Sikuabliani na Magufuli kuhusu somo la Historia. Kama ni Uzalendo, watoto watajifunza kwenye somo la URAIA

Lengo kubwa la somo la historia ni kumfanya mwanadamu ajifunze yaliyopita ulimwenguni kote (siyo Tanzania tu) na hivyo kumwepusha kurudia makosa ya huko nyuma. Na wala siyo kufundisha uzalendo.

BTW, nani kamdanganya JPM kuwa uzalendo unafundishwa darasani? Uzalendo maana yake ni upendo wa raia yeyote kwa nchi yake?

Sasa nani amewahi kufundishwa kupenda kitu, mtu(mke/mume/dada/kaka/baba/mama) au nchi? Upendo kwa nchi ni zao la Uhuru, Haki na usawa kwa raia.

Sasa kama hata haki ya kuchagua na kuchaguliwa inaporwa nani ataipenda nchi hii? Kama watu wanalalamika kuhusu ajira, mishahara duni masoko ya mazao hakuna, biashara zinakufa, Uhuru wa kujieleza unabinywa nani ataipenda Tanzania?

Kwahiyo hapa ninaona JPM ana nia ya kutaka jina lake liandikwe kwenye vitabu vya historia, awe anasomwa kama msukuma wa kwanza kuwa rais.

Ndiyo hicho tu anachokitafuta JPM hakuna kingine. Kutafuta sifa tu ndiyo kuna msumbua. Ningemwelewa kama angeshauri uzalendo utiliwe mkazo kwenye somo la uraia.
 

Fiati

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
1,443
2,000
Mkuu paragraph ya kwanza si kweli kwamba Historia haimfanyi mtu kuwa Mzalendo, moja ya faida ya Historia ni kuwafanya watu wawe wazalendo na nchi yao. Mtu hawezi kuwa Mzalendo hasipojua ilikopitia nchi yake Mpaka pale ilipofikia.

Mengine hutajua mwenyewe.
 

Ukana Shilungo

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
2,846
2,000
Hapa naamua kuwa OBJECTIVE, somo la history ndilo linalompa mtu "sprit of Patriotism "

Hiyo ni moja ya OBJECTIVE ya somo la HISTORIA.

Mathalani Kitendo cha MKWAWA, BWANA HERI, ABUSHIRI, YUSUPH BIN OMARY MAKUNGANYA, KINJEKETILE, Kuupinga utawala wakoloni kwa kuchukua silaha.

Wanafunzi wansposoma, wanahamasika kabisa, wanakuwa inspired kuipigania nchi, kuipenda wakitumia mfano mzuri wa hao mashujaa Waafrika waloishi miaka ya 1880's

Mh Rais kama kazungumzia kuwa somo la history linawajenga watu kuwa wazalendo YUPO SAHIHI asilimia 100%.

Kuhusu Civics somo la Uraia kiasi kikubwa linabase kwenye haki za Raia na wajibu.

MIMI NI MWALIMU MTAALAMU WA MASOMO HAYO MAWILI.

2018 nilifaulisha civics na darasa langu lilikiwa 20 kitaifa, 2019 History tena 20 kitaifa.

Nimetoa maoni kama Mtaalamu mbobezi katika masomo hayo.

Katika kauli ya Rais yupo sahihi 100% tusiwe tunampinga kwa kila kitu, mambo mengine tuwe OBJECTIVE.

UKANA SHILUNGO.🙏🙏
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
84,372
2,000
Mkuu paragraph ya kwanza si kweli kwamba Historia haimfanyi mtu kuwa Mzalendo,moja ya faida ya Historia ni kuwafanya watu wawe wazalendo na nchi yao.Mtu hawezi kuwa Mzalendo hasipojua ilikopitia nchi yake Mpaka pale ilipofikia.
Mengine hutajua mwenyewe.
Ni kipi ambacho wewe binafsi hujasomeshwa shuleni kuhusu historia ya Tanzania hadi liletwe somo jipya?
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,281
2,000
Mkuu paragraph ya kwanza si kweli kwamba Historia haimfanyi mtu kuwa Mzalendo,moja ya faida ya Historia ni kuwafanya watu wawe wazalendo na nchi yao.Mtu hawezi kuwa Mzalendo hasipojua ilikopitia nchi yake Mpaka pale ilipofikia.
Mengine hutajua mwenyewe.
Historia ya kinjekitile ngwalu na mangungo imekusaidiaje kuwa mzalendo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom