figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Salaam Wakuu,
Waliposema Nchi ataiongoza Samia Suluhu niliogopa sana kwani niliona Wanamuangushia jumba Bovu. Pia nikasema hawa mafisadi atawamudu kweli?
Sasa ananiumbua.. Kweli Samia ni mwanamke Shupavu.
Sababu Maguli alikuwa one man army kama arnold schwarzenegger. Hakimu yeye, Polisi yeye, dereva yeye, mpiga ngoma yeye, Mchezaji yeye, muendesha mashitaka yeye.
Alifikia hatua ya kuamua ufe au uishi kama vile yeye ni Mungu. Nikajiuliza, hii roho ya hivi huyu mama hana, je, akibadilisha muelekeo itakuaje?
Nimeshangaa kuona nchi ipo kwenye Mstari bila polisi kupiga Mabomu, bila kuwananga Watendaji kwenye majukwaa ya Siasa, Bila watu kutekwa na Wasiojulijana, Shule zinajengwa za msingi hadi zawekwa tiles.
Hakika Wasiojulikana Wamezikwa na Magufuli. Tarehe 30 Tundu Lissu anarudi mambo yawe mwemelemwemele.
Tumuombee Rais wetu Samia Hassan aendelee kuwa na hofu na Mungu. Sasa tunaiona Kesho ya Tanzania tofauti na yule rais akiamka alikuwa anaamka na akili mpya.
Hakukuwa na wakumfunga kengere mzee yule mwendazake