Serikali inatakiwa kujenga vivuko vya juu kwa ajili ya wavuka kwa miguu barabara ya Morogoro (Kimara-Mbezi)

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Hii barabara ni muhimu sana kwasababu inayotumiwa sana kuingia na kutoka Dar es Salaam, ni barabara ambayo iko busy muda wote ikipitisha magari ya kutosha huku pia watembea kwa miguu nao wakiwa wengi sana.

Mara chache sana huwa natumia hii barabara nikiwa na gari binafsi au gari la umma, huwa naona adha inayotokea pale watembea kwa miguu wanapotaka kuvuka barabara. Kwakweli baadhi ya vivuko siyo salama kabisa jambo linalohatarisha usalama wao.

Hasa vivuko vilivyo karibu na vituo vya daladala naona serikali ingefanya namna kuweza kujenga vivuko vya juu ili kuokoa maisha ya wanaotumia barabara hiyo.

Nchi zinazojielewa zikiwa zinajenga miundombinu huwa zinazingatia maeneo kama haya ambayo yana wingi wa watu wanaotakiwa kuvuka barabara, Tanzania bado hatujachelewa tunaweza kufanya namna ili kupunguza ajali nchini.

Ni hayo tu.

Wavuka Miguu.JPG

Pich kutoka mtandaoni​
 
Vivuko viwe underground

Vivuko vya juu walemavu na wazee

Watapata shida

Ova
 
Back
Top Bottom