Sikieni hoja za wazanzibar

Sikieni hoja za wazanzibar

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
16,456
Reaction score
34,266
Zanzibar ilijitoa katika sheria za Jamhuri ya muungano ya usafiri wa majini ya mwaka 2003 na kuunda sheria yake ya bahari na usafiri ya mwaka 2006 na kuanzisha chombo chao, Zanzibar Maritime authority((ZMA) 2006.

ZMA haijaandikishwa na shirika la International Maritime organization(IMO) isipokuwa kupitia Jamhuri ya muungano wa Tanzania(JMT) ambayo inalipa ada za usajili. JMT haipati mapato kutoka ZMA au biashara zinazotokana.

Meli ilizosajili Zanzibar ni 400 kupitia wakala wake aiyeko Dubai kampuni ya Philatex. Mapato yatokanayo huingia SMZ na JMT haipati chochote isipokuwa jukumu la kulipa ada kwa chombo huru na chenye mamlaka kamili cha SMZ

Mwezi June meli zilizosajiliwa na Zanzibar zilikiuka vikwazo vya UN kwa kusafirisha mizigo ya Iran na kuiweka JMT katika wakati mgumu ikiwa ni pamoja na kuwekewa vikwazo vya uchumi.

Wiki hii meli yenye tani 30 zenye thamani ya bilioni milioni 125 zikiwa zimesajiliwa na ZMA chombo cha SMZ imekamatwa huko Italia. Hiyo ni sehemu tu ya meli mbovu ambazo zimesajiliwa. Umoja wa Ulaya (EU) umeiweka Tanzania katika nchi zenye vyombo hatari vya majini na vinavyohitaji ukaguzi.(Siyo SMZ ni JMT).
Ikumbukwe SMZ ilishajitoa kuhusu masuala ya usafiri wa majini tangu mwaka 2006 na kuwa na mamlaka kamili

Jana waziri wa mawasiliano na miundo mbinu wa SMZ Rashid Seif suleiman amevilaumu vyombo vya habari vya Tanzania BARA kuhusu kuandika habari hizo. http://www.habarileo.co.tz/index.ph...meli-zilizosajili-zanzibar-zaichafua-tanzania na http://www.dailynews.co.tz/index.php/local-news/22134-katiba-still-a-thorny-issue

Waziri wa SMZ haoni tatizo la kusafirisha mzigo wa bangi lilivyoichafua JMT ambayo Zanzibar ilishajitoa katika sheria na kuanzisha ZMA ila anaona tatizo habari hizo kuandikwa

Waziri Mwakyembe wa JMT ameingilia kati kufuatilia kadhia hiyo kwasababu Tanzania ndiyo yenye bendera na usajili wa IMO (Siyo meli) inakabliwa na kibano cha kimataifa kama ilivyokuwa kwa meli za Iran.
Gharama za ZMA kule IMO zinalipwa na JMT na waziri anatumia muda na gharama za JMT kuzuia uharibifu wa meli yenye mzigo wa Bangi ya SMZ.

Waziri huyo wa miundo mbinu wa SMZ alikaririwa na gazeti jana akisema faini inayotokana na kukiuka mkataba kati ya wenye meli na SMZ ambayo ni dollar 500,000 italipwa kwa SMZ(Siyo JMT)

Nilidhani waziri wa SMZ alitakiwa aeleze nini kimetokea hadi mzigo wa bangi tani 30 ukamatwe kwa jina la nchi ya Tanzania (Siyo Zanzibar)huku tukifahamu mapato yatokanyo na shughuli za meli hizo ikiwa ni pamoja na faini tarajiwa ni ya SMZ.

Ninajiuliza:
1. Kama Zanzibar ilishajitoa na kuanzisha ZMA kwanini meli zake hazisajiliwi na SMZ tukijua wana bendera yao
2. Kwanini kodi ya JMT ambayo ni ya Mtanganyika itumike kuhudumia shughuli za SMZ
3.Kwanini waziri Mwakyembe ashughulikie suala hili ambalo si la muungano

4. Je waziri Mh Suleiman wa SMZ anajua madhara yatakayomkumba Mtanganyika kutokana na biashara ya SMZ ambayo haimhusu kwa namna yoyote?

5. Kuna tatizo gani vyombo vya habari kuandika kuhusu kakamatwa kwa mzigo wa biashara wa meli zilizosajiliwa na ZMA ambacho ni chombo halali cha SMZ? Vyombo vya habari vimekosea nini na wapi?

Hebu tuellimishane kwa pamoja wanajamvi wote

JokaKuu GHIBUU Nonda Mzee Mwanakjiji Mchambuzi Jasusi EMT Ngongo platozoom Barubaru Zitto Mnyika Ritz chama Mkirua Zinedine AshaDii gfsonwin The Bigshow Kimweri Fundi Mchundo Bongolander Bu'yaka

Ahsanteni
 
Last edited by a moderator:
Kwa haya yote na sisi Watanganyika tuna sehemu ya lawama, nayo ni moja tu.......Tumewalea sana.
Na kawaida mtu ukimlea sana anabweteka, na ndiyo haya yanayochagiza 'Muungano wa Mkataba'.

Maadam tulikosa fursa ya kupiga kura ya maoni juu ya kuwepo ama kutokuwepo Muungano, nafikiri sasa tuanze
kufikiria tuwe na transition period tunapoelekea kwenye Serikali tatu.

1. Mawaziri na viongozi wanaoshughulika na mambo yasiyokuwemo kwenye Muungano waache kushiriki ama kutoa fedha
kuisaidia ama ku-support masuala yasiyokuwa ya Muungano (la usajili wa Meli mojawapo).

2. Nafasi za kazi zisizokuwa za Muungano na ambazo zimeshikwa na Wazanzibar ziondolewe ama kupewa Watanganyika.

3. Tuanze kufikiria Wazanzibar wanaoishi Tanganyika wapewe vitambulisho maalum (angalau vinavyofanana na working
permit kwa raia wa kigeni).

4. Vyama vya kisiasa vianze kufikiria miundo yao ya uongozi kulingana na mfumo mpya wa Serikali tatu.
Budget support kwa Serikali ya Zanzibar lazima ipitishwe na Bunge na iwe soft loan na sio sadaka.

Kwa sasa ni hayo.
 
Mambo yao ya zanzibar waachieni wenyewe nyinyi hayakuhusuni mbona mnawabana kwenye mambo mengi sana
Tumewaachia wakaanzisha ZMA, wakawa na bendera yao. Sasa kwanini wanasajili meli kwa jina la JMT na bendera yake ikiwa walikataa mwaka 2003 na kuanzisha mamlaka yao mwaka 2006? Hatuna shida na mambo yao lakini bangi zinapokamatwa kwa jina la Tanzania ni tatizo letu sio lao. Umeona hapo? Meli zikivusha mizigo ya Iran tunawekewa vikwazo sisi si zanzibar.

Gharama za uasajili wa meli ni zetu, mapato ni yao, umeona?

Hili ni tatizo letu tutake tusitake, lakini je ni sisi tumelisababisha?
 
Kauli ya Waziri wa Mawasiliano na Miundo mbinu wa SMZ, Rashid Seif Suleiman ya kuvilaumu vyombo vya habari vya Tanzania BARA ilinishangaza sana.

Ni kweli kabisa kuna kitu viongozi wetu waasisi wa 'muungano' walikiona kama kilikuwa ni cha muhimu sana kuziunganisha nchi zetu, lakini vile vile makosa ya kutokuelimishwa na kutoshirikishwa kwa wananchi wengi katika kufikia uamuzi huo ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwa chanzo cha mitikisiko na utegemezi katika 'muungano'.

Imedhihirika kuwa viongozi wakuu waliokuja baada ya marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na pia Wazanzibari wengi hawakutaka kuendelea kuwepo muungano na kwa sababu hiyo ilibidi viongozi wetu wawabembeleze kihoja na ilipobidi pia yalitumika mabavu ili waendelee kuwepo mwenye 'muungano' . Hii ilipelekea wananchi wengi wa Zanzibar na pia wachache wa bara kuamini kama viongozi wakuu wa bara walikuwa na ajenda fulani za siri ambazo kuzitimiza ilibidi tuwaombe na kuwashinikiza Wazinzibari waendelee kuwepo kwenye 'Muungano'.

Fikra na mitazamo hii imekuja kujisimika zaidi pale badhi ya viongozi wakuu wa Zanzibar walipotiwa misukosuko pale walipohoji uwepo wa muungano na manufaa yake.

Kwa sasa wanafanya kila wanachotaka bila kujari mshikamano, sheria na taratibu za nchi wakidhani kuwa Tanganyika inawahitaji sana zaidi ya wao kuihitaji Tanganyika.

Hata kujitoa kwao katika sheria za Jamhuri ya muungano zinazohusu usafiri wa majini za mwaka 2003 na kuunda sheria zao za bahari na usafiri na kuwa chini ya Zanzibar Maritime authority((ZMA) mwaka 2006 ilikuwa ni katika mwendelezo wa fikra hizo.

Waswahili wanasema, mdharau mwiba mguu huota tende!.

Tumezidharau na wakati mwingine kuzipuuzua chokochoko za 'muungano' kwa muda mrefu huku tukiwadekeza Wazinzibari kwa kuwapa kila kile wanalichokuwa wanakitaka na matokeo yake kwa sasa tunayaona. Kwa sasa imekuwa chao ni chao lakini chetu pia ni chao na wakati mwingine wanataka wakichukue chote.

Tulianza muungano vibaya na inavyoonekana pia tutaachana nao vibaya, na kwa maana hii, dawa ya muungano kwa sasa siyo serikali tatu kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali ni kuachana kabisa na muungano ili pande zote zipate ukweli halisia kama kuna umuhimu katika muungano. Hatutakuwa wa kwanza wala wa mwisho katika kuvunja muungano kwa sababu kuna nchi zimevunja muungano na zikapiga hatua zaidi za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hata katika ndoa, watu wanapokinzana sana, huwa wanafikia maamuzi ya kuachana ili kujipima na kuona umuhimu wa wao wakiwa pamoja au wakiwa single (space) na wakipatwa na reality, wengi wao hurudiana tena.
 
Ukweli ni kwamba zanzibar iko kimaslahi kwenye huu muungano. Na ukweli ni kwamba yale yanayoiumiza bara wao huwa hawayapi kipaumbele la wanaona sawa tu.

Waziri wao katuonyesha wazi kwamba hata uelewa juu mahusiano yetu ya majini hayajui na hivyo hajali kwake yeye liwalo na liwe.
 
Swali la msingi hapa ni kwamba Zanzibar ni nchi au si nchi... Hili swali hata mzee wa "wapingwe tu, kwani tumechoka" alishindwa kujibu pale bungeni...
 
Ndugu yangu Nguruvi, Zanzibar ni ya Wazanzibari na Tanzania ni ya Watanzania wote; Wazanzibari wanataka kuwa na mamlaka kamili kwa kadiri ya kwamba mamlaka hayo kamili yamejificha ndani ya Muungano. Jambo la kwanza ambalo Wazanzibari walitakiwa kufanya ni kujiunga na chombo cha vyombo vya majini cha kimataifa ili waweke bendera yao halafu waanze kurusha bendera yao.

Ndio maana wengine tulipata ahueni kidogo baada ya tukio la watu kumwagiwa Tindikali vyombo vyote vya kimataifa vilisema hilo limetokea "Zanzibar"! ...
 
Tumewaachia wakaanzisha ZMA, wakawa na bendera yao. Sasa kwanini wanasajili meli kwa jina la JMT na bendera yake ikiwa walikataa mwaka 2003 na kuanzisha mamlaka yao mwaka 2006? Hatuna shida na mambo yao lakini bangi zinapokamatwa kwa jina la Tanzania ni tatizo letu sio lao. Umeona hapo? Meli zikivusha mizigo ya Iran tunawekewa vikwazo sisi si zanzibar.

Gharama za uasajili wa meli ni zetu, mapato ni yao, umeona?

Hili ni tatizo letu tutake tusitake, lakini je ni sisi tumelisababisha?

Basi waachieni tu
 
Waletaka nchi yao siku nyingi tu nyinyi bado mnaikumbatia sasa ndio mtatia akili wale hawana nguvu za kivita kama nyinyi sima watatumia akili ya hali ya juu mpaka mtawapa nchi yao na wale vibaraka wenu wale cufccm wanajua hilo
 
Mkuu Nguruvi3,

Mtoto akifanya kosa la uharibifu wa mali, au trespass yoyote, anayewajibika kushitakiwa na kulipa fidia ni mzazi!.
Vivyo hivyo mke, ambaye ni mama wa nyumbani, akifanya kosa, anayewajibika kulipa faini ni mumewe!.

Zanzibar ni sehemu ya JMT, tumeungana kama mke na mume, yaani Tanganyika na Zanzibar zimeona na kuzaa Tanzania.
Zanzibar ni "mke", mbele ya jicho la kimataifa, na Tanzania ndie "mume", hivyo kosa lolote la kimataifa "mke" huyu atakalotenda, anayewajibika ni "mume".

Kwani OIC ilikuwaje?, acheni tuendelee kuwajibika, Zanzibar ni "mke" wetu, tumempenda wenyewe, lazima tumvumile na kwa vile tunampenda kwa dhati, talaka hatutoi ng'o!.

Mpenda maendeleo yoyote, humsupport mkewe afanye biashara ndogo ndogo za "ubuyu", kuuza "asikirimu" juisi, visheti etc, na fedha zinazotokana na biashara hiyo, hujinunulia kanga, mitandio, wanja, udi, chetezo na nguo za kujisitiri, hivyo kujikuta anakupunguzia wewe matumizi ya kukidhi mahitaji ya nyumbani, na siku nyingine, fedha hizo hutumika hata kununulia vitafunio, mboga au hadi chakula!.

Kwa biashara ndogo ndogo anayoifanya mkeo, hakukuondolei wewe mume, jukumu la kumlisha na kumvisha eti tuu kwa sababu anaingiza kipato!. Mwachieni mke wetu ile faini ni yake, mumu ataendelea kumlipia umeme, kugharimia gharama za safari zake za nje, kugharimia gharama za kuendesha muungano, kuendelea kuwahudumia ndugu wa mke wanaishi nyumbani kwako, kuendelea kuwatafutia kazi mashemeji kama kila kibarua cha wizara ya ulinzi, Afya, mambo ya nje, muungano, mabalozi etc. Hizi ndizo gharama za ndoa, ndizo gharama za kupenda na tunazilipa zote kwa roho kwatu "nyeupe" kwa sababu tumependa!.

Sisi Watanzania tuko wengi wa aina tofauti na dini tofauti, kuna dini za wenzetu wanasema "mke kama hakutaki, mwache aende zake!". Au Mke kama umemchoka, mpe talaka yake!" hivyo wao wanataka "mke huyu" apewe talaka ende zake, kama ataolewa tena ni juu yake!.

Mimi ni Mkristu Mkatoliki, ndo ni mpaka kifo kitutenganishe, hakuna talaka, hakuna kuachana wala kutengana!. Mke hata umchoke vipi, au akuchoke vipi, ndio itaendelea tuu kwa lazima!. Hata kama mapenzi ndani ya nyumba yamekwisha, utavumilia tuu, utaendelea kuubeba msalaba wako hadi mwisho wa safari!.

Muungano wetu ni ndoa ya Kikristo!, hauna talaka!.
Pasco.
 
Zanzibar ilijitoa katika sheria za Jamhuri ya muungano ya usafiri wa majini ya mwaka 2003 na kuunda sheria yake ya bahari na usafiri ya mwaka 2006 na kuanzisha chombo chao, Zanzibar Maritime authority((ZMA) 2006.

ZMA haijaandikishwa na shirika la International Maritime organization(IMO) isipokuwa kupitia Jamhuri ya muungano wa Tanzania(JMT) ambayo inalipa ada za usajili. JMT haipati mapato kutoka ZMA au biashara zinazotokana.

Meli ilizosajili Zanzibar ni 400 kupitia wakala wake aiyeko Dubai kampuni ya Philatex. Mapato yatokanayo huingia SMZ na JMT haipati chochote isipokuwa jukumu la kulipa ada kwa chombo huru na chenye mamlaka kamili cha SMZ

Mwezi June meli zilizosajiliwa na Zanzibar zilikiuka vikwazo vya UN kwa kusafirisha mizigo ya Iran na kuiweka JMT katika wakati mgumu ikiwa ni pamoja na kuwekewa vikwazo vya uchumi.

Wiki hii meli yenye tani 30 zenye thamani ya bilioni milioni 125 zikiwa zimesajiliwa na ZMA chombo cha SMZ imekamatwa huko Italia. Hiyo ni sehemu tu ya meli mbovu ambazo zimesajiliwa. Umoja wa Ulaya (EU) umeiweka Tanzania katika nchi zenye vyombo hatari vya majini na vinavyohitaji ukaguzi.(Siyo SMZ ni JMT).
Ikumbukwe SMZ ilishajitoa kuhusu masuala ya usafiri wa majini tangu mwaka 2006 na kuwa na mamlaka kamili

Jana waziri wa mawasiliano na miundo mbinu wa SMZ Rashid Seif suleiman amevilaumu vyombo vya habari vya Tanzania BARA kuhusu kuandika habari hizo. http://www.habarileo.co.tz/index.ph...meli-zilizosajili-zanzibar-zaichafua-tanzania na http://www.dailynews.co.tz/index.php/local-news/22134-katiba-still-a-thorny-issue

Waziri wa SMZ haoni tatizo la kusafirisha mzigo wa bangi lilivyoichafua JMT ambayo Zanzibar ilishajitoa katika sheria na kuanzisha ZMA ila anaona tatizo habari hizo kuandikwa

Waziri Mwakyembe wa JMT ameingilia kati kufuatilia kadhia hiyo kwasababu Tanzania ndiyo yenye bendera na usajili wa IMO (Siyo meli) inakabliwa na kibano cha kimataifa kama ilivyokuwa kwa meli za Iran.
Gharama za ZMA kule IMO zinalipw
 
Tatizo sio zanzibar, tatizo ni muungano huu tulio nao ambao upo mparaganyiko haujulikani kichwa wala mguu, kwa mfano zile sector ambazo haziko katika orodha za muungano, zinashindwa kujiendesha kimataifa kutokana na muungano wenyewe, mfano suala la michezo, sio suala la muungano, Watanganyika wakachukua timu ya Tanganyika na kuitambulisha kama tanzania, ZFA imeshindw akupata usajili FIFA kutokana TFF tayari inawalihsa tanzania, Yaani Jamuhuri ya muungano wa tanzania, pale kunapotea misaada katika suala la micheza kutoka kimataifa zanzibar haipati chochote kutoka TFF.
 
Tumewaachia wakaanzisha ZMA, wakawa na bendera yao. Sasa kwanini wanasajili meli kwa jina la JMT na bendera yake ikiwa walikataa mwaka 2003 na kuanzisha mamlaka yao mwaka 2006? Hatuna shida na mambo yao lakini bangi zinapokamatwa kwa jina la Tanzania ni tatizo letu sio lao. Umeona hapo? Meli zikivusha mizigo ya Iran tunawekewa vikwazo sisi si zanzibar.

Gharama za uasajili wa meli ni zetu, mapato ni yao, umeona?

Hili ni tatizo letu tutake tusitake, lakini je ni sisi tumelisababisha?
acha upumbavu hivi pale mnapoipeleka jmt yako katika vita unafikiri wazanzibari tunakubalianb na hayo take the consequencies
 
weweupo na akili lakini?kwani jmt ninini.. ni umoja wa kwetu sote ------- wa mawazo wewe.. eti tuliwaachia... chombo hicho unachojifany akukikaliani cha kwetu pamoja akili ndogo wewe.. anzisha nyikayako kwanza
 
Back
Top Bottom