DOKEZO Siku dereva akishindwa kulimudu gari hapa Mbezi barabara ya stendi ya Malamba itakuwa kilio kikubwa sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Hapa Mbezi Luis Stendi barabara ya kwenda Kinyerezi ilivyojaa msongamano wa machinga na bidhaa zao ambazo ziko kando ya barabara na kusababisha barabara kuzidi kuwa finyu licha ya wembamba wake tangu kutengenezwa, siku dereva yoyote akishindwa kulimudu gari likaenda pembeni litaua watu wengi sana.

Tena si machinga pekee bali hata wapita njia na wanunuzi, maana hali ilivyo ni msongamano wa watu barabarani kutokana na kukosa njia ya kupita maana njia zote za watembea kwa miguu zimezibwa na machinga na kulazimika watu kupita barabara kuu kama magari ivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kugonjwa na gari, bajaji, bodaboda na wao wenyewe kugongana kwa kuwa wanapita kwa kulazimisha huku wakikwepa magari.

Wafanyabiashara wa hapa wamejimilikisha eneo la barabara na la watembea kwa miguu huku wakiwa hawana wasiwasi wa kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kukaa barabara, wengine wameweka ndoo na kuzikalia huku wakiipa mgongo barabara hali ya kuwa wapo pembezoni mwa barabara na magari na vyombo vingine vya usafiri vikipita na wala hawajali wao huendelea kuuza bidhaa zao ambazo wameziweka kwenye kinjia kilichokuwa kimeachwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Sijui mamlaka ziko usingizini au eneo hili hakuna viongozi wanaoweza kuona hatari kabla haijatokea na wakachukua hatua ya kudhibiti kabla ya majanga husika. Narudia tena siku ikitokea gari ikachochora hapo ni balaa tutabaki kulaumu wakati tungeweza kuzuia hali hiyo.

Hao machinga kama wameshindikana kuondolewa kama ambavyo mwanzo walikuwa wakitolewa basi wawekewe namna nzuri ya kukaa, wasikae barabarani, wasizuie njia za watembea kwa miguu ili kuepuka hatari ambayo inaweza kuepukika.

1690512132794.png

 
Back
Top Bottom