Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
15,197
Reaction score
24,568
NI SHIIDA!

"Ha! Ha! Ha! Huyo binti yako anaitwa nani?"
"Ah! Achana naye, naona hasira hata kulitaja jina lake," alisema mama Juliana huku akionesha hasira za waziwazi kwa binti yake huyo.

Muda wa makesheshe uliwadia, mama Juliana ndiye aliyeanza kumchokoza kijana wake huyo huku akiwa anahema kwa mihemo ya kimahaba niue…

"Mpenzi wangu Bitungu," alisema mama Juliana huku akichekacheka kimahaba.
Bitungu hakumwitikia mama Juliana bali alimshika na kumwangushia kitandani…
"Lakini leo sitaki ile njia yako, nataka njia yangu," alisema mama Juliana.

"Noo! Sitaki mpenzi, nilishakwambia tangu siku ya kwanza uliponionjesha njia ile kwamba sitaki kusikia njia nyingine, ulitaka mwenyewe lazima tuitumie njia hiyo," alisema kijana huyo kwa sauti iliyojaa uchu.
Mama Juliana hakuwa na jinsi ilibidi akubaliane, walipanda kitandani na kuanza kuchezeana kwanza katika hali ya kupasha misuli ili waingie uwanjani.

"Mpenzi, hebu nionjeshe njia nyingine basi jamani," mama Juliana alijaribu bahati yake lakini Bitungu akakataa katakata.
Muda ulifika, mama Juliana akajitega kwa njia ile ili mambo yaishe ambapo Bitungu naye akaingia uwanjani kuanza soka.
***
Mara ya kwanza, Bitungu kukutana na mama Juliana alishangaa sana. Sehemu kubwa ya kufahamiana kwao kulianzishwa na mwanamke huyo licha ya kuwa na umri mkubwa na kijana huyo alikuwa kama mwanaye tu.

Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti, Butungu alishtuka wakati wa mechi kuanza kumwona mwanamke huyo anamwelekeza kupita kwenye njia tofauti kabisa na aliyoizoea.

Hali hiyo ilimpa wakati mgumu sana Bitungu, hata mama Juliana alilijua hilo. Lakini kwa vile alikuwa akimpa pesa nyingi kijana huyo, akajikuta anazoea mpaka mwishowe akawa hataki njia nyingine zaidi ya ile aliyofundishwa na mwanamke huyo.

Tabia hiyo ndiyo iliyosababisha Bitungu akaachana na demu wake, Siliani baada ya kukutana naye siku moja na kutaka kumpitia kwa njia aliyofundishwa na mama Juliana. Mzozo mkubwa uliibuka mpaka Siliana akataka kumvaa Bitungu.
***
Baada ya siku hiyo kwa mama Juliana, Bitungu aliendelea na mambo yake kwa ahadi ya kukutana siku tatu mbele. Walikuwa wakikutana mara tatu au nne kwa wiki moja yenye siku saba.
***
Siku hiyo isiyokuwa na jina, simu ya Bitungu iliita, alipoangalia jina halikuwepo, akaipokea …
"Haloo…""Haloo, naitwa Juliana, tulikutana benki…"
"Ooo, baby wangu, vipi?" alisema Bitungu…
"Poa, mzima wewe?"

"Mi mzima sweetheart, umenitosa halafu mbaya zaidi siku ile namba hukunipa zaidi ya wewe kuchukua ya kwangu ukasema utanibip lakini hukufanya hivyo."
"Mambo mengi jamani, nisamehe bure."
"Nimeshakusamehe baby, niambie."
"Uko wapi?"

"Nipoo…nipo wapi hapa, panaitwaaaa…yaani ni jirani na Amana…"
"Ndiyo unaishi hapo au?"
"Hapana, kuna mtu nilikuwa naongea naye ndiyo nimemalizana naye sasa. Je, naweza kukuona? Si uliniambia unaishi Ilala!"
"Yap! Unataka nije?"

"Ndiyo maana yake jamani Juliana…"
"Basi nakuja.""Chukua Bajaj, ukifika jirani na Amana nipigie please."
"Poa."

Bitungu alijipongeza sana kupigiwa simu na binti mzuri kiasi kile, hakuamini hata chembe hivyo alikaa mkao wa kusubiri…"Ikibidi nisimkawize, leoleo nikamalizane naye. Tena siku ile alionekana kama ni mtoto wa mjini, si ajabu anajua kutumia njia ile," alisema moyoni Bitungu.

Ni hadithi yenye kisa cha mapenzi ambapo mama na binti yake walikuta wakizama kwenye pezi la kijana mmoja, ndipo kla mmoja alipoamua kukamia juu ya penzi lake kwa kijana huyo je nini kitaendelea...... Endelea na Muvi hiyo............

Ujumbe: Uaminifu ni nguzo muhimu katika ndoa michepuko haifaiiiiii....!!!
cc :willzkichaa,Pasco,NAMTUMBA,Honey Faith,Mamndenyi,Rich Pol,immaJ,Mbu,tamuuuuu,kuku87,Ennie,mrsleo,Kaizer,josefast,Zamaulid
 
NI SHIIDA-2

ILIPOISHIA
"Ikibidi nisimkawize, leoleo nikamalizane naye. Tena siku ile alionekana kama ni mtoto wa mjini, si ajabu anajua kutumia njia ile," alisema moyoni Bitungu.
ENDELEA SASA…


Ndani ya dakika kumi, simu ya Bitungu iliita, aliyepiga Juliana…
"Umefika wapi baby?"
"Ndiyo nashuka kwenye Bajaj hapa Amana."
"Oke, utaona baa kushoto kwako kama unaenda Boma."
"Nimeiona."
"Njoo hapa."

Juliana alitembea hadi kwenye baa hiyo na kuungana na Bitungu ambaye alisimama na kumbusu Juliana baada ya kufika huku akimwita baby kibao.
"Karibu ukae mama."

"Asante," aliitika Juliana. Moyoni Bitungu alipenda sana anavyomwita Juliana mama na yeye amwite baba. Au baby na yeye amwite sweet lakini Juliana kwake ilikuwa ni mapema sana kufanya hivyo.
Juliana alifikia kuagiziwa kinywaji chenye pombe lakini si kali. Katika kunywa, maongezi yalikuwepo pia. Muda mwingi Bitungu ndiye alikuwa msemaji, Juliana anajibu mpaka pale naye Juliana alipoanza kuchangamka kwa pombe wakaanza kwenda sawasawa.

"Kwani we huna mchumba?" aliuliza Juliana kwa sauti ya kukatakata…

"Sina mama."
"Mpenzi je?"
"Hata mpenzi sina."
"Mmmh! Rafiki wa kike je?"
"Pia sina."

"Huo uongo sasa."
"Hata huo sina."
"Nini?"
"Huo uongo."

Kifupi walishakolea wote, wakacheka na kuendelea kunywa. Mara simu ya Bitungu iliita, akawahi kuangalia kwenye kioo…
"Huyu mwanamke naye msumbufu sana," alisema.
"Ni nani kwani?"

"Ah! Mama mmoja hivi, ananisumbua sana."
"Anataka nini kwani?"
"Eti anataka awe mpenzi wangu."
"Si umkubalie sasa?"

"Baby, kumbe hunipendi wewe. Nimkubalie wakati ni mke wa mtu."
"Sasa kama ni mke wa mtu kwa nini anakufuatafuata?"
"Si ndiyo namshangaa, halafu muda mrefu sana sipokei lakini haachi kunipigia."

"Achana naye, ukiona hivyo si ajabu hata huyo mume hana anajishaua tu," alisema Juliana bila kujua kwamba mwanamke mwenyewe anayepondwa hapo ni mama yake mzazi na wala maneno ya kijana huyo hayakuwa yakitoka moyoni.
"Sasa inakuaje baby?" Bitungu aliuliza swali hilo…
"Kuhusu?"

"Si tunaondoka?"
"Kwenda wapi?"
"Aaa! Maeneo."
"Maeneo ndiyo wapi?"

Bitungu akagundua kwamba, Juliana ni msichana anayependa uwazi, hivyo akaamua kumpasukia…
"Twende gesti."
"Poa," Juliana alijibu kwa mkato kiasi kwamba, Bitungu alihisi hajasikia japokuwa alisikia…
"Umejibuje?"
"Nimesema sawa."
"Sawa nini?"

"Si umesema twende gesti."
"Oke, basi tumalizie vinywaji vyetu twende."
Juliana alivuta kinywaji chake na kuanza kusimama huku Bitungu naye akimalizia, naye akasimama. Simu ya Juliana iliita, akaiangalia na kusema…
"Mama huyo anapiga." Alimwangalia Bitungu kama anayeomba msaada kwake amjibu nini mama yake…

"Pokea, mwambie upo kwa rafiki yako."
"Haloo mama…eee….nipo kwa Zaina hapa nyuma…sichelewi mama…kweli tena."
Baada ya kukata simu, Bitungu alimuuliza Juliana kama anaishi na baba pia…
"Ndiyo, lakini baba si mkali sana lakini hata mama yangu si mkali kabisa ila hapendi ujingaujinga japokuwa na yeye huwa simwelewagi."

"Humwelewagi kivipi?"
"Yaani nahisi kama anachepuka."
"He! Yaani mama yako unasema anachepuka, we vipi?"
"Si ndiyo ukweli lakini."

Walifika gesti, wakapanga chumba kwa siku nzima japokuwa Juliana alisema hataweza kulala.
Ilikuwa dakika chache lakini zenye mahaba mazito kwani Bitungu alianza na kumchezeachezea Juliana sehemu mbalimbali za mwili wake huku msichana huyo naye akionesha ushirikiano wa hali ya juu.
Mchezo ulipoanza, Juliana alishtuka na kuruka baada ya kubaini kwamba, Bitungu alikuwa akitaka kumpitia kwa njia nyingine.

"He! Vipi tena?" aliuliza Juliana akiwa amemsukumia mbali Bitungu…
"Kwani vipi?"
"Kwani vipi kivipi? Unakwenda wapi huko?"
"Aaa! Ina maana hujui?"

"Aka! Sitaki sitaki sitaki, kumbe ndivyo ulivyo, doo! Basi mi naondoka."
"Sikia Juliana. Unajua kupenda kunajumuisha na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukubaliana na ujinga wa mwenzako, kama mimi nakupenda kweli, hata ujinga wako unakuwa wangu, siwezi kusema sikupendi kwa sababu una kidonda, sasa kama umeona mimi nina kidonda ambacho kina kukera kubaliana nacho tu," alisema Bitungu kwa sauti iliyojaa ushawishi wa hali ya juu.
 
NI SHIIDA!-3

ILIPOISHIA
"Sikia Juliana. Unajua kupenda kunajumuisha na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukubaliana na ujinga wa mwenzako, kama mimi nakupenda kweli, hata ujinga wako unakuwa wangu, siwezi kusema sikupendi kwa sababu una kidonda, sasa kama umeona mimi nina kidonda ambacho kinakukera kubaliana nacho tu," alisema Bitungu kwa sauti iliyojaa ushawishi wa hali ya juu.
JIACHIE MWENYEWE…


"Pamoja na lugha tamu anko, lakini mimi siko tayari kwa matumizi hayo, sijawahi kujihusisha hata siku moja," alisema Juliana kwa sauti iliyojaa masikitiko…
"Hata hiyo uliyoizoea si ulianza siku moja kwanza Juliana?"
"Ndiyo."

"Sasa inakuwaje unashindwa hilo?"
"Hapana kwa kweli, siwezi anko."

Bitungu aliamini kuwa, Juliana alikuwa hajui hata hiyo njia halali. Na kama atakuwa anajua basi ni juujuu tu lakini si kwa kina maana alijua mademu wote wa mjini ni watundu siku hizi.
"Angekuwa mtundu kwanza asingeniita anko wakati tumekuja wote mpaka chumbani gesti sasa uanko unatokea wapi?" alijihoji mwenyewe Bitungu akiwa amekata tamaa kupita kwa Juliana kwa kutumia njia ile nyingine.

Ilibidi akubaliane na matakwa ya Juliana, kwenda kwa njia ya kawaida ambapo walianza kwa kuchezeana kwanza huku Juliana akiwa tayari ameanza kuhema kwa nguvu kuashiria kwamba, tayari alikuwa amefika mbali na alichotaka kwa wakati ule ni uhalisia tu.

Bitungu aliishangaa sana hali ya Juliana, hasa alipomwona amebadilika kwa kila namna, akihema sana, akiwa hatulii kitandani na zaidi sana akionesha macho yaliyojaa ulegevu wa kimahaba.
"Juliana baby," aliita kijana huyo.
"Niambie anko…"

"Aaah! Mimi siyo anko wako bwana, mimi ni mpenzi wako."
"Jamani…hilo litakuja automatiki," alijibu Juliana huku akiweweseka pale kitandani.
Ni Juliana ndiye aliyetoka kitandani na kusimama kisha akamshika mkono Bitungu na kumtoa kitandani, wakasimama wote.

Juliana alianza kumvua nguo jamaa akianzia na juu hadi chini. Alipomaliza akajigeukia yeye, akajivua nguo zote na kutangulia kitandani.
***
Mama Juliana alimpigia simu Bitungu kwa dakika tano nzima lakini ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa…
"Huyu leo ana nini? Mbona si kawaida yake kutopokea simu, ameiacha wapi?" alisema mwanamke huyo huku akiwa amejiinamia, akakumbuka kwamba, Juliana naye licha ya kumwambia yupo jiraji na kwamba hatachelewa kurudi lakini alikuwa hajarudi, akashikwa na hasira…

"Huyu mtoto naye mpaka saa hizi? Amekwenda wapi? Na hii tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani kisa yuko kwa majirani ameianza lini kwanza?"

Alichukua simu na kumpigia Juliana. Simu iliita kwa muda mpaka ikakata yenyewe. Wakati simu hiyo ikikata, Juliana alikuwa katikati ya uwanja akiserebuka na Bitungu.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kijana huyo kuoneshwa staili mbalimbali za uwanjani na mwanamke. Hakuzoea, mara nyingi yeye ndiyo anayekuwa kiongozi wa staili.
"Baby, twende chini sasa," alisema Juliana akiwa tayari ameshuka…
"Baby turudi kitandani…"
"Baby wewe kaa kwa hivi."

"Baby geukia kule mimi nigeukia kwa hivi."
Hayo yote yalikuwa maneno ya Juliana kwa Bitungu kiasi cha kumchanganya kijana huyo na kujikuta hajui amweke kwenye fungu gani msichana huyo...

"Kumbe kuniita baby lilikuwa suala la muda tu," alisema moyoni Bitungu akiwa anatoka jasho na kufutwa kwa shuka huku akiangaliwa usoni kwa macho yaliyojaa mahaba mazito kwake.
Hata pale Bitungu alipotangaza kuwasili kwenye kituo cha safari yake, Juliana alimwambia bado, avute subira kidogo.

Bitungu alipata mtihani mzito, alikuwa akijizuia kwa kupunguza kasi, wakati mwingine alipozidisha kasi na kutangaza kufika safari yake akaambiwa bado, alisema moyoni…
"Nimepatikana leo."

Kumbe kwa Juliana, dakika arobaini na tano nzima za mchezo bado anakuwa moto, kuanzia hapo ndipo anaweza kutangaza kufika kwenye kilele cha mlima wanaoupanda. Sasa Bitungu yeye alizoea dakika saba au kumi za mchezo awe kama amecheza kipindi cha kwanza.

Ilikuwa wakati Bitungu yu hoi kabisa akitamani Juliana augue ghafla ili waache, ndipo alipotangaziwa kuwa sasa wafike wote lakini wakati huo kijana huyo alikuwa amejizuia kiasi cha kuwaza mambo mengine tena yale ambayo ni kero ili amudu kwenda na biti za demu huyo.

"Haa! Haa! Daa!" alikuwa akihema Bitungu huku Juliana akiwa katika pozi la kawaida sana kama vile alitoka kubeba godoro tu kutoka sebuleni kupeleka chumbani.
"We Juliana," aliita Bitungu…
"Abee…"
"Abee nani?" Bitungu aliuliza akitaka kujua kama bado anakubalika kuitwa baby au lilikuwa jina la kitandani tu!
"Abee sweetheart."

Bitungu akafurahi sana kusikia kwamba hata nje ya kitanda ameitwa jina zuri zaidi kimahaba…
"Hivi nani amekufundisha?"
"Nini?"

"Kufanya haya uliyonifanyia kitandani leo?"
"Mimi mwenyewe utundu wangu."
"Mh! Usiniache baby?" alisema Bitungu.
"Siwezi kukuacha dear labda uniache wewe. Mimi nataka tufike mbali sana zaidi ya hapa."
"Hata mimi, natamani ikibidi tufunge ndoa."
"Kweli sweet?"
"Sana tu."

Simu ya Juliana iliita tena…
"Mungu wangu…yaani huyo ni mama bila ubishi wala kujiuliza," alisema Juliana akiifuata simu yake…
"Si nilisema…sasa ngoja niweke loud speaker usikie mitusi yake," alisema Juliana huku akiiseti simu hiyo.
"We nguchiro usiyefaa kufungwa na binadamu, mwana wa shetani mtesa wanadamu, kenge mwenye mabaka uko wapi?"
 
NI SHIIDA!-4

ILIPOISHIA
"Mungu wangu…yaani huyo ni mama bila ubishi wala kujiuliza," alisema Juliana huku akiifuata simu yake…"Si nilisema…sasa ngoja niweke loud speaker umsikie mitusi yake," alisema Juliana na kuiseti simu hiyo ili sauti ya mpigaji isikike.
"We nguchiro usiyefaa kufugwa na binadamu, mwana wa shetani mtesa wanadamu, kenge mwenye mabaka, uko wapi?"
JIACHIE KIVYAKO…


"Nipo njiani narudi mama…"
"Nipo njiani narudi mama," mama mtu aliirudia kauli ya bintiye huku akiwa ameziba pua…
"Unarudi na ndege au gari dogo, mbona sisikii kelele?"
"Natembea kwa miguu mama. Si nilikwambia nipo hapa jirani."
"Nakuuliza mbona sisikii kelele?"

"Mama, mtaa huu watu wametulia sana, si kama hapo kwetu, ndiyo maana."
"Kwa hiyo unataka kuniambia wewe ni mwenyeji sana na huo mtaa kuliko mimi mama yako siyo?"
"Hapana mama."

Wakati Juliana anazungumza na mama yake, Bitungu alimsogelea hadi jirani ili kuisikiliza sauti hiyo vyema kama anayeijua…"Mh," aliguna Bitungu.

Baada ya kukata simu, Juliana alimuuliza ni kwa nini alimsikilizia kwa karibu sana…
"Sauti kama naijua kwa mbali."
"Kama ya nani?"

"Mtu mmoja hivi lakini najua siye," alisema Bitungu. Waliachana na hayo, Juliana alijiandaa harakaharaka na kuondoka baada ya kumpiga busu zito kijana huyo…
"Nitakumisi sana baby," alisema Juliana.
"Hata mimi."
***
Bitungu alikaa kitandani akijifikiria. Alimuwaza Juliana akahisi kama anafaa kuwa mpenzi wake wa moja kwa moja…
"Sijui ndiyo awe mchumba wangu?" alijiuliza Bitungu. Mara simu yake iliita, alikuwa mama Juliana. Safari hii akaipokea…

"Jamani baby, mbona hukuwa unapokea simu yangu, ulikuwa na malaya gani leo?"
"Hamna baby bwana, nililala sehemu sikuwa najisikia vizuri."
"Ulilala sehemu wapi, ina maana si nyumbani kwako siyo?"
"Siyo."
"Wapi?"

"Nipo hapa Ilala Amana."
"Ilala Amana? Uko na nani?"
"Mwenyewe."
"We mwongo, kama kweli niruhusu nije."
"Njoo."

Mama Juliana alikata simu bila kutaka kuuliza Amana sehemu gani. Alimpigia simu mumewe kumuuliza anarudi saa ngapi, akamwambia atachelewa.
"Oke," mama Juliana alikata simu kwa mumewe. Akaondoka muda huohuo, anafika nje anapishana na Juliana…"Ndiyo unafika sasa, siyo?"

"Ndiyo mama."
"Mimi narudi muda si mrefu."
"Kwani unakwenda wapi?"
"We, koma ukomaye. Swali gani unaniuliza mimi mama yako?"
***
Mama Juliana aliposhuka Amana ndiyo akampigia simu Bitungu na kumuuliza aliko…
"Ukishashuka vuka barabara, mbele kuna mtaa umeingia, fuata huo hadi jirani na nyumba moja ina genge nje utaona gesti kwa mbele," alisema Bitungu akiwa anatoa maelekezo kwa mama Juliana.

Kwa jinsi mama Juliana alivyokuwa na hamu na kijana huyo, hakusema sawa baada ya maelekezo, yeye alikata simu tu na kuanza kutembea kuelekea alikoelekezwa.

Aliingia kwenye gesti hiyo akiwa amesahau kumuuliza Bitungu namba ya chumba. Mbaya zaidi simu yake ilizima chaji, hivyo aliamua kugonga kila chumba na kuuliza…
"Ngo ngo ngo!" aligonga mlango akasimama mwanaume…
"Nikusaidie?"

"Samahani, kumbe si hapa!"
Akaenda mlango mwingine….
"Ngo ngo ngooo!"

Akatoka msichana, akasimama mlangoni akiwa na taulo…
"Unamjua Bitungu?"
"Bitungu! Ndiyo nani?"
"Kijana mmoja hivi, nilidhani uko naye."

Yule msichana aligeuka kuangalia ndani, mama Juliana akaamini kweli msichana huyo alikuwa na Bitungu ndiyo maana aligeuka kuangalia ndani, akamsukuma msichana yeye akazama ndani…
"He! We mama vipi?"

"Bitungu unadiriki kuni…oooh! Sorry kijana, nisamehe bure nilidhani ni Bitungu."
Kijana aliyelala kitandani akiwa kama alivyozaliwa alimrukia mama Juliana akitaka ajue ni kwa nini aliingia bila maelewano…

"Huwezi kusema sorry halafu ukavamia hivihivi, nani amekwambia mimi ni Bitungu?" alihoji kijana huyo, akamshika mama Juliana na kumwangusha kitandani na kutaka kumwingia kwa mabavu…
"Noo, Bwakila usifanye hivyo," alisema yule msichana…

"Noo, huyu mama ndiyo dawa yake hii, ndicho alichotaka lazima akipate."
Ilibidi yule msichana amkabe kwa nguvu Bwakila ili amtoe mama Juliana ambaye wakati huo alishashindwa kwa pumzi na nguvu pia."Mwanangu nisamehe sana, kweli kabisa nilidhani wewe ni Bitungu, nisamehe sana baba."
 
Michepuko ya sasa ni kula kuku na vifaranga vyake...Ni Shiiiidaaa!!!!...
Wanawake watu wazima siku hizi wanajirahisi sanaa kiasi kwamba hata mtoto wa miaka 15 anaweza kumpanda bila shida yoyote naye akaona sawa tena akafikia hatua ya kuchukia anapoingiliwa kwenye anga zake ni sheeeeeedar!
 
NI SHIIDA!-5

ILIPOISHIA
"Noo, Bwakila usifanye hivyo," alisema yule msichana…
"Noo, huyu mama ndiyo dawa yake hii, ndicho alichotaka lazima akipate."

Ilibidi yule msichana amkabe kwa nguvu Bwakila ili amtoea mama Juliana ambaye wakati huo alishashindwa kwa pumzi na nguvu pia.
"Mwanangu nisamehe sana, kweli kabisa nilidhani wewe ni Bitungu, nisamehe sana baba."
TAMBAA NAYO MWENYEWE…


Bwakila aliamua kusamehe na kumpa onyo kwamba akirudia tabia ile sehemu nyingine atajikuta akibakwa…"Ni kweli mwanangu maneno yako," alisema mama Juliana akitoka na jasho jembamba.

Alikwenda kubisha hodi kwenye mlango mwingine, akafungua mtu mzima f'lani, alipokutana macho na mama Juliana, mtu mzima huyo akaanza kuachia tabasamu…
"Ni wewe?" aliuliza yule mtu mzima fulani…

"Aliye?" alihoji mama Juliana akidhani labda mtu huyo yupo ni Bitungu…
"Tuliyekuwa tukiwasiliana kwenye Facebook, si tumekubaliana kukutana hapa?"
"Akha!" mama Juliana akaondoka hapo, akaenda kugonga mlango chumba kingine ndiyo akatokea Bitungu sasa.

Mama Juliana aliingia ndani na kuangukia kitandani huku akichuruzika machozi…
"Vipi tena?" alihoji Bitungu…"Kidogo nibakwe."
"Kidogo ubakwe! Na nani?"

Mama Juliana alisimulia kisa chote kuanzia kuzimikiwa na simu na yaliyompata ndani ya gesti ile.
"Duu! Pole sana.""Kiranga chote kimeniishia," alisema mama Juliana huku akijifuta machozi na kumkumbatia kijana huyo kama anayasema ‘afadhali nijipoze na wewe sasa'.

Bitungu alichoshwa sana na majambozi ya Juliana mwenyewe, sasa mama mtu kufika pale naye akawa anataka kwa sehemu yake.Alimchombezachombeza kijana huyo kwa kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili ili kumchajisha na huku akimbembeleza kwa maneno matamumatamu ya mahaba…
"Bitungu…"

"Naam…"
"Unajua wewe ulitakiwa uwe mume wangu?"
"Kweli mpenzi?""Kweli kabisa. Wewe unadhani nani alistahili kuwa mume wangu miye?"
"Ni mimi mpenzi."

"Kumbe unajijua, yaani nakupenda wewe mpaka basi jamani," alisema mwanamke huyo mtu mzima huku akiwa anashughulika na kipaza sauti.Ilifika mahali Bitungu akachaji, kila kona ya mwili wake ikakaa sawasawa kwa mechi ya kirafiki isiyokuwa na refa.

"Leo nataka njia ile nyingine," alisema Bitungu lakini mama Juliana akakataa…
"Mimi nataka njia ya siku zote mimi na wewe," alisema mwanamke huyo huku akimfosi kijana huyo kuanza mpambano kwa kumwingiza mwenyewe uwanjani.

Ulikuwa mpambano wenye kumwelemea Bitungu kwa namna yoyote ile. Alionesha uchovu wa waziwazi mpaka mwanamke huyo akamuuliza…"Mpenzi leo vipi, umevurugwa na nani kabla yangu?" aliuliza mama Juliana lakini kabla hajajibiwa, simu ya Bitungu iliita.

Kwa kuwa pozi lao la muda huo, mama Juliana ndiye aliyekuwa upande wa stuli yenye simu, aliichukua na kuiangalia skrini kidogo aliyepiga huku akiipeleka kwa Bitungu. Kwenye skrini ilionekana jina Julie…

"Ah! Nitampigia baadaye," alisema Bitungu akikata simu hiyo kisha kuizima kabisa…
"Julie ndiyo nani?" mama Juliana aliuliza akiwa amebadilika sura ghafla.
"Mtoto wa shangazi yangu bwana, anataka nimtafutie kazi."
"Mh!"

"Mbona umeguna?"
"Nimeguna maana na mimi nina mtoto anaitwa Julie," alisema mwanamke huyo akimaanisha kifupi cha Juliana ni Julie lakini Bitungu akampuuza na wala hakutaka kujiongeza kwamba pengine Julie wa mwanamke huyo ndiye Juliana anayemjua yeye.

Aliamini Julie si Juliana akafurahi moyoni kwamba, amemchenga mwanamke huyo kwa kumsevu Juliana kama Julie…"Mbalimbali, huyu ni Julie mtoto wa shangazi yangu. Labda wewe ndiyo uwe huyo shangazi yangu," alisema Bitungu…

"Naweza kuwa, maana hata mimi Julie wangu anatafuta kazi," mama Juliana alitia neno kidogo likamwingia Bitungu kwani ni kweli Juliana alimwambia anatafuta kazi wakati wamekaa baa walipokutana kabla ya kwenda gesti.

Ikumbukwe kwamba wakati wanayazungumza hayo walikuwa wakiendelea na mechi kama kawaida kwa kutumia njia ile ya mama Juliana na si ya Juliana mwenyewe.

Mama Juliana ndiye aliyeanza kutangaza kupata ushindi kwani Bitungu alikuwa mchovu kwa wakati huo.
Ilishindikana kabisa kwa Bitungu kukamilisha ngwe ya safari yake na hivyo kutoka uwanjani akiwa ameshindwa kukomboa.
***
Ilikuwa siku ya pili, simu ya Juliana iko mezani sebuleni, mama yake akiwa anapita hapo, mara simu hiyo iliita, akaangalia kwenye skrini huku akimwita Juliana mwenyewe…
"Simu yako inaita huku wewe…Bituu," alisema mama Juliana.

Juliana alifika akiwa mbio na kuhema juu…
"Bituu anapiga."Juliana aliichukua simu na kwenda mbali…
"Haloo…sijambo…niko nyumbani mbona…haya sawa…haya."
Baada ya kukata simu, mama Juliana aliita…
"Juli…"

"Abee mama."
"Bituu ni nani?"
"Siyo Bituu mama, nilikosea kusevu tangu mwanzo, ni Bitte."
"Ndiyo nani?"

"Nilisoma naye kule chuo mama."
"Hebu namba yake," alisema mama Juliana huku akinyoosha mkono kutaka simu ya mwanaye huyo.
 
NI SHIIDA!-6

ILIPOISHIA
"Abee mama."
"Bituu ni nani?"
"Siyo Bituu mama, nilikosea kusevu tangu mwanzo, ni Bitte."
"Ndiyo nani?"

"Nilisoma naye kule chuo mama."
"Hebu namba yake," alisema mama Juliana huku akinyoosha mkono kutaka simu ya mwanaye huyo.
SONGA NAYO MWENYEWE…


Wakati Juliana anampa mama yake simu, mkono ukalegea, ikaanguka chini na kuvunjika kioo…
"Mama simu yangu jamani."
"Mbona umelegea mikono wewe, ala!" alifoka mama mtu. Akaendelea…
"Hakijaaribika kitu, toa laini niweke kwenye simu yangu, nataka kumjua huyo Bitte unayemsema wewe ni nani?"

"Kwani mama wewe umefikiria ni nani?"
"Ndiyo nataka kumjua."
Moyoni Juliana akasema…
"Ungejua si Bitte ni Bitungu…"
Naye mama mtu moyoni akasema…

"Ungejua nafananisha jina hilo na la dogodogo wangu Bitungu."
Juliana alitoa laini, akampa mama yake huku simu yake ikiwa imezima baada ya kuanguka. Naye mama mtu aliichukua laini na kuipachika kwenye simu yake, akawasha. Yalikuja majina mengi sana lakini jina la Bitte halikuwepo. Maana yake ni kwamba, jina liliseviwa kwenye simu yenyewe ‘hand set', au wanasema ‘phone book'.
"Hebu lete simu yako."

Juliana alimpa mama yake simu, akatoa laini na kuipachika humo tena, akawaisha, simu haikuwaka kutokana na kule kuanguka.
Akamtupia simu mtoto wake huku akisema…
"Nitataka kumjua huyo Bitte."
"Sawa mama."

***
Bitungu alishangaa kumkosa Juliana kwa siku hiyo, kila alipompigia ilionekana simu yake imezimwa…
"Huyu leo vipi tena?" alijiuliza kijana huyo.

Juliana alifika kwa fundi na kueleza shida ya simu yake, akaambiwa ni lazima ibadilishwe kioo lakini gharama aliyotajiwa ilimshinda, akaamua kwenda kununua simu ya tochi kwanza.
Hata hivyo, alijua hataweza kumpata Bitungu kwa sababu namba zake ziko kwenye simu iliyokufa kioo.
Alinunua simu, akarudi nayo nyumbani ili kuiweka kwenye chaja kwa muda. Lakini nyumbani hakumkuta mama yake na akashindwa kujua aliko.

Baada ya nusu saa, Juliana alichomeka laini kwenye simu yake ya tochi, akaiwasha. Ndani ya dakika moja meseji kibao zikaanza kuingia mfululizo, ikiwemo ya mama yake akimwambia anatoka kidogo.
Ikaingia nyingine iliyomwonesha kwamba ni ya Bitungu kwani ilisema…

"Baby mbona sikupati hewani? Ujue unanipa wakati mgumu sana mwenzio?"
Juliana aliipiga simu hiyo. Wakati simu inaita, Bitungu alikuwa amekaa na mama Juliana…
"Hebu pokea simu kwanza mpenzi wangu ndiyo tuendelee na mambo mengine," alisema mama Juliana, lakini naye Bitungu alipoona ni Juliana aliogopa. Hata hivyo, ili kuua soo aliipokea huku akipunguza sauti…

"We vipi mbona hupatikani kwenye simu?"
"Simu mbovu my dear, kweli tena!"
"Pole sana, mi nilikuwa sijui."
"Ndiyo hivyo. Uko wapi?"
"Nipo mitaa ya Sinza Palestina, nitakutafuta baadaye."
"Poa."

Baada ya kukata simu, mama Juliana alishangaa kuona simu yake iikimpa mrejesho kwamba meseji aliyotuma kwa Juliana muda fulani ndiyo inamfikia sasa, akampigia…
"Umetengeneza simu?"
"Bado mama, pesa ni nyingi nimeamua kununua simu ya tochi kwanza."
"Sawa, ilimradi simu."
"Uko wapi mama?"

"Nipo maeneo ya Sinza Palestina japokuwa sipendi kuulizwa nilipo na wewe," alisema mwanamke huyo huku akimshikashika mwilini Bitungu. Walikuwa ndani ya gesti.
Baada ya kukata simu, Juliana alijiuliza maswali mawili ya msingi sana…
"Mama anasema yupo maeneo ya Sinza Palestina, Bitungu naye anasema yupo mitaa ya Sinza Palestina. Inawezekana wapo wote?

"Mmh!" aliguna baada ya kukosa jibu na kuamua kuachana na hayo.
Muda ulivyozidi kwenda alihisi kwamba mama yake akirudi lazima atataka kumjua Bitte kwa maana ya kumuuliza maswali mengi. Lakini pia aliisevu namba ya Bitungu upya, akaandika Stella Goms, yaani Stella wa Gongo la Mboto.

***
Siku hiyo, Bitungu kwa hasira za kumkosa kwa muda mrefu Juliana, msichana aliyempenda sana na furaha ya kumpata baadaye, aliamua kumchakaza mama Juliana kwa mechi kali isiyokuwa na mfano huku akitumia njia ambayo mama Juliana ndiyo anaitaka.

***
Mama Juliana alikuwa sebuleni kwake amechoka sana na mechi ya Bitungu, akamwita mwanaye…
"Abee mama."
"Kaa hapa."
Juliana alikaa sawasawa na maelekezo ya mama yake…
"Bitte ni nani?"

"Mama si nilikwambia nimesoma naye kule chuo."
"Unaweza kumfuata ukamleta hapa?"
"Ndiyo."

"Mfuate haraka sana."
Kwa Juliana zilikuwa habari njema kwani ilikuwa saa kumi na mbili jioni, kupewa kibali cha yeye kutoka Ilala kwenda hadi Gongo la Mboto ni furaha kwake. Alipanga akitoka tu akaonane na Bitungu popote alipo.

Alijiandaa harakaharaka na kuchomoka zake…
"Haya mama nakwenda kumleta," alisema Juliana akiwa na amani jambo lililomshangaza sana mama yake.
 
NI SHIIDA!-7

ILIPOISHIA
Kwa Juliana zilikuwa habari njema kwani ilikuwa saa kumi na mbili jioni, kupewa kibali cha yeye kutoka Ilala kwenda hadi Gongo la Mboto ni furaha kwake. Alipanga akitoka tu akaonane na Bitungu popote alipo.

Alijiandaa harakaharaka na kuchomoka zake…
"Haya mama nakwenda kumleta," alisema Juliana akiwa na amani jambo lililomshangaza sana mama yake.JIONGEZE MWENYEWE SASA…


"We hebu rudi hapa kwanza," alisema mama mtu. Juliana alirudi huku akionesha sura ya mshangao.
"Mbona umefurahia sana safari ya kumfuata huyo shoga yako asiyekuwa na akili kama wewe?"
"Hapana mama, nipo kawaida tu ila nimefurahi sana kwa sababu najua sina tatizo baya kama unavyonifikiria zaidi ya kwenda kumleta Bitte."
"Haya nenda."

Juliana alisimama kwa mikogo, akaondoka, eti anakwenda kumleta Bitte kwa mama yake kama alivyomuagiza.Juliana alipotoka nje tu, akaweka simu yake sawa na kumtwangia Bitungu…
"Baby mambo jamani?""Poa. Vipi wewe mpenzi wangu? Nimekumisi sana mwenzako."
"Mimi je?"

"Kumbe na wewe umenimisi mpenzi wangu?"
"Sana."
"Uko wapi kwani?"
"Nipo mitaa ya Sinza."

Bitungu aliposema yupo mitaa ya Sinza, Juliana akakumbuka ile hali ya mwanzo ya mama yake kusema yupo Sinza Palestina na Bitungu pia…"Huko Sinza kuna nini leo, halafu hata mama yangu alisema yupo Sinza Palestina leo lakini yeye alisharudi."

"Mimi kuna mtu namsubiri dear," alisema Bitungu akiogopa kusema alikuwa ana mtu angeulizwa ni mtu gani? Si mnajua tena mambo ya wivu."Oke, naweza kukuona leo mpenzi wangu?"
"Wewe tu, si uje.""Oke, nipe kama nusu saa."

Juliana alipanda daladala kwenda Sinza kuonana na Bitungu. Moyoni aliamua kwamba, atakapokuwa kule ampange Bitte kuhusu mama yake. Alitaka amwambie kwamba kesho yake aende nyumbani kwao ana shida naye.
***
Bitungu alimpokea Juliana akiwa baa ambayo pia ina gesti. Na gesti hiyo ndiyo aliyokuwa amechukua chumba akiwa na mama Juliana. Sasa alitaka akae na Juliana pale baa halafu baadaye ajifanye anakwenda kuchukua chumba ndani ili ampeleke Juliana huko kwenye kitanda alicholala na mama yake.

"Baby sasa umekuja kunisalimia tu au na mambo mengine?" aliuliza Bitungu kwa sauti isiyojiamini.
"Na mambo mengine kama yapi?""Kama yapi, mimi si mpenzi wako jamani?"
"Ee, hata kama, mambo mengine kama yapi sasa?"
"Mambo f'lani yale. Ili nikachukue chumba."

Juliana alicheka huu akinywa soda lakini mwishowe akakubali…
"Haya, nimekuelewa, p..."Bitungu hakutaka Juliana amalizie neno oa kwenye poa, akawa ameshasimama kwenda ndani.

Alichokifanya, baada ya kufika chumbani alitandika kitanda vizuri sana kisha akatoka…
"Twende dear, tayari."Juliana alisimama, wakashikana mkono kwenda ndani huku baadhi ya wateja wakiwaangalia kwa macho pima!Waliingia ndani ya chumba hicho lakini Bitungu alipitiliza chooni na kumwacha Juliana amejitupa kitandani.

Ilikuwa katika hali ambayo hakuitarajia kabisa, Juliana aliona hereni chini kando ya kitanda. Hereni hiyo alivyokumbuka ni moja ya hereni alizomnunulia mama yake miezi miwili nyuma.
"Mh!" aliguna Juliana huku akiiokota. Akajiuliza…"Au mama alipokuwa huku Sinza aliingia hapa nini?"
Lakini alipata wazo kwamba asiichukue, aiache palepale chini ili aone kitakachotokea kama Bitungu ataiona.

Bitungu alitoka chooni kwa kujiamini sana, akakaa kitandani. Lakini na yeye jicho lake likatua moja kwa moja kwenye ile hereni ambapo alionekana kushtuka sana.Kama vile haitoshi, kwa sababu Juliana alilala, yeye alikaa, aliinuka na kuifuata kiaina huku akikumbuka…

"Hii hereni si ndiyo alisema yule mama kwamba ameipoteza, kumbe iliangukia hapa?"
Wakati anaifuata hereni hiyo, Juliana alimwona, akashtuka zaidi kwani sasa alijiridhisha kwamba alichokifikiria ndicho."Lakini huyu si alikuja kuchukua chumba sasa hivi, sasa hereni inamhusu nini? Au na yeye anashangaa kuona hereni ndani ya chumba?" aliwaza Juliana akakaa mkao wa kusubiria atakachosema Bitungu lakini hakikuwepo.

Ghafla Juliana alikosa amani ndani ya moyo wake. Alianza kuingiwa na wasiwasi na hofu ya mambo mengi akivuta matukio kadhaa ya nyuma."Inawezekana mama anatembea na Bitungu? Hilo haliwezekani hata kidogo, yaani Bitungu alale na mimi na mama yangu?"

"Baby vipi?" Bitungu alimuuliza Juliana huku na yeye akipanda kitandani. Juliana alipoitika poa, aliinuka kitandani kiaina na kuangalia ile sehemu aliyoiona hereni, haikuwepo!"Mh!" aligunia moyoni Juliana, alikosa nguvu na raha.

"Baby, mbona kama umekosa raha ghafla?" aliuliza Bitungu akijipendekeza kwa kumshikashika Juliana sehemu mbalimbali za mwili wake."Usinishike bwana, nini?" alikuja juu Juliana. Ni kweli alikosa raha kwani asingeweza kusema maneno hayo kama angekuwa na amani…
"Ha! Ina maana yamekuwa hayo leo mpenzi wangu?" aliuliza Bitungu…
"Ndiyo ee..."

"Kosa langu ni nini..?"
"Unalijua mwenyewe."
Bitungu alijaribu kujiongeza akiamini anaweza kupata mwanga au jibu lakini wapi! Hakuona kosa lake.
Mara, mlango uligongwa na mhudumu, Bitungu akaenda kufungua…
"Samahani kaka, kumbe ni wewe, nilifikiri kaingia mtu mwingine."
 
NI SHIIDA!-8

ILIPOISHIA
Bitungu alijaribu kujiongeza akiamini anaweza kupata mwanga au jibu lakini wapi! Hakuona kosa lake.
Mara, mlango uligongwa na mhudumu, Bitungu akaenda kufungua…
"Samahani kaka, kumbe ni wewe, nilifikiri kaingia mtu mwingine."
JIACHIE MWENYEWE SASA…


"Ni mimi?"
"Lakini ulitoka umerudi tena?" aliuliza mhudumu swali ambalo lilimshtua Juliana pale kitandani.
"Mh! Ina maana kumbe Bitungu alikuwemo humu ndani? Mbona mimi aliniambia anakuja kutafuta chumba alipokipata ndiyo akaniita tuje?" alijiuliza Juliana.

Bitungu hakujibu swali la mhudumu huyo badala yake alifunga mlango tu na kurudi kitandani…
"Baby," aliita Juliana…
"Yes baby…"

"Kumbe ulikuwemo humu ndani?"
"Hapana, amejichanganya yule."
"Mm! atajichanganyaje bwana, we ulikuwemo humu na uniambie ukweli ulikuwa na nani?"
"Baby, mimi sikuwemo humu ndani ya chumba, yule amejichanganya tu, naomba unielewe."
"Hamna bwana, mimi tayari kuna mambo yameniambia ulikuwemo."

"Mambo kama yapi?"
"Wewe unajua mwenyewe."
"Khaa! Mimi sijui mbona."
"Basi yaishe," alisema Juliana na kumfanya Bitungu ajisikie vibaya zaidi kwani na yeye alianza kuhisi kwamba ile hereni aliyoiokota ya mama Juliana ilishaonwa na mrembo huyo ndiyo maana amepoteza furaha kwa ghafla kuliko alivyoingia…

"Yaishije baby wakati najua kwako bado?"
"Yaishe tu! Halafu leo mimi tumbo linaniuma kwelikweli, wala sijisikii kufanya kitu chochote kile," alisema Juliana kauli iliyompotezea dira Bitungu kwani alishajitiuni kwamba anakwenda kushinda mechi ya siku hiyo.

Bitungu ili ajue kama madai ya Juliana ni ya kweli au alitaka kutingisha kiberiti tu, alijifanya kuanza kumshikashika Juliana sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimchombezea kwa maneno matamu sana yenye kuchochea mahaba niue!

"Nimesema leo sijisikii kufanya chochote kile si nilishasema mapema lakini baby?"
"Aaa! Juliana, usinifanyie hivyo mimi."
"Mimi sijakufanyia baya lolote lile…"
"Ila..?"
"Basi tu."

"Sasa ikiwa ni hivyo tutafika mbali kweli baby wangu?"
"Hatuwezi," alisema Juliana kwa sauti iliyoendelea kuonesha kuwa, hakuwa sawa kichwani mwake.
Jitihada zote za kutaka kushinda mechi na Juliana ziligonga mwamba kwani mrembo huyo hakuwa tayari kwa njia yoyote ile."Bitungu," aliita Juliana kwa sauti iliyojaa utulivu wa hali ya juu…
"Yes."

"Una uhusiano na nani?"
"Mimi?"
"Wewe ndiyo, mwingine nani?"
"Sina."
"Si kweli. Ile hereni ilikuwa pale iko wapi?"
"Hereni gani?"
"Pale chini palikuwa na hereni sasa hivi haipo, we umeiokota. Na ndiyo nathibitisha kwamba kweli wewe ulikuwemo ndani."

"Hapana, siijui mbona."
"Nikupapase?"Bitungu hakutaka kupapaswa kwani ni kweli aliiweka hereni hiyo kwenye mfuko wa bukta.
"Ina maana huniamini baby?"
"Ndiyo sikuamini. Tena kuna kitu nafuatilia kama ni kweli mimi na wewe basi."
"Kitu gani tena baby jamani?"
"Nakijua mwenyewe."
***
Mama Juliana alihisi dakika zinakatika binti yake hajarudi, akampigia simu.
Juliana alishtuka sana kuona simu ya mama yake ikiingia kwenye simu yake…
"Huyo ni mama, please naomba subiri kwanza kufanya lolote lile kwa sasa," alisema Juliana ili apokee simu hiyo…

"Mama…"
"Uko wapi wewe?"
Ili ajulikane yupo njiani anatembea, Juliana aliwahi kwenye dirisha na kuongelea hapo ili kelele za nje ya gesti hiyo ziingie kwenye simu na kumfikia mama yake…
"Mama natembea nakuja."
"Na huyo Bitte?"

"Hapana mama, nimemkuta ana kazi nyingi sana lakini atakuja kesho asubuhi sana."
Mama alikata simu, Juliana akamgeukia Bitungu…
"Naomba hiyo hereni Bitungu please."
"Yaani dear hayajaisha tu?"

"Hayawezi kwisha labda uamue kuwa wazi kwangu kuhusu mwanamke aliyekuwemo ndani na uhusiano wake na hiyo hereni uliyoiokota."
"Sikia nikwambie ukweli baby wangu…"
"Nakusikiliza."

"Ni kweli nilikuwa na mwanamke kabla yako. Lakini ni yule mke wa mtu niliyewahi kukwambia kwamba ananing'ang'ania mimi simtaki."
"Ulikuwa naye humu ndani ya chumba hiki?"
"Ndiyo."

"Mnafanya nini?"
"Yeye alichukua hiki chumba, akaniita akisema anataka kunipa kazi nimfanyie ili anipe pesa lakini si suala la mapenzi."

"Amekupa hiyo kazi?"
"Ndiyo.""Kwanza huyo mwanamke anaitwa nani?"

Itaendele baadayeee.......
 
Hadithi lazima iwe ndefu kwani inazungumzia mlolongo wa matukio
Hadithi ni nzuri sana na inaenda haraka kwa mpangilio na huenda ikawa fupi
zipo Hadithi nyingine humu JF haziendi kabisa yaana mwandishi mpaka akaendelee na shughuli zake akute Post za kumsifia zimejaa ndio anaenelea? daud1 umejitahidi lakini naomba Hadithi hii (Mkasa wa huyu Mama Juliana na mwanae Julie) uwe unaziendeleza katika Post yako # 1 hapo juu huku chini tuachie sisi wachangiaji
Mapumziko mema ya j2
 
Last edited by a moderator:
Hadithi ni nzuri sana na inaenda haraka kwa mpangilio na huenda ikawa fupi
zipo Hadithi nyingine humu JF haziendi kabisa yaana mwandishi mpaka akaendelee na shughuli zake akute Post za kumsifia zimejaa ndio anaenelea? daud1 umejitahidi lakini naomba Hadithi hii (Mkasa wa huyu Mama Juliana na mwanae Julie) uwe unaziendeleza katika Post yako # 1 hapo juu huku chini tuachie sisi wachangiaji
Mapumziko mema ya j2
Tuko pamoja mkuu utapata uhondo mpaka mwisho
 
Dah michepuko hadi inatisha...Bitungu anakula kuku na mayai yake ila mama na mwana wote wameshajihisi...patamu sana hapo. Nitag/mention mkuu Daudi1 ikiendelea
 
Last edited by a moderator:
Tuko pamoja mkuu utapata uhondo mpaka mwisho
Haya Mkuu tunakisubiri hicho Kijogoo (Bitungu) maana kinakamua au kukamuliwa mm sipati picha
saa hizi naona umeweka Pause au DVD imekwama huko Guest Julie ataangusha makofi au kilio
mm sitoki hapa kwenye hii thread wacha wakombe MB zao nitaweka GB nikusome haswa!!!!
 
Haya Mkuu tunakisubiri hicho Kijogoo (Bitungu) maana kinakamua au kukamuliwa mm sipati picha
saa hizi naona umeweka Pause au DVD imekwama huko Guest Julie ataangusha makofi au kilio
mm sitoki hapa kwenye hii thread wacha wakombe MB zao nitaweka GB nikusome haswa!!!!
Kaa mkao wa kula dk si nyingi naiendeleza
 
NI SHIIDA!-9

ILIPOISHIA
“Yeye alichukua hiki chumba, akaniita akisema anataka kunipa kazi nimfanyie ili anipe pesa lakini si suala la mapenzi.”
“Amekupa hiyo kazi?”
“Ndiyo.”
“Kwanza huyo mwanamke anaitwa nani?”
JIONGEZE…

“Mh! Jina lake linanitokaga sana.”
“Kwa nini ushindwe kumjua mtu anayekufuatafuata kila wakati mpaka mnaitana gesti?”
“Imetokea tu.”
“Anaishi wapi?”

“Mwenyewe anasemaga Ilala.”
Moyo ulimlipuka Juliana, alianza kuuona ukaribu wa mama yake kutembea na Bitungu. Alitamani sana kumuuliza lakini alishindwa, akaendelea kutumia maswali ili kumchimba kwa undani.
“Umewahi kufika nyumbani kwake?”
“Sijawahi.”
“Ni Ilala gani?”
“Sijui Ilala gani!”
“Yukoje?”

“Mwanamke f’lani hivi hajatulia ndiyo maana mimi namkataa maana najua nitaangukia pabaya.”
“Ameolewa?”
“Hapana, shangingi tu,” alijibu Bitungu kwa kukwepesha ukweli kwani alijua akikubali kwamba ameolewa, ataonekana anacheza na hatari kwa wake za watu lakini hakujua kama jibu hilo lilipunguza kiwango cha mawazo cha Juliana kutaka kumhusisha mama yake.
“Kwa hiyo humu chumbani ulikuwa na huyo mwanamke wako?”
“Ndiyo.”

“Umesema ndiye aliyekodi chumba?”
“Yes baby.”
“Kwa hiyo mimi umeniingiza kwenye chumba alichochukua mwanamke mwenzangu siyo?”
“Juliana, punguza hasira mama, punguza maswali pia, usimuwazie sana huyo malaya, wewe shughulika na mimi tu, mimi ni mumeo mtarajiwa Juliana, mtoto mzuri kama wewe unataka kujilinganisha na mwanamke mtu mzima, mzee yule.”

Maneno hayo yalimpa faraja kubwa Juliana, akajijua tena kwamba kumbe yeye ni mzuri sana na anapendwa pia kumbe anaweza kuwa mke wa mtu ndoto ambazo zimekuwa zikimkaa kichwani muda mrefu kwamba atafurahi sana siku moja atakapobahatika kuolewa na kuwa nyumbani kwake.
Kwa mbali, Juliana alianza kuchangamka huku akipeleka mkono wake kumshikashika mwilini kijana huyo na kuachia tabasamu, akasema…

“Lakini ujue baby mimi ni msichana mwenye wivu mkubwa. Kwa hiyo uwe unaangalia unapotaka kunitenda kwani utakuwa unaniumiza sana.”

“Miye wala sikutendi mpenzi wangu, unajua kama ningekuwa na nia mbaya nisingekuita uje hapa.”
Bitungu naye baada ya kumwona Juliana amelegeza uzi aliitumia nafasi hiyohiyo kuhakikisha wanaangukia kitandani na kuanza mechi ya haraka maana dakika zilikuwa zimekatika sana.
“Jamani, nitalala mwenyewe,” alisema Juliana wakati akipelekwa kitandani…
“Si nakusaidia tu baby wangu jamani na wewe!”

“Nitajisaidia mwenyewe jamani sweet,” alilalamika Juliana kwa sauti isiyokuwa na msisitizo, akaenda kitandani na kuangukia puu!

Macho yalishamlegea, sehemu kubwa ya mwili wake ikawa kitandani huku akianza kuongeza mhemo na mhemko wake. Hali ilikuwa mbaya kwa Juliana…
“Baby njoo basi, si umenitanguliza mwenyewe,” alisema Juliana kwa sauti tamu, sauti nzuri, sauti ya kumtoa mwanajeshi kwenye handaki.

Juliana huyohuyo alimvuta Bitungu kitandani na kuanza kumvua bila kujali tabu zake. Bitungu naye alikuwa akijipindapinda, akijinyonganyonga ili kuruhusu nguo zake kutoka mwilini wakati wa kuvuliwa.
Wote wakawa kama walivyozaliwa, Juliana alimwangalia Bitungu kwa macho malegevu sana, kusinzia si kusinzia, kulala si kulala…
”Baby,” akaita…
“Yes dear.”

“Nakupenda,” alisema Juliana kwa sauti iliyotoka nje kwa kupitia tundu za pua…
“Hata mimi baby nakupenda pia.”
“Kweli baby?” aliuliza Juliana akipeleka mkono na kushika maiki ambapo alianza kuimba nyimbo nzuri za mapenzi huku macho yake yakimwangalia Bitungu usoni hali iliyomchanganya kijana huyo na kujikuta akitetemeka kwa kiu ya kulisataka kabumbu.
“Baby,” aliita tena Juliana…
“Yes…”

“Mimi tayari.”
“Tayari nini sweet wangu?”
“Aaah! Bwana, unajua namaanisha nini!”
Bitungu alimtega vizuri Juliana na kuanza naye soka huku akitembeza mikiki ya mbali na kumfanya Juliana kuhema sana na kutoa mlio wa kubembeleza kwa mbali.

Kitu kimoja ambacho alikisahau Juliana ni kuacha simu yake palepale kitandani hivyo akailalia. Sasa wakati makasheshe yakiendelea, aliiminya na mgongo, akajikuta anabonyeza vitufe mpaka akafika eneo la namba ya mama yake ambayo alimpigia yeye kwenye ‘received call’.
Mama Juliana aliipokea haraka simu ya binti yake akijua huenda kuna tatizo kwani walishatoka kuongea muda mfupi tu uliopita…

“Huyu anasemaje tena?” alijiuliza mwenyewe akiwa anaipokea bila kujua kwamba upande wa Juliana, simu hiyo ilijipiga yenyewe.
“Haloo…” alipokea na kuita…
“Haloo…”
“Halooo…wee Juliana!”
Mama Juliana alishtuka wakati akiita kwenye simu, upande wa pili alisikia maneno haya…
“Baby…baby jamani…oooo….baby…”
Alisimama…

“Wewe Juliana…”
CC: Ukwaju
 
NI SHIIDA!-10

ILIPOISHIA
"Haloo... wee Juliana!"
Mama Juliana alishtuka wakati akiita kwenye simu, upande wa pili alisikia maneno haya...
"Baby...baby jamani... oooo...baby..."
Alisimama...
"Wee Juliana..."
SONGA NAYO SASA...

"Juliana si naongea na wewe?"
"Halooo..."
Alihisi presha ya ajabu kumtembelea, hakutaka kuamini kile alichokuwa akiendelea kukisikia kwenye simu.
Muda wote Bitungu na Juliana bado walikuwa katika mechi ngumu, mechi ilikuwa imeshawazidia kwani tayari walikuwa wamefungana mabao ya kutosha na wapo katika mapumziko ya kipindi cha pili.

Juliana hakushtuka kama ile simu ilikuwa imempigia mama yake, ndiyo kwanza aliendeleza mahaba kwa Bitungu.
"Baby..."

"Sema mpenzi wangu..."
"Tupumzike tuendelee basii, ila leo umeniweza kweli!"
"Tena una bahati leo!"
"Bahati? Bahati wapi wakati kawaida yangu kumaliza mechi na ushindi."

Wakiwa katikati ya maongezi, Bitungu akaiona simu kwa Juliana, simu ambayo Juliana alikuwa ameikalia bila kujitambua kuwa imejipiga na mbaya zaidi imempigia mama yake.
"Mpenzi mbona umeikalia simu..."
"Simu? Simu ipi?"

"Ina maana huijui simu yako, au si ya kwako hiyo?"
Harakaharaka Juliana alijisogeza na kuichukuwa ile simu yake, ilikuwa bado iko hewani kwani maneno yote mama yake alikuwa bado anaendelea kuyasikia. Juliana akaanza kutetemeka sambamba na kuumana meno. Akaikata simu ile na kuanza kuangua kilio kana kwamba yupo msibani.
"Nini tena sweet?"
"Hapana..."

"Hapana nini?
"Niache kwanza, niache tu..."
"Siwezi kukuacha sweet wangu wakati umeiangalia simu yako na kuanza kulia kama ni msiba nijuze kuliko kupeana presha..."
"Bora ingekuwa msiba Bitungu..."

"Ila! Nini sasa kinachokufanya uendelee kulia tena kwa sauti ya juu hapa na unajua hapa ni gesti?"
"Bitungu, yale yote tuliyokuwa tunafanya na kuongea mama ameyasikia!"
"Unasemaje?"
"Mama ameyasikia yote!"

"Sweet ina maana hukuweka loki kwenye simu yako?"
"Hapana! Wakati tupo kwenye mechi simu yangu ilijipiga yenyewe bila kujua, mama akapokea na kusikiliza yote..."
"Kwa hiyo ndo ameshajua kila kitu.."
"Ndiyo amesikia Bitungu!"

"Ahhh! Haiwezekani sweet, mama yako amesikia kila kitu?"
Bitungu alihisi kuwa mdogo kama piritoni, bado alikuwa mtupu kama alivyozaliwa, mzuka wote wa kuendelea na mechi ukawa umekwisha rasmi, alichokifanya alitupa shuka upande wa pili huku ghadhabu ya hali ya juu ikiendelea kumtoka...
"Lakini..."

"Lakini nini niache kwanza Bitungu..."
"Unatakiwa kwanza tuyazungumze na kupanga jinsi ya kumwambia mama yako..."
"Bitungu unajua kabisa kitumbua kimeshaingia mchanga hapa na hakuna cha kukipangusa, ni bora kiliwe hivyohivyo tu!"

"Una maana gani Sweet?"
"Mambo yameshaharibika hapa, si salama tena!"
"Ngoja, ngoja! Tuliza kwanza jazba."
"Hapana Bitungu... hapana!"

Juliana alikuwa hataki kusikia lolote, ile raha ya mechi iliyokuwa imemtembelea aliona kama moto, moto tena ule wa kuni. Alitamani ardhi ipasuke atumbukie pengine angefarijika.

Alichokifanya, alichukua nguo zake zote na kuanza kuvaa moja baada ya nyingine huku akiendelea kulia kwa sauti ya juu iliyochanganyika na kwikwi. Muda wote Bitungu alikuwa akimtazama tu pasipo kumsogelea karibu, alishajiona ni mkosaji wa hali ya juu kwa kuwachanganya.

Ndani ya muda mfupi, Juliana alikuwa ameshamaliza kuvaa nguo, kitendo cha kuweka nywele zake sawa, mara simu yake ikaita tena."Ona sasa! Mama anapiga simu tena!"
"Sasa?"

"Sasa nini? Ndiyo hivyo anapiga tena..."
"Cha kufanya simu yake usipokee iache kama ilivyo..."
"Hapana Bitungu ni bora nipokee pengine hasira zake zitakwisha maana namjua mama yangu kwa hasira!"

"Juliana! Juliana nisikilize kwanza ninavyokwambia!"
Juliana alitii yale aliyokuwa ameambiwa na Bitungu, hakuipokea ile simu ya mama yake, aliiacha ikaita hadi ikakata yenyewe. Alitoka nje ya ile gesti na kuongoza moja kwa moja nyumbani kwao huku akimwacha Bitungu akimalizia kuvaa nguo mule ndani. Hakuwa Juliana wa kawaida kwa jinsi alivyokuwa amechanganyikiwa akili mpaka mwili.

Muda wote Mama Juliana alikuwa ametulia nje ya kibaraza amefura kwa hasira akimsubiri Juliana, alishaujua mchezo wote aliokuwa anachezewa. Kitendo cha kuonana uso kwa uso na Juliana hasira zikamzidia.
"Juliana?"

"Abee mama! Shikamooo!"
"Sitaki shikamooo yako!"
"Niambie ulikuwa wapi?"

"Mama nisamehe nilikuwa..."
Kabla Juliana hajamalizia kujibu alishangaa kupigwa vibao mfululizo kutoka kwa mama yake.
"Usifikiri sijui chochote, najua kila kitu, niambie ukweli ni nani ulikuwa naye gesti..."
 
Back
Top Bottom