Barabara ya Mbezi Chini (Barabara ya Mwaikibaki) ni hatari kwa watembea kwa miguu, mpaka itokee ajali mbaya ndio ifanyiwe kazi?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema? Niende moja kwa moja kwenye mada.

Barabara hii mbali na kuwa ni kero kwa watembea kwa miguu lakini pia ni hatari sana kwa usalama wao.

Kwanza hakuna njia kwaajili ya watembea kwa miguu, halafu maajabu ni kwamba kuna vivuko kwaajili ya watembea kwa miguu. Sasa unaweka vivuko kwaajili ya watembea kwa miguu vya nini wakati hakuna njia kwaajili yao? Mtu anakuwa ndani ya barabara muda wote akiwa anatembea pembeni kiasi kwamba gari likiyumba kidogo tu umeisha.


Video hii ni maeneo ilipo KFC na Pizza Hut, ambako kama unatokea Kawe, hapa hakuna zebra ya kwaajili ya kuvukia, ili uweze kupata zebra inabidi uvuke barabara inayoenda Shoppaz usogee mbele ndio ukutanae na zebra? Kwanini?

Yaani kuvuka hapo ni shida hata kwa mtu mzima sasa fikiria kwa mtoto anayekwenda shule. Bodaboda zenyewe zinaogopa kuvuka.

Wakati wa asubuhi na jioni hatari inaongezeka, madereva wengi hawafuati sheria kabisa, na hivi huwa hakuna askari watu wanafanya watakavyo tu kama unavyoona kwenye video. Hapo ilikuwa majira ya asubuhi, wanaotoka Mbezi wanajikuta ndio wana haraka sana wao ni kutanua tu.

Sasa unahangaika hakuna zebra, lakini wakati huo huo ni kama umesimama barabarani hivyo inabidi uwe makini ili usije kugongwa, bado tena uongeze umakini usije kugongwa na madereva wanaotanua, kweli jamani?

Hivi, na mpango wa kuanzisha ruti ya daladala kwenye njia hii uliishia wapi?

Ni mpaka litokee tukio wananchi wachome gari ama kituo cha polisi karibu ndio suala hili lifanyiwe kazi?

Mamlaka angalieni barabara hii kwa jicho la tatu kabla halijatikokea la kutokea.


 
Back
Top Bottom