Sikilizeni CHADEMA hakuna aliewakataza kushiriki katika michezo

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Friends and our Weak Enemies,

Husikeni na kichwa Cha habari hapo juu.

Siasa za Afrika ni Kwa waafrika, demokrasia ya waafrika ni Kwa waafrika, hawezi kuja muarabu,au muhindi,au mzungu eti aje aseme siasa zetu sisi au demokrasia yetu sisi ifanane na wao la hasha,na ndiyo Kwa maana unaona nchi za jiran watawala ambao wamefeli kisiasa jeshi linachukua nchi au wengine wanaangukia kwenye machafuko baada ya uchaguzi na kadhalika.

Tukirudi kwenye kichwa Cha habari,hivi niwaulize chadema na vyama vingine,wanawaona CCM ni wapuuzi au wajinga jinsi wanavyojiweka karibu na hizi Team mbili kubwa ndan ya nchi hii,au CCM wanavyojiweka karibu na michezo mingine hawa hawaoni kuwa ni karata dume ambayo inawamaliza?

Sikilizeni chadema hakuna aliewakataza kushiriki katika michezo,na Wala siyo mwiko au dhambi nyinyi kujiunga Jukwaa Moja la michezo ambapo pia CCM anaonekana amejiunga kwenye majukwaa hayo,ni sehemu ambayo nyinyi mngepata Nafas atleast ya kujumuika na wanachama wenu, siasa za harakati na chuki na kauli za hovyo hovyo zimepitwa na wakati.

I heard kwamba Mbowe ni Simba,but angejifunza basi hata Kwa mwenzake Zitto kabwe ambae atleast anaonekana na kujihusisha na michezo na kadhalika.

Kwa Ujinga wao na kutotumia Fursa kama hizo watazidi kulia Kila siku kuwa CCM imegoma kutoka madarakini,kumbe ni wao wenyewe wamedumaa katika ulingo wa siasa.

Na Mbowe,unataka kuwa mwenyekiti hapo chadema hadi umauti ukukute??unaacha legacy ya aina Gani hapo,why wenzako kina Mtei na Bob Makani walithubutu kuachia ngazi Nini unachoshindwa kumtengeneza Mrithi wako??unakuwa kama Mugabe??
 
Fursa kwa mjinga aliyeshindwa kujibu hoja za watanganyika kuhusu ule mkataba wa hovyo wa bandari, badala yake akaamua kuwazibia masikio.

Sasa ndio ameamua kujitokeza mbele za watu kama pambo, akiwa amejipaka make up na wanja, anaenda kujichekesha pale uwanjani akijidanganya harakati za kukomboa bandari zetu zitaishia pale, hajui akitoka uwanjani atakutana na moto ule ule.
 
Chadema hawako kwenye comfort zone, Chadema wana kazi kubwa ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa katiba na mambo mengi.

CCM hadi leo mmeshindwa kutoa huduma za kimsingi zilizo bora. Elimu duni, nchi haina maji safi na salama.

CCM ni chama kisichojali watu wake, kinawapumbaza kwa matamasha na burudani
Nakuunga mkono kwa 100%.

Ccm hawapo madarakani kwa manufaa ya wananchi bali ni kwa wao kuendelea kulinda maslahi yao
 
Back
Top Bottom