East African Eagle
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 3,759
- 2,209
Jambo ambalo silielewi ni kuwa lazima kiongozi wa hii dini aitwa Nabii Eliya? Nafahamu mwanzilishi aliitwa Thebeti Eliya ambaye alikuwa na wake kama 30 na kijiji chake kule Upareni Kilimanjaro baada ya yeye kufa akachukua uongozi huyu Munuo ambaye naye kaitwa Nabii Eliya Munuo. Je jina la Thebeti kabla ya kuitwa au kujiita nabii Eliya lilikuwa lipi? Na hili jina la Eliya kuna uhusiano wowote na Nabii Eliya wa Biblia ya Wakristo ambayo Siloam wanakiita kitabu hicho jina jingine? Naomba kuelimishwa kwa hayo.
Mkuu huyo mpare hakuanzisha dini ya Sloamu.Jina la huyo mpare alikuwa ni Eliya Msangi na alikuwa na wake 30 NA DINI ALIYOANZISHA HUKO UPARENI INAITWA UWATA akishirikiana na mnyakyusa mmoja mwenye wake KIBAO anayeitwa MWAKISWALELE wote wawili Eliya Msangi na Mwakiswalele walishakufa wakiacha nyuma UWATA ambayo bado ipo na ina mashule na miradi mingi tu.
SLOAMU NI DINI ILIYOANZISHWA NA NA NABII ELIYA MUNUO IKO TOFAUTI KABISA NA ILE DINI YA UWATA YA ELIYA MSANGI.
Hayo mengine ya kuwa Eliya hawa wakina MSANGI NA mUNUO NDIO ELIYA YULE WA biblia ? Hayo siwezi kujibu nawaachia wagalatia watusaidie kujibu KAMA akina PASCO,MISS CHAGA NA WENGINEO HUMU JAMII FORUMS.