Somo la Stadi za Kazi ni muhimu kuliko Uraia

escrow

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
371
321
Katika historia ya elimu yetu Tanzania kuliwahi kuwa na somo la stadi za kazi kwa shule za msingi ambalo lilikuwa msingi mzuri kwa wanafunzi waliokuwa na ndoto za ufundi.

Somo hilo lilifutwa miaka kati ya 1997,1998,1999 na hakuna mbadala wake katika kuendeleza vipaji vya ufundi kwa wanafunzi wa Kitanzania.

Badala yake tumebakia na shule za sekondari za ufundi na vyuo vya ufundi pekee, mf. Mtwara Tech , Arusha Tech, Iyunga Tech.

Kwa ngazi ya vyuo tumebakia na vyuo kama MUST, DIT, NIT etc. Swali la msingi unaloweza kujiuliza ni wanafunzi gani wanapaswa kuingia kwenye vyuo vya ufundi kwa sasa? Bila shaka utakuta ni hawa wanaosoma masoma ya kawaida, na ajabu zaidi hata shule za sekondari za ufundi wanafundisha history na uraia kama kawaida.

Nadhani kwa sera yetu ya elimu ya wakati huo ilikuwa na maono mazuri kwamba mwanafunzi anaebobea kwenye ufundi toka ngazi ya shule ya msingi, basi apate mwendelezo mzuri kwenda Technical school na Technical College ili kupata watalaam wengi kwenye sector ya viwanda.

Sasa masomo muhimu sana yalifutwa sio tu stadi za kazi ni pamoja na Somo la kilimo, na sayansikimu, haya yote yalikuwa masomo ya kumwandaa mwanafunzi kujitegemea.

Masomo haya yamefutwa kwa sababu zisizo na msingi na ukiwasiliza wanasiasa wanasisitiza wahitimu wa masomo ya uraia kujiajiri, kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa, maswali ya ni mengi hayana majibu.

Unafuta somo la kilimo, kuanzia shule za msingi unabakiza vyuo vya kilimo, je akasome nani kwenye Chuo cha kilimo kama Sokoine University? Na vyuo vya Veta ambavyo serikali inajenga kwa nguvu akasome nani,?

Kama Taifa tujitafakari na kurudia sera zetu upya. Akili inaniambia mabeberu yanapitia sera zetu na kuona mambo mazuri kwa Taifa siku zijazo then wanarubuni watu wachache kuvuruga sera zetu.

Unapeleka mtu wa history akasome Veta? DIT, na MUST? Kuna watu wanahujumu Nchi hii sio bure.

Naomba kuwasilisha wadau kwa mjadala. waziri wa Elimu.
 
Back
Top Bottom