KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,679
- 4,835
Mbowe na CHADEMA wana lengo la kupeleka ujumbe duniani juu ya demokrasia ya Tanzania na watatumia maandamano kufikisha ujumbe huo.
Kwa kuwa CHADEMA kinakabiliwa na kutokukubalika na wananchi wa hapa nchini hivyo wanaamini wakifanya jambo litakalochochea vurugu na ikitumika nguvu kudhibiti lawama zitaiendea Serikali na hapo kutapelekea kuingilia Kwa mataifa makubwa ambayo yatahitaji kuwepo Kwa upatanishi kama kuanzishwa Serikali ya mseto ambalo litakuwa ni sharti la kuendelea kupata mikopo na misaada ya kigeni.
Nafikiri hiki ndicho Mbowe na CHADEMA wanalenga kifanyike hivyo basi kauli ya RC wa Dar es Salaam ya kusema Jeshi litakuwa linafanya usafi katika siku waliyopanga kufanya maandamano itakuwa imesaidia pakubwa utekelezaji na ufanikishaji wa mpango wao. Na hapa ujumbe ambao watafikisha ni kwamba Tanzania inatumia Jeshi kuzuia utekelezaji wa demokrasia.
Tukichora picha kubwa zaidi ya lengo la CHADEMA tutabaini yafuatayo:
Kwanza, CHADEMA wanaona demokrasia ni mzigo na hawawezi kuiondoa madarakani CCM Kwa sanduku la kura hivyo watatumia maandamano na migomo kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani ambayo itapelekea kuundwa Kwa Serikali ya mseto kama mahali pengine duniani ambalo Serikali za mseto zimeanzishwa Kwa njia kama hiyo.
Katika kukazia hiki ikimbukwe CHADEMA katika mkutano wa wadau wa kupendekeza Sheria za uchaguzi walipendekeza kuanzishwa utaratibu wa wabunge wawili Kwa Kila jibu jambo ambalo zaidi ya kuonesha tamaa na uchu wa madaraka lakini pia halioneshi nia njema kabisa.
Pili, CHADEMA wanajaribu kuichokonoa CCM ili iende na mdundo wake. Kujaribu kuyaponda maridhiano ambayo mpaka sasa yameonesha muafaka wa masuala mbalimbali ya kisiasa ni kujaribu kuifitinisha CCM na wananchi kwamba CCM ilibuni maridhiano bandia ili kuwamezeshea mate upinzani ,kitu ambacho sio kweli.
Hivyo basi mpaka sasa Mbowe anaamini kwamba 2025 wanaingia madarakani au kutakuwa na Serikali ya mseto kama mipango yao itakwenda ilivyopangwa na ninaamini maandamano ni Moja ya mipango yao.
Wito:
Binafsi Mimi sio muumini wa maandamano na anayefanya maandamano ninaamini anastahili kudhibitiwa Kwa nguvu zote ila Kwa maandamano ya 24/01/2024 tafadhali waachwe wafanye na ninaamini yakifanyika na wakapewa na ulinzi lengo la Mbowe litakuwa halijatimia na hapo watakuwa wamejiweka pabaya zaidi kisiasa.