Sheikh Ponda: Mahakama itende Haki kesi ya Lissu

Sheikh Ponda: Mahakama itende Haki kesi ya Lissu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,309
Reaction score
18,490
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameitaka Mahakama ya Rufani Tanzania kuhakikisha inatenda haki kwa usawa katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

PICHA za Matukio ya Leo Julai 03, 2026 za Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHAD...jpg

Akizungumza na MwanaHALISI Digital Julai 16, 2026 katika ofisi zake zilizopo llala Bungoni, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ponda alisema ni muhimu vyombo vya utoaji haki vikazingatia misingi ya haki na usawa bila upendeleo, ili kulinda imani ya wananchi katika mfumo wa sheria.

Pia, Soma: Dkt. Benson Bana: Hamuwezi kuridhiana wakati Tundu Lissu yuko Gerezani, ana kesi ya kujibu, tungoje Mahakama itoe hukumu

Alisisitiza kuwa kila mtu anayefikishwa mbele ya vyombo vya sheria anapaswa kupewa haki zake kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi, bila kujali nafasi yake kisiasa au kijamii.

Kauli hiyo imekuja wakati kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu ikiendelea kuvutia mjadala mpana miongoni mwa wadau wa siasa, sheria na haki nchini.

Huwezi kuwasikia Masheikh wa Bakwata wakiongelea kuhusu uonevu anaofanyiwa Lissu! Na haiji kutokea.

Huwezi kuwasikia wakiongelea kuhusu haki na usawa kwenye jamii! Isipokuwa utawasikia mara zote wakiongelea kuhusu wananchi kuienzi amani na utii kwa mamlaka.
 
Hao hata wale mashekhe ambao wako mahabusu kwa tuhuma za ugaidi miaka na miaka huwezi kuwasikia wakiwaongelea,wanawaza kuchinja wanaotumia haki yao ya kuandamana tu.
 
Huwezi kuwasikia Masheikh wa Bakwata wakiongelea kuhusu uonevu anaofanyiwa Lissu! Na haiji kutokea.

Huwezi kuwasikia wakiongelea kuhusu haki na usawa kwenye jamii! Isipokuwa utawasikia mara zote wakiongelea kuhusu wananchi kuienzi amani na utii kwa mamlaka.
Bakwata ni jumuiya ya CCM kama ilivyo UVCCM tu, naona tartiiib KKKT nayo inasogezwa huko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom