Simanjiro: James Millya vs Ole Sendeka

Hivi Sendeka hakuwepo katika kikao cha bunge kilichofunga mjadala wa Richmond?

Alikuwepo kwenye hilo bunge na alizungumza kulaani RICHMOND na alijaribu kuelezea tofauti kati ya bunge la wazalendo na mamluki. Kauli yake kwenye kikao kile cha kufungwa kwa mjadala wa RICHMOND bila shaka itakuwa imeingia kwenye vitabu vya historia yetu kama kauli ya kizalendo na bila shaka itatumika sana kama rejea siku za usoni.
 
Naona mawazo ya jumla ya wengi yanashindwa kuangalia vipengele vingine vinavyotia mashaka kama alivyosema Millya, IMEKAA KAAJE SHAHIDI MUHIMU WA MASHTAKA KUANDAA MAPOKEZI YA MSHTAKIWA?

Mnadhani hapo hakuna mikakati miovu iliyofanyika?


Huyo milya nae LLB yake ni mashaka matupu. Yeye kama mwanasheria anafikiri mtu kuwa shahidi wa upande wake ni lazima awe adui wa yule anayemtolea ushahidi?. Eti vyombo vya mengi vimenhujumu. Maana yake nini kama sii anataka kutuaminisha kuwa vyombo vya habari ndio vinavyokata kesi mahakamani na wala sio sheria. Milya anasema je kwa vile vyombo anavyoamini viko rational? Vina mamlaka kidogo kuliko vya Mengi? Uanaharakati wa milya umeshindwa nini kutetea mtoto anaedaiwa kukatizwa masomo na badala yake nae anabaki mlalamishi tu? Basi Ole ni gari kubwa kwani hata waziri wa utawala bora nae kabaki akilalama kuwa kama nchi hii ingekuwa inafuata sheria Sendeka angekuwa gerezani hivyo milya pisha njia kari kubwa ipite!!
 
Daah,inasikitisha sana kwa kweli kwa baadhi ya wasomi wetu;tena eti ana degrees mbili za sheria!!

Kasema mwenyewe kama kuna tuhuma za Mbunge Sendeka ti alimpa mimba mwanafunzi,kaogeza tena kuwa kesi hii ilikuwepo na eti ilifungwa kiujanja ujanja!

Then akaniacha nicheke hadi nianguke chini aliposema "anamuomba Mama Salma Kikwete aingilie kesi hii,kichekesho hapo ni kikubwa mno jamani;Mama Kikwete sio mwanasheria na Milya ni Mwanasheria,why sasa amuachie kesi hii Mama Kikwete na wala asiisimamie yeye ambayo amedai anaijua na ana taaluma ya sheria?

Naam hawa ndiyo wasomi wetu,wa kuwaita waandishi wa habari na kutaka kuingiza sheria kwenye siasa.

Milya huna jipya na Mzee Korne anakudanganya sana,mwenyewe alishindwa vibaya mwaka 2005 na likely hata ww utashindwa vibaya maana bado miezi 4 tu kura za maoni zipigwe lkn wewe badala ya kujipanga unaleta mambo yasiyo na tija kwa wapiga kura wako!

Millya will be another Loser,who wana bet>?
 
Pole sana Mallya. Nimepokea maelezo yako kwa masikitiko ila hayana maudhui sahihi ya taaluma uliyonayo ya Sheria. Mimi naona kama unatoa hadithi hivi. Ebu jaribu kuona wanasheria wenzako wakusaidie namna ya kuzipanga hizo tuhuma zako na kutueleza kuwa umezifikisha kwenye vyombo husika na hatua zilizochukulia (unao ushahidi - hasa hilo la mimba).
Masuala ya ugomvi wa Mengi na Lowasa hayatusaidii sana watanzania zaidi nakuomba utueleze jinsi Mengi anavyotuibia Tanzanite zetu na tufanyeje kumdhibiti.
 
Naona mawazo ya jumla ya wengi yanashindwa kuangalia vipengele vingine vinavyotia mashaka kama alivyosema Millya, IMEKAA KAAJE SHAHIDI MUHIMU WA MASHTAKA KUANDAA MAPOKEZI YA MSHTAKIWA?

Mnadhani hapo hakuna mikakati miovu iliyofanyika?
Kama Millya anaiheshimu mahakama vile vile anatakiwa ayaheshimu maamuzi yake mahakama haikumuona Sendeka na hatia kuna ubaya gani kwa mtu yeyote akiwemo yule anayemuita shahidi muhimu kuungana na kusalimiana na mtu huru

kuandaa au kutoandaa si hoja kubwa hapa hata kama aliandaa mapokezi basi huyo jamaa kaonesha hana kinyongo kabisa nafikiri naye Millya angeonesha kukomaa hasa kiakili kama personally angekuwepo kwenye hayo maandalizi na kupeana mikono ya heri baada ya kuendeleza majungu mitaani
 
Eti hapa nilipo ninashada 2, So what? Shahada 2 bado limbukeni Mkubwa!
Jaribu mbinu nyingine! Ole wala hatumii nguvu! Ni kuusimamia ukweli na ndio viongozi tunaowataka! Ooooh kapiga mimba mtoto wa shule..... mpeleke mahakamani! Oooh alimtishia Mzee Guninita! Upuuzi mtupu!!
 
“Matumizi ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vina lengo la kuandika habari potofu na zile tu ambazo zinanikandamiza mimi...”
Kama viliandika habari potofu kwa nini Millya (Kama umo humu JF) usiwafungulie mashitaka ya defamation hao waliondika habari potofu?
“Kuingia kwa mfanyabiashara Reginald Mengi tangu siku ya kwanza ya kutajwa kesi ambapo yeye mwenyewe alihudhuria mahakamani na kisha kufuatia taarifa za kupotosha jamii kuhusiana na kesi hiyo...”
Hivi ni wapi ambapo sheria za za nchi yetu zinamzuia mtu kuingia kwenye mahakama in public galleries... hata kama mtu huyo alikuwa mfanya biashara, mtu wa kawaida au la ama aliikngia siku ya kwanza ya pili au ya mwisho?
“Tafakari niliyofanya baada ya kubaini kuwa, mshtakiwa Ole Sendeka ana rekodi ya tuhuma za uhalifu wa kutishia na tabia nyingine chafu katika jamii....”
Hii haiwezi kuhusiana moja kwa moja na kosa la sendeka kukushambulia... au ndo iwe motivation yako kumfungulia kesi.... Millya unapwa kujua sheria ikoje katika mambo ya evidence... nakushauri urudi tena darasani maana elimu haina mwisho kama wahenga walivyosema.. nina wasiwasi na elimu yako ya LLB na LLM unatuangusha wenye taaluma kama zako tafadhali...
Kama Sendeka alifanya makosa yalioamuliwa kwa sheria za kimira na mjadara wa makosa hayo kufungwa... Millya ulipaswa kujua kwamba sheria za kijadi zinatambulika na serikali ya Tanzania katika conflict resolutions... labda ndo maana sendeka alienda huko... kuwa makini tu kusema mambo ya hear say usije ukafunguliwa mashitaka ya contempt of court au defamation na wabaya wako...
 
Wazee, huyu millya ni kilaza kupita maelezo. Chuo alichosoma mtu akimaliza masters lazima afanye publication in pieer reviewed journal. Lakini thesis yake haijatoa paper hata moja na ni 54 pages. Sasa hii kazi alinakili mahali au alifanya utafiti? na kama ni tafiti why not published? Was it of low quality or not even needed in journals. maojiano yake na waandishi yamenifanya nifikie kuuliza hayo maswali hapo. Wana jamvi nisaidieni.
 
Kusoma na kuelimika ni vitu viwili tofauti, mambo ya Mahakama ni magumu sana, na nadhani kwa Watanzania wengi tunapenda kulaumu hukumu za mahakama, lakini tatizo linakuwa lipo kwenye ushahidi na hiyo ndio weakness yetu kubwa,
kesi yako bwana Millya ilikuwa haina ushahidi wa kutosha, hata kama Ole Sendeka alikuwa na mamkosa lakini mahakama haiwezi kuhukumu bila ushahidi

kesi ya Zombe, hata JK anajua kuwa Zombe kausika moja kwa moja, lakini DPP alipeleka ushahidi shallow wa kumtia Zombe hatiani;

KUNA KIKUBWA PIA CHA KUANGALIA HAPA, KUNA TOFAUTI KUBWA SANA YA MENGI NAKUNDI LAKE NA RA/EL NA KUNDI LAO

MENGI SIO MWANASIASA WA WAZI KWA HIYO YUPO FREE SO FAR HANA CHA KULOOSE, HATA KAMA ANAUTAKANA URAISI BASI SIO KWA SASA NA NDIO MAANA UTAONA ANAUWEZO WA KUJA MPAKA MAHAKAMANI AU KWENYE MIKUTANO YA WANAHARAKATI WAKE (Mwakyembe, Sitta etc), kwa upnade wa kina Lowasa na RA wao lazima watumie third part (Wapambe), kwa hiyo kama uko kwenye Mtandao wao hata siku moja huwezi kuwaona hao jamaa mahakamani au kwenye Kampeni za kisiasa za wanamtandao wao, kwa sababu wao wana vitu vya kuloose

Kuhusu hili la vyombo vya habari nadhani ni Busara kama Millya angesema Vyombo vyote vya Habari TanzaniaViko biased, maana hata TBC1 ambacho ni cha serikali pia kina favour Mambo ya CCM
 
Mfianchi , Gengder Sentive
Naadhani ni jambo zuri na busara zaidi ukiona umuhimu wa kunuu taarifa ya mtu ukanukuuu (Quote )kipengele cha muhimu kuliko kunukuu habari nzima tena ndefu. It is redunducy sijui wengine wanachukuliaje.
.
Hata mimi huwa nashangaa watu humu wanaquote habari nzima halafu wanacomment mstari mmoja! Kwa nini usinukuu sehemu ya habari unayoona unataka kuitolea comments? Kama unataka kutolea habari yote, kwa nini sasa unanukuu? Kwa kufanya hivyo vertical scrolling inakuwa ndefu na inaboa!
 
James Ole Milya kachokoza nyuki, subirini mshuhudie jinsi Ole Mangi atakavyo mshukia.
Mimi binafsi sijaridhishwa na presentation hii ya Ole Milya kama holder wa LL.M, nitafurahi kama nitasikia hiyo LL.B yake aliichukulia wapi, maana anaandika kama just a layman. Kama mwanasheria, he should have known better.

Kama Ole Milya unaingia JF, nakushauri achana na kukata rufaa, Jamaa huwawezi!. Mtandao wao ni mkubwa!. Futalia kesi ya Silverdale Farm, kuna mzungu ameondoka nchini akilia, kamaliza mahakama zote na bado kalizwa, utakuwa wewe Ole Milya?.

Concetrate na kumng'oa Ole Sendeka kupitia vikao vya chama chako, hayo machafu uliyoyaeleza, yapeleke kwenye vikao vya chama ili Sendeka aenguliwe, usimame wewe kwa tiketi ya CCM, Sendeka atasimama na Chadema, CCM itakula mweleka wa nguvu huku kambi ya upinzani ikiimarika.
Kaka unanivunja mbavu huku, mh kama haya maneno ni kweli basi Mungu anajua nchi hii inaenda wapi?
 
Bwana Millya, kwa mara nyingine umetuthibitishia kwamba ama usomi wako haujakusaidia kuelimika au haya unayoyatenda na kuzungumza yanasukumwa na nguvu iliyo nyuma yako. Ni nguvu hiyo hiyo ambayo iliamini kwamba unaweza kuunga unga maneno uakayapeleka kwenye vyombo vya haki na wakakusikiliza. Nikiamini kwamba wewe kweli ni mhitimu wa sheria (ingawaje si lazima uwe mwanasheria), nilitarajia uelewe hata basic principle ya sheria kwamba mahakama hufikia maamuzi ya kutia mtu hatiani pale mtu anapokuwa amethibitisha tuhuma dhidi ya mshitakiwa kwa kiwango muafaka (beyond reasonable doubt). Kwa waliokuwa wanafuatilia kesi hii, wanajua kwamba hakuna hata shahidi mmoja ukiwemo wewe mwenyewe aliyeishawishi mahakama kwamba tukio hilo lilitokea. Hata yule uliyemuita shahidi muhimu (Telele) alikana kuona tukio hilo likitokea hivyo. Ulitarajia Mahakama ikusikilize na kumhukumu Sendeka kwa sababu tu wewe huipend sura yake? Wewe ulitarajia nini kama hata aliyetayarisha PF 3 ni mfunga vidonda tu ambaye hana hata elimu ya kidato cha nne?

Umemtuhumu Mengi kwa coverage ya "kuudhi" na kumbeba Sendeka kutokana na urafiki wake. kwanza nikuambie si kosa la kisheria kwa mtu mwenye media kushawishika na msimamo wa mtu fulani hasa pale kunapokuwa na hisia kwamba mtu huyo anonewa na kukandamizwa kutokana na msimamo wake au kwa vile anashikilia nafasi ambayo watu wa aina yako wanadhani hastahili. Lakini tumeshuhudia vyombo vya habari 'vikitoa hukumu' dhidi ya au kwa manufaa ya mtu fulani lakini bado mahakama ikaongozwa na ushahidi na sheria na kuamua vinginevyo. Mfano mzuri ni kesi ya Zombe au ile ya Babu Seya. Ni matusi kwa mhimili wa Mahakama kudhani kwamba ushawishi wa Mengi ungeweza kui-sway mahakama dhidi yako, kama ambavyo isingewezekana kwa vyombo vya Habari Corporation vilivyokuwa vinakuunga mkono wewe, kuifanya mahakama ikupe haki usiyostahili.

Millya umeonyesha kushindwa kupambanua kati ya facts na material facts. Masuala ya mimba, kufeli shule na hata hizo tuhuma nyingine hazina uhusiano wowote kwenye kesi hii hasa pale kunapokuwa hakuna popote alipotiwa hatiani kwa tuhuma hizo. Kwa kuzileta sasa ni kuthibitisha kwamba kumbe wewe huna focus na hata tuhuma za kupigwa ni kisingizio cha chui kwa mwana kondoo (kwa waliosoma Hadithi za Esopo). Vipi kama mwanafunzi aliyetiwa mimba ni wa chuo? Ni kwa vipi Mama Salma anaweza kugeuka chombo cha dola? Kama una ushahidi wasilisha kunakohusika ili Sendeka atiwe adabu na siyo kuendesha kesi Habari Maelezo.

Hivi kwa akili yake Millya anadhani kuna Wakili wa Serikali anaweza kuharibu jina la Jamhuri kwa kesi ambayo mtu nataka ku-settle political scores? No wonder Mlalamikaji ni yule anayewania jimbo na shahidi ni yule aliyeng'olewa mwaka 2005 na Sendeka, na hao wote tunajua ni proxies wa mtu fulani. Kwa ujumla hakuna triable issue inayohitaji kupoteza muda, financial resources na hata human resources katika kesi hii. The guy has failed to cause the State to discharge the burden of proof beyond reasonable doubt.

Mwisho nimshauri bwana Millya asome mood on the ground. Kule Simanjiro watu wanajua kwamba yeye anakuwa imposed on the electorate ili kumkomoa Sendeka na vile vile kufanikisha mkakati wa kuwa na bunge lililo loyal kwa mafisadi. kwa vile malengo haya bado yapo na kwa vile wananchi wanakataa tutarajie kwamba sinema hii itaendelea hata baada ya uchaguzi.
 
Hivi huyu James anataka kugombea ubunge kwa Sendeka?

Naona hii si kumchafua tu hii ni kumwaga radhi kwa nguvu.

Mzee mwinyi inabidi asuruishe tena hapa. Hapa si salama
Kumwaga radhi si ndo zao humo sisiem? unakumbuka ya SS.
tehe tehe!!
 
Sasa hapa ngoja tuone hili game:
Ole Millya, Ole Sendeka na Ole Mengi aka Ole Mangi
 
.

Mzee Mengi na Media Zake ni kikwazo kikubwa sana katika demokrasia ya nchi hii.Huyu mzee kuna siku yatakuja kumpata ya kumpata.

Tatizo kubwa hapa jf,wengi ni washabiki na hawamjui huyu mzee kwa undani alivyo yeye na media zake..

basi kama ni hivyo iseme hata starTv nyakati za uchaguzi, mbona haionyeshi issues za wagombea wasio wa CCM?
acha chuki binafsi.
 
.

Mzee Mengi na Media Zake ni kikwazo kikubwa sana katika demokrasia ya nchi hii.Huyu mzee kuna siku yatakuja kumpata ya kumpata.

Tatizo kubwa hapa jf,wengi ni washabiki na hawamjui huyu mzee kwa undani alivyo yeye na media zake..
Ni vizuri umesema fikra zako waziwazi, lakini dua ya kumpata yatakayompata mwenzio sio murua sana, kwa sababu maneno ya mtu huunda kitu. Isije ikatokea ya kumtokea Mengi ukakumbukwa nawewe kuhusishwa. Tusiombeane mabaya, sisi sote ni watoto wa dugu moya.

Huyu bwana anasema Sendeka katia mimba mtoto wa shule, huenda ni kweli, lakini yeye kama mtetezi wa haki za binadamu kwa nini alinyamaza kimya mpaka avizie wakati anapojitetea kesi inayomhusu binafsi? Kwani yule binti sio binadamu anayestahili kutetewa na yeyebwana huyu?

Kwamba hajaridhika na hukumu sawa, akate rufaa na sio kukimbilia vyombo vya habari. Kama Sendeka alivyotumia vyombo vya IPP, mbona naye huyu bwana katumia vyombo vya Habari visivyokuwa vya IPP? Amesema anaamini nguvu ya mahakama, asitafute huruma kupitia waandishi wa habari kwa kuwa mahakama haitumii reference ya vyombo hivyo anavyovitumia sasa.

Alikataa kusuluhishwa chini ya mila zao, sasa si asiyewaheshimu wakuu wake huvunjika guu?
 
Jamani eeh, mimi nadhani kama jamii kuna matatizo makubwa somewhere, kwamba kundi fulani likitoka kwenye media na kutukana watu, ni sawa, tena mashujaa wakubwa, lakini akiibuka mtu mwingine yoyote mwenye mtazamo tofauti, hapana, anakosea, either amenunua media au ni makosa kwasababu anatafuta sympathy tu. Tukumbukeni jambo moja wandgu, huyu bwana Millya na yeye ni mwanasiasa, perception is everything. Jamii imeaminishwa huyu jamaa katumwa na akatengeneza kesi kumuumiza sendeka. Leo anakuja anatupa historia ndefu ya uhalifu wa Sendeka nchi nzima, bado watu tunakataa kuiona, na ameeleza ni kwanini alikataa usuluhishi wa mila pamoja na kuziheshimu sana, kwasababu ndiyo kawaida ya sendeka, na kama msomi kwenye jamii wa wafugaji alitaka aonyeshe tofauti, iwe mwisho. Mimi niashukuru kwamba watu wachache (shabiki wa sendeka) kwenye JF wamemfahamu vizuri huyo jamaa, kwamba kumbe alipata DIVIZION ZERO shuleni, balaa kubwa! Hata kama elimu ya darasani siyo kipimo cha uongozi, ni aibu kubwa, sijui unategemea asaidie nini kwenye jamii karne hii.

Huruma nayopata ni mahakama zetu hapa nchini kwa mtu kama Millya, kwakweli kama huna pesa ni ngumu kushindana na mtu mwenye pesa, tena hasa mwenye uzoefu wa kuzichezea mahakama kama Mengi, lakini kama kiongozi, lazima apiganie haki yake mpaka mwisho, ili jamii ifahamu kweli kwamba alishambuliwa na yeye hakutunga kesi au Sendeka amuombe radhi hadharani. Ndugu Millya, Great thinkers of JF are behind you, kila la kheri!
 
Hata mimi huwa nashangaa watu humu wanaquote habari nzima halafu wanacomment mstari mmoja! Kwa nini usinukuu sehemu ya habari unayoona unataka kuitolea comments? Kama unataka kutolea habari yote, kwa nini sasa unanukuu? Kwa kufanya hivyo vertical scrolling inakuwa ndefu na inaboa!

Hili nakumbuka wakat ndo najiunga jf nìlilianzishia thread. Inaboa sana.

Lakin siku hizi naona nizoee tu coz ni kawaida sasa imekua watu kukopi mambo meengi kumbe anataka aelezee kipoint kimoja tu
 
Njaa mbaya sana huyo dogo mbona anatapa tapa sana aliaidiwa donge nono nini akimfunga Ole Sendeka? Kaa pembeni bana sio unaleta hadithi za kusadikika. Wewe EL anakufadhiri unafiki watu hawajui? Njaa mbaya sana unakuta mtu na taaluma yake anageuka kuwa mtumwa wa njaa.
 
Njaa mbaya sana huyo dogo mbona anatapa tapa sana aliaidiwa donge nono nini akimfunga Ole Sendeka? Kaa pembeni bana sio unaleta hadithi za kusadikika. Wewe EL anakufadhiri unafiki watu hawajui? Njaa mbaya sana unakuta mtu na taaluma yake anageuka kuwa mtumwa wa njaa.

THIS IS WRONG. Kwasababu tu ya umaskini wake ndiyo maana asipate haki yake? Hayo mambo ya kufikirika kuwa aliahidiwa nini au nini, haitusadii, lets deal with the facts na tumhukumu kama mtanzania mwingine yoyote. Sijui kama mtu mmejaribu kufikiria kupigwa hadharani mpaka ukaanguka chini, its a very humilitiang incident, na hiyo ilitokea na ndiyo maana sendeka alienda kwa wazee wa kimila wamuombe msamaha, kama asingempiga, asingeenda kwa wazee. Sasa leo tunaingiza siasa za kina EL na Mengi kumkandamiza this educated young man, its just not fair! Fikiria tu angekuwa ndugu yako. I love my country, and then I hate my country and then I love it even more. Its painful and exciting at the same time.
 
Back
Top Bottom