Kwenu wataalamu wa mambo ya siasa, je ilikuwa sahihi kamati ya mazishi ambayo inaongozwa na PM kuandaa historia ya hayati Lowasa bila kuhusisha kuhamia upinzani?
Mama alipokuja kuhutubia yeye binafsi hakutaja neno Chadema ila alihusisha historia ya Lowasa na upinzani kwa namna fulani ambapo alisema "Lowasa alihamia upande mwingine".
Pia, mama alikuwa anasoma hotuba yake. Sasa sijui alibadilisha upepo baada ya hotuba ya Mboye au alikuwa amedhamiria kuhusisha historia ya Lowasa kuhamia upinzani, anajua yeye!.
HABARI KAMILI
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hauwezi kuiandika historia ya waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, na ukaliacha neno CHADEMA.
Ameyasema hayo akitoa salamu baada ya maziko ya Lowasa yaliyofanyika leo tarehe 17-02-2024, kijijini Ngarashi wilayani Monduli mkoani Arusha.
"Rais nashindwa kujua niseme nini kuhusu Lowasa lakini niombe kwa sababu ya rekodi niweke kumbukumbu sahihi"
"Huwezi kuiandika historia ya Lowasa ukaliacha neno CHADEMA. Huwezi ni kujidanganya tu na kujaribu kuiua historia ambayo huwezi kuiua" Amesema Mboye.
Mbowe amesema ameisikiliza na kusoma historia ya Lowasa kama ilivyowasilishwa na kuongeza;
"Binafsi ni mtu mkweli na nimesikitika kwa sababu amefanya mambo makubwa ndani ya serikali, ndani ya CCM na vyama vya upinzani na katika taifa letu na taifa hili ni letu sote.
"Unawezaje kuandika historia ya Lowasa ukasahau utumishi wake wa miaka minne kama mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, mgombe wa urais wa mwaka 2015 ambaye alijenga demokrasia kwa viwango ambavyo haijawahi kufikiwa na mgombea yoyote wa upinzani katika taifa letu hili" Amesema Mboye.
"Wenzangu mtatambua Lowasa alianza safari ya matumaini ndani ya CCM baada ya hapo mimi siyazungumzi, na baadaye akahamia safari ya mabadiliko ndani ya CHADEMA. Huyu alileta kasi ya mabadiliko ya demokrasia ndani ya ncgi yetu" Amesema Mbowe.
Mbowe amesema pia "Lowasa alilifanya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na wabunge 115 kutoka vyama vinne vya upinzani. Hili linapaswa kuzungumzwa kwa sababu ni hatua ya ujenzi wa demokrasia katika katika taifa letu"
"Huyu kiongozi aliongoza uchaguzi na kuwezesha vyama vya upinzani kupata madiwani 2000 karibu nusu ya madiwani wa nchi"
"Vyama vingine tofauti na CCM vikaongoza jiji la Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Moshi, Mtwara, Iringa na Mbeya. Hampaswi kupuuza historia hii viongozi wangu. Tunatakiwa wakati wote tumuenzi Lowasa kwa sababu ni katika ujenzi wa demokrasia na ujenzi wa taifa letu zote" Amesema.
"Lowasa ni muathirika wa mifuno yetu ya uchaguzi lakini alikuwa mgombea wa upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita. Halikuwa jambo dogo, ni kwa sababu ya karama yake" Ameongeza Mboye.
Chanzo: Mwananchi