Wamemtafutia Polepole sababu ya kumfunga mdomo kwa kuwatumia hao kina Gwajima na Silaa kama chambo.

Hapo kitakachofuata Polepole ataambiwa adhabu yake akae kimya miezi sita yuko chini ya uangalizi, awe makini huko kikaoni kama Gwajima alivyofanya na "mic"

Huu ujinga ndio unafurahiwa na wenye mawazo mgando wenye "chama chao".

Hawajui kufungana midomo kunatengeneza taifa la majuha, na vile elimu yetu iko chini, ndio tunaandaa kizazi cha malofa na adui ujinga ataendelea kututesa miaka yote mpaka mwisho wa dunia, CCM ni wajinga sana.

Nachomshauri Polepole kwanza awaambie hao CCM wenzake hajavunja sheria yoyote ya nchi kutoa mawazo yake, pili, afuate taratibu alizoambiwa na TCRA ili arudi hewani, na nyie TCRA mfanye kazi yenu kiuweledi, msijigeuze wanasiasa.
 
Kolimba aliitwa 1997 yeye hakufurushwa kwny chama ila hakutoka kikaoni!
Ni kawaida hata Membe bila shaka aliitwa then akafurushwa ndani ya Chama.....sio jambo la kushangaza ni utaratibu wa CCM kwa wanachama wake....

Bila shaka hata vyama vingine vina taratibu zake, tuheshimu taratibu za vyama vyetu....Ndio demokrasia, ukikosea unaitwa unasikilizwa then hukumu inatoka...
 
Waliokosoa kipindi Cha JPM nao walikiona Cha mtemakuni!Mpaka wengine wakamiminiwa risasi,kesi za kubambika NK!
Lakini CCM wakawashukia Hadi wazee wa Chama waliokosoa na kuwatukana na kuwapiga mkwara!
Inashangaa ya Leo?Huo ndio utamaduni wa CCM!Kumlamba viatu mtawala,basi!
 
Kujikosoa ni msingi imara wa taasisi yoyote ile. Maana mnapojikosoa ndio hapo mnajiweka sawa na kujirekebisha.

Kwa muda mfupi tangu hayati JPM atutoke watanzania kwa macho yao wameshuhudia mabadiliko makubwa.

kuna dalili mradi mkubwa kama JNHP hautakamilika kama ilivyopangwa, kuna dalili za rushwa kama za Escrow kurudi kupitia mgao wa umeme, harufu za ufisadi kila kona mbaya zaidi ni hata mwaka haujaisha tokea hayati JPM afariki.

Je kwa mwanaCCM kama Polepole kuhoji na kukosoa haya mabaya yanahochafua serikali na chama cha CCM ni kosa?
Kwangu mimi kuitwa kuhojiwa kwa mwanaCCM au Kiongozi wa CCM sio jambo geni. Ila hoja inakuja kwamba akiwaambia ukweli watakubali? Wataufanyia kazi?
 
Back
Top Bottom