Hadithi: Kichaa cha Mpenzi

Mommadou Keita

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
230
237
Sehemu ya 1

JINA lake kamili aliiitwa Meddie Manyara. Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukanyaga katika majengo ya Shule ya Sekondari ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Meddie alikuwa amehamia katika shule hiyo na kujiunga kidato cha nne akitokea Tabora alikokuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ya Uyui.
Sababu kubwa ya kujiunga na shule hiyo, ilikuwa ni kukaa karibu na kaka yake, Omary Manyara ambaye alikuwa maarufu zaidi kwa watu wengi kwa jina la Ommy.

Ommy alikuwa mtoto wa kwanza wa familia ya Mzee Tuesday Manyara iliyokuwa na watoto saba, alikuwa mwajiriwa wa serikalini.

Pamoja na kufanya kazi serikalini hakukuwa ndugu yake yeyote aliyefahamu kwa ufasaha hasa kaka au ndugu yao huyo alikuwa akiifanya kazi gani. Hakuna aliyekuwa akiijua taaluma yake.

Ndugu na jamaa wengi waliridhika tu walipofahamu kaka yao, ndugu yao alikuwa akifanya kazi serikalini.

Na hata Ommy, hakupenda kuyaweka maisha yake hadharani. Alikuwa msiri sana katika mambo na mipango yake mingi. Ndugu, jamaa na marafiki walifarijika zaidi kutimiziwa shida zao bila ya kufahamu undani zaidi wa kazi yake.

Shida za maisha yao zilimhusu moja kwa moja lakini kazi yake haikuwahusu ndugu na jamaa zake, hivyo hawakutambua alikuwa akijihusisha na nini.

Uwezo wake wa kifedha ulizua maneno kwa baadhi ya watu, wengi walisema alikuwa akitumia majini kupata pesa na wengine wakidai alikuwa akitumiwa na baadhi ya viongozi wakubwa wa serikalini katika kazi zao binafsi. Baadhi ya watu walimhusisha Ommy na makundi ya Freemason.

Hata hivyo, kulikuwapo na vitu vichache vilivyowafanya watu hao washindwe kumhusisha navyo. Vitu hivyo ni biashara za kuuza madawa ya kulevya na ujambazi. vitu vilivyowafanya washindwe kumhusisha Ommy na mambo hayo ni kutokana na kumuona akiendesha au kuendeshwa katika magari yalikuwa na nembo za serikali, Adam na Hawa.

Lakini walimpa tuhuma nyingine ambazo hata mwenyewe alipozisikia zilimshangaza na kumfanya aishie kutabasamu kwa uchungu. Wapo waliodai mali zote alizokuwa akizimiliki zilikuwa za vigogo wa serikalini ambao walikuwa wakificha umiliki wao kupitia yeye.

Mbali na kufanya kazi serikalini, Ommy alikuwa na vyanzo vingine vingi vya kumuingizia mapato ya kila siku.
Alikuwa na ukwasi mkubwa kwa kumiliki nyumba kadhaa za kupangisha, hoteli na magari ya kutosha, alikuwa na magari ya biashara kwa ajili ya kukodisha katika shughuli mbalimbali.

Pia, alimiliki malori ya mizigo yaliyokuwa yakisafiri kwenda nchi za jirani. Pia, alimiliki magari kadhaa ya kifahari kwa ajili ya matumizi ya familia yake na ndugu zake. Pamoja na kumiliki nyumba na vitu vingine lakini bado Ommy alikuwa akiishi katika nyumba ya serikali maeneo ya Kichangachui, Masaki jijijni Dar es Salaam.

Kaka huyo mkubwa wa familia ya Mzee Manyara, aliendesha maisha yake na mkewe, Fetty Amma wakiwa na watoto wao wawili, mmoja akiwa shule ya msingi katika mojawapo kati ya shule za msingi mojawapo kati ya zenye umaarufu mkubwa jijini Dar es Salaam.

Mwingine akiwa bado mdogo zaidi.
Pamoja na yote, watu wengi walivutiwa na kumpenda Ommy kwa sababu alikuwa mtu wa kujichanganya katika makundi ya watu tofauti. Hakuwa na tabia ya kuwabagua watu kwa hali zao za maisha, aliwasaidia wote ndugu na marafiki kwa misaada ya aina mbalimbali. Alifanya hivyo bila ya kinyongo wala hinda.

Ni Ommy ndiye aliyewaomba wazazi wake wamruhusu Meddie ahamie Dar es Salaam kutoka Tabora ili aweze kumsaidia kwa karibu zadi katika masomo yake na baada ya kuhitimu amtafutie kibarua cha kumfanya aendeshe maisha yake.

Ommy alichukua jukumu la kumsomesha mdogo wake ili kuwasaidia wazazi wake.
***
MEDDIE tayari alishayazoea mazingira ya Shule ya Kinondoni, alipata marafiki wengi aliokuwa akisoma nao katika darasa moja kutokana na uchangumfu wake.

Mbali na wanafunzi wa darasa lake pia, Meddie alifahamiana na marafiki waliokuwa wakisoma katika madarasa mengine shuleni hapo.

Lakini kati ya marafiki zake wote, mmoja tu kati yao ndiye aliyekuwa mtu wake wa karibu zaidi kuliko wengine wote, huyu aliitwa Harry Mikael. Wawili hao walitokea kufanana kwa baadhi ya tabia na matendo yao. Na siku zote waswahili wanasema, ‘ndege wa rangi moja huruka pamoja’.

Wote walikuwa ni vijana wanaojipenda kwa kuwa unadhifu, pia muda mwingi walizungumza kuhusu michezo hususan soka, ngumi, muziki na kupenda wasichana. Katika hili la kupenda wasichana, Meddie alimwacha rafiki yake kwa umbali mrefu sana.

Hakuwa mtu aliyeweza kuficha hisia zake, mara nyingi alipenda kuwaangalia na kuweka msimamo wake kwa mwanamke aliyetokea kuvutiwa naye, hakuwa muoga.

Unaweza kusema Harry alikuwa ni muoga, kwani alikuwa akifanya mambo yake kwa taratibu sana, alikuwa akichukua muda mrefu kutafakari jambo na kulitolea au kulifanyia uamuzi.

Harry hakuwa mwepesi kutekwa na hisia za kimapenzi na alikuwa mgumu kuonyesha hisia zake kwa mapema.
Pamoja na tofauti hizo, bado ilikuwa ni vigumu kuwatenganisha wawili hao, ambao muda mwingi walikuwa pamoja hata baada ya kutoka shuleni.

Kama hawakuwa pamoja, basi kila mmoja alifahamu mwenzake alikuwa wapi wakati huo na alikuwa akifanya nini.

Hata wikiendi ambayo walikuwa hawakutani shuleni lakini walipanga mipango yao na kukutana kwa ajili ya mazungumzo katika viunga mbalimbali.

Wakati mwingine waliambatana na dereva kwenda kutanua kwenye viwanja vya burudani au kufundishwa jinsi ya kuendesha gari. Haijkuwa jambo la ajabu kuwakuta katika Ufukwe wa Bahari ya Hindi, maeneo ya Oysterbay, maarufu kama Ufukwe wa Coco.
Hiyo ndiyo sababu iliyowafanya kila alipokuwepo Meddie na Harry awepo na kila alipokuwepo Harry na Meddie alikuwapo. Na kila mmoja alifahamu siri, udhaifu na nyendo za mwenzake kwa ufasaha.

Maswahiba hao hawakufichana kitu, pamoja na Meddie kuishi Kichangachui, Masaki na Harry alikuwa akiishi Upanga. Baada ya wiki moja tangu ajiunge shuleni, Meddie aliyazoea mazingira ya shule hiyo iliyoko katika kitongoji cha Kinondoni.

Hali hiyo ilitokana na uchangamfu wake pamoja na ukaribu wake na rafiki yake aliyechukua jukumu la kumtambulisha kwa watu mbalimbali shuleni kwao.

Asubuhi moja Meddie alikuwa akiingia shuleni akiwa ndani ya gari ya kaka yake, Toyota Cresta Gx 100. Hakuwa nyuma ya usukani, bali aliketi pembeni akiendeshwa na mmoja kati ya madereva waliokuwa wakilipwa na kaka yake.

Gari lilikuwa getini kwa ajili ya kusubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya uzio wa shule na dereva alikuwa akisubiri geti lifunguliewe. Kwa bahati nzuri macho ya Meddie yakanaswa na kitu. Tangu yaliponaswa na kitu hicho hayakuweza kujinasua na kuangalia pembeni, yalibaki katika mtego ule uliyoyanasa.

Macho yake yalivutiwa na mmoja kati ya wanafunzi wa kike aliyekuwa akiingia shuleni hapo kupitia geti la watembea kwa miguu. Macho ya Meddie hayakubanduka kutoka kwa msichana yule aliyekuwa akitembea kwa mwendo wa haraka kuwahi kuingia ndani ya shule hiyo.

Meddie alikamatwa na pumbazo la akili kadiri alivyoendelea kumwangalia mwanafunzi yule.

Hakuacha kumwangalia. Aliendelea kumwangalia hadi alipopotea kwenye upeo wa macho yake. Hata baada ya kupotea kwenye upeo wa macho yake, bado Meddie hakutosheka, aliendelea kutazama upande ule aliokuwa ameelekea msichana yule. Alikuwa akiangalia upande ule kama vile bado alikuwa akimuona yule aliyekuwa akimwangalia.

Taswira ya mwanafunzi yule wa kike ilibaki akilini mwake. Mara baada ya gari kuruhusiwa kuingia ndani ya geti, haraka Meddie alishuka na moja kwa moja alifuata uelekeo ule ambao mwanafunzi yule wa kike alikuwa ameelekea.

Tayari alikuwa ameshachelewa, aliyemfuata alishaenda zake na ingekuwa vigumu kutambua safari yake ilikuwa imeishia wapi.

***
HAKUWA na budi kurudi darasani kwake. Meddie alionekana kutawaliwa na furaha au hali ya ushawishi wa kutaka kufahamu kitu fulani. Harry alipomuona rafiki yake akiingia darasani, alihisi siku hiyo alikuwa na kitu ambacho hakikuwa cha kawaida. Meddie alionekana kutawaliwa na furaha ya kati kwa kati.

Harry alimwangalia rafiki yake hadi alipoketi karibu yake. Marafiki hao walikuwa wakikaa karibu kabisa darasani ili kurahisisha mazungumzo ya habari zao za hapa na pale. “Aisee… kuna kitu nimekiona leo hatariii….” Alisema Meddie baada ya kusalimina na jamaa yake kwa sauti ya chini, kuonesha hakutaka mtu mwingine asikie kile alichokuwa akikizungumza.

“Kitu gani…?” alinong’ona Harry huku akiachia tabasamu lenye udadisi.
“Nimemuona mtoto mkali sana… yaani kama sio malaika basi atakuwa ni malkia fulani hivi kutokana na mwonekano wake…” “Umemuona wapi?” Harry aliendelea kudadisi.

“Hapo nje, alikuwa akiingia shuleni tena ameelekea madarasa ya huku, nilijaribu kumfuatilia lakini nilikuwa nimechelewa….” alisema Meddie.
“Huku…” alisema Harry huku akionyesha mkono kule ambako Meddie alikuwa amemwelekeza.

“Ndio,” aliitikia Meddie.
“Huku kuna madarasa ya kidato cha pili na cha tatu,” Harry alifafanua.
“Basi acha tu…” Meddie hakuweza kumalizia kauli yake baada ya mwalimu kuingia darasani na wao kutakiwa kusimama na kutoa salamu kwake.

Baada ya vipindi viwili vya masomo kumalizika, marafiki hao walitoka darasani kwa ajili ya mapumziko ya saa nne, Meddie na Harry kama kawaida yao walikwenda kutafuta kifungua kinywa.

Walitoka nje kabisa ya shule wakielekea kwenye mgahawa maarufu uliopachikwa jina la Kuti Kavu, njia nzima Meddie alikuwa akizungumzia habari zilizommhusu yule msichana aliyemuona asubuhi. Harry alitamani sana kumwona ili aweze kumtambua, pamoja na sifa zote alizopewa na rafiki yake bado hazikutosha kumfanya amtambue msichana huyo.

“Nakushangaa, Harry yaani wewe umenitangulia shuleni lakini macho yako hayajamuona yule binti....? Haiwezekani,” alisema Meddie.

“Inategemea, unachokiona wewe sicho ninachokiona miye, kila mtu ana macho yake,” alijitetea Harry.

“Hata kama lakini sio kwa kiumbe kama kile, naamini, shule nzima hakuna msichana mrembo kama yule,” alisisitiza Meddie.

“Unajua Kinondoni imesheheni wasichana warembo na wa aina mbalimbali na wote ni warembo. Kuna wasichana wa Kiarabu, Kihindi na hata Maafrikasti wa kila aina, sasa siwezi kujua wewe umemuona nani?”
“Niliyemuona hakuwa Mwarabu, hakuwa Mzungu wala hakuwa Mhindi na sio shombeshombe kama unavyofikiria.

“Ni mswahili na sidhani kama kuna Mhindi, Mwarabu, Mzungu au shombe yeyote anayeweza kumfikia kwa uzuri wake…. Yule anafaa kuvikwa taji la Miss Kinondoni au kuitwa malaika kama sio malkia wa Kinondoni.”

“Sijui atakuwa ni nani huyo binti….?” Alijiuliza Harry huku akijaribu kuwafikiria baadhi ya wasichana wanaliokuwa wakisoma shuleni pale ambao waliaminika kuwa ni walimbwende haswa.

“Anaweza kuwa nani?” Harry alitafakari kwa mara nyingine akiwaza kisha akaendelea;

“…Labda anaweza kuwa Mwantumu, Jackie, Maua, Edna, Asia, Raya au Nancy kama sio Suzzie…” “Kuna majina matamu umeyataja, yanafanana na urembo wa binti yule, lakini siwezi kulijua jina lake halisi ni lipi kati ya hayo,” alisema Meddie wakati Harry alipowataja baadhi ya wasichana walioaminika na kutajwa na watu wengi kuwa ni warembo shuleni kwao.

Meddie hakujua binti yule alikuwa akimiliki jina gani kati ya majina hayo mazuri yaliyotajwa na Harry.
ITAENDELEA JUMATANO
 
Waiting!
 
KICHAA CHA MAPENZI - 2
BAADA ya kumaliza kifungua kinywa, muda wa kurudi darasani ulikaribia. Marafiki hao wakatoka katika mgahawa na kurudi shuleni. Wakiwa wanatembea kwa mwendo wa pole huku wakizungumza hili na lile, hawakuwa mbali sana na shuleni. Ilikuwa ni takribani kama mwendo wa dakika tano tu.
Walishafika getini na wakaanza kuingia shuleni, walishalivuka geti la shule, ghafla Meddy akamuona mtu wake.
Ni yule msichana aliyemuona asubuhi na kujaribu kumfuatilia na baadaye kumhadithia habari zake rafiki yake.
Wakati huu binti yule alikuwa peke yake, akitembea kwa mwendo wa taratibu kama aliyekuwa akiogopa kuikanyaga ardhi. Alikuwa katika mwendo wa pole, uliomfanya kuonekana kama anatembea kwa maringo. Ulikuwa ndio mwendo wake pindi anapokuwa hana haraka.
Mwendo wake ulimfanya aonekane kama mmoja kati ya washiriki wa Miss Tanzania waliokuwa wakitembea juu ya jukwaa katika harakati za kumsaka mshindi wa taji hilo.
Kitendo bila ya kuchelewa, Meddie alimgeukia Harry na kumwambia; “Yees… Ni yule pale… Ni yeye….”
Kauli hiyo ilimfanya Harry kumwangalia msichana yule na kuachia tabasamu na kuamini alipatia katika ubashiri wake wa kutaja majina ya wasichana aliokuwa akiwafikiria.
Kwani moja wapo kati ya majina aliyoyataja mojawapo lilikuwa la msichana yule aliyekuwa akimuona mbele yake.
“Nilihisi angekuwa ni mmoja kati yao tu,” alisema Harry na kumwambia rafiki yake msichana yule alikuwa akiitwa Asia.
“Kumbe unamjua?” Ilikuwa ni zamu ya Meddie kushangaa.
“Namfahamu … ni kweli ni msichana mrembo sana lakini….” alisema Harry.
“Tafadhali sitaki kusikia kitu chochote kibaya kuhusu yeye …” Meddie alimkatisha Harry alipoanza kutaka kumweelezea wasifu wake.
“Sitaki kumzungumzia kwa ubaya isipokuwa nataka kukwambia kitu kuhusu...” Harry hakumaliza kauli kumwambia rafiki yake alichotaka kumwambia, alishachelewa.
Na laiti kama Harry angeendelea kuzungumza, basi angejikuta akizungumza peke yake.
Meddie tayari alishachomoka kumkimbilia msichana yule aliyekuwa akienda upande uleule aliokuwa akielekea asubuhi. Kulikuwa na tofauti kubwa alivyokuwa akitembea asubuhi na alivyokuwa akitembea muda ambao Meddie alipomuona kwa mara ya pili. Safari hii Asia alivutia zaidi kwa mwendo wa pole na wa madaha zaidi tofauti na asubuhi.
“Asia… Asiaaah!.... Asi… samahani….” Meddie alisema huku akitweta na kumfanya Asia asimame na kugeuka sauti iliyotaja jina lake ilipokuwa ikitokea.
Macho yao yakagongana, Meddie alijikuta akichanganyikiwa zaidi baada ya kushudia macho mazuri ya msichana yule. Ni kama Meddie alikuwa amepigwa na shoti ya umeme kwa mshutuko alioupata.
Asia hakuwa msichana wa kawaida. Alikuwa ni mrembo zaidi ya alivyoonekana kwa mbali. Meddie aligwaya na kubabaika kidogo na kupoteza mwelekeo, alipoteza ulimi wake kinywani na kushindwa kuyapangilia vizuri maneno mbele ya msichana aliyekuwa amesimama mbele yake.
Kabla hajasema neno lolote nafsi yake ilikubali siku hiyo alikuwa amekutana na mmoja kati ya wasichana warembo duniani. Wanawake adimu kuwatia machoni katika kizazi cha miaka ya hivi karibuni.
Meddie alithibitisha Asia hakuwa mrembo wa kawaida. Asia alikuwa mrembo ambaye mwanaume yeyote angebabaika pindi alipokutana naye kwa mara ya kwanza.
Haikutosha kusema tu Asia alikuwa msichana mrembo, bali alikuwa ni zaidi ya msichana mrembo.
Alikuwa na urefu usiochusha. Nywele laini zilizosukwa katika mtindo wa kiasili na sura yake ndefu kama ile ya Kimanga. Nyusi zake za mwezi mwandamo, macho makubwa meupe ambayo Meddie alihisi yaliweza kuuona hata moyo wake jinsi ulivyokuwa ukidunda kwa kasi kadiri alivyokuwa akimkaribia.
Alikuwa na sura ndefu ya kihabeshi na pua ya mchongoko. Mashavu yaliyotengeneza alama ya dimpozi pindi alipotabasamu, midomo myembamba iliyotengeneza alama ya kopa kila pale alipoifumbua na kuifumba.
Kidevu chake kidogo kinachofanana na ncha ya yai la kuku wa Kiswahili. Shingo ndefu kiasi ambayo iliitwa ya twiga au shingo ya upanga. Kifua kilichohifadhi matiti machanga kama embe sindano.
Tumbo dogo, jembamba ambalo si rahisi mtu yeyote kutambua ni wakati gani Asia alikuwa ameshiba na wakati gani alikuwa na njaa. Asia alivutia zaidi upande wa kiuno, alikuwa na kiuno cha Kisomali na hispi zilizovimba kama pofu wa Mbuga ya Tarangire. Kwa kifupi, alikuwa amevimba sehemu za mwili alizotakiwa kuvimba na alikuwa amebonyea sehemu zilizotakiwa kubonyea.
Kuanzia kichwani hadi usawa wa tumbo alikuwa mwembemba lakini aliongezeka sehemu za hips, makalio kwa asilimia hamsini. Asia, alikuwa na mikono inayofanana na ile ya Kabila la Kihaya, ilikuwa kama imevunjika hivi wakati alipoirusha kwenda mbele na kurudi nyuma wakati alipotembea kwa mwendo wake unaofanana na twiga wa Mbuga ya Mikumi. Umbile lake lilitengeneza kile kitu ambacho wale wanaoijua Lugha ya Kiingereza walikiita ‘Willow Figure’ na wale wenyeji wa Pwani ya Afrika Mashariki na Kati wanaojua Kiswahili fasaha wakaita umbile lake ‘Namba Nane’. Umetosheka! Hapana bado, miguu ya Asia ilisheheni ujazo uliostahili wastani, ilikuwa na ujazo wa 0.5.
Ilikuwa ni vigumu kumtambua kwa haraka, alikuwa akitokea sehemu gani ya Tanzania.
Kila mmoja alisema lake katika kumwelezea kuhusu kabila lake, wapo walidai alikuwa na mchanganyiko wa Kihaya na Kinyarwanda, wengine waliomwita Msomali na hata waliokuwapo waliosema, Asia ni Mbulu wa Arusha.
Bado Meddie hakuwa ameyabandua macho yake kukiangalia kiumbe kile kilichokuwa kimesimama mbele yake. Ni kama alikuwa akiaangalia picha ya iliyochorwa kwa ustadi mkubwa lakini macho yake yalikuwa bado hajatosheka.
Meddie aliendelea kuyapa fursa yaendelee kushuhudia uumbaji wa Mwenyezi Mungu ambao haukuwa na dosari hata chembe. Kilichompagawisha ni rangi ya ngozi ya msichana yule iliyokuwa iking’ara na kufanana na mafuta yanayotokana na tunda la peponi.
Tunda la Zaytuni.
Ndiyo alikuwa na ngozi yenye rangi inayofanana na mafuta ya Zaytuni. Ungeweza kusema labda Asia hakuwa akitumia maji ya Ruvu Juu au Ruvu Chini wakati wa kuoga. Ungedhani labda alikuwa akiyatumia mafuta hayo kuusafisha mwili wake.
Meddie alionyesha wazi kupagawa, hakuwa akimwangalia mtu mwingine isipokuwa ni Asia. Binti mwenye mchanganyiko wa makabila manne ya Kimasai na Kisomali kwa upande wa baba na alikuwa na mchanganyiko wa mbegu za Kisukuma Kimanyema kwa upande wa mama yake.
“Umeniita unasemaje…?” Sauti yenye mirindimo mwanana kama ya kinanda ya Asia alizipasua ngoma za masikio ya Meddie. Ghafla Meddie alizundukaa kutoka katika lindi zito la mshangao kama sio mawazo.
“Samahani…” alisema tena Meddie na kusogea zaidi na kusimama mbele ya msichana yule aliyekuwa karibu yake.
“Naitwa Meddie… nilikuona leo asubuhi na nimekuona tena muda huu... Natamani tufahamiane zaidi…” alisema katika hali ya wasiwasi na hofu iliyotokana na kupoteza kujiamini.
“Kufahamiana si ushanifahamu…. Mi naitwa Asia… na wewe umesema unaitwa nani…?” alihoji Asia huku akimtazama moja kwa moja Meddie usoni.
“Meddie…” pamoja na kulitaja vyema jina lake lakini bado alihisi labda Asia hakuwa amelisikika vizuri, akarudia tena kutaja jina lake… “Naitwa Meddie…Meddie Manyara… nasoma kidato cha nne,” alisema kwa haraka na kufanya Asia atoe tabasamu mwanana lililompagawisha zaidi Meddie. Lakini haikuchukua muda Meddie aling’amua alikuwa anaelekea kupoteza mwelekeo wake kama hakuwa mwaume shupavu.
Ni kama kengele ya hatari iligonga akilini mwake na kuamini kama asingejiweka sawa alikuwa anaelekea kupoteza pambano kwa kupigwa knock-out na msichana huyo.
“Kuna la zaidi…” Asia kwa mara nyingine tena alizifanya ngoma za masikio ya Meddie kurudiwa na uhai.
Wakati huu Asia alikuwa akimwangalia Meddie kama kuku anavyoiangalia ndege inayopasua mawingu angani.
Msichana huyo alikuwa akimshusha na kumpandisha kijana huyo juu hadi chini, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye katika viunga vya shule hiyo.
“Sawa…ninaweza kukutafuta tena baada ya leo?” Meddie aliupata ulimi wake kwa ufasaha na kuzungumza na kutoa sauti ya chini kidogo kuogopa kusika na wanafunzi wengine waliokuwa wakipita eneo walilokuwa wamesimama.
“Unataka kuniambia nini ambacho unashindwa kuniambia hapa…?” Asia alihoji kwa sauti yake tamu huku akichia tabasamu na kuzidi kumchanganya Meddie aliyeyashashuhudia meno meupe ya msichana huyo kama theluji ya Mlima wa Kilimanjaro yaliyojipanga vyema na kuachia kipande cha mwanya.
“Nina mazungumzo marefu zaidi na wewe, haya sio mazingira mazuri kuzungumza kila kitu …,” alisema Meddie akiwa kama aliyepata uhai na kurudiwa na nguvu za ziada.
Asia aliangalia chini kama aliyetafakari jambo, hapo Meddie alijisifu kimoyomoyo kwa kuamini alikuwa amepata pointi ya kumdhibiti mpinzani wake katika kona, baada ya awali kuona alikuwa akizidiwa kete na mrembo huyo.
Meddie aliona huo ulikuwa ni muda wa wake mzuri wa kuyatawala mazungumzo hayo tofauti na ilivyoanza kuzungumza awali.
“Unajua watu wengi huwa wanakutana sehemu tofauti na … na hatimaye kufahamiana na kuwa marafiki…” alisema Meddie.
“Sawa, utanitafuta basi…” alisema Asia na kugeuka kuanza kuondoka kwa mwendo wake wa hatua za kuhesabu.
Bado Meddie hakuondoka, alikuwa amesimama palepale tena vilevile bila ya kutikisika. Alikuwa akiendelea kumwangalia Asia alivyokuwa akitembea kwa hatua zake za kuhesabu.
Bado hakutaka kuondoka wala kuangalia pembeni, ilikuwa ni burudani tosha kumwangalia Asia akitembea. Ilikuwa ni sawa na kumwangalia Beyonce akiwa anaoga katika jakuzi lake.
Kama ilivyokuwa wanaume wengi, katika kuendelea kumwangalia, Meddie alifika mbali, alimwangalia Asia kwa zaidi ya alivyokuwa akionekana.
Alimwangalia kama vile alikuwa yuko naye katika maeneo ya faragha. Aliendelea kumwangalia msichana yule kama vile ndio kwanza alikuwa akimtia machoni kwa mara ya kwanza.
Asia alipopotea kwenye upeo wa macho yake, Meddie alishusha pumzi nzito, akagundua kijasho kilikuwa kikimvuja katika paji la uso wake, kwa dakika tano alizozungumza na Asia aliona ugumu wa kumtongoza msichana mrembo wa kariba yake. Meddie aliamini haikuwa kazi rahisi kumshawishi msichana kama Asia na kuwa na uhusiano naye wa ukaribu kama alivyokuwa akiutarajia.
Kutokana na mambo yalivyokwenda kwa haraka, Meddie alishindwa kujipongeza lakini pia hakutaka kuamini kama alikuwa amefeli kwa kupoteza pambano katika jaribio lake la kwanza la kumnasa msichana yule.
Kilichompa matumaini ni ile kauli ya Asia: ‘Sawa utanitafuta…’ ambayo bado ilikuwa ikielea katika akili yake kama mawimbi ya bahari.
Meddie aliamini kauli ile ilikuwa ikionyesha kulikuwa na nafasi nyingine ya mazungumzo kati yake na Asia.
Sauti na maneno ya Asia yaliendelea yakijirudia akilini mwake, aliamini angeweza kupata nafasi ya kujipanga vizuri zaidi katika mazungumzo ya awamu ya pili.
Nafasi hiyo ilikuwa ni muhimu kwake na alikuwa akiitaka kwa haraka sana, kwa sababu aliaamini atakuwa na nguvu mpya na atazipanga hoja zake katika mpangilio uliojaa ushawishi ili kuweza kukabiliana na Asia.
“Kwa sasa ni firty- firty,” alijisemea na kujipa matumaini ya kufanikiwa kwa asilimia hamsini ya kile alichokijenga katika uhusiano huo aliotarajia ungekuwa mpya kwake.
Bado Meddie alisimama pale akishauriana na Halmashauri Kuu ya ubongo wake huku akiangalia kule Asia alikokuwa ametokomea.Baada ya kuhakikisha amepotelea kwenye madarasa ya wanafunzi wa kidato cha tatu, Meddie alirusha ngumi hewani kuonyesha ishara ya ushindi kama mpigania uhuru mwenye matumaini ya kushinda mapambano dhidi ya wakoloni. Baada ya kujipongeza akageuka kurudi pale alipomwacha rafiki yake, Harry.
ITAENDELEA KESHO
 
KICHAA CHA MAPENZI- 3
MTUNZI MOHAMMED KUYUNGA
MEDDIE alimkuta Harry akiwa amesimama pembeni kidogo na pale alipomwacha alipomkimbilia Asia.

“Vipi mwamba umefanikiwa nini?” Harry alianzisha mazungumzo baada ya kuuona uso wa rafiki yake ukichanua kwa tabasamu.
“Kama ni nyumba ndio kwanza nimeanza kujenga msingi… tena msingi imara,” alijisifu Meddie akiendelea kuonekana kuwa na furaha.
“Hongera…”
“Asante lakini si kazi rahisi, yule msichana ni mrembo zaidi ya nilivyomuona asubuhi, kadiri unavyosogelea ndivyo anavyozidi kupendeza zaidi.
“Alinifanya nipate kigugumizi cha ukubwa wakati nilipoanza kuzungumza naye…” alisema Meddie huku akishusha pumzi na kutoa kitamba kujifuta jasho usoni pake.
“Kwa hiyo ulikuwa unamuogopa au…?” Harry alimhoji.
“Sio kumuogopa, nilikuwa natetemeka, mtoto akikupiga jicho utadhani umeguswa na shoti ya umeme,” Meddie alisema na kuwafanya wote waangue vicheko.
Walishaingia darasani na mwalimu wa somo husika alikuwa ameshaingia.
Siku hii Meddie alikuwa na furaha sana na alikuwa mchangamfu kwa kila mtu ndani ya darasa lao.
Pia, alionyesha uwezo mkubwa wa ufahamu kwa kujibu maswali mengi yaliyoulizwa na walimu. Tena alijibu kwa ufasaha maswali ambayo yaliaminika yalikuwa magumu na kuwashinda wanafunzi wengine.
Siku hii alikuwa nyota ya mchezo darasani na kuwafanya walimu na wanafunzi kushangazwa na ufahamu wake.
***
BAADA ya siku ile aliyoonana ana kwa ana na Asia, kwa kipindi kirefu Meddie hakumuona tena binti yule na kila mara alifanya jitihada za kumtafuta lakini hazikuzaa matunda.
Katika mojawapo ya jitihada alizojaribu kuzifanya ni kuwahi shuleni na kukaa karibu na geti la shule kumsubiri labda angemuona akitokea na kutembea kwa mwendo wake wa pole au ule wa haraka kuwahi darasani, lakini aliambulia patupu. Malengo ya Meddie yalikuwa ni kuzungumza na Asia ili kuendeleza pale walipoishia siku ile ya kwanza lakini hakufanikiwa.
Bahati mbaya zaidi, siku mbili za mbele zilikuwa ni za mwishoni mwa wiki ambazo zilikuwa zimeambatana na sikukuu ya kitaifa. Siku ambazo shule zilifungwa na wanafunzi hawakutakiwa kwenda shuleni kwa ajili ya masomo.
Katika watu walioishi katika mateso makubwa kipindi hiki mmoja kati hyao alikuwa ni Meddie.
Maisha kwa upande wake hayakuwa na furaha hata chembe. Alikuwa mnyonge muda wote na kila wakati picha ya Asia ilikuwa ikimjia katika fikra zake. Picha iliyojirudia sana mara kwa mara ni ile aliyokuwa akizungumza naye siku ya mwisho walipokutana.
Meddie alikumbuka jinsi Asia alivyokuwa akitembea kwa mwendo wa pole. Alikumbuka jinsi alivyosimama kumsubiri baada ya kumwita jina lake, alikumbuka vile alivyokuwa akizungumza na hata alivyokuwa akifunga na kufumbua midomo yake mwananana. Aliyakumbuka macho ya Asia yalivyomwangalia na hisia alizozipata, aliyakumbuka jinsi macho yale yaliyokuwa meupe na mazito yaliyojaa dalili za usingizi.
Na kama haitoshi Meddie alikumbuka jinsi msichana yule alivyokuwa akitoa ishara pale alipokuwa akifafanua au kulielezea jambo kwa kurusha mikono yake.
Pia, alikumbuka jinsi Asia alivyokuwa akizungumza kwa utulivu na sauti yake yenye mvuto ilivyokuwa akipenya katika masikio yake. Meddie ilifikia hatua akawa anakumbuka hadi maneno ya Asia, ni kama vile alikuwa akimuona akiwa amesimama mbele yake akizungumza naye ana kwa ana.
Kutokana na kumbukumbu hizo mara kadhaa Meddie alijikuta akitabasamu peke yake baada ya kukumbuka kila kitu cha msichana yule mrembo aliyewahi kupata kumuona maishani mwake. Kwa kutomuona Asia, Meddie alikuwa katika mateso makubwa, kwani hakuweza kufanya chochote cha maana.
Alipoteza hamu ya kula, na hata alipokuwa akila hakuwa akishiba kama ilivyokuwa kabla ya kumuona mlimbwende yule. Mara nyingi alimwambia msichana wa kazi aliyekuwa akiwahudumia nyumbani kwa kaka yake asimwekee chakula, alimwambia alikuwa hajisikii kula kitu chochote. Na hata siku alizoachiwa chakula kilikuwa kikiharibika na kuishia kwenda kumwagwa.
Kibaya zaidi ilifikia hatua Meddie alikuwa akizungumza peke yake hata pale alipokuwa akitembea njiani kama mtu aliyeanza kupatwa na aina fulani ya ugonjwa wa akili kama sio wazimu.
Na mazungumzo yake yalikuwa yakimhusu mtu mmoja tu, sio mwengine bali ni Asia.
Mateso aliyoyapata Meddie yalimfanya kupungua uzito hadi kilo mbili mpaka tatu kwa muda mfupi sana.
Usiku ulipoingia, hakuweza kupata usingizi kwa haraka. Muda mwingi aligalagala kitandani huku akitawaliwa na mawazo tele kuhusiana na msichana aliyemuona shuleni kwao. Usingizi wake ulikuwa kilomita nyingi kutoka katika chumba kama sio kitanda chake.
Katika kipindi hiki, Meddie alifanya kazi kubwa sana kuutafuta usingizi, kwani ulimpaa na fikra zake zikahamia moja kwa moja kwa Asia. Kuna wakati alipata usingizi lakini ilikuwa ni baada ya kuvuta hisia kama vile alikuwa amelala chumbani mwake na Asia. Alichokifanya ni kuuchukua mto mmoja na kuukumbatia huku akiubembeleza na kuvuta hisia kama vile alikuwa amelala na msichana yule aliyeukamata moyo wake kisawasawa.
Katika kuvuta hisia kuna wakati alikuwa akilitaja jina la msichana huyo, sio tu kuliita jina la Asia, bali kitu cha ajabu hisia zilimwambia ni kweli alikuwa amelala na na msichana yule chumbani mwake. Alihisi kabisa alikuwa naye kitandani mwake. Hisia zake zilipomwambia hivyo, hapo ndipo alipoweza kupata faraja, kwani aliweza hata kuisikia sauti yake tamu akizungumza naye.
‘Sawa, utanitafuta basi…’ Meddie aliisikia sauti hiyo ikimwambia maneno hayo ya mwisho pale walipozungumza walipokuwa shuleni. Ilipotokea Meddie hisia zake kumfanya kuisikia sauti hiyo aliachia tabasamu huku akiwa ameukumbatia mto wake. Hisia za kusikia sauti hiyo ndio ikawa salama, dawa yaka au faraja iliyoweza kumfanya kupata usingizi na kulala fofofo.
****
KATIKA siku hizo za mapumziko, Meddie na Harry walizitumia kwenda katika Ufukwe wa Coco kupumzisha akili na wakati mwingine kujifundisha kuendesha gari. Ni wakiwa katika ufukwe huo, walikuwa wamemaliza kula mihogo na kunywa maji ya madafu na nyama zake, ghafla Meddie alisimama na kuangalia upande mmoja wa ufukwe huo.
Kilikuwa ni kitendo cha ghafla mno kutokea, Meddie alikuwa ameacha kufanya kila kitu alichokuwa akikifanya na macho yake kuyaelekeza katika vilima vilivyoko Kaskazini mwa ufukwe. Ni kama alikuwa amekiona kitu kisichokuwa cha kawaida kilichomfanya aduwae kwa muda mrefu kukiangalia.
Macho yake yaliendelea kutazama katika vilima vile na kwa mwendo wa pole, Meddie akamsogelea Harry aliyekuwa hatua kadhaa na kumshika bega. Rafiki yake huyo alipogeuka kumwangalia, Meddie alinyoosha mkono wake wa kuume na kidole chake cha shahada kikiwa mbele kumwonyesha kitu Harry.
“Nini…?” Harry alihoji baada ya kuangalia kule alikokuwa akionyeshwa na Meddie na kutoona kitu chochote cha kumfanya astaajabu.
“Umemuona…?” Meddie alimuuliza rafiki yake huku macho yake yakiganda kuangalia kulekule alikokuwa akiangalia.
“Naniii…?” Harry alimuuliza kwa saiti ya ukali kidogo huku akiyahamisha macho yake kutoka katika vilima vile na kumwangalia Meddie usoni.
“Mbona sioni kitu wala mtu, kuna nini kwani?” Harry alihoji.
Meddie alibaki kimya na kuonekana kama mgojwa aliyepandwa na ugonjwa wa Malaria kichwani, Harry alimuuliza.
“Kwani wewe unaona nini ambacho miye sikioni…?”
“Asia…” alisema Meddie na kuendelea….. “Asiaa… Asiaa… Asiaaa..” alisema Meddie na kufanya Harry ageuze tena na tena macho yake kuangalia kule alikoonyeshwa na Meddie lakini bado hakuweza kuona uwepo wa msichana katika eneo alilokuwa akionyeshwa na Meddie.
Kitendo bila ya kuchelewa, Harry alishtukia tu akimuona Meddie akichomoka kwa kasi na kuanza kukimbia kuelekea upande ule aliokuwa akimwonyesha na kudai Asia alikuwapo.
Harry akajaribu kuangalia tena na tena, upande ule na safari hii kwa umakini zaidi kama angeweza kukiona kile alichokuwa akikiona rafiki yake lakini wapi, sio Asia tu, bali hakuona dalili ya kuwepo kwa mtu katika eneo lile la kilima.
Harry akahisi labda rafiki yake alikuwa amechanganyikiwa na laiti kama angekuwa anavuta bangi, basi angesema zilikuwa zimemchengua akili na kumpanda kichwani.
Lakini Harry alitambua, Meddie hakuwa akivuta hata sigara, Harry akaona isiwe tabu, akachomoka kumkimbilia ili kumuwahi asiende kupata madhara kule alikokuwa akikimbilia.
Meddie alikuwa mbele na Harry alikuwa nyuma akimkimbiza ili kumuwahi hata kabla ya kufika katika vilima vile.
Ni wakati akimkimbiza na alipokuwa akimkaribia, Harry alimsikia Meddie akiliita kwa nguvu zake zote jina la msichana yule aliyekuwa akimuona mbele yake.
“Asia…. Asiaah…. Asiaaah,” aliita Meddie huku akizidi kukimbia kwenye mchanga wa Fukwe wa Coco kukaribia vilima alivyokuwa akiviona kwa mbali.
Meddie alikuwa wa kwanza kufika juu ya kilima kile, Harry akaendelea kumfuata.
Meddie alipofikia juu ya kilele cha kilima kile akaonekana kama mtu aliyekuwa akitafuta kitu. Alikuwa akizunguka na kuangaza kila sehemu lakini kitu alichokuwa akikitafuta hakikuwa kikionekana tena.
ITAENDELEA KESHO IJUMAA
 
KICHAA CHA MAPENZI-4
MTUNZI MOHAMMED J. KUYUNGA
Meddie aliendelea kuzunguka katika eneo lile akitafuta hicho alichokuwa akikitafuta hadi Harry alipomfikia.
“Meddie… Meddie… Meddie…” Harry alimwita na kumshika rafiki yake na kumtingisha kwa nguvu, kitendo ambacho ni kama kilimzindua kutoka katika hali isiyoeleweka.
Meddie alizinduka na kuanza kurudiwa na hali yake ya kawaida. Alishutuka na kuanza kujishangaa, ni kama vile alikuwa amezinduka baada ya kukumbwa na jinamizi kama sio kupotelewa na fahamu.
“Meddie…” Harry aliita tena huku sauti yake safari hii ikiwa kali zaidi.
“Naam…” aliitikia kwa sauti ya unyonge na kuanzaa kugeuka na kujikagua huku akiendelea kujishangaa.
“Kwani umeona kitu gani…?”
“Asia…” alisema Meddie huku akiendelea kujishangaa na kugeuka huku na kule kutazama kama kuna kitu angeweza kukiona au kumuona msichana huyo.
“Kuna kitu kinanishangaza,” alisema tena Meddie na kumeza mate.
“Nilipokuwa kule mbali nilimuona Asia akiwa hapa, alikuwa amevaa mavazi ya Kihindi na alikuwa akicheza wimbo mmoja mzuri wa Kihindi na alikuwa akiniita kwa kuniashiria kwa mikono yake nimfuate hapa,” alisema.
“Sasa unamuona hapa?”
“Hapana simuoni, sijui ameenda wapi?” alihoji Meddie kama vile rafiki yake ndiye aliyekuwa na jibu.
“Unaweza kuwa umeliona jini?” Harry alimwambia rafiki yake huku akimkumbusha stori za majini yanaokaa baharini na wenye uwezo wa kujigeuza kuwa binaadamu.
“Hapana sio jini ni Asia… Asia kabisaa,” alisema Meddie na kuanza kuangua kilio.
Harry alimkumbatia rafiki yake na kumbembeleza, kisha akamkokota kurudi naye pale walipokuwa wameketi awali.
Tangu lilipotokea tukio hilo, ufukweni kukawa sio sehemu salama tena kwa Meddie, Harry akamtaka rafiki yake waondoke kurudi nyumbani na yeye ndiye akaushika usukani kuendeesha gari wakati huo akimwacha Meddie kwenye kiti cha abiria.
Awali Meddie ndiye aliyekuwa akiendesha gari kutoka Masaki hadi Palm Beach kumfuata Harry na wakati huu, Harry alilazimika kumpeleka rafiki yake hadi Masaki kisha ilimlazimu kuafuta usafiri mwingine wa kurudi Upanga.
Wakiwa njiani, Harry alimuonya rafiki yake kwa tabia yake ya kuendekeza sana mapenzi.
“Sikia, Meddie sote tunapenda lakini mwenzetu umezidi, umefikia hatua mbaya sana…”
“Hata sijielewi imekuwaje nahisi nimerogwa…” alisema Meddie.
“Hakuna kitu kama hicho, siku zote anayerogwa hawezi kujitambua kama amerogwa….Ni kujiendekeza tu,” alisema Harry kwa ukali kidogo.
“Najiendekezaje sasa…?” alijhoji.
“Ni kwa kumuweka mwanamke akilini mwako muda wote. Imefikia hatua unamuwaza hadi anajaa akilini mwako na kuteka hisia zako.”
“Unadhani napenda, hiyo sio amri yangu lakini…”
“Wewe ndiye unayaruhusu mawazo hayo, saa nyingine Asia ameshakutoa akilini mwake, wala hakukumbuki tena, amesahau hata kama mlikutana na kuzungumza.”
Kauli hiyo haikumpendeza Meddie, ilimfanya anune njia nzima, hadi walipofika Masaki.
****
MAPUMZIKO ya sikukuu yaliisha na wanafunzi walirudi shuleni. Meddie alikuwa mmoja kati ya wanafunzi waliowahi shuleni. Ilimlazimu kuwahi akiamini angeweza kupona ugonjwa uliokuwa umeaanza kuisumbua akili yake.
Alihisi alikuwa akisumbumbuliwa na maradhi ambayo hakuyajua, isipokuwa aliijua dawa ya maradhi hayo.
Dawa yake ilikuwa ni kumuona Asia, ingawaje kwa siku alizokuwa akiwahi shuleni pia hakufanikiwa kumuona msichana huyo na kuyafanya maradhi yake yaongezeke na kuendelea kumsumbua zaidi.
Ilifika hatua Meddie alihisi labda msichana yule hakuwa binaadamu wa kawaida, labda alikuja mara moja shuleni hapo na kuondoka zake.
“Lakini mbona alivaa sare za shule?” alijiuliza akiwa ameketi peke yake.
“Lakini mbona Harry aliniambia kuwa anamfahamu?” lilikuwa swali lingine alilojiuliza akilini mwake kutokana na fikra nyingi zilizokuwa zimemtawala.
Meddie aliendelea kujiuliza maswali na kujijibu ingawaje hakuwa na uhakika wa maswali aliyokuwa akijiuliza na majibu aliyojijibu kama yalikuwa sahihi.
Ilikuwa ni siku nyingine tena, aliingia shuleni akiwa mpole, alijipa matumaini labda angeweza kuonana tena Asia.
Meddie alipofika shuleni, alikata shauri la kwenda kulitafuta darasa alilokuwa akisoma Asia baada ya kusubiri kumuona akipita kuelekea darasani bila ya mafanikio.
Alifika katika darasa ambalo alihisi ndilo Asia alilokuwa akisoma, aliingia baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na mwalimu.
Ni kutokana na makelele ya wanafunzi ndiyo yaliyomfanya kujivisha ushujaa huo wa kuamini kwamba hakukuwa na mwalimu ndani.
Mara baada ya kuingia aliwakuta wanafunzi wengine wakiwa wameketi juu ya madawati.
Wapo walioshtuka na kurudi kukaa katika sehemu zao wakidhani aliyeingia ni mwalimu, walipogundua ni mwanafunzi, walirudi kukaa juu ya madawati na kuendelea kupiga soga zao.
Kwa haraka, Meddie alizungusha macho yake ndani ya darasa lile la kidato cha tatu, huku wanafunzi wengine wakiendelea kumwangalia.
Meddie alimtafuta mtu aliyeamini angeweza kumpa msaada na kupata ufumbuzi wa jambo lake.
Ndani ya darasa kulikuwa na wanafunzi mchanganyiko wa kike na wa kiume. Baada ya kuzungusha macho yake kwa haraka alifanikiwa kumwona mtu aliyeamini angeweza kuyajibu maswali yake kwa ufasaha.
Alikuwa mvulana mmoja aliyekuwa ameketi peke yake kwenye dawati akiandika, alimfikia na kumsalimia.
“Samahani hili ndilo darasa analosoma Asia?” alimtupia swali baada ya salamu.
“Ndio, si Asia Abdulmalik?”
Meddie hakuwa na uhakika na jina la pili la msichana yule lakini aliamini hakukuwa na Asia mwingine shuleni hapo au katika darasa lile zaidi ya yule aliyekuwa akimfahamu yeye.
“Yaa, ndiye yeye huyo,” alisema kwa kujiamini huku akitikisa kichwa chake kuonesha msisitizo.
“Sijamuona shuleni wiki nzima….” Aliongeza swali baada ya kujiaminisha.
“Ni kweli, alipatwa na msiba ndio maana hajafika shuleni, nadhani atarudi wiki ijayo….”
“Oooh! Sawa, asante sana,” alisema Meddie na baada ya kutoa shukrani zake akageuza na kutoka darasani humo.
Kwa kiasi, fulani imani ikamrudia kwamba hakuwa ameliona jini, bali alizungumza na binaadamu mwenye jina la Asia Abdulmalik
Kikubwa kilichomfurahisha ni kulikuwa na uwezekano mwingine wa kuonana naye tena kwa mara nyingine.
Lakini alisikitika kwa kutopata taarifa za msiba na akajishangaa kwa kushindwa kumdodosa yule kijana na kujua Asia alikuwa amefiwa na nani.
Meddie alidhani alipaswa kuhudhuria mazishi na kumfariji msichana huyo aliyetokea kuziteka hisia na fikra zake kama sio kuuiba moyo wake kabisa.
****
ALIPOKUWA akirudi darasani, njiani alikutana na rafiki yake, Harry ambaye ndiye alikuwa akiingia shuleni muda huo.
Siku hii hawakuja shuleni pamoja baada ya Harry kuamka muda wa kawaida na Meddie kuwahi zaidi shuleni kuliko muda wa kawaida.
Malengo yake yalikuwa ni kuwahi na kuamini labda angeweza kumuona Asia wakati akiingia shuleni.
“Kuna kitu naomba unisaidie…” alisema Meddie baada ya kusalimiana na rafiki yake huyo.
“Ni kuhusu masomo au Asia...?” Harry alimdodosa kwa utani huku akiangua kicheko cha kificho.
Kabla ya kujibu, Meddie alitabasamu na kugeuka pembeni kisha akayarudisha macho yake kumwangalia Harry.
“Wewe unadhani itakuwa nataka kukuuliza kuhusu nini?” Meddie naye alimuuliza swali Harry.
“Nahisi itakuwa ni kuhusu Asia maana…” Harry alichomekea huku akimwangalia Meddie kwa jicho la wizi.
“Sina haja ya kukutaka unipe mji, umepata, umetegua vizuri kitendawili changu,” alijibu Meddie.
“Haya niambie naweza kutoa msaada gani kuhusu huyo malkia wako?”
Wakati Harry akiuliza swali hilo, kuna mwanafunzi wa kike aliwapita na akawatolea salamu huku macho yake yakiwa kwa Meddie.
“Mambo zenu…?”
“Poa…” alijibu Harry. Meddie wala hakujisumbua kuitikia salamu hiyo, sio kuitikia tu hata hakupoteza muda wake kugeuza shingo kumwangalia msichana aliyetoa salamu.
“Kwanza nataka nikusahihishe, yule haitwi Asia…ukitaka kulitamka jina hilo vizuri, usilitamke kama linavyotamkwa kwa kiswahili.
“Usilitamke kama linavyoandikwa… litamke kama linavyotamkwa lile Bara la Mashariki ya Mbali. Yaani siku zote unatakiwa utamke Eshia,” kwa utulivu mkubwa Meddie alitoa darasa la jina hilo kwa rafiki yake.
“Wewe tena…?” Harry alisema huku akiendelea kuangua kicheko.
Yule mwanafunzi aliyewasalimia na kuwapita wala hakuwa na nyendo, alipiga hatua kama kumi na tano akageuka na kurudi zake. Hata safari hii alipokuwa akirudi, bado macho yake yalikuwa kwa Meddie.
“Hivi Asia anakaa wapi?” lilikuwa swali la Meddie kwa Harry aliyekuwa akimalizia kicheko chake.
“Yule nasikia baba yake alifariki….”
“Tafadhari Harry… kuwa muungwana hata kidogo, usinitese, acha maneno mengi kama kasuku, kwa nini unazunguka? Nimekuuliza Asia anaishi wapi full stop!” Meddie alimkatisha rafiki yake na kuongeza maneno ya Lugha ya Kiingereza kuonyesha msisitizo.
“Anaishi Magomeni…tena ni Magomeni Mapipa…”
“Unapajua…?”
“Magomeni Mapipa napajua, ila mtaa na namba ya nyumba anayoishi ndio sivijui, kwa kifupi nyumbani kwao sipajui…”
“Oooh! Ila tuache utani, unaonekana unajua baadhi ya mambo ya Asia…” Meddie alitumia nafasi hiyo kumtania rafiki yake.
“Ndio maana siku ile nilitaka kuzungumza na wewe kabla hujamfuata lakini ukanidharau na kuniacha na kumkimbilia mtu wako…” alisema Harry na kumeza mate kidogo.
“Ulitakiwa kabla ya kumfuata yule msichana unisikilize nilitaka kukwambia nini. Halafu sio lazima uukubali ushauri wangu, kama ungeuona ni wa kipuuzi ungeendelea na safari yako.
“Laiti kama ungeuona ushauri wangu una maana ungeufuata, lakini mwenzangu sijui ulikuwaje, ukanipuuza bila hata ya kunisikiliza…” alizungumza Harry kwa hisia.
“Kwa kweli niwie radhi, siku ile nisingeweza kukusikiliza maana hata nilikuwa sijielewi, leo ndio siku yako ya kunishauri, naomba uniambie ulichotaka kuniambia siku ile kuhusu Asia …”
“Sawa, itakuwa ni busara kama utanisikiliza kwa umakini na kunielewa nitakachokwambia… na usinibishie...”
“Sawa nakusikiliza ndugu yangu,” alisema Meddie huku akijiweka vizuri kumsikiliza rafiki yake.
Nini kiliendelea? Usikose simulizi hii kesho Jumamosi
 
JAMANI NAHESHIMU KAULI YA HUYU MDAU... MAANA NI YEYE PEKEE ALIYEJITOKEZA KUTOA MAONI YAKE ASANTENI SANA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom