Mimi nitoe haraka kwenye diva list ya wapenzi wako unaotaka kujadiliana nao!
Mimi nitoe haraka kwenye diva list ya wapenzi wako unaotaka kujadiliana nao!
Mimi sishiriki kwenye mijadala ambayo washiriki wana kinga!
Nataka kusikia mawazo ya kiumbe chochote na naweza ku face off na kiumbe chochote, na wala mimi sio mtaalam wa masuala ya Muungano na wewe sio, maana ungekuwa ndio usingeogopa mawazo wala kujijengea kiota cha kuji protect as if nyinyi ndio mna busara saaana kumbe ni kujenga club ya ma prima donna dhaifu ambao hawawezi kujichanganya bila kulindwa.
Unaalika "wanajamvi wote" halafu unatutajia wapenzi wako watano unaowataka kwenye mjadala. Could not be more ridiculous. Ni vema JF libaki kuwa jamvi huru, hao wapenzi wako watano watumie pm mkanywe chai pembeni huko!
Sikuona mahali pa kujibu kwasababu hoja zako hazina mantiki kwa uchache. Si kila hoja inajibiwa kwasababu nitajibu vipi matusi? Umesema mimi ni mpuuzi sasa hapo nijibu nini. Hata hivyo nakushukuru japo kwa kuandika.
Unaweza kuanzisha thread yako na si lazima nianzishe.
Najua hii nyuzi inawaudhi sana wzn lakini ndiyo habari ya mjini. Ukishaona matusi basi ujue hoja zimegota au kisu kimekula mfupa.
Waziri wa miundo mbinu wa Znz amejitokeza na kusema atalitolea ufafanunuzi suala hili.
Ameona wapi alipokosea, aheri basi kuliko wavurumisha matusi.
Kitu kimoja uelewe, nipo hapa kusimamia ninachokiamini kuwa ni sahihi kwa mtazamo wangu, nitakuambia ninachokusudia si kile unachotaka kusikia.
Mkiambiwa ukweli mtu ana chuki. Leo Mzaninzibar anakubali kuitwa Mtanzania!! ama kweli mumeshikwa pabaya.Lipo la tusi kwa kuambiwa kuwa unakuwa na chuki kwa masuwala ya Zanzibar? Unataka tukupembejee kwa mambo yasiyo na mantiki bali kuendeleza chuki kwa pande mbili sasa kama si upuuzi ni nini? unafikiri upuuzi ni matusi, la si matusi bali ni marejeo ya lugha isiyostahiki kusemwa na Mtanzania dhidi ya Mtanzania mwegine.
Nimesema uanzishe thread nyengine kwani wewe ni expert juu ya kuikashifu Zanzibar na elewa maadam tuna uhuru wa kutowa mawazo yetu tutakujibu kwa jinsi ile ile unayokuja nayo. Lete mjadala wa kujenga ili tujenge!
Hasara ya ku compromise on a principle, principle of open-sourced forum, na kushindwa kutumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe, kwamba, kualika "wanajamvi wote" kwenye mjadala halafu unatutajia majina matano ya unaowapenda ndio waje wachangie ni unafiki, moja, la pili, hasara ya kupunguza wigo wa mawazo yanayoweza kuletwa jamvini kuhusu Muungano kwa kualika wapenzi wako wachache.Yaani yote haya kwa sababu tu amekutaka na wewe uone alichoandika! Ungejikalia kimya ungepata hasara gani?
Hee ndugu yangu hawa ni wafanyakazi.
Mmiliki wa meli ni zanzibar.
Ukiwa rubani wa Qatar au Emirate wewe humiliki ndege, ni mfanyakazi tu.
Wenye meli ndio watoke watuambie nini kilitokea.
Habari za Polisi kutafuta mzigo zaidi ndani ya meli ya Zanzibar zimeandikwa kumbe!! sasa waziri alipowashukia waandishi wa Habari wa Tanzania bara alikuwa na maana gani. Kuwa mbara basi ni kosa kuandika habari za bangi la Zanzibar!!
Yeye alitakiwa atoke aeleze meli hiyo iliyokuwa na bendera ya znz na iliyosajiliwa na ZMA kwa ushirikiano na Philatex ambayo JMT haijui kimetokea nini.
Hao mabaharia hawakubeba bendera kwa hiari yao, ilikuwa ni lazima waweke bendera. Nani alitoa bendera ni Philatex, kwa kibali cha nani -ZMA, inayowakilisha serikali gani SMZ.
Kuna uhusiano kati ya SMZ na JMT jibu ni ndio, lakini kwa hili la shughuli za majini jibu ni hapana.
Sasa kama unadhani hakuna mznz mbona waziri Mwakyembe ameingilia kati, mbona waziri wa miundo mbinu wa zanzibar amelizungumzia kwa kigugumizi bila kulaani.
Si lazima wawepo wznz kinachoangaliwa ni usajili na mmiliki ambaye ni SMZ. Hili zigo la biashara msilikatae, mtakuja kukataa waziri wenu siku mkijiunga na Oganization of Islamic conference(OIC) kama hali ikitengemaa
Mkiambiwa ukweli mtu ana chuki. Leo Mzaninzibar anakubali kuitwa Mtanzania!! ama kweli mumeshikwa pabaya.
Tupeni nafasi tupumue
Mkuu Nguruvi3, unakuwa kama hujui kupenda!, Mke ukimpenda, unamhudumia kama jukumu lako ikiwemo kumlisha, kumvisha, kumtunza na kumpendezesha, na sio hayo tuu, kwa sababu una mpenda, unampa kila anachokita, hata kama wewe hukipendi!, mfano anapenda ubuyu, utamletea hata kama wewe huupendi!.
Hiyo faini ya dola 500,000 ni hela tuu ya kununulia ubuyu na wanja na vipondozi, mwache mama aitie kwenye kijaluba chake! na endelea kumhudumia!.
Kuna watu humu hawajui kupenda!, mimi nakumbuka enzi zangu za ujana, wakati huo mishahara ilikipiwa dirishani, niliwahi kuhonga bahasha nzima za mshahara wote, ile nimetoka tuu dirishani, nikakabidhi bahasha yote vile vile ilivyo mpaka na coins zake, kwa ka binti fulani cheupe kalichokuwa ndio kwanza kameajiriwa!.
Leo mnalalamikia mke Zanzibar baada ya miaka 49 ya ndoa!, tena kipindi hiki tunapopanga kusheherekea Diamond Jubilee! April 26 mwakani!. Mke nitaendelea kumhudumia, kudumisha ndoa!.
Pasco.
Well said mkuu. Nianze na ulipomalizia, wengi hapa jamvini tumeshatoa ushauri wa namna Zanzibar wanavyoweza kuwa na mamlaka kamili. Wazanzibar wamekataa na kufuata njia zile zile wanazolaumu.
Njia ya pili ni kura ya maoni, lakini nayo kwa kujua inaweza kuzaa wasichokitaka hawaitilii mkazo.
Mkazo upo katika masilhai yao kwa lugha yao ni muungano wa mkataba. Tanganyika haihitaji mkataba na Zanzibar!
wa nini?Kwakuelewa wanaihitaji Tanganyika sasa wanakuja na mlango wa mkataba.
Ushahidi kutotaka kuvunja muungano umetolewa na vinara wa wao akina Jusa na Moyo. Kwamba, kuwepo na passport ya Tanzania-Tanganyika, Tanzania-Zanzibar baada ya kuona rasimu na ujio wa Tanganyika.
Rasimu imeondoa utegemezi kama ajira na ardhi n.k huku ikiweka wazi sheria ya pande moja itatumika pande nyingine kama kibano cha ubaguzi wao.
Haitawezekana kukaa na Tanganyika na kutoa masharti wanayotoa sasa. Ili kuweza kuendelea kunufaika na fursa zilizopo ndio wamekuja na kituko cha passport wakitaka mafao yao watumie neno Tanzania kama ambavyo wanalipiwa ada za ZMA wakati wanasafirisha bangi. Hili tumeling'amua na ni ushahidi wa wao kun ng'ang'ania muungano!
Maana ya kufanya mambo watakavyo ni kwasababu hakuna Tanganyika.Mathalan wanatumia umeme wa JMT bila malipo kwasababu nani awaulize, hata kama hawana mchango, si wana jina?
Wanasajili meli za bangi kwa ada za JMT nani awaulize hata kama wana bendera yao na wimbo wao wa taifa.
Tanganyika ikirudi hakutakuwa katika upuuzi wa kuendeshwa na watu milioni 1.2 tena lakini tano wakiwa wanaishi Tanganyika.
Kwa msingi huo akina Nape tuwaeleze wazi kuhusu wizi na hujuma dhidi ya taifa na kwamba sasa tunataka Tanganyika. Kama hilo halitafanyika kwa amani ninatabiri hali mbaya sana siku za mbeleni hasa kwa wazanzibar kwasababu Mtanganyika hatavumilia tena kodi yake itumike kusafirisha bangi za nchi nyingine.
Na hii ni wake up call kuwa lazima sasa tuamue, tumejitahidi lakini haiwezekani.
Inapofikia wanataka makao makuu ya JMT yahamie kwa watu laki tano bila kujali sababu za kijiografia, uchumi na siasa hapo hakuna la ziada bali kuachana nao. Hatujui wanadai nini hasa ! hatuwezi kuishi namna hiyo, tuvunje jahazi
N akutumia bendera ya JMT kufungia tani za bangi nalo linahitaji Tanganyika irudi? Kwanini wasifungie na bendera ya znz ambayo imepugiwa kelele sana kuwa ipo na inagfanya kazi. Real! Kwanini BAYAZA imuathiri mtu wa matombo Morogoro?
Mkuu Mag3 , uongo ukirudiwa mara nyingi hugeuka kuwa ukweli. Ndugu zetu wa zanzibar kwa kujua au kutokujua wamezusha maneno mengi yasiyo na ukweli. Hawa unaowaona mtandaoni ni ''elite''sijui mvua samaki inakuwaje.Ndugu yangu Nguruvi3, hawa ndugu zetu kuliko kubishana nao heri ubishane na meza! "Mtuache tupumue", ndicho kilio chao huku wametukumbatia kama kupe anavyomganda ng'ombe! Kupe anao uhuru kabisa wa kujiondokea wakati wowote lakini je, huo mlo wa siku utoke wapi? Wakati kamganda ng'ombe kupe hana wasiwasi wa kula, hana wasiwasi wa kuhangaika juani na hana wasi wasi na usalama wake!
Katiba wanayo, Raisi wanaye, bunge wanalo, bendera wanayo na wimbo wa taifa wanao halafu bado wana jeuri ya kudai eti waachiwe wapumue. Ni kama mtu kudai katekwa na kufungiwa huku yuko huru na milango na geti zote ziko wazi...ni kiasi tu cha kuaga lakini wapi! Waache vinono vya bara, thubutu! Hakuna hukumu mbaya kwa kupe kama ile inayotia kufuli milango ya ghala walikozoea kupata lishe bora bila bughdha.
Hakika mimi nipo katika rekodi ya kuunga mkono harakati za znz kujikomboa. Nimewahi kuwahsuri mara nyingi sana. Tatizo ni wzn kuwa waoga na sijui wanaogopa nini. Znz inaweza kuwa kama Luxembourg, Mauritius, Dubai n.k. Znz inaweza kuwa na neema kama ile ya nyakati za sultan na utumwa.Mzee naona kama tayari umesha data... Harakati za ukombozi wa Zanzibar hakuna aneweza kuziziwia tena. Mimi nataka unune mpaka upasuke, na huo unga sasa itabidi wauziyane wenyewe kwa wenyewe hapo Tanganyika...
Hapana hakuna sababu za mzanzibar kulilia Tanganyika. Tanganyika ndio Tanzania kwasababu nchi ni gharama si jina. Ninyi mna serikali yenu kitu gani kinawashughulisha na Tanganyika?Unajuwa ni kitu cha kushangaza sana kuona watu na akilizao wanazungumza mambo bila ya kufikiri.
1. Ni nani alieiondowa Tanganyika hata sasa mtwambie sisi kuwa mnataka Tanganyika yenu? Tanganyika yenu mliitowa wenyewe kwa kutaka sifa na kukubali kuchezewa akili na mtu mmoja tu, Nyerere. Angalau sisi tulitiwa katika muungano kwa nguvu ya silaha na tukawa hatuna la kusema , lakini Watanganyika mliitowa Tanganyika nyie wenyewe kwa akili ya mtu mmoja. Sasa alieitowa hayupo lakini mjukuu wake yupo. Ni Nape,basi mwambieni yeye sio sisi akupeni Tanganyika yenu, kwetu sisi ni sawa tu Zanzibar yetu ipo naitaendelea kuwepo hata hapo mtapoweza kumshinda mzuka wa Nyerere.
2. Mbona tunapofanya jitihada ya kuirudisha Tanganyika yenu mnaungana kutupiga vita? Tulifanya 1984, tukakutengenezeeni njia miaka ya 90 mkafikia hata kuunda G55 mkakubali kuzimwa. Ikaja rasimu ya Katiba na tukaichana hadharani na kutaka swala la muungano lijadiliwe mkawabatiza watu UAMSHO (Awareness sasa inakuwa mbaya). Baada ya rasimu kuambiwa serikali tatu ili Tanganyika iwepo mnaruka kimanga eti gharama, lakini mnapoteza pesa kutaka umoja ambao hamtakiwi EAC.
Nionavyo mimi sisi Wazanzibari tusiwe wagomvi wenu bali tuungane ili kuhakikisha kuwa Tanganyika yenu mnairejesha. Hili la Zanzibar itakuwaje lisikupeni hofu kwani angalau mtakuwa hamna mzigo. Tuwachieni mje kutembea na kupata watoto wa Kiarabu baada ya kwisha kutajirika na gesi na mafuta!
Meli imesajiliwa na SMZ kupitia ZMA na Philatex. Hawa wanajua mmiliki ni nani.Mkuu mimi simjui mmiliki wa meli wewe kama unamjua basi nitajie inaonekana unajua mambo mengi ya zanzibar
Fundi , nilipoacha kumtaja ilikuwa gubu, nilipomtaja imekuwa kuwa gubu. sijui huyu bwana anatataka nini. Hajazuiwa kuchangia wala kulazimishwa. Nadhani ni kumu ignore tu ii kumsaidia avae nguo alizovua.
Yaani yote haya kwa sababu tu amekutaka na wewe uone alichoandika! Ungejikalia kimya ungepata hasara gani?
John Legend atakushangaa sana na tantrum yako.
Amandla.....