Skuli ina maana pale ambapo itaeleweka.
Ni kwa msingi huo kitu gani kinakushinda kueleza na kufafanunua hadi ubaki kutaja herufi za vifungu?
Eleza na fafanua ndio maana ya mjadala, weka wazi ili kila mtu ajue unasimamia hoja gani
Tofauti baina yangu na yako ni kuweka mambo ili kila mtu aelewe.
Siku zote nasisitiza kuwa hata kama una degree 20 kama hutazifanyia kazi kwa kueleweka basi ni kama hakuna.
Sifa moja ya Nyerere si kuwa msomi wa kiwango cha profesa.
Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na hadhira yake na kumwelewa.
Mwalimu mzuri ni yule anayeeleweka si yule mwenye 'material'.
Nimeweka hoja zangu, ulichopaswa kufanya ni kuchambua ukionyesha udhaifu au upotoshaji wake.
Hujaweza kufanya hivyo na msomaji yoyote atanielewa kuliko wewe.
Mathalan, nimesema kuwa kwanini tufikiriea misaada tusifikirie namna ya kujikwamua ili tusiombe misaada.
Msomi wa PhD kama wewe hapaswi kufikiri kama mvuvi wa samaki.
Misaada ni jambo la dhalili kwa watu wenye taifa.Haipaswi kuwa ajenda hata siku moja tena ikishikiwa bango na mchumi wa PhD.
Nimekuambia Wanafunzi 1000 wa znz wanasoma kwa pesa za mikopo ya Watanganyika tena bila kurudisha.
Kiwango hicho ni kikubwa kuliko wanafunzi 800 wanaodhaminiwa na SMZ.
Suala la elimu ya juu halipo katika mambo ya muungano, ambayo ni hoja ya wazanzibar.
Mwanafunzi wa Tanganyika anaumia kwa kodi isiyomfaidisha tena ya baba yake kufadhili mzanzibar.
Hoja hiyo ijibu na si kutaja kifungu 1, 2, bila kusema kinaeleza nini.
Nikatoa hoja bajeti ya znz mwaka 2013 ni bilioni takribani 700. Hoja hiyo kataa kuwa si kiwango hicho.
Nikasema bajeti ya ulinzi na usalama ni zaidi ya 1.5 Trilioni (bilioni 1500 kwa hesabu unayoweza kuelewa).
Katika gharama hizo znz haichangii kwasababu itachangia nini wakati bajeti yake haifiki nusu ya bajeti nzima.
Hoja ni hiyo ijibu.
Mwisho, huwezi kusema znz ni ndogo ina watu 1.2 milioni kwahiyo isichangie bajeti ya ulinzi na usalama.
Kama utasema hivyo ambavyo ndivyo ulivyosema basi kwanini
1. Itake kugawana madaraka sawa tena hadi urais wa kupokezana wakati tunaelewa kuwa znz peke yake haiwezi kuendesha serikali ya shirikisho kwa miezi 2 tu.
2. Kwanini wajumbe wa tume wawe sawa kama huko nyuma umekubali kuwa ina watu 1.2 na haiwezi kuwa sawa kwa gharama na Tanganyika.
3. Kwanini znz isikatae pesa zisizo na audit zinazotoka JMT ambazo ni bilioni 32, wakati unapiga kelele za misaada.
Muhimu sana ni kuwa kama unadhani misaada ni muhimu(stupid idea so as to speak) kwanini znz hiyo hiyo isidai madeni ya taifa yawe pasu pasu.
Halafu lazima ufikirie gharama amabazo znz haina katika muungano.
-Nimekuambia wabunge wa znz wanalipwa na pesa ya Tanganyika. Jibu hoja kama ni kweli au si kweli.
-Wabunge wa BLW wanaokuja Dodoma wanalipwa na Tanganyika, kanusha kama si kweli.
-Zanzibar hailipi bili ya aina yoyote ndani ya muungano zaidi ya jina. Kanusha kwa hesabu kama si kweli
Hata umeme wameshindwa kulipa, sasa wanataka ubia gani! Hawa wasioweza kulipa bill ya umeme bila sababu bali ukatili tu unaweza kuwaweka meza moja kama wabia sawa. Kanusha kama si kweli
Hizo ni baadhi ya hoja unazotakiwa kukabiliana nazo. Kwasababu unaongea ukiwa hujui unachoongea matokeo yake umejikuta unazungumza kichekesho kiwango cha PhD.Msomi unawezaje kudai eti Znz isilipe gharama za ulinzi na usalama kwasababu ya watu 1.2 milioni halafu unageuka na kudai misaada(pathetic and stupid idea) igawanywe pasu pasu.
Shame on you
Barubaru