Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 15,234
- 24,661
- Thread starter
- #21
NI SHIIDA!-11
ILIPOISHIA
"Abee mama! Shikamooo!"
"Sitaki shikamooo yako!"
"Niambie ulikuwa wapi?"
"Mama nisamehe nilikuwa..."
Kabla Juliana hajamalizia kujibu alishangaa kupigwa vibao mfululizo kutoka kwa mama yake.
"Usifikiri sijui chochote, najua kila kitu, niambie ukweli ni nani ulikuwa naye gesti..."
PAA NAYO SASA...
Kifupi ni kwamba, mama Juliana alimsikia mwanaume akizungumza lakini hakujua kama ni Bitungu, ila kilichomshangaza sana ni kubaini kumbe binti yake ameanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume.
"Mama nisamehe."
"Niko tayari kukusamehe, niambie ulikuwa na nani?"
"Nilikuwa na kijana mmoja hivi."
"Anaitwa nani? Hana jina?"
"Mama mi simjui jina lake."
"Wee, koma kama ulivyokoma kunyonya kwenye ziwa langu, uingie na mwanaume gesti halafu uwe humjui jina?"
Juliana aliamua kumdanganya mama yake akiamini si vizuri kumtaja jina Bitungu...
"Anaitwa Sylvester."
"Anaishi wapi?"
"Kigamboni."
"Mmeanza uhusiani tangu lini?"
"Siku ya tatu leo."
"Umeshalala naye mara ngapi?"
"Mara ya kwanza leo."
"Ina maana amekutoa usichana wako?"
"Hakuweza mama."
"Kwa sababu gani asiweze?"
"Hakuweza tu."
"Unataka nikukague?"
"Hapana mama."
"Sasa kwa nini unanidanganya?"
"Sikudanganyi mama."
"Kwanza hebu niambie, hiyo gesti iko wapi?"
"Ipo Sinza."
"Ipo Sinza? Ina maana wewe hapo muda huu unatokea Sinza?"
"Ndiyo mama."
"Sinza sehemu gani?"
"Mimi siyo mwenyeji sana wa Sinza mama," alijibu Juliana bila kujua kuwa, mama yake alitaka kujua Sinza sehemu gani kwa sababu na yeye alitoka huko muda si mrefu....
"Shekilango unapajua?"
"Ndiyo mama."
"Ukitoka Shekilango ni kituo cha ngapi?"
"Sikumbuki, nilikwenda na bodaboda."
"Hebu nenda ndani haraka sana. Usije ukarudia tena," alisema mama Juliana huku akiiseti simu yake vizuri ili kumtwangia Bitungu. Lakini huku akiwaza...
"Isije ikawa alikuwa na Bitungu! Halafu isijekuwa Bitungu ndiyo yule Bitu wa kwenye simu yake akasema ni Bitte alikosea kusevu? Huyu mtoto isije ikawa anatuchanganya mimi na mwanangu?
"Lakini haiwezekani. Kwa mechi tuliyoicheza leo pale kitandani sidhani kama angeweza kumudu mchezo mwingine tena."
Simu ya Bitungu ilipokelewa, mama Juliana akaanza kumuuliza maswali...
"Baby, wewe ni msaliti kwangu siyo?"
"Wala, kwa nini baby?"
"Huna mpenzi mwingine kweli wewe?"
"Wala! Nani amekwambia?"
"Sijaambiwa na mtu, nawaza mwenyewe tu."
"Ondoa hayo mawazo mpenzi, mimi ni wako peke yako."
"Kweli mpenzi wangu?"
"Kabisa mpenzi."
"Basi nimefurahi sana kusikia hivyo," alisema mama Bitungu na kukata simu. Roho yake ikawa imefarijika kwa siku hiyo.
***
Asubuhi ya siku iliyofuata, Juliana aliamka akiwa na wogawoga wa kuonana na mama yake ana kwa ana. Lakini alipokumbuka kuhusu ile hereni aliyoiona gesti akiwa na Bitungu ambayo ni moja kati ya hereni alizomnunulia mama yake, aliamua kuanza upelelezi wake hapo.
Kwanza alimvizia mama yake amekwenda kuoga, yeye akazama chumbani maana baba yake naye alishakwenda kazini mapema.
Alifungua kwenye kikopo ambacho mama yake anakitumia kuwekea hereni zake, hakuona hereni hata moja. Akaangalia juu ya dressing table, akaiona hereni moja tu, akatingisha kichwa huku akisema moyoni...
"Ile niliyoiona gesti hii mwenzake, kwa vyovyote vile. Ina maana mama ndiye mwanamke aliyekuwa na Bitungu gesti...itakuwa yeye na ndiyo maana alinibana kuhusu Sinza sehemu gani niliyokuwepo mimi," alisema moyoni Juliana huku akichomoka kutoka chumbani humo.
Aliendelea na mambo yake mengine lakini kuanzia muda huo akawa hamwogopi tena mama yake kufuatia kubaini uozo wake na Bitungu.
Jiliana alianza kufanya utafiti wake kwa kutumia akili ya kujiongeza. Aliamua kwamba siku mama yake akitoka na yeye atoke, amfuate kwa nyuma kwa siri mpaka atakapoingia na yeye aingie.
Lakini pia aliamua kuendelea na uhusiano na Bitungu akiamini kwamba, atatumia akili yake ya ziada ili kijana huyo ammwage mama yake.