Sikutarajia kuumizwa namna hii!

Sikutarajia kuumizwa namna hii!

Ushauri wangu kutoka katika nafsi yangu, naomba uendelee na maisha yako tafuta mwanamke mwingine oa, achana naye kwanini alikukataa na sasa anarudishwa na nani? wewe ulimlilia kwa dhati sasa leo kwanini uruhusu majonzi yarudi tena? Ila kabla mtu hajaomba ushauri anakuwa tayari anaushauri katika nafsi yake. Isikilize nafsi yako inakuambia nini. Ila naomba usimrudie kabisa.
 
run
stay away from her.
she doesn't care about you
she cares about "her"
 
achana nae atakutenda tena kwani sasa dini imebadilika?

wa kwako yupo usijejuta ndani ya ndoa ndugu yangu,huyo hakupendi hata kidogo
 
Aseeh pole sana mkuu,..Muombe mungu akupe busara tu, aya maisha ya mapenzi sijui vp,... Unaweza kudhan mtu anakuja kweny maisha yako ili akukomoe tu,... Kukumiza ni kama anajisikia furaha moyoni mwake,... Nachokushauri Mimi nimepitia vitu ivo ivo,... Sasa nilichofanya ni kutuliza moyo wangu maumiv maisha yaendelee, uyo ata ukiwa nae kumsamee 100% haiwezekan,... Things will never be the same again... Mi nakushaur fata maisha yako, and live your life,.... Uwez msamehe uyo,..
 
MPE sharti la kubadili Dini kwanza then ndo mrudiane
 
Kwanza ushukuru sana Mungu umeweza kuondokana na maumivu wa huyo mtu.
Najaribu kufikiri kwamba ukirudiana naye ipo siku yeye na jamaa ake aliyekusababishia maumivu wataendelea na mahusiano kama kawaida ijakapokuwa jamaa ameoa mwanamke mwingine.
Kumbuka kuwa msimamo wa kutokuchepuka katika mahusiano unabaki kwa mwanamke na si mwanaume, wanaume asilimia kubwa ni wadhaifu haijalishi ameoa au hajaoa.
Sasa, swali je huyo mwanamke ataweza kumudu usumbufu kutoka kwa x wake pale atakapohitaji tunda? Kwa vyovyote si rahisi, japo kwa sasa atakudanganya kuwa na msimamo wa kutokurudiana naye lakini kamwe haitatokea.
Kwa sasa binti amekosa uelekeo hivyo kwako limekuwa kimbilio hana namna nyingine, na wewe imekuwa the last priority kwake, ila akishapata pa kujiegesha (ambapo anapategemea kwako) ipo siku utakuja kulia kilio zaidi ya hiki kama si kujiua kabisa.
 
"Nikwamwambia achukue gari mimi nimeshapona na sina amani kumiliki Mali ambazo tulichuma pamoja akakubali nikamuachia gari ."

Hapo juu nimeshindwa kukuelewa, kua na maamuz usirud nyuma utakua miongon mwa wapumbafu
 
Kwanni huku oa mapema laiti kama ungelikiwa na mwenza wako leo hii asingekuwa nabujasiri wa kukukabili. Ushauri kaa nae kitako mweleze kinagaubaga kuwa haiwezekani daima na kumbuka mapenzi ni upofu udipoona leo basi hutoona kesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini mko poa.
Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa tunapendana sana. Nilikutana nae jijini Mwanza nilipokwenda kikazi July 2015.

Safari yetu ya mapenzi ilipamba moto kila mmoja akiwa na mapenzi ya dhati kwa mwenzio.

Tukiwa tumekubaliana kufunga ndoa hapo baadae. Tulifanya mambo mengi pamoja ikiwa kujenga nyumba na kununua gari pamoja, pia niliweza kufanikiwa kumuhamishia Moro kikazi angalau awe karibu.

Hatukuwa wa imani moja, yeye alikuwa mkristo na mimi muislam lkn hili halikuwa tatizo la kutuzuia kupendana.

Tulitembeleana na kuwasiliana Mara kwa Mara bila kikwazo.

Baada ya kumwambia kuwa wakati umefika tuanze taratibu za kufunga ndoa tulikubaliana kuwa ndoa tutafungia serikalini lkn kila mtu atabaki na imani yake.

Alipowaeleza wazazi wake utofauti wa imani wazazi walilipinga kwa nguvu zote, nikamuuliza yeye mwenyewe anasemaje akajibu ananipenda na asingetamani tuachane lkn pia hawezi kufanya kinyume na wazazi wake.

Basi wakati tunaendelea kulitafakari hilo mwenzangu akabadilika, nikimpigia simu anakata meseji hajibu, baadae akaniblock kabsa.

Kitendo kile kiliniumiza sana, nikaamua kumfuata Moro nikakuta alipokuwa anaishi amehama, kwasababu nilikuwa najua shule aliyokuwa anafundisha nikaamua kumfuata shuleni.

Nilipofika shuleni sikuamini kile nilichojimbiwa...niliumia sana..nikamsihi na kumpigia magoti mbele ya walimu wenzie lakini yeye akanijibu hatoweza kuendelea na mimi tena kwani tofauti za dini hazivumiliki , pia kaendelea kusema kuwa alikuwa na mpenzi wake zamani walipotezana lakini wamekutana tena na kuamua kurudiana.

Maneno yale yalikuwa ni mkuki ndani ya moyo wangu, nillilia kama mtoto, sikuweza kula kwa siku kadhaa.

Nikaamua kujiua maana nilijisemea moyoni sitaweza kumuona mwanamke ninampenda akiolewa na mwanaume mwngine. Lkn nilikuwa nao wakanisihi nisifanye vile. Sikujua nini cha kufanya nilikuwa mtu wa kulia tu.

Sikwenda kazini kwa siku mbili mpaka rafiki yangu ambaye tunafanya nae kazi alipofanya kazi ya ziada.

Baada ya mwezi kupita nilifunga safari tena kumfuata nikiwa na lengo la kutaka kujua kuhusu gari na nyumba ambavyo tulinunua pamoja na vyote vilibaki kwangu.

Alichonijibu nikwamba vyote ameniachia kwasababu alichonitendea anajua kiliniumiza sana.

Nikwamwambia achukue gari mimi nimeshapona na sina amani kumiliki Mali ambazo tulichuma pamoja akakubali nikamuachia gari .

Utendaji wangu wa kazi ukawa mbovu sana maana kila nilipokumbuka sikuweza kufanya chochote.
Nilikuwa nafanya kazi kwenye NGO ya wa Marekani, kufuatia kuwa na ufanisi mbovu kazini nilisitishiwa mkataba wa kazi.

Mapenzi yanauma sana jamani usiombe ukimpenda mtu halafu akakuzingua.

Hapo ndipo shida ikazidi kuwa kubwa maana sikuwa na cha kunikeep busy ikafika wakati nikawa napoteza mpaka fahamu.

Wazazi walipofahamu shida yangu wakanitumia mtu wa kuwa nae maana nilikuwa naishi peke yangu.

Hali ile ilinichukua miezi saba ndipo niliporudi normal.
Baadae Mungu akajalia nikapata kazi sehemu nyingine.

Maisha yakaendelea tatizo ikawa ni ile nyumba kila nikiona namkumbuka , nikaamua kuiuza na kujenga sehemu nyingine.

Maisha yakaendelea nikamtoa moyoni kbsa nikawa namuona wakawaida sana.

Baada ya mwaka mmoja kupita akaanza kunitafuta nakuomba turudiane maana jamaa amemtosa na kuoa mwanamke mwngine.

Nimemkatalia mara kadhaa lkn bado ananing'ang'ania , kila nikitaka kumkubalia nakumbuka mateso niliyopata kwasababu yake.

Naomba ushauri wenu wakuu nipo njia panda sitaki kuumia tena.

Mkuu awali ya Yote Pole kwa ulilolipitia na Mshukuru Mungu ameweza kukupitisha na Umeweza kusonga Mbele. Hakika kwa Mtu ambaye hajawahi kupenda atakuona kuwa wewe ni Chizi. Kwa kuwa siku hizi Mapenzi ni Vitu na Mapenzi siyo Utu. Kwa maana Nyingine Mtu atakushanga kwa hatua uliyofikia na kukuona zuzu lakini hilo ulilolifanya na kulipitia ni ishara ya Upendo wa Kweli na Ambao ni Vigumu kuja Kumuamini Mwanamke Mwingine maisha yako Yote. Ngoja Nikwambi sijasoma Michango ya wengine ila Mapenzi ya Siku hizi yameshangiliwa kwa Kiwango Kikubwa na Vitu, Yaani Mtu atakupenda kwa kuwa Una Degree, Aatakupenda kwa kuwa Unafanya kazi, atakupenda kwa kuwa Unaishi Nyumba nzuri, Atakupenda kwa kuwa Unampa Zawadi, atakupenda kwa kuwa kuna kitu kinachoshikilia Upendo kwako.

Lakini Kwa jinsi nilivyokuelewa wewe ulimpenda huyo Mdada bila kujali chochote na ndiyo maana uliweza hata kuona kuwa huna sababu ya kile ambacho mlikivuna pamoja kukifurahia Pekee yako. That is True Love.

Kutokana na hali iliyokupitia kuna kitu ambacho kinaitwa Maagano kwenye kila maisha ya Mwanadamu. Mfano wewe kinachokufanya umuwaze sana huyo Msichana ni Maagano ambayo uliyaingiza Moyono mwako wakai Mwenzako hajaweka agano lolote kwake juu yako. Na Ndiyo Maana hata alivyoamua kusonga mbele hakujali maumivu utakayopitia ila alijali furaha yake itakuwje.

Cha Kukushauri Kwanza Kiri kwa kinywa chako kuwa Umeshaachana na Huyo Mwanamke Kwa kuwa hamkuwa na Common Maagano.. Common Understanding , Common Vision, Common Lookup.

Kwa kuwa umeweza kujitibu na ukarejea katika hali yako ya Kawaida japo bado haijakuisha Kubali kuwa uliamua kuanza upya na usigeuke Nyuma .

Hata akikukumbusha mauno mliyokuwa mnafanya enzi zile za uchanga wenu wa Mahusiano , Usikubali aslani.

Mungu amekulipizia pale ambapo hukusitahi kufanyia mabaya na Mwache aendelee na maisha yake. Usimpe nafasi hata ya kumsikiliza neno lolote kutoka kinywani Mwake kwa kuwa Ka maumbile na UUmbaji Mwanamke ni Nyoka, Wamejawa na Huruma, na Huruma zao zipo Usoni lakini hazipo machoni Mwao. Ni wepesi kusahau yale Mazuri Uliyomtendea na ni wepesi kukumbuka baya moja tu na kuweza.

Usifanye kosa kuruhusu Moyo wako kumpokea tena kwa kuwa Gharama ya maumivu aliyokutendea hayatakuja kulipika hata kidogo..

Ebu Jiulize Kama ungekuwa Kichaa angekutafuta Tena? Kama Jibu ni Ndiyo, Anajuaje kama Kipindi hiki siyo Kicha? Unajua Gharama ya Kupiga Magoti na Machozi uliyoyatoa Mbela ya Watu ambao hata hawajui mlikotoka, Watu ambao siyo Ndugu au ...

Ndugu Yangu najua utapewa Ushauri Mwingi Ushauri wangu Kwako KLubali kuwa Ulipoteza, Chukulia huyo Mwanamke kama Shamba ambalo Ulilima Mazo na Baadaye Jua likawaka na kuangamiza Mazo yote. Je Utarudi kuliomba Shamba likurudishie Mazao yako wakati kilichosababisha na Jua au Ukame?

Hivyo Yeye hana sababu ya kusema atakuja kukupenda tofauti na Mlivyokuwa mkipendana awali. Siku Zote Mapenzi hayajaribiwi wala hayosomewi wala haya Mtalaamu. Kwa maana Nyingine asikudanganye kuwa anajutia Uamzi wake alioufanya Kukuacha au alidanganywa na Wazazi au Dini Imebadirika. Kumbuka sababu alizozitoa hapo awali bado hazijafutika na bado zipo.

Samahani kwa kuandika Mengi ila Nimeguswa na napshwa kukwambia kuwa MAPENZI HAYASOMEWI WALA HAYAIGWI.
ASANTE
 
Mkuu nakutahadharisha sana chondechonde hapo njia panda patakuponza, m-block kama yeye alivyo ku-block ila sasa wewe m-block hadi kwenye real life, mawazo etc etc............ukipuuza huu ushauri nakuahidi utarudi tena hapa jukwaani ukiwa na majuto makubwa kuliko ya awali.
 
Mkubalie kwa moyo mmoja na muanze kuishi maisha mapya.Muonyeshe unampenda zaidi ya mwanzoni.Hakikisha unampenda na kumuonyesha kuwa unamjali sana na yeye ndo kila kitu katika maisha yako.Hata ikibidi pangeni tarehe ya harusi haraka iwezekanavyo.Wakati maandalizi ya ndoa yakiendelea,tafuta kipindi hayuko ameenda safari uza kila kitu na uhame kabisa eneo.Then badilisha number zote za simu na uanze maisha mapya.

Tit for Tat is a fair game.
Well said, awez niumiza alafu arudi kirahisi ivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndoa za dini tofauti Mara nyingi zinaleta maumivu baadae kama hamtakubaliana kuwa katika Omani moja.

Nilisoma na watoto mama yao alikuwa mwislami wa sala tano baba mkristo, waliamua watoto watachagua dini wakiwa wakubwa. Baba aliwapeleka wale watoto katika shule ya Roma, watoto wale wote sasa wamekuwa wa kubwa wote wameolewa kanisani wanamwambia mama yao wamezoea sala za kikristo.
Amna shida kwani Mtoto kuwa Na dini tofauti Na mzazi kuna tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ila ndio ukubwa na ndio ladha halisi y maisha ilivyo,maisha bila ladha ya uchungu hayanogi kabisa,so hapo ni sawa na pilipili ktk kachumbari,kali lakin inaleta ladha,ndio kama matatizo yako,yanaumiza lakin ndo maish yenyewe.

Kila mara nasema hapa na nitazid kusema,ni heri kuachwa kuliko kuacha.,anaeacha mara nyingi hafanikiwi huko anakokwenda,maana hakuna binadamu mwenye afadhali,kila mmoja ana mapungufu yake,so ukiacha hakika huko mbele utakwama,na ukikwama utakumbuka ulipotoka,na kuanza kujuta bora kule nilipotoka. Machozi yako Mungu kayaona,na amejibu haraka km ni kwel,hii ni funzo kwamba tusipende kuumiza watu ambao hawatuumizi,kuna usemi unatuhusu sisi wanaume zaid kwamba tunawaacha wanaotupenda na kuwapenda wanaotuumiza,kuna vitu vingi sana vya kujiuliza kuhusu jambo hili lako na kuna walakin nying japo sio vema kuziweka hapa ila tu kumbuka furahia kuumizwa na jifunze kumshukuru mungu kwa linalokutokea na usimshtaki kwa yyte hata kwa mungu,ili mungu ajibu kupitia haki.

Kiukwel mm siwez kuumia kwa ajil ya mapenz tena,nilivyoumizwa mara moja nikajifunza hapo hapo,japo sikuumizwa kwa namna yako lakin yale maneno yake yalikua ni mwiba ambao umenifanye niwe imara kiakili,kiuchumi na kitabia.

niliambiwa wewe Xav sio size yangu tena,nimechoka kutembea na masikini maana hata nikipata shida huwez kunisaidia so take hamsin zako wacha nikadate na wenye kujielewa. Iliuma kias sabab ni kwel sina kitu na hata shida ambayo ingetokea hata 20k sikuwa na uwezo nayo. So nikajitahid kuvumilia na kuyatafuta maisha ili yu nisikutane na maumivu yale ya mwanzo,na uzur nilimwambia hela siku zote zinatafutwa,na hakuna mwenye kuzaliwa nazo na kuitwa mtoto wa hela,wote tukiwa na malengo tunaweza kuzitafuta na kuzipata na kula maisha,leo unaniacha sbu sina kitu lakin kumbuka ipo siku utanitafuta na historia hii itakuhukumu,leo kipo wap,kwisha ndembendembe kifo cha mende hata hela ya kod ya nyumba hana,halaf nikimkuta lift nampa na kumtoa kidogo namtoa hata 10k ili azid kuumia.

Furahia kuachwa jombaaa,maana leo una furaha japo unatamani taman bado ule mzigo wake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom