Simanjiro: James Millya vs Ole Sendeka

Excellent mkuu. Kupata kwake ziro si kwamba hakuwa na akili, kumbuka kule Simanjiro ndipo kitovu cha tanzanite. Utajuaje kama Sendeka alikuwa pia anazamia migodini na kusoma pia hivyo muda wake ukagawanyika??

once again we are discussing about the merit of people instead of issues

Hivi Kingunge ana division gani? let alone kusoma? Does politics needs someone to have a division? mbona US kuna marais hawakwenda hata darasa moja but wamekuwa marais? Acheni kucomplicate issue mie nadhani la muhimu ni mtu kuwajali wananchi na kuwa na hekima na busara basi.

Swali la shule ni additional qualification tu!!!!
Sielewi Mdondoaji unam challenge nini Maane, Maane alisema kupata kwake Div 0 si kwamba Sendeka hakuwa na akili wewe ukamwambia asi discuss Merit a discuss issues nikakwambia issue ya Div0 ni Millya mwenyewe kaileta nafikiri mlaumu Millya na si mwingine afterall naona hata wewe sasa unaongelea yaleyale
 
Safi sana but let me ask u a question Milya anacholalamika ni yeye kunyimwa haki yake baada ya kutishiwa maisha au uhusiano wake na bwana Ole sendeka?

Binafsi sheria inasema no one is above the law kama bwana Ole Sendeka aliona atishie maisha ya mnyonge kwa kuwa yeye ni mbunge hilo ni kosa na nafikiri bwana millya anayo kesi ya kuraise kama anazo evidence. Ingelikuwa wewe ukitishiwa maisha yako ungelifanyaje?

Millya araise kesi mara ngapi alikataa ushauri wa wazee wa kimila akasema mahakama itatoa haki sasa haki imetolewa anasema hakuridhika anakimbilia media naona anatapatapa tu mwisho wake uko karibu sana
 
Maane na Luteni someni biography ya 7th president wa US anaitwa Andrew Jackson aliyeongoza miaka 8 marekani tafuteni kama alisoma hata darasa moja.
Naona wewe huna hoja mimi nasema Sendeka ameonyesha uwezo wa kujenga hoja bungeni kuwazidi walio na PhD sasa what is the difference with your argument au unataka ligi tu isiyo na mbele wala nyuma hata Maane amejaribu kuelezea hivyo hivyo wewe ndiyo ukasema asi discuss issue hiyo which is which sasa
 
Join Date: Sat Mar 2010
Posts: 8
Thanks: 1
Thanked 11 Times in 6 Posts
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif


Huyu amejoin juzi tu, wenye akili wanajua ni kwa nini!

Huu ndiyo ujinga ambao tuwahi kujadili huko nyumba.
Mtu ku-join jana inamaanisha alikuwa hasomi post za jf?.
Badala ya kuuda hoja na tujadili,mtu anaanza kuangalia mtu ali join lini?.
 
Naona wewe huna hoja mimi nasema Sendeka ameonyesha uwezo wa kujenga hoja bungeni kuwazidi walio na PhD sasa what is the difference with your argument au unataka ligi tu isiyo na mbele wala nyuma hata Maane amejaribu kuelezea hivyo hivyo wewe ndiyo ukasema asi discuss issue hiyo which is which sasa

tuko pamoja mkuu samahani sana kwa kukuelewa vibaya respect!!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 14, 2010


Utangulizi
Ndugu waandishi wa habari, kwanza kabisa nikushukuruni kufika hapa leo. Siku zote mmekuwa watu wa karibu nami na ndio maana baada ya kufika hapa Dar es Salaam juzi kuhudhuria kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM-Taifa kilichoanza tarehe 12, mwezi huu, nilianza kupata simu za baadhi yenu wakitaka kusikia maoni yangu juu ya kesi yangu dhidi ya Christopher Ole Sendeka. Kutokana na simu hizo kuwa nyingi, nilionelea bora nizungumze nanyi pamoja ili kila mmoja aliyekuwa na nia ya kupata taarifa zangu aweze kuzipata kwa kuzingatia muda na sehemu. Hivyo basi nipo hapa mbele yenu kwa jukumu hilo.

Historia yangu
Historia ya maisha yangu imeambatana na mambo mengi kama ambavyo ilivyozoeleka katika maisha ya Watanzania na hasa jamii ya wafugaji. Nimezaliwa Wilayani Simanjiro na kusomea shule ya msingi huko. Hapa nilipo nina shahada ya pili katika Sheria za Haki za binadamu na demokrasia niliyoipatia katika vyuo vikuu vya Pretoria, Afrika Kusini na American University of Cairo.

Tangu nikiwa mdogo nimejihusisha katika harakati mbalimbali zinazohusu kutetea haki za makundi ambayo nimekuwa nayo na jambo hili kwa kiasi kikubwa ndilo lililonisukuma kusomea taaluma ya sheria. Ninao uzoefu wa kina baada ya kufanya kazi za ndani ya nchi na kimataifa. Nimefanya kazi na Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji sambamba na hapa Tanzania katika mahakama ya kesi za mauaji ya kimbari ya huko Rwanda, ICTR.

Katika maisha yangu nimeweza pia kuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali. Kwa sasa nashikilia nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa. Nafasi hizi nimezipata kutokana na historia ya uwajibikaji wangu usiotiliwa shaka na moyo wangu wa kujitoa katika kusaidia kufanikisha majukumu yanayokuwepo mbele yetu katika taasisi yoyote niliyobahatika kufanya nayo kazi.

Nini maana ya Historia Hii
Nimeamua kutaja historia hii fupi kwa lengo moja ama mawili. Kwanza kuwafahamisha mimi ni nani na pili kuwaonyesha kuwa mimi ni mtu makini, mwenye akili timamu na ninayeweza kufanya maamuzi yangu bila kuhamasishwa na kitu, watu ama kundi lolote.

Kwa nini nilifungua kesi
Zipo sababu mbalimbali ambazo zilinisukuma kufungua kesi yangu dhidi ya Ole Sendeka. Sababu hizi ni kama ifuatavyo:

· Imani yangu kuwa binadamu wote sawa na kwamba haki ya binadamu inayokwapuliwa hupatikana katika vyombo vya sheria. (Katika shahada yangu ya pili nimesomea masuala haya ya haki za binadamu na demokrasia)
· Utambuzi wangu kuhusu mahakama kuwa chombo cha kutenda haki, kinachosimamia haki za kila mtu anayedhulumiwa na kunyanyaswa bila kubagua. Nikiwa mhitimu wa taaluma ya sheria na pia muhanga wa tukio kupigwa na kutishiwa bastola nililofanyiwa na Christopher Ole Sendeka, niliamini njia muafaka ni hii ya kutumia mahakama kupata haki yangu.
· Tafakari niliyofanya baada ya kubaini kuwa, mshtakiwa Ole Sendeka ana rekodi ya tuhuma za uhalifu wa kutishia na tabia nyingine chafu katika jamii. Katika tafakari hii nilitazama matukio na historia yake na kubaini kuwa, amekuwa akifanya matukio mengi lakini kwa kutumia mfumo wa kimila na mifumo ambayo siyo rasmi, amekuwa akifanikiwa kuzima matukio hayo. Nitataja matukio machache kama ifuatavyo;
I. Kumtishia kwa bastola ndugu Paulo Yamat ya tarehe 20 Mei 2001. Baada ya tukio hili kesi yenye RB namba KIB/IR/282/2001 ilifunguliwa na kisha kufutwa baada ya Sendeka kutumia vikao vya wazee wa kimila. Maelezo ya vikaohivyo yapo..
II. Tukio la kumchokoza, kumtishia na kugombana kati yake na Marehemu Mzee Soipe aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na mzee wa Kimila.
III. Tena, kuna tuhuma za kumpachika mimba mwanafunzi na kumfanya kupoteza haki yake ya kusoma. Upo ushahidi wa kesi aliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hii lakini ilifungwa katika mazingira ya kutatanisha. Nisisitize hapa, juzi nilikuwa nikimuona Mama Salma akizungumza na chama cha walimu wanawake, ambao walikuwa na kampeni ya kupambana na mimba mashuleni, nadhani nitumie fursa hii kumuomba Mama Salma aanze na Simanjiro maana huko kuna viongozi wasiotambua maana ya elimu na ambao wanaonyesha mfano mbaya kwa jamii yetu.Inawezekana tabia hii pia akawa anaifanya kwa kuwa yeye mwenyewe alipata division 0 katika matokeo yake ya kidato cha sita, hivyo anaona wengine hawana haki ya kupata elimu bora kwa kuwa yeye alishindwa.
IV. Akiwa mkuu wa utawala wa UVCCM alipata tuhuma za kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wakati huo na sasa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ndugu Guninita
V. Akiwa na nafasi hii hii ya ubunge, zipo tuhuma za yeye kumtemea mate mbunge mwenzake. Lakini la kuashangaza hapa ni kuwa, vyombo vya habari hasa vya swaiba wake Mengi, vimemfanya mtu huyu kuonekana katika jamii kuwa ni mwenye haki na mtetezi wa wanyonge. Hii ni hali mbaya sana kwa kuwa inapotosha ukweli na kuwafanya wananchi wa nchi hii kutopata watu wa kweli wa kuwaamini na wanaoweza kusimama na kuwa mfano bora wa jamii yetu.

Kwa mtindo huo huo usio rasmi aliweza kuwatumia wazee wa kimila, viongozi wa kidini na watu wengine maarufu katika maeneo yetu ya Umasaini ili niitwe katika vikao vyetu vya kimila ili niweze kumsamehe. Hii imekuwa historia yake, na amefanya mfumo huo kuwa kinga yake. Ni wazi katika mfumo huo amefanikiwa. Binafsi sikuona umuhimu wa kuendeleza orodha ya wahanga ambao wamekwapuliwa haki zao na Sendeka kwa kutumia mbinu ya mila. Niliamua kwenda mahakamani kutafuta haki yangu ili iwe fundisho kwake na kwa wale wote waliopewa dhamana ya uongozi wa wananchi na wenye mali. Tena nililenga kujenga na kudumisha utamaduni wa watu kuheshimu utawala wa sheria.

Nini matokeo
Baada ya mimi kwenda mahakamani, mengi yametokea. Mambo haya yaliyotokea ni wazi yamenisikitisha na kunionyesha picha ya kuwa, haki ya mtu inaweza kuchezewa kwa maslahi ya mtu ama kikundi fulani. Baadhi ya mambo haya ambayo hata nanyi mmeyaona ni kama ifuatavyo;

· Matumizi ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vina lengo la kuandika habari potofu na zile tu ambazo zinanikandamiza mimi. Hapa nazungumzia vyombo vya habari vya IPP. Na kwanza nitambue uwepo wa waandishi kutoka katika vyombo hivi, najua wazi kuwa nafasi yenu katika mioyo yenu ni safi sana na wala hamkuhusika kwa mioyo yenu kufanya jambo hili ambalo ni kinyume na taaluma yenu. Ndio maana nimewaita hapa pamoja na wenzenu, najua kulikuwa tu na mashinikizo fulani yaliyosababisha taarifa za Televisheni na habari za magazeti ya kampuni hii kuwa na mlengo huo wa kunikandamiza mimi. Ndugu waandishi wa habari, niwakumbushe tu jambo hili; hivi kweli zipo kesi ngapi nchini ambazo hazipati kuonyeshwa katika televisheni na badala yake iwe hii ya kwangu tu? Mnaweza kujiuliza hii ililenga nini?Mimi ni kijana mdogo tu kutoka katika jamii ya wafugaji, sasa nguvu ile ya kunikandamiza vile ililenga kitu gani?
· Kuingia kwa mfanyabiashara Reginald Mengi tangu siku ya kwanza ya kutajwa kesi ambapo yeye mwenyewe alihudhuria mahakamani na kisha kufuatia taarifa za kupotosha jamii kuhusiana na kesi hiyo. Vyombo vya IPP, vilinihusisha mimi kutumwa na wanasiasa na hasa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kwenda kumshtaki Sendeka. Lengo la kumuingiza Lowassa katika kesi hii lilikuwa kujitafutia umaarufu kwa Sendeka mwenyewe na kutafuta huruma na kusaka misaada ya kumsaidia katika kesi ile hasa kwa wabaya wa mheshimiwa Waziri Mkuu mstaafu. Upotoshaji huu ni wazi ulilenga kupotosha maana nzima ya kesi yangu na kukwapua haki yangu mahakamani. Naomba nisisitize hapa, kabla ya kufungua kesi hii na kwa kuwa ilitokea katika kikao ambacho Lowassa alikuwepo kama kiongozi rasmi, yeye binafsi akiwa na Askofu Laizer waliniiita nami nikaitikia wito wa kuwaona. Hoja yao ilikuwa nijadiliane na Sendeka ili nimalize jambo hilo kwa taratibu zetu. Nilitafakari yote waliyonieleza lakini, mwisho niliwashukuru na kuwaeleza msimamo wangu wa kuamini katika utawala wa sheria. Lakini pia ndugu waandishi nieleze pia kidogo, mimi nafahamu vizuri sana athari za kutofautiana ama kisiasa au kibiashara kwa mzee Mengi na baadhi ya watu hapa nchini, mfano anaweza kuwa rais mstaafu Benjamin Mkapa ambapo mtaona namna ambavyo amejitahidi kupitia vyombo vyake kumchafulia taswira kiongozi huyo wa nchi hii. Sawa tu mimi ni kijana wa familia duni, lakini naamini katika nguvu ya Mungu kwa kuwa katika yeye siku zote haki ya mtu haipotei. Haya nayaona kama majaribu na pepo wa Ibilisi tu, mwisho nitabakia nimesimama na nikiwa imara zaidi.
Kutokana na mambo haya niliyoyaeleza hapo juu, naamini ilikuwepo mbinu chafu iliyochezwa kuhakikisha kuwa sipati haki yangu mahakani. Kwa mfano ni pale ndugu Telele ambaye alikuwa shahidi muhimu wa serikali dhidi ya Sendeka kukanusha ukweli wa kuona tukio la shambulio la Sendeka na baadaye kuwa ni mhusika na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mapokezi ya Sendeka baada ya kutangazwa kufutiwa mashtaka.

Nilijiuliza pia tangu siku ya kwanza nilipoingia mahakamani pale nilipomuona Mzee Mengi ambaye ni mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari nchini, nikajiuliza kulikoni? Nikatafakari na kuwaza labda mzee huyu ambaye ni mchimbaji mkubwa wa madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro ni swahiba wa karibu wa Sendeka katika maslahi yao binafsi. Najua uwekezaji huu wa Mengi wilayani kwetu hauna manufaa ya wazi kwa wakazi wa Simanjiro zaidi yake yeye na swahiba wake Sendeka. Labda hiki ndicho kilichomleta yaani kusimamia maslahi ya mdau mwenzake katika kutafuna maliasili za Simanjiro.

Naomba ieleweke kuwa, kesi yangu haikuwa na haitakuwa na mahusiano ya aina yoyote ya kisiasa ama ya kundi fulani. Sikushinikizwa, sikutumwa na wala sikumtuma Sendeka kunishambulia baada ya kushindwa nguvu ya hoja. Sikulazimishwa kwenda mahakamani kumshitaki kama ambavyo vyombo vya habari vya IPP na washirika wao wanavyotaka kuiaminisha jamii ya Kitanzania.

Nimesimamia hili kwa sababu naamini mahakama ndicho chombo kinachoweza kumsaidia mnyonge yeyote hapa nchini kupata haki yake. Imani hii nitabaki nayo siku zote za maisha yangu na nitakuwa tayari kuwasaidia wengine kuipata haki hiyo kwa namna ninavyoweza kutokana na taaluma yangu ya sheria na utashi wangu binafsi.

Hitimisho
Baada ya kushauriana na wakili wangu, ndugu zangu na wengi wenye mapenzi mema nami ambao wanaamini katika mfumo wa sheria, haki na uhuru wa mahakama; nimeamua yafuatayo;
1. Kuiomba serikali kwa kuwa ndiye mshtaki katika kesi hii kufikiria namna ya kukata rufaa katika kesi hii kwa kuwa inaonyesha kulikuwa na mazingira yaliyojengwa mapema kabisa ili kupoteza maana ya kesi hii wakati ikisikilizwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Mnaweza kuona hata tukio la shahidi mmoja aliyetakiwa kutoa uashahidi na serikali kisha anakuwa mmoja wa wana kamati ya maandalizi ya mapokezi ya mashatakiwa.

2. Ni wazi kuwa binafsi sijaridhishwa na hukumu iliyotolewa naamini kuwa Sendeka ana kesi ya kujibu. Lakini nisisitize pia hapa, ninayo imani kubwa na sekta ya mahakama na vyombo vingine vya dola hapa nchini hivyo kuteleza katika ngazi moja siyo kuwa ni mwisho wa mahakama hiyo kutoa haki katika kesi hii. Naamini mahakama na vyombo vinavyohusika vya serikali vitaungana nami kama ambavyo vimeshafanya katika jitihada za kutafuta haki yangu mpaka ipatikane.
Nawaombeni ndugu zangu wana habari kuwa, tujenge Tanzania yenye kujali habari zilizofanyiwa utafiti na za kweli. Tufikirie mara mbili mbili kabla ya kuandika na tutazame kwa mfano; kama ingekuwa ni wewe, ndugu yako ama mtu mwingine yeyote anafanyiwa jambo na kisha wanaoandika wanapindisha ukweli, je ungefurahia jambo hilo?
Niwafahamishe pia ndugu zangu wa Simanjiro, mimi nimelelewa vema kwa mila zetu, naziheshimu sana. Tena nathamini sana maamuzi ya wazee wangu wa Kimila na kufungua kwangu kesi hakukulenga na hakutalenga kuwadharau ama kuwapotezea heshima. Nilibaini kuwa huu ni uamuzi sahihi wenye lengo la kusaidia jamii yetu dhidi ya wapotoshaji wa mila. Mila zetu hazihamasishi ukorofi na tabia ya kutisha ama kupiga watu. Mila zetu zinahubiri upole, udugu na urafiki na sio mmoja kujigeuza mkubwa kwa kila anayekutana naye na wakapingana kwa hoja.

Nakushukuruni kwa kunisikiliza na asanteni sana.

James Millya
...watanzania wengi inaonekana wana akili za rojo rojo, kuthibitisha hili angalia habari za magazeti mengi ya kila siku,ndio maana si ajabu kuitikia mwaliko wa mpumbavu mwenzao kujadili UPUMBAVU!!!
 
Huruma nayopata ni mahakama zetu hapa nchini kwa mtu kama Millya, kwakweli kama huna pesa ni ngumu kushindana na mtu mwenye pesa, tena hasa mwenye uzoefu wa kuzichezea mahakama kama Mengi, lakini kama kiongozi, lazima apiganie haki yake mpaka mwisho, ili jamii ifahamu kweli kwamba alishambuliwa na yeye hakutunga kesi au Sendeka amuombe radhi hadharani. Ndugu Millya, Great thinkers of JF are behind you, kila la kheri!

Ole Sendeka ameshinda kesi yake. Kama katumia fedha za Mengi au zake mwenyewe huo ndio utamaduni uliopo Tanzania siku hizi. Money speaks! Millya katika taarifa yake amesema:
sasa nashikilia nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa.

Huyu unayem-brand umaskini aliwezaje kupata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha wakati tunaelewa dhahiri kwamba vyeo ndani ya CCM havipatikani bila kutumia pesa? Kama maskini alitoa wapi pesa za kuweza kushinda na kuwa Mwenyekiti. Acheni kutudanganya. Lisemwalo lipo. Huyu kijana inaelekea anatumiwa tu! Nani asiyejua makundi yaliyopo ndani ya CCM?

Ilishasemwa hapo awali kwamba kama Millya ni Morani, Morani huwa hawalii-lii hovyo hadharani! Yeye bado kijana, kama anaipenda nchi yake na chama chake aachane na kutafuta kumshinda Ole Sendeka badala yake aelekeze nguvu zake kwenye shughuli za UVCCM kwa manufaa ya umoja huo na CCM kwa ujumla.
 
Millya pole sana ila tangu siku ile pale steers Dar ukiwa na wapambe wako akiwamo tule mwanamke mwana CCM niliwasikia maongezi yenu nikashindwa kujua kama kweli hata ka tone ka elimu mlikuwa nako .Niliwasikia mkipanga na kujitapa juu ya kumliza Sendeka . Kama unasoma kumbuka mlikuwa watu 3 na yule mwanamke wa Arusha mnajitapa mwezi ulio pita kabla hamjaangushwa mahakani. That was very low kwa mtu kama wewe kuongea na kuwa na plan zile . Nakuhakikishia kama ume ajiriwa shikilia ajira na achana kabisa na Siasa maana si wewe wala wapambe wako wanajua la kufanya .Hutashinda hatama kama ulidai na yule mwanamke kwama Sendeka hakupewa Jimbo na Mungu . Mbinu chafu tokea steers will never help you na sasa unakimbilia kwenye media unaharibu zaidi .

Ila pia kumbuka sisi tunacheka maana CCM baada ya kutula sasa mbinu zenu chafu mnaanza kuonyeshana wenyewe kwa wenyewe . Laana kubwa inakuja juu yenu .
 
kwanza jamii pls ondoeni hii option ya kuquote wakati mmoja wetu anajibu inachukua muda sana lakini haya ni mani yangu.

ole millya mwachie mungu tu kwani huonekani kama legal man for real,asingekushinda huyu mahakamani. na kukata rufaa hutoshinda maana you must have a new and profound evidence nayo utaipata wapi wakati principal witness wamegeuka. achilia mbali,

muundie kesi ingine maana tabia haina dawa atarudia tena.

Mkuu,

Sasa wewe hujatofautiana na Sendeka.Mara muachie Mungu mara Muundie kesi nyingine.

Hapa mkuu msimamo ni upi?hayo hapo juu ni kama mafuta na maji
 
Tanzania kuna siasa za chuki na majungu sana. Wanasiasa jamani leteni maendeleo katika Taifa hili na sio majungu na chuki zitakazoingiza taifa katika machafuko. Historia inaaonyesha kuwa sehemu zilizowahi kuwa na machafuko na mauaji ya raia Afrika kwa asilimia kubwa inasababishwa na wanasiasa.
Tuijenge Tanzania isiyo na siasa za chuki na majungu jamani
 
Binafsi sheria inasema no one is above the law kama bwana Ole Sendeka aliona atishie maisha ya mnyonge kwa kuwa yeye ni mbunge hilo ni kosa na nafikiri bwana millya anayo kesi ya kuraise kama anazo evidence. Ingelikuwa wewe ukitishiwa maisha yako ungelifanyaje?

Sasa bw. mdondo, mbona unaongea huku unajing'ata ng'ata?

Kama sendeka alimtishia na kweli ni kosa kisheria kutishia, na bw.millya akaamua kwenda mahakamani baada ya kudharau ushauri wa wazee wa kimasai kutaka wayamalize, sasa analalamika kitu gani? Yani leo ndio anakumbuka vyombo vya habari na kutafuta public sympathy? sisi tunaomfahamu bw millya wala hatuna sababu ya kumhurumia hata kidogo, kwakuwa aliyataka mwenyewe kusikiliza ushauri wa mzee wa richmond sasa akaze msuli sio kulialia.

Kama anadhani vyombo vya habari vya mzee mengi ndivyo vimemuangusha mahakamani si atumie radio five na ABC tv (kama imeanza kuruka hewani) ili kukabiliana na IPP media!!

Kama iktokea Millya akamshinda Sendeka kwenye kura za maoni ndani ya ccm na wakaamua agombee ubunge simanjiro, hilo litakuwa jimbo litakalochukuliwa na upinzani kwa uhakika na kwa ulaini.

Tatizo la bw. milya ni uwezo wake bado ni mdogo, pamoja na kutwambia ana LL.M, cha msingi aendelee tu na ajira aliyonayo bad hajaiva kisiasa.
 
Milya Olesendeka kwa hili kakuzidi maarifa tafuta mbinu nyingine, kung'ang'niza mbinu hii moja kuta kushushia hadhi wewe bado kijana mdogo una safari ndefu mno kisiasa usijichafue mapema hivi.
Jifunze mbinu mpya.
 
jamani lazima watanzania tuwe na shukrani, huyu mzee mengi ndo aliyetufungua macho, Tanzania kulikuwa hakuna TV lakini huyu mzee alituwezesha na kutufix kwenye nchi zenye ustaarabu, sasa kwa kuwa cku hizi kuna series ya TV then mnamuona is a scambag, hey folks, kumbukeni tulikotoka and figure out
 
..naona watu kama hawako impartial ktk taarifa hizi.

..CCM wameamua kupatana, kwamba sasa hivi mafisadi na "wapiganaji" wamekuwa kitu kimoja kuelekea uchaguzi mkuu. hii ndiyo strategy ya CCM dhidi yetu wananchi.

..Ole Sendeka vs Ole Millya ni masuala binafsi. wanagombea ulaji tu hao. hakuna yeyote kati yao anayeweza kudai ameisaidia jamii yake kupiga hatua ya maendeleo. jimbo lina utajiri kibao lakini limechoka kama nini.
 
IMEKAA KAAJE SHAHIDI MUHIMU WA MASHTAKA KUANDAA MAPOKEZI YA MSHTAKIWA?

Mnadhani hapo hakuna mikakati miovu iliyofanyika?
Kwa kawaida mahakama huamua kesi kulingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani. Ushahidi wa kimazingira uhusishwa pale tu ambapo unahusina moja kwa moja na tukio - wakati linatokea au kabla halijatokea - kulingana na mazingira yaliyosababisha litokee. Sina uhakika iwapo ushidi wa kimazingira wa matukio yanayotokea baada ya kesi kuamuliwa yanaweza kutumika kama hoja kwenye rufaa
 
Millya: Sijatumwa na Lowassa kumshtaki Sendeka

na Mwandishi Wetu


amka2.gif
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James ole Millya, amesema hakutumwa na aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kumshtaki mbunge wa Simanjiro Christopher ole Sendeka.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, alisema yeye alifikia uwamuzi huo baada ya kupigwa kofi na Sendeke kitu kilichomvunjia heshima mbele ya jamii.
"Lengo la kumwingiza Lowassa katika kesi hii ilikuwa kujitafutia umaarufu kwa Sendeka mwenyewe na kutafuta huruma na kusaka misaada ya kumsaidia katika kesi hasa kwa wabaya wa Lowassa.
"…Naomba nisisitize kuwa kabla ya kufungua kesi hii na kwa kuwa ilitokea katika kikao ambacho Lowassa alikuwepo mgeni rasmi, yeye binafsi na Askofu Thomas Laizer waliniita nami nikaitikia wito wa kuwaona," alisema Millya.
Alisema hivi sasa anakusudia kukata rufaa dhidi ya Sendeka kwa vile hakuridhishwa na mwenendo mzima wa kesi hiyo iliyoendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
"Ni wazi kuwa binafsi sijaridhishwa na hukumu iliyotolewa na naamini kuwa Sendeka ana kesi ya kujibu, lakini napenda kusisitiza kuwa nina imani kubwa na mahakama na vyombo vingine vya dola, hivyo basi kuteleza katika ngazi hii si mwisho wa mahakama kutoa haki katika kesi hii.
"…Naamini mahakama na vyombo vingine vinavyohusika vya serikali vitaungana nami kama ambavyo vimefanya katika jitihada za kutafuta haki yangu mpaka ipatikane," alisema Millya.
Alisema anafikiria namna ya kuiomba serikali kwa kuwa ndiye mshtaki katika kesi hiyo kufikiria namna ya kukata rufaa kwa vile inaonyesha kulikuwa na mazingira yaliyojengwa kupoteza maana ya kesi wakati ikisikilizwa.
"Kila mmoja anaweza kuona hata tukio la shahidi mmoja aliyetakiwa kutoa ushahidi na serikali amegeuka kuwa mmoja wa wana kamati ya maandalizi ya mapokezi ya mshtakiwa," alisema Millya.
Kutokana na hali hiyo, Millya ameitaka serikali kumfungulia mashtaka kwa kuidaganya mahakama kwa vile hakuwa mkweli pindi alipotakiwa kutoa ushahidi.
Alisema baada ya yeye kwenda mahakamani, ameshuhudia mambo mengi kutokea ikiwa ni pamoja na haki ya mtu kuchezewa kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi fulani.
‘Baadhi ya mambo hayo ni matumizi mabaya ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa na lengo la kuandika habari potofu na za kunikandamizi… naelewa nia hiyo," alisema Millya.
Sendeka alikuwa akikabiliwa na kosa la shambulio la kudhuru mwili na kutishia kwa silaha. Ilidaiwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 9, mwaka jana majira ya saa 10:00 jioni katika Chuo cha Ualimu Monduli.

Maoni yangu: Huyu dogo kafulia, ajitafutie mkakati mbadala wa kutafuta ubunge kule simanjiro
 
Back
Top Bottom