Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,039
- 3,480
Mawazo kinzani ya wanasiasa hasa wapinzani Tanzania ni MFU, UPOFU, KENGEUFU na ni adui wa MAENDELEO. Hawana jema, hawathamini utamaduni uliowakuza, hawaelewi ni kwanini Ujerumani, China, Urusi ili ujifunze maarifa ya kitaaluma ni sharti ufunzwe lugha yao kwa miaka miwili kwanza? Wanaopinga mpango huu ni vilema wa kufikiri na watabaki hivi hadi mwisho wa dahari.kuna mambo ya maana ya kupewa msisitizo kwenye elimu lakini sio upumbavu HISTORIA, yaani awamu imewafanya watanzania wawe wajinga zaidi na wasiotambua wanataka nini.
Ngoja niachane na huu ujinga nienda kuangalia mechi
Mtu anayepinga anatakiwa aoneshe kile alichojifunza kwa kutumia lugha ya kigeni kimemnufaisha yeye na jamii inayomzunguka namna gani kama mfano chanya wa kuigwa.
Wapinzani hamjui nafasi yenu mhimu ya kuhamasisha mambo yenye tija kwa taifa badala yake mnatumika na mabwanyenye kupiga mayowe kuhusu haki, demokrasia na uhuru wakati hamyaishi hayo kwenye maisha yenu ya kawaida katika familia, jamii na kazini-HUFAI wewe na wenzio-Ukiulizwa hapo kuongea lugha yako ya mama utadai nimezaliwa mjini sikufunzwa.
Msisitizo ni kwamba pamoja na masomo historia, kiswahili na uraia lugha za kiingereza, kifaransa, kichina nk ziendelee kufundishwa kwa ustadi, kiufasaha kwa nia ya kuchochea fikra za uzalendo sio mawazo mgando ya kikoloni kama ya kwako. Hapo ulipo kwanza hujui kuzungumza na kuandika lugha ya kiinereza fasaha lakini unashabikia umangi meza.