Simanjiro: James Millya vs Ole Sendeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simanjiro: James Millya vs Ole Sendeka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KICHAKA, Mar 14, 2010.

 1. KICHAKA

  KICHAKA Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Machi 14, 2010


  Utangulizi

  Ndugu waandishi wa habari, kwanza kabisa nikushukuruni kufika hapa leo. Siku zote mmekuwa watu wa karibu nami na ndio maana baada ya kufika hapa Dar es Salaam juzi kuhudhuria kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM-Taifa kilichoanza tarehe 12, mwezi huu, nilianza kupata simu za baadhi yenu wakitaka kusikia maoni yangu juu ya kesi yangu dhidi ya Christopher Ole Sendeka. Kutokana na simu hizo kuwa nyingi, nilionelea bora nizungumze nanyi pamoja ili kila mmoja aliyekuwa na nia ya kupata taarifa zangu aweze kuzipata kwa kuzingatia muda na sehemu. Hivyo basi nipo hapa mbele yenu kwa jukumu hilo.

  Historia yangu
  Historia ya maisha yangu imeambatana na mambo mengi kama ambavyo ilivyozoeleka katika maisha ya Watanzania na hasa jamii ya wafugaji. Nimezaliwa Wilayani Simanjiro na kusomea shule ya msingi huko. Hapa nilipo nina shahada ya pili katika Sheria za Haki za binadamu na demokrasia niliyoipatia katika vyuo vikuu vya Pretoria, Afrika Kusini na American University of Cairo.

  Tangu nikiwa mdogo nimejihusisha katika harakati mbalimbali zinazohusu kutetea haki za makundi ambayo nimekuwa nayo na jambo hili kwa kiasi kikubwa ndilo lililonisukuma kusomea taaluma ya sheria. Ninao uzoefu wa kina baada ya kufanya kazi za ndani ya nchi na kimataifa. Nimefanya kazi na Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji sambamba na hapa Tanzania katika mahakama ya kesi za mauaji ya kimbari ya huko Rwanda, ICTR.


  Katika maisha yangu nimeweza pia kuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali. Kwa sasa nashikilia nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa. Nafasi hizi nimezipata kutokana na historia ya uwajibikaji wangu usiotiliwa shaka na moyo wangu wa kujitoa katika kusaidia kufanikisha majukumu yanayokuwepo mbele yetu katika taasisi yoyote niliyobahatika kufanya nayo kazi.


  Nini maana ya Historia Hii
  Nimeamua kutaja historia hii fupi kwa lengo moja ama mawili. Kwanza kuwafahamisha mimi ni nani na pili kuwaonyesha kuwa mimi ni mtu makini, mwenye akili timamu na ninayeweza kufanya maamuzi yangu bila kuhamasishwa na kitu, watu ama kundi lolote.

  Kwa nini nilifungua kesi
  Zipo sababu mbalimbali ambazo zilinisukuma kufungua kesi yangu dhidi ya Ole Sendeka. Sababu hizi ni kama ifuatavyo:

  · Imani yangu kuwa binadamu wote sawa na kwamba haki ya binadamu inayokwapuliwa hupatikana katika vyombo vya sheria. (Katika shahada yangu ya pili nimesomea masuala haya ya haki za binadamu na demokrasia)

  · Utambuzi wangu kuhusu mahakama kuwa chombo cha kutenda haki, kinachosimamia haki za kila mtu anayedhulumiwa na kunyanyaswa bila kubagua. Nikiwa mhitimu wa taaluma ya sheria na pia muhanga wa tukio kupigwa na kutishiwa bastola nililofanyiwa na Christopher Ole Sendeka, niliamini njia muafaka ni hii ya kutumia mahakama kupata haki yangu.

  · Tafakari niliyofanya baada ya kubaini kuwa, mshtakiwa Ole Sendeka ana rekodi ya tuhuma za uhalifu wa kutishia na tabia nyingine chafu katika jamii. Katika tafakari hii nilitazama matukio na historia yake na kubaini kuwa, amekuwa akifanya matukio mengi lakini kwa kutumia mfumo wa kimila na mifumo ambayo siyo rasmi, amekuwa akifanikiwa kuzima matukio hayo. Nitataja matukio machache kama ifuatavyo;

  I.
  Kumtishia kwa bastola ndugu Paulo Yamat ya tarehe 20 Mei 2001. Baada ya tukio hili kesi yenye RB namba KIB/IR/282/2001 ilifunguliwa na kisha kufutwa baada ya Sendeka kutumia vikao vya wazee wa kimila. Maelezo ya vikaohivyo yapo..

  II.
  Tukio la kumchokoza, kumtishia na kugombana kati yake na Marehemu Mzee Soipe aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na mzee wa Kimila.

  III.
  Tena, kuna tuhuma za kumpachika mimba mwanafunzi na kumfanya kupoteza haki yake ya kusoma. Upo ushahidi wa kesi aliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hii lakini ilifungwa katika mazingira ya kutatanisha. Nisisitize hapa, juzi nilikuwa nikimuona Mama Salma akizungumza na chama cha walimu wanawake, ambao walikuwa na kampeni ya kupambana na mimba mashuleni, nadhani nitumie fursa hii kumuomba Mama Salma aanze na Simanjiro maana huko kuna viongozi wasiotambua maana ya elimu na ambao wanaonyesha mfano mbaya kwa jamii yetu.Inawezekana tabia hii pia akawa anaifanya kwa kuwa yeye mwenyewe alipata division 0 katika matokeo yake ya kidato cha sita, hivyo anaona wengine hawana haki ya kupata elimu bora kwa kuwa yeye alishindwa.

  IV.
  Akiwa mkuu wa utawala wa UVCCM alipata tuhuma za kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wakati huo na sasa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ndugu Guninita

  V.
  Akiwa na nafasi hii hii ya ubunge, zipo tuhuma za yeye kumtemea mate mbunge mwenzake. Lakini la kuashangaza hapa ni kuwa, vyombo vya habari hasa vya swaiba wake Mengi, vimemfanya mtu huyu kuonekana katika jamii kuwa ni mwenye haki na mtetezi wa wanyonge. Hii ni hali mbaya sana kwa kuwa inapotosha ukweli na kuwafanya wananchi wa nchi hii kutopata watu wa kweli wa kuwaamini na wanaoweza kusimama na kuwa mfano bora wa jamii yetu.

  Kwa mtindo huo huo usio rasmi aliweza kuwatumia wazee wa kimila, viongozi wa kidini na watu wengine maarufu katika maeneo yetu ya Umasaini ili niitwe katika vikao vyetu vya kimila ili niweze kumsamehe. Hii imekuwa historia yake, na amefanya mfumo huo kuwa kinga yake. Ni wazi katika mfumo huo amefanikiwa. Binafsi sikuona umuhimu wa kuendeleza orodha ya wahanga ambao wamekwapuliwa haki zao na Sendeka kwa kutumia mbinu ya mila. Niliamua kwenda mahakamani kutafuta haki yangu ili iwe fundisho kwake na kwa wale wote waliopewa dhamana ya uongozi wa wananchi na wenye mali. Tena nililenga kujenga na kudumisha utamaduni wa watu kuheshimu utawala wa sheria.


  Nini matokeo
  Baada ya mimi kwenda mahakamani, mengi yametokea. Mambo haya yaliyotokea ni wazi yamenisikitisha na kunionyesha picha ya kuwa, haki ya mtu inaweza kuchezewa kwa maslahi ya mtu ama kikundi fulani. Baadhi ya mambo haya ambayo hata nanyi mmeyaona ni kama ifuatavyo;

  · Matumizi ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vina lengo la kuandika habari potofu na zile tu ambazo zinanikandamiza mimi. Hapa nazungumzia vyombo vya habari vya IPP. Na kwanza nitambue uwepo wa waandishi kutoka katika vyombo hivi, najua wazi kuwa nafasi yenu katika mioyo yenu ni safi sana na wala hamkuhusika kwa mioyo yenu kufanya jambo hili ambalo ni kinyume na taaluma yenu. Ndio maana nimewaita hapa pamoja na wenzenu, najua kulikuwa tu na mashinikizo fulani yaliyosababisha taarifa za Televisheni na habari za magazeti ya kampuni hii kuwa na mlengo huo wa kunikandamiza mimi. Ndugu waandishi wa habari, niwakumbushe tu jambo hili; hivi kweli zipo kesi ngapi nchini ambazo hazipati kuonyeshwa katika televisheni na badala yake iwe hii ya kwangu tu? Mnaweza kujiuliza hii ililenga nini?Mimi ni kijana mdogo tu kutoka katika jamii ya wafugaji, sasa nguvu ile ya kunikandamiza vile ililenga kitu gani?

  · Kuingia kwa mfanyabiashara Reginald Mengi tangu siku ya kwanza ya kutajwa kesi ambapo yeye mwenyewe alihudhuria mahakamani na kisha kufuatia taarifa za kupotosha jamii kuhusiana na kesi hiyo. Vyombo vya IPP, vilinihusisha mimi kutumwa na wanasiasa na hasa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kwenda kumshtaki Sendeka. Lengo la kumuingiza Lowassa katika kesi hii lilikuwa kujitafutia umaarufu kwa Sendeka mwenyewe na kutafuta huruma na kusaka misaada ya kumsaidia katika kesi ile hasa kwa wabaya wa mheshimiwa Waziri Mkuu mstaafu. Upotoshaji huu ni wazi ulilenga kupotosha maana nzima ya kesi yangu na kukwapua haki yangu mahakamani. Naomba nisisitize hapa, kabla ya kufungua kesi hii na kwa kuwa ilitokea katika kikao ambacho Lowassa alikuwepo kama kiongozi rasmi, yeye binafsi akiwa na Askofu Laizer waliniiita nami nikaitikia wito wa kuwaona. Hoja yao ilikuwa nijadiliane na Sendeka ili nimalize jambo hilo kwa taratibu zetu. Nilitafakari yote waliyonieleza lakini, mwisho niliwashukuru na kuwaeleza msimamo wangu wa kuamini katika utawala wa sheria. Lakini pia ndugu waandishi nieleze pia kidogo, mimi nafahamu vizuri sana athari za kutofautiana ama kisiasa au kibiashara kwa mzee Mengi na baadhi ya watu hapa nchini, mfano anaweza kuwa rais mstaafu Benjamin Mkapa ambapo mtaona namna ambavyo amejitahidi kupitia vyombo vyake kumchafulia taswira kiongozi huyo wa nchi hii. Sawa tu mimi ni kijana wa familia duni, lakini naamini katika nguvu ya Mungu kwa kuwa katika yeye siku zote haki ya mtu haipotei. Haya nayaona kama majaribu na pepo wa Ibilisi tu, mwisho nitabakia nimesimama na nikiwa imara zaidi.

  Kutokana na mambo haya niliyoyaeleza hapo juu, naamini ilikuwepo mbinu chafu iliyochezwa kuhakikisha kuwa sipati haki yangu mahakani. Kwa mfano ni pale ndugu Telele ambaye alikuwa shahidi muhimu wa serikali dhidi ya Sendeka kukanusha ukweli wa kuona tukio la shambulio la Sendeka na baadaye kuwa ni mhusika na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mapokezi ya Sendeka baada ya kutangazwa kufutiwa mashtaka.

  Nilijiuliza pia tangu siku ya kwanza nilipoingia mahakamani pale nilipomuona Mzee Mengi ambaye ni mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari nchini, nikajiuliza kulikoni?
  Nikatafakari na kuwaza labda mzee huyu ambaye ni mchimbaji mkubwa wa madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro ni swahiba wa karibu wa Sendeka katika maslahi yao binafsi. Najua uwekezaji huu wa Mengi wilayani kwetu hauna manufaa ya wazi kwa wakazi wa Simanjiro zaidi yake yeye na swahiba wake Sendeka. Labda hiki ndicho kilichomleta yaani kusimamia maslahi ya mdau mwenzake katika kutafuna maliasili za Simanjiro.

  Naomba ieleweke kuwa, kesi yangu haikuwa na haitakuwa na mahusiano ya aina yoyote ya kisiasa ama ya kundi fulani. Sikushinikizwa, sikutumwa na wala sikumtuma Sendeka kunishambulia baada ya kushindwa nguvu ya hoja. Sikulazimishwa kwenda mahakamani kumshitaki kama ambavyo vyombo vya habari vya IPP na washirika wao wanavyotaka kuiaminisha jamii ya Kitanzania.


  Nimesimamia hili kwa sababu naamini mahakama ndicho chombo kinachoweza kumsaidia mnyonge yeyote hapa nchini kupata haki yake. Imani hii nitabaki nayo siku zote za maisha yangu na nitakuwa tayari kuwasaidia wengine kuipata haki hiyo kwa namna ninavyoweza kutokana na taaluma yangu ya sheria na utashi wangu binafsi.


  Hitimisho

  Baada ya kushauriana na wakili wangu, ndugu zangu na wengi wenye mapenzi mema nami ambao wanaamini katika mfumo wa sheria, haki na uhuru wa mahakama; nimeamua yafuatayo;

  1. Kuiomba serikali kwa kuwa ndiye mshtaki katika kesi hii kufikiria namna ya kukata rufaa katika kesi hii kwa kuwa inaonyesha kulikuwa na mazingira yaliyojengwa mapema kabisa ili kupoteza maana ya kesi hii wakati ikisikilizwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Mnaweza kuona hata tukio la shahidi mmoja aliyetakiwa kutoa uashahidi na serikali kisha anakuwa mmoja wa wana kamati ya maandalizi ya mapokezi ya mashatakiwa.

  2. Ni wazi kuwa binafsi sijaridhishwa na hukumu iliyotolewa naamini kuwa Sendeka ana kesi ya kujibu. Lakini nisisitize pia hapa, ninayo imani kubwa na sekta ya mahakama na vyombo vingine vya dola hapa nchini hivyo kuteleza katika ngazi moja siyo kuwa ni mwisho wa mahakama hiyo kutoa haki katika kesi hii. Naamini mahakama na vyombo vinavyohusika vya serikali vitaungana nami kama ambavyo vimeshafanya katika jitihada za kutafuta haki yangu mpaka ipatikane.

  Nawaombeni ndugu zangu wana habari kuwa, tujenge Tanzania yenye kujali habari zilizofanyiwa utafiti na za kweli. Tufikirie mara mbili mbili kabla ya kuandika na tutazame kwa mfano; kama ingekuwa ni wewe, ndugu yako ama mtu mwingine yeyote anafanyiwa jambo na kisha wanaoandika wanapindisha ukweli, je ungefurahia jambo hilo?

  Niwafahamishe pia ndugu zangu wa Simanjiro, mimi nimelelewa vema kwa mila zetu, naziheshimu sana. Tena nathamini sana maamuzi ya wazee wangu wa Kimila na kufungua kwangu kesi hakukulenga na hakutalenga kuwadharau ama kuwapotezea heshima. Nilibaini kuwa huu ni uamuzi sahihi wenye lengo la kusaidia jamii yetu dhidi ya wapotoshaji wa mila. Mila zetu hazihamasishi ukorofi na tabia ya kutisha ama kupiga watu. Mila zetu zinahubiri upole, udugu na urafiki na sio mmoja kujigeuza mkubwa kwa kila anayekutana naye na wakapingana kwa hoja.

  Nakushukuruni kwa kunisikiliza na asanteni sana.


  James Millya
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Naona vita vinaendelea.Kwenye bold hapa niingii akilini kabisa.Kusoma au kufanya harakati mbalimbali hakumaanishi kutumika ama kutotumika...Lakini pili atuletee CV yake humu kuzungumza kama kasuku hakuna impact yeyote.
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Hapa kuna kazi.

  sasa hilo la sendeka kumpachika mimba mwanafunzi limekaaje?

  -Ila hizi tuhuma kwa Mengi sidhani kama kamtendea haki hapa.Sendeka kama mtuhumiwa pia anayo haki ya kupata sapoti kutoka kwa marafiki zake

  -mbona hakueleza juu ya maelezo ya Lowassa kuhusu hilo tukio?

  -Vipi kuna mgongano wa kimaslahi kweli ktk hii kesi na migodi ya Tanzanite?
  -Sasa kama jamaa kaamua kumuachia Mungu mbona anataka serikali ikate rufaa tena?
   
 4. a

  afande samwel Senior Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  .

  Mzee Mengi na Media Zake ni kikwazo kikubwa sana katika demokrasia ya nchi hii.Huyu mzee kuna siku yatakuja kumpata ya kumpata.

  Tatizo kubwa hapa jf,wengi ni washabiki na hawamjui huyu mzee kwa undani alivyo yeye na media zake..
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wote ni wachafu, Milya na Sendeka... na wote wanapata msaada toka kwa gugumen... Sendeka alipata support ya mengi na Milya alipata ya lowassa!!!

  sasa sielewi Milya anahangaika nini... He is losing even that remote respect some people give him!!
   
 6. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi huyu James anataka kugombea ubunge kwa Sendeka?

  Naona hii si kumchafua tu hii ni kumwaga radhi kwa nguvu.

  Mzee mwinyi inabidi asuruishe tena hapa. Hapa si salama
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,242
  Trophy Points: 280
  James Ole Milya kachokoza nyuki, subirini mshuhudie jinsi Ole Mangi atakavyo mshukia.
  Mimi binafsi sijaridhishwa na presentation hii ya Ole Milya kama holder wa LL.M, nitafurahi kama nitasikia hiyo LL.B yake aliichukulia wapi, maana anaandika kama just a layman. Kama mwanasheria, he should have known better.

  Kama Ole Milya unaingia JF, nakushauri achana na kukata rufaa, Jamaa huwawezi!. Mtandao wao ni mkubwa!. Futalia kesi ya Silverdale Farm, kuna mzungu ameondoka nchini akilia, kamaliza mahakama zote na bado kalizwa, utakuwa wewe Ole Milya?.

  Concetrate na kumng'oa Ole Sendeka kupitia vikao vya chama chako, hayo machafu uliyoyaeleza, yapeleke kwenye vikao vya chama ili Sendeka aenguliwe, usimame wewe kwa tiketi ya CCM, Sendeka atasimama na Chadema, CCM itakula mweleka wa nguvu huku kambi ya upinzani ikiimarika.
   
 8. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hizi gharama ndugu Millya anazotaka serikali iingilie kati ili kesi iendelee jamani si hizo hela zisaidie mambo mengine asikubali kushindwa si mshindani,watu wazima mnapoteza muda na rasli mali nyingi kwa ajili ya upumbavu,wote tunajua yote hayo ni mambo ya kisiasa zaidi,jamani kuwaletea wananchi maendeleo sio lazima uwe mwanasiasa au mbunge
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Unayemjua Mzee Mengi tumwagie data zake hapa ni kweli si kila mtu anaweza kumjua kila mtu,haya tunasubiri ulete hizo data ASAP
   
 10. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inaonekana wewe unamjua kwa undani alivyo huyo Mengi, kwanini usiwasaidie wana JF wengine hapa jamvini waweze kumjua ili waache huo ushabiki? We dare to talk openly, the ball is on your court!
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Haya malumbano yana faida gani kwa Watanzania wakati mbapo mmoja wao ameshaamua kwenda Mahakamani?
   
 12. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Naona dissertation yake hapa, .

  I, JAMES MILLYA KINYASI, hereby declare that this dissertation is original and has never been presented in any other institution. ...
  https://www.up.ac.za/dspace/bitstream/2263/5843/1/millya_2007.pdf
   
 13. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  GS,
  Huna sababu ya kuitisha CV yake kwani maelezo yake yanaweza kabisa kukuelezea ni mtu wa aina gani.
   
 14. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  BInafsi nilikuwa nategemea kwa mwanasheria wa shahada ya uzamili kutoa ushahidi wote huu mahakamani na sio kwenye ukumbi wa maelezo. Naungana na Mwanakijiji kuwa hawa ndio wasomi wetu.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mfianchi , Gengder Sentive
  Naadhani ni jambo zuri na busara zaidi ukiona umuhimu wa kunuu taarifa ya mtu ukanukuuu (Quote )kipengele cha muhimu kuliko kunukuu habari nzima tena ndefu. It is redunducy sijui wengine wanachukuliaje.

  Otherwise
  I like it nikiona wana CCM wanaparurana na matatizo yao yanataoka hata nje ya vikao.
   
 16. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ben,
  Milya ni mwanasheria mwenye shahada mbili, mojawapo ni haki za binadamu na demokrasia. Inaniwia vigumu kuamini mtu wa aina hii anashindwa kupambana na uhalifu wa mpinzani wake kisiasa kama huu wa kumtia mimba mwanafunzi na kuomba huruma ya mama Kikwete, huu ni upunguani.
  Kuhusu suala la mgongano wa kimaslahi sidhani kama upo, mengi ni mfanyabiashara, na kwa kuwa hakuwa hakimu ana haki zote za kumsuport awaye yote bila ya kuwa na mgongano wowote ule wa kimaslahi. Ktk hilo la mwisho ndipo na mimi nimeshindwa kuelewa hitimisho la mkutano wake na waandishi.
   
 17. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jamani yote kwa yote nimeshitushwa na taarifa ya elimu ya mbunge wetu Sendeka....Div-0 ya form six???
   
 18. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  AS,
  Naomba unijulishe ni Media ipi Tanzania ambayo ni nguzo ya demokrasia? Ni kweli hatumjui vizuri mzee Mengi, wewe unayemjua kwanini usitujulishe? BTW, Mengi hayumo bungeni, au kwenye CC-CCM, NEC-CCM au kwenye tume ya uchaguzi, je hicho kikwazo kwa demokrasia kinatokea wapi?

  Nafikiri vikwazo vikubwa vya demokrasia ni wamiliki wa vyombo vya habari ambao wapo bungeni, CC-CCM na NEC-CCM.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks pascal for this useful post!!!


  1. Milya ameshindwa kutuaminisha usomi na uanaharakati wake kama alivyojisema
  2. Pia milya ameshindwa kuoanisha mashitaka na relevance ya hii press conference kwani hatujui ni kuijibu mahakama au kum-attack sendeka baada ya kushindwa case mama
  3. kibaya zaidi milya once again, amewadhalilisha viongozi wa kimasai kwa kuonyesha kwamba wanafumbia macho mambo muhimu, nijuavyo mimi hii itakula kwake kwani mambo ya kimila huwa hayawekwi hadharani
  4. kuhoji uwepo wa mengi mahakamani ni tatizo jingine kwake kwani yule mkuu wa mkoa wa singida naye ilikuaje? au mmoja anaruhusiwa kuleta watu wazito mwingine haruhusiwi?
  5. Milya ni kijana sana, na anachojaribu kufanya kimeshaangusha vijana we ngi kabla hawajasimama
  Namshauri ndugu yangu Milya (namfahamu presonally) aache hizi siasa za maji taka, arudi jimboni, arecruit vijana wampigie kura za maoni. Juzi nimeona heshima aliyopewa sendeka na vijana pale arusha hadi nikakubali kwamba kwa wamasai ni mila sasa milya "usinye unapolala" - kuhoji wazee wa au kuweka mambo yetu hadharani inawza kwenda against you kule orkesumet, machimbo na bwawani!!

   
 20. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mmmh! Siasa za siku hizi, mbona watu wazima wanalialia tu kama watoto wadogo?

  Haya kuyasema ukiwa kwenye politics ni dalili za utoto.

  Pole kijana, but you have to grow up.
   
Loading...