu kuelekea Simba SC, Coulibally anaoiga lakini mpira unatoka nje.

Naaam mpira umekwisha ambapo Simba SC wanatoka wakiwa mbele kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya ASEC Mimosas

FT, CAFCC; Simba SC 3-1 ASEC Mimosas

......... Ghazwat..........
 
Kila la kheri Mnyama. Hii ndio ligi yenu. Japo sijazisikia zile kauli mbiu zenu za Do or Die.

𝐊𝐈𝐊𝐎𝐒𝐈 𝐂𝐇𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐁𝐀 𝐃𝐇𝐈𝐃 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐄𝐂 𝐌𝐈𝐌𝐎𝐒𝐀𝐒
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Joash Onyango
5. Enock Inonga
6. Jonas Mkude
7. Peter Banda
8. Sadio Kanoute
9. Meddie Kagere
10.Rally Bwalya
11.Sakho
SUB
Ally, Israel, Gadiel, Wawa, Nyoni, Mzamiru, Bocco, Muhilu, Jimmyson
 
Dk 56:
Dk 54: ASEC wanafanya shambulizi kali lakini mpira unapaa juu.
Dk 52: Banda anapiga pasi nzuri lakini Kagere anachelewa kumalizia mpira.
Dk 50: Simba wamepunguza kasi, Kocha Pablo anasimama kutoa maelekezo.
Dk 47: ASEC wameanza vizuri, wanamiliki mpira na kutengeneza mashambulizi.
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

Dk 45: Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.
Dk 44: Banda anapata nafasi nzuri,a kibaki yeye na kipa, anapaisha mpira juu.
Dk 40: Anatoka Sakho, nafasi yake nachukuliwa na Mzamiru.
Dk 38: Mchezo unaendelea.
Dk 35: Sakho anakaa chini, anashindwa kuendelea, mchezo unasimama, anatolewa nje kwa matibabu zaidi.
Dk 33: Simba wanajipanga taratibu, ASEC wanakabia juu.
Dk 30: ASEC wanapata nafasi nzuri lakini shuti linatua mikononi mwa Aishi Manula
Dk 27: Mwamuzi anaruhusu timu zote zipumzike kwa dakika moja kutokana na joto.
Dk 23: Mchezo unakuwa mkali, timu zote zinafunguka
Dk 21: Meddie Kagere anapiga shuti kali mpira unagonga nguzo na kurejea kisha walinzi wa ASEC wanaokoa.
Dk 18: Sakho anaumia, mchezo unasimama kwa muda.
Dk 17: Kasi ya mchezo imeongezeka, timu zote zinacheza kwa kasi.
Dk 14: ASEC wanaonekana kuamka sasa, baada ya awali kuanza mchezo kwa kasi ndogo.
Sakho anaipatia Simba bao la kwanza, amemalizia krosi nzuri ya Kapombe.
Dk 11: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
DK 8: Simba wanaonekana kujipanga.
Dk 5: Simba wanafanya shambulizi, Sakho anaingia na kupiga krosi nzuri lakini walinzi wa ASEC wanaokoa.
Dk 2: ASEC wanaonyesha utulivu.
Dk 1: Simba wameanza kwa kumiliki mpira, wanacheza pasi nyingi.

Mchezo umeanza.

Timu zimeshaingia uwanjani.

Muda si mrefu wachezaji watatoka kwenye vyumba kwa ajili ya kuanza kwa mchezo huu.

Timu hizi zipo Kundi D katika michuano hii iliyopo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF)

Kundi D
1. RS Berkane (Morocco)
2. Simba (Tanzania)
3. ASEC Mimosas (Ivory Coast)
4. USGN (Niger)

Timu zote zinapasha misuli uwanjani

Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa leo Jumapili 13, 02, 2022 mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu. Mashabiki wanaendelea kuingia uwanjani.



FLeZp3tXIAYeOUE.jpg
 
Go Asec..

Go Mimosa..

You have come d'slaam to hunt a lioness that can't roar without 'chupli chupli'

0-2
 
Back
Top Bottom