NI SHIIDA!-15
ILIPOISHIA
Kitendo cha kutoka bafuni na kuelekea kitandani ile sauti iliyokuwa ikilia ndiyo kwanza ikazidi.
"Bitu, acha nikaone anayelia mbona sauti kama ya mwanangu!"
"Mwanako? Afuate nini huku? Embu jifute tuagize chakula tupumzike kidogo urudi hayo mambo mengine waachie hukohuko hayatuhusu."
"Bitu kwangu miye nahisi kama yananihusu."
SEREBUKA NAYO SASA...
"Hayakuhusu sweet wangu embu nisikilize basi!"
"Bitu?"
"Nakusikia!"
"Kwa kuwa nakupenda! Nimeamua siendi tena!"
"Sawasawa, ndiyo maana nakupenda sweet wangu!"
Mama Juliana aliamua kutii amri mbele ya Bitungu japokuwa kelele alizokuwa akizisikia kwa mbali zilimaanisha. Alitoa mafuta yaliyokuwepo kwenye mkoba wake na kuanza kujipaka kisha akampaka na Bitungu.
"Haya mpenzi kwa sasa tupumzike."
"Lakini..."
"Lakini nini tena!"
"Hapana itabidi nirudi tu sasa hivi kwani kulala nitachelewa jamani na si unajua kuna mwanangu nimemuacha."
"Najua, wee tulale, nitatega mlio wa kutuamsha hapa kwenye simu baada ya nusu saa ndo utaondoka."
"Sawa mpenzi!"
Aliitikia mama Juliana huku akiachana na dera alilokuwa anataka kuvaa, aliendelea kuishikiza khanga yake kifuani kisha wakavutana na Bitungu hadi wakajikuta wamelala kitandani huku Bitungu akiwa juu yake na baada ya muda kidogo usingizi ukawapitia.
***
Bado Juliana alikuwa katika machungu makubwa, machungu ya kushuhudia mama yake akicheza mechi ya nguvu na Bitungu, tena mechi ya mchangani bila viatu. Bitungu aliyekuwa amemuamini lakini kumbe alikuwa akimficha siku zote.
Kwa muda huu Juliana alikuwa ameshindwa kabisa nguvu na wale wahudumu wa ile Gesti ya Tupendane. Alikuwa amejikalia zake nje ya ile gesti akitafakari huku pembeni yake akiwa na dereva bodaboda.
"Turudi tu nyumbani!" aliongea dereva bodaboda akimwambia Juliana.
"Hapana, siwezi ni bora uniache!"
"Nikuache?"
"Ndiyo niache hujaelewa nini?"
"Hasira zako hukohuko, haya nipe changu nirudi zangu?"
"Sh. Ngapi?"
"Unajifanya hujui bei tuliyokuwa tumeongea? Nipe elfu 10 zangu."
Juliana alikuwa ameshajipanga kwa kiasi hicho cha pesa. Pesa ambazo alikuwa akiwekeza nyumbani kwao kidogokidogo. Alifungua kipochi chake kidogo kilichokuwa na zaidi ya shilingi elfu 50 kisha akachomoa noti ya elfu 10 na kumpatia na kuondoka zake.
Macho, mwili viliashiria Juliana kukata tamaa ya kitu flani, hakuwa Juliana wa kawaida kutokana na kitu kilichomtokea. Alijiapiza na moyo wake asiondoke mpaka amshuhudie mama yake akitoka pale nje na Bitungu."Lazima Bitungu achague moja leo, kati yangu na mama nani anastahili kuwa naye!"
Alijikuta akijisemea mwenyewe Juliana huku akikazia macho eneo la mbele ya ile gesti kwa kila aliyekuwa akitoka ama kuingia.
Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya nusu saa, giza lilianza kuomba njia. Juliana wala hakutetemeka kurudi kwani mtu aliyemhofia kama akichelewa kurudi alikuwa ni mama yake na siyo baba yake anayechelewaga kurudi nyumbani.
Hatimaye mama Juliana akatoka akiwa ameongozana na Bitungu. Bitungu aliyekuwa amevalia bukta na tisheti ya bluu huku mkono mmoja ukiwa kiunoni mwa mama Juliana.
Hasira kwa Juliana zilikuwa zaidi ya simba jike mwenye njaa kali. Alitamani kwenda kuwasambaratisha lakini moyo wake uligeuka na kuwa mzito kwa kuona kama mapenzi yake na Bitungu yanaweza kuelekea ukingoni. Macho yake yalibaki njia panda yakiwaangalia tu. Baada ya muda alishuhudia bajaj ikifika eneo hilo kisha mama Juliana akampiga busu Bitungu la kumuaga.
"Bitungu! Bitungu! Bitungu!"
Juliana uzalendo ulimshinda na kujikuta akilitaja jina la Bitungu kwa sauti ya juu. Ndo kwanza Bitungu akawa kama hajasikia zaidi ya kuiachia ile Bajaj ikiondoka na mama Juliana. Juliana alichokifanya ni kumsogelea Bitungu karibu.
"Umefuata nini huku? Na nani kakwambia nipo eneo hili?"
"Unanigombeza au unaniambia?"
"Nakuuliza nani kakwambia nipo huku?"
"Uliniambia mwenyewe kwenye simu!"
"Kuwa?"
"Kuwa upo Bagamoyo kikazi!"
"Ndiyo nipo kikazi na hapa wafanyakazi wenzangu wengine wapo ndani!"
"Hata miye naona maana kuna mfanyakazi mwingine wa kike nimemuona umetoka naye na kumuangushia mabusu kisha akaondoka na bajaj!"
"Unasemaje Juliana?"
"Mfanyakazi mwenzenu wa kike nimemuona tena mnashikana hadi viuno?"
"Acha kunikosea mpenzi hebu kwanza twende tukakae kwanza pale tupate japo kinywaji!"
"Hapana nataka twende ndani!"
"Ndani kuna wafanyakazi wenzangu."
"Ndiyo vizuri ukawatambulishe kwangu au vibaya?" Juliana alikuwa akicheza na akili ya Bitungu kwa makusudi. Alikuwa ameshaujua mchezo mzima hadi chumba walichokuwa wakicheza mechi ya mchangani.
"Haya twende lakini..."
"Hakuna lakini Bitungu miye ndiye mpenzi wako wa pekee hao wengine si wafanyakazi wenzako?"
"Ndiyo!"
Kitendo cha Bitungu kuongozana na Juliana hadi chumbani, Juliana alimuwahi na kumsukuma hadi kitandani na kuanza kumshambulia kwa mabusu kadhaa. Wakiwa katika mahaba mazito mara simu ya Bitungu ikaita...
Je ni simu kutoka kwa nani? usikose uhondo Jumamosi..........hapa hapa