Leo asubuhi kanisani SILOAM wakati wa maombi ya asubuhi waliweka CD ya nabii Eliya, majirani wakaanza kushangaa kuwa huenda nabii huyu hajafariki au amefufuka.
Habari za uhakika hata ndugu zake hawakuwa wanafahamu km amefariki, inasemekana kuwa mdogo wake anayeitwa Swai aliposikia taarifa hizi aliamua kwenda kanisani, alipofika pale hakuona km kuna msiba, aliwauliza waumini kuhusu viongozi walipo wao wanawaita makuhani wakiwa na kikao juu ghorafani, alipofika walimkarisha kwa kumpa hongera sana, akashangaa kwa nini alikuwa anapewa hongera, aliuliza zaidi kwa nini hongera? alojibiwa kuwa Nabii Eliya alikuwa ameshinda umauti amenyakuliwa na MUNGU, nasikia ndugu yake akauliza kwa hiyo hayupo akajibiwa yeye hayupo amenyakuliwa ili mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Lugulo. kwa taarifa zaidi mazishi yatakuwa siku ya J4 ambayo ndiyo km jumapili ya kwao.
Hivyo wao wanapeana hongera lkn kwa sasa kumepooza sana. Nabii huyu kwa jina jingine alijiita adamu wa pili. makazi yake yapo bao bao km unaenda bagamoyo, kuna mjengo wa ghorofa km 3, na magate 3 kabla ya kufika mjengoni.