Rayvanny wa jamiiForums
Senior Member
- Apr 7, 2023
- 132
- 347
JINA LA STORY: GAMBOSHI>>>>>EPISODE : 01<<<<<<<<<
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 01
Whatsapp No.: +255687409189
call/Text:+255687409189
*
GAMBOSHI
(Malkia Wa Wachawi.)
**
...Ilkuwa ni jioni tulivu mida ya saa kumi na mbili abiria wa basi liendalo mikoani katika nchi ya Tanzania ikiwa kama usafiri uliozoeleka zaidi kutoka mkoa mmoja hadi mwingine. Abiria wale walikua wamekaa kwenye basi zuri lililokua likifanya safari zake kutoka Dar es salaam kwenda mikoa ya kanda ya ziwa, baadhi yao wakiwa wamesinzia na wengine wakiwa wanaangalia runinga iliyokuwemo ndani ya basi lile, dereva alikuwa akiendesha kwa umakini mkubwa huku kwa nje kukionekana miti mikubwa na minene kama ya kwenye msitu. Kwa kupitia kioo cha mbele (windshield) kulionekana barabara ya lami iliyonyooka vizuri, mara ghafla akilitokea kama kivuli cha mtu mbele ya basi lile na dereva kwa uwezo na utaalamu wake wa kushika usukani alijaribu kumkwepa mtu yule bila mafanikio, dereva yule alisahau sheria ya kwanza ya udereva na kosa lile liligharimu maisha yake pamoja na uhai wa abiria aliowabeba ndani ya chombo kile cha usafiri. Gari lilipoteza uelekeo na punde si punde lilikua likibingirika pembezoni mwa barabara na kutokana na uwepo wa miti mikubwa basi lile lilijibamiza kwenye baadhi ya miti na kupelekea kuharibika vibaya sana. Kosa dogo alilofanya dereva la kutaka kunusuru uhai wa mtu mmoja ambaye alimuona mbele ya barabara lilisababisha ajali mbaya sana, baadhi ya abiria walipiga kelele za kuomba msaada kutokana na majeraha waliyoyapata na maumivu makali, lakini sauti zao zilimezwa na uwepo wa miti minene ndani ya msitu ule uliopo pembezoni mwa barabara.
Ghafla walitokea watu wa ajabu waliokua wamevaa kaniki nyeusi na vilemba vyekundu huku wakiwa wameshikilia mitungi pamoja na vibuyu vilivyozingushiwa shanga na irizi, watu wale waliokua takribani kumi na tano, nywele zao zilikua ndefu na zilizokua zimepakwa matope, kucha zao zilikua chafu na ndefu huku wakiwa na macho mekundu sana, baadhi yao walikua na siraha za jadi vilivyozungushiwa irizi nyekundu huku vikichuruzika damu. watu wale wa ajabu wake kwa waume walilifuata basi lile lililokua limeanguka huku wakitembea kwa mwendo wa madaha na kuringa mithili ya mtu aliyeona chakula kitamu huku akiwa na njaa kali sana. "Mama tusaidie!" aliongea mmoja wa abiria huku akilia baada ya kuwaona wale watu wakilisogelea basi lile kwa kupoitia kioo cha nyuma ambacho kilikua kimevunjika vibaya. mtu yule ambeye mguu wake wa kuume ulikua umevunjika vibaya huku chuma kikubwa kikiwa kimeingia ndani ya bega lake la kushoto aliwaona watu wale lakini hakuweza kufanya lolote wala kunyanyuka. Baadhi ya majeruhi wengine walijitahidi kutoka kwenye basi lile lakini ghafla kilisikika kitu kizito kikitua juu ya basi lile lilolala kiubavuubavu. mtu mmoja aliyekua amekatika mguu na kwa ujasiri mkubwa alijitahidi kutoka nje ya basi lile kwa kupitia dirishani ghafla alivutwa kwa nguvu kuelekea nje na alisikika akipiga kelele kwa nguvu sana "mamaaaaaa nakufaaaaaa...." alisikika mtu yule lakini ghafla sauti yake ilianza kuzimika kama vile alikuwa akinyweshwa maji hivyo alishindwa kuongea, hii ilikua damu iliyokua ikizuia koo lake kutoa sauti hivyo kufanya damu kuingia kwenye koo la hewa. Abiria wengine waliokuwemo ndani ya basi lile lililopata ajali waliduwaa kwa hofu lakini ghafla kioo cha mbele cha basi lile kilitolewa kisha watu wale waa ajabu waliingia ndani ya basi lile na kuwanza kumpoteza mtu mmoja mmoja mmoja huku wakijaza vibuyu vyao damu zilizokua zikimiminika kutoka kwa majeruhi wa ajali ile.
kwa nje basi lile lilionekana likichezacheza huku sauti za abiria wakiomba msaada zilisikika lakini hawakua na huruma na waliendelea kuvuna damu kwa abiria mmoja mmoja mpaka waliwamaliza wote. Hawa wanataka kufanyiaa nini} ni moja ya mawazo ambayo yalikua yakizunguka vichwani mwa baadhi ya abiria. "mama tusaidie.... wachawiiii wanatumalii..." alisikika abiria mmoja ambaye hakufanikiwa kumaliza kauli yake. mara sauti ziliishilia kwa mbali....
Watu wale waliovaa kaniki walitoka ndani ya basi lile huku wakiwa na mitungi pamoja na vibuyu vyao mikononi vikiwa vinavuja damu, iliyokua ikichuruzika taratibu sana, kwa mwendo wa ajabu wachawi wale walitoka kwenye basi lile na kutokomea kwenye ule msitu uliopo pembezoni mwa ile barabara, sauti za bundi pamoja na fisi zilisikika kutokea ndani ya msitu ule huku wakilia kwa kupeana zamu, mara alitokea mtu mmoja kati ya wale wachawi huku mkono wake wa kuume alikua ameshikilia usinge mweusi uliokua umelowa damu, akiwa amepanda fisi mkubwa mwenye macho mekundu huku mdoomo wake wenye meno makubwa yakiwa yamechongoka ulimi wake ulikua nje huku akidondosha udenda kama mbwa, alipita kwa kasi karibu na basi lile na pembeni kidogo kulikua na kibao kilichoandikwa kwa herufi kubwa "KARIBU HAPA NDIO GAMBOSHI.... ghafla wachawi wale walipita kwa kasi wakimfuata yule mchawi wa kwanza ambaye alionekana kama ni mkubwa wao, damu iliyokuwemo kwenye moja ya mtungi uliokua umejaa vizuri na umepakiwa kwenye mgongo wa fisi mmoja iliruka na kumwagikia kwenye kibao kile na kuyafanya maandishi yale kuwa alama nyekundu na kutishia mtu yeyote ambaye atayasoma.
**
Upande wa pili, Akiwa amekaa kwenye meza ndogo anapata chakula cha jioni Nyangeta, binti mrembo alieumbika kisawasawa mwenye shepu nzuri na rangi inayoendana na ngozi safi laini yenye mvuto wa aina yake, nywele fupi zilizopangika vizuri kichwani huku akiwa ameweka blitch ya rangi ya kahawia ilimfanya aonekane binti wa kisasa, huku akiwa amevalia nguo za kulalia (night dress) mkononi mwake akiwa ameshikilia mnofu wa nyama ya kuku akiutafuna taratibu na kwa mbali akisikiliza mziki laini kutoka kwenye sabufa iliyomo ndani ya chumba chake ghafla simu yake aina ya samsung Galaxy S 5 Active iliita, aliisogelea na kuiangalia kwenye kioo ilikuwa imeandika Inspecta Rashid aliipokea kwa adabu na kuiweka sikioni
"Hallow afande..."
"Ndio afande,
"Sawa afande, ntakuwa tayari baada ya dakika tano"
"..... Sawa afande"alijibu kwa adabu Nyangeta huku akinyanyuka kwa haraka
na kuanza kubadili nguo pamoja na viatu. Alichukua koti kubwa kabatini na kulivaa juu huku akichukua na bunduki yake aina ya bastola burrete 9mm na kuiweka kiunoni, alifungua kabati lingine pembeni na kutoa magazine ndogo kisha akaiweka kwenye mfuko wa koti alilolivaa, mara alisikia mlio wa gari ukitokea nje, alisogea dirishani na kusogeza pazia lililopo dirishani ili kumpa uwezo wa kuchungulia nje, gari ndogo nyeusi aina ya rav4 ilipaki nje ya nyumba yake na kupiga honi,,, Nyageta alitoka nje na kufunga mlango wa nyumba yake, kwa nje kisha aliingia kwenye gari lile kisha dereva wa gari akaliondoa kwa kasi,,, ITAENDELEA
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
USIKOSE EPISODE: 02
©Copyright "haki zote zimehifadhiwa"