Kuingiza siasa kwenye elimu ni kitu kibaya sana. Sioni kama kuna umuhimu wowote wa kuanzisha somo la Historia ya Tanzania

Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
236
Tumekuwa tukipiga kelele kuhusu matatizo yaliyopo kwenye mfumo wetu wa elimu. Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na mitaala inayotumika kutowapa wanafunzi maarifa na uwezo wa kujitegemea baada ya kumaliza masomo yao.

Cha kushangaza badala ya kuumiza vichwa kutafuta suluhu ya haya matatizo tunaongeza tena matatizo mengine kwa kuwarundikia wanafunzi mzigo wa somo la historia ya tanzania ambalo sina uhakika kama lina manufaa yoyote kwa wanafunzi katika maisha ya kawaida.

Leo mwanafunzi wa kidato cha sita anayesoma mchepuo wa PCB, PCM, PGM, CBG, CBA,ECA unamwongezea somo la historia la nini kama sio kumtwisha mzigo tu?

Kama inshu ni historia ya tanzania, wanafunzi mpaka sasa wanaisoma katika maarifa ya jamii, uraia na historia, kuna haja gani tena ya kulifanya kuwa somo?. Kwanini lisifundishwe tu kama mada 'topic' inayojitegemea ndani ya masomo mengine kama vile history au maarifa ya jamii?

Labda ni kipya gani kitaongezewa kwenye hilo somo la historia ya Tanzania?. Hivi kuna mwanafunzi anayemaliza darasa la saba asiyejua chimbuko la Tanzania kuwa ni muunganiko wa nchi mbili za Tanganyika na zanzibar?

Au kuna ajenda iliyojificha ambayo hatuijui katika hilo somo la historia ya Tanzania?

Mimi kwa mawazo yangu naona badala ya kuwaongezea wanafunzi vitu ambavyo havina tija ni bora serikali kupitia wizara ya elimu ingetumia huu muda kufumua mitaala ya elimu iliyopo na kuunda mipya itakayowezesha wanafunzi kufundishwa elimu ya vitendo na stadi za kazi ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea katika mazingira ya sasa.

Nawasilisha.

Tusisahau kauli mbiu ya sera ya elimu inasema Elimu bora na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa inawezekana, wote tutekeleze wajibu wetu.
 
Bado udhaifu wetu kama Taifa unazidi kuleta matatizo. Kila hulka, mwenendo na mapungufu ya Magufuli yanawekewa Sheria na kanuni. Kuhusu historia sikubalani Kama ifuatavyo;

1. Siyo kweli kwamba somo la Historia ya Tanzania halifundishwi. Huko ndiko tumesoma vita vya maji maji, mtemi Mkwawa, Zwangendaba, harakati za Uhuru, TAA hadi TANU nk. Na ni kati ya masomo 7 compulsory hadi O-Level

2. Kuwa watoto waanze Std 1 kusoma Historia ni kuwachanganya. Tuendelee na ule mfumo wa 3K (Kuandika, Kusoma & Kuhesabu) kwa darasa la 1-3. Unamfundishaje Historia wakati hajui kusoma.

3. Tujielekeze kwenye mitaala itakayowapa vijana ajira za kujiajiri, wajifunze stadi za kazi kama ufundi, kilimo, ufugaji, teknoliji etc

4. Kuwa wataanza Julai 1, Ni over ambition. Mitaala iko wapi?, vitabu vimeandaliwa lini? Na je waalimu wametayarishwa?

5. Ni bora kama kuna resources za kuboresha mtaala tuelekeze kwenye masomo ya sayansi kwa kuwa dunia sasa hivi inatawaliwa na sayansi.
 
Tumefikia mahali pabaya sana kwenye hii Nchi! Yaani mawazo na akili ya mtu mmoja tu imegeuka kuwa ni mawazo ya watu milioni 55!!!

Hakuna utafiti ulio fanyika! Ni suala tu la mtu mmoja kulala usiku, na alipoamka asubuhi akaja na wazo la kuanzisha "somo la historia ya Tanzania"

Angebadili mfumo wa elimu kwa kuirejesha ile Elimu ya Kujitegemea iliyo asisiwa na Mentor wake Mwl. Nyerere, huku akiifanyia marekebisho ili kuendana na wakati tuliopo, hakika ningemuunga mkono! Maana Elimu tuliyo nayo, haina tofauti kabisa na ile ya Kikoloni (Colonial Education)

Ifikie wakati Rais akubali kuwashirikisha wadau ili wamweleze ukweli sababu halisi ya Watanzania kukosa huo Uzalendo kama ni kutokana na kutosoma Historia ya Tanzania, au kuna sababu nyingine na zenye mashiko zaidi.
 
Hivi hiki raisi ana mamlaka ya kuweka kitu kwenye elimu bila bunge kujadili? Mbona lile sakata la kubadilisha aliyeongoza vita vya majimaji lilijadiliwa kwanza bungeni afu akarenguliwa kuwa siyo KINJEKITILE NGWALE sasa hili jambo linalo affect Taifa zima tena enzi na enzi kutolewa hoja na mtu mmoja bila kijadiliwa ni kilio.
 
Back
Top Bottom