Sikieni hoja za wazanzibar

Sikieni hoja za wazanzibar

Mzee mwanakijiji.hapo nakukosa kidoogo wazanzibati na watanganyika sio watanzania.la pili wazanzibari washazoea kupakwa matope na serekali ya tanganyika.nakupa mfano: kulitokea uhalifu wa makanisa znz.waziri wa ulinzi alikuja moja kwa moja znz na akatangaza kwamba kuna ugaidi znz mbele ya waandishi wa habari ila sasa palipotokea kuripuliwa arusha kule hatujamsikia kusema kuna ugaidi tanganyika.swali langu kwann. Yupo tayari kuwapaka matope wazanzibar ila watanganyika yanayotokea anabana mdomo.jeee haki hii kwelii kwa kuwaharibia jina la wazanzibar ili watali wasije ndio maana yake.mana znz kikubwa wanategemea kipato cha watalii.so amesema vile ili kuwaharibia.inasikitisha sanaa😕
Walipomwagiwa tindikali waingereza nchi zote duniani ziliandika Zanzibar. Huo ni ukweli kwasababu katika katiba ya znz hakuna kitu kilichotajwa zaidi ya znz.

Padre alipouawa hiyo ikawa issue Dunia nzima bila waziri kusema lolote. Sijui kwanini usilaumu BBC na CNN

Juzi kamwagiwa tindikali padre mwingine, sijui ulitaka nani aseme au watu waseme kanyeshewa na mvua.

Sikiliza sifa ya znz inajengwa na kuharibiwa na wazanzibar wenyewe. Mzigo wa bangi umekutwa katika meli iliyosajiliwa znz na ZMA na SMZ. Yameandika mazeti yote duniani, je huoni kama doa kubwa kuliko kauli ya waziri mmoja.

Mwisho, lazima utambue kuwa kosa halifutwi na kosa. Kama waziri angesema Arusha kuna ugaidi hilo halizuii mtalii kubaini kuwa kuna kumwagiwa tindikali, kuchomwa moto(niulize) n.k.

Kama unadhani Tanganyika ndio tatizo basi endeleeni kumwagia watu tindikali ili muweze kuwa sawa na Tanganyika.
 
Ndugu yangu Nguruvi3, hawa ndugu zetu kuliko kubishana nao heri ubishane na meza! "Mtuache tupumue", ndicho kilio chao huku wametukumbatia kama kupe anavyomganda ng'ombe! Kupe anao uhuru kabisa wa kujiondokea wakati wowote lakini je, huo mlo wa siku utoke wapi? Wakati kamganda ng'ombe kupe hana wasiwasi wa kula, hana wasiwasi wa kuhangaika juani na hana wasi wasi na usalama wake!

Katiba wanayo, Raisi wanaye, bunge wanalo, bendera wanayo na wimbo wa taifa wanao halafu bado wana jeuri ya kudai eti waachiwe wapumue. Ni kama mtu kudai katekwa na kufungiwa huku yuko huru na milango na geti zote ziko wazi...ni kiasi tu cha kuaga lakini wapi! Waache vinono vya bara, thubutu! Hakuna hukumu mbaya kwa kupe kama ile inayotia kufuli milango ya ghala walikozoea kupata lishe bora bila bughdha.

Umewaeleza kwa maneno machache na mfano mmoja kwa usahihi sana, noone can do better than this.
Nimeipenda sana hii.
 
Mr nguruvi.ni kweli maneno yako tuachieni tupumuweeeeeeeee jamaniii.mshatutaguna sanaaaaa.fedha zetu mshakula sanaaaaa.lkn nashangaaaa bado mnataka muungano.mnalazimisha muungano kwasabau mtakosa mnachokipata kwetu. Hatutakiii jamaniiii tuacheni tupumuweeeeee

hivi sensa ya 2012 ilionyesha idadi ya watu zanzibar ni wangap?
 
Hakika mimi nipo katika rekodi ya kuunga mkono harakati za znz kujikomboa. Nimewahi kuwahsuri mara nyingi sana. Tatizo ni wzn kuwa waoga na sijui wanaogopa nini. Znz inaweza kuwa kama Luxembourg, Mauritius, Dubai n.k. Znz inaweza kuwa na neema kama ile ya nyakati za sultan na utumwa.
Znz inawekana nje ya muungano, hakuna anayeweza kuifuta historia yake na znz itasimama yenyewe.

Huu upuuzi wa muungano wa mkataba au serikali 3 haupaswi kupigiwa upatu na mzanzibar mwenye akili.
Kinachotakiwa n kufanya haya
1. Kususia tume ya Warioba na kuzuia wajumbe wake au kujitoa
2. Kususia bunge la katiba
3. Kumrudisha makamu wa rais aliyepatikana kwa uzanzibar wake
4. Kuzuia wabunge wasije Dodoma
5. Kujadili kujitoa ndani ya BLW kama ilivyokuwa kwa mafuta na gesi, baraza la mitihani na ZMA n.k
6. Kuwarudisha wafanyakazi wote wa SMZ kutoka bara
7. Kuzuia wanafunzi kuchukua mikopo ya bara na kuja kusoma huku bara
8. Kuwashawishi wafanyabiashara kuondoka na kurudi kuwekeza znz
9. Kunzisha balozi zao kama walivyoanzisha wakala wa Philatex

Hadi hapo muungano utakuwa umekufa na harakati za kuiokomboa znz zitakuwa zimetimia.

Kama hawaweza kutumia fursa hiyo wakabaki na upuuzi wa mkataba ambao mzee amekwama nao chumbe, wakaleta hoja za kugawana vyeo bila gharama na kudai kisicho chao basi wajiandae kuwa chini ya kivuli mwanana cha Tanganyika kama mkoa. Hakuna njia ya mkato ni ima kunyoa au kusuka, ukombozi utabaki kuwa ndoto na simuliz mwanana. period.

Sasa kile kiapo cha kuulinda muungano kwa gharama zote umekifuta ? au ndio unajitoa fahamu? kwanza mufute kile kiapo cha kulinda muungano kwa gharama zote, vinginevyo bado unaendelea kuwa wanafiki.
 
Walipomwagiwa tindikali waingereza nchi zote duniani ziliandika Zanzibar. Huo ni ukweli kwasababu katika katiba ya znz hakuna kitu kilichotajwa zaidi ya znz.

Padre alipouawa hiyo ikawa issue Dunia nzima bila waziri kusema lolote. Sijui kwanini usilaumu BBC na CNN

Juzi kamwagiwa tindikali padre mwingine, sijui ulitaka nani aseme au watu waseme kanyeshewa na mvua.

Sikiliza sifa ya znz inajengwa na kuharibiwa na wazanzibar wenyewe. Mzigo wa bangi umekutwa katika meli iliyosajiliwa znz na ZMA na SMZ. Yameandika mazeti yote duniani, je huoni kama doa kubwa kuliko kauli ya waziri mmoja.

Mwisho, lazima utambue kuwa kosa halifutwi na kosa. Kama waziri angesema Arusha kuna ugaidi hilo halizuii mtalii kubaini kuwa kuna kumwagiwa tindikali, kuchomwa moto(niulize) n.k.

Kama unadhani Tanganyika ndio tatizo basi endeleeni kumwagia watu tindikali ili muweze kuwa sawa na Tanganyika.

Bangi, madawa ya kulevya (nyunga), tindikali na mabalaa yote hayo chanzo chake ni Tanganyika...mzigo wa bangi ulitokea Tanaganyika. Au ilaumiwe meli bila ya kuwataja waliouza na kununua na kupakia kwenye hiyo meli. Sasa kama bangi inasafirishwa katika magari ya polisi huko Tanganyika ,leo hii tuone ajabu meli kupakia tani 30 za bangi kutoka Tanganyika?
 
Ni kweli kabisa unayoyasema mkuu Nguruvi anajitoa ufahamu amesahau bangi iliyokamatwa
kwenye gari la polisi amesahau mfanyabiashara maarufu mwenye Home shopping center alivyo
mwagiwa tindikali au na hiyo ilikuwa ni Zanzibar Nguruvi fanya fear kwa wazanzibar.
 
mr nguruvi.ni kweli maneno yako tuachieni tupumuweeeeeeeee jamaniii.mshatutaguna sanaaaaa.fedha zetu mshakula sanaaaaa.lkn nashangaaaa bado mnataka muungano.mnalazimisha muungano kwasabau mtakosa mnachokipata kwetu. Hatutakiii jamaniiii tuacheni tupumuweeeeee

si bure,wewe ni wa kupimwa.
 
Nikuulize suala dogo tu. JE KWANINI UMEAMUA KUUKANA UTAIFA WAKO WA TANGANYIKA NA JINA LA NCHI YAKO TANGANYIKA NA KUJIVIKA UTANZANIA? KWANINI NA NYIE MSIWE TAIFA NDANI YA TANZANIA ILI KUNDA JAMHURU YA MUUNGANO WA TANZANIA? Kuliko ilivyo sasa JAMHURU YA MUUNGANO YA TANZANIA

nIMEKUULIZA HUKO AWALI KUWA JE KWANINI MISAADA MNAYOPEWA HAMGAWANI PASU KWA PASU NA ZNZ?

Mkuu BARUBARU, haiwezi kugawanywa kwa usawa kwn hugawanywa kutokana na uwiano sawa wa watu lakini pia hata kwny actle kumeeleza hvyo nadhani hoja ya msingi hapa hebu tujitengenezee tanganyika yetu na tuwaachie zbr yao kwn ht haya mambo ya bangi yangekuwa ya kwao. na cyo hayo tu kwn wanapewa misaada toka falme za kiarabu ila cyo kupitia bank na ndo maana inakuwa cyo rahisi BOT kujua.
 
Mr Nguruvi nadhani itakua bora zenj wakawa full members wa IMO hata ikibidi JMT iwape msaada wapate status hiyo. Itaepusha matatizo mengi.
 
Ndugu yangu, huu ni uthibitisho mwingine kuwa Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya JMT. Huyo waziri nilimsikia alipokuwa akiongea na kwa kweli hakuna la maana aliloongea maana alikuwa analalamika kuhusu vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii kwa kuhituhumu Zanzibar kuhusu kusajili meli huku zikibaki kutambuliwa kuwa zimesajiliwa na mamlaka ya JMT wakati SMZ ina mamlaka kamili ya usajili wa meli. Kiukweli alichotakiwa kusema ni kuwa licha ya Zanzibar kuwa na mamlaka ya kusajili meli bado bendera yake na serikali yake haitambuliwi kimataifa.
 
Mr Nguruvi nadhani itakua bora zenj wakawa full members wa IMO hata ikibidi JMT iwape msaada wapate status hiyo. Itaepusha matatizo mengi.
...

Walijaribu walishindwa kupata Membership kwa kuwa Zanzibar si nchi. IMO inasajili nchi na sehemu ya nchi. Kimataifa Zanzibar sio sovereign state hivyo haina hadhi ya kuwa member wa Mashirika hayo ya kimataifa lazima ipitie kwa mgongo wa JMT.

http://www.imo.org/About/Membership/Pages/MemberStates.aspx
 
Mkuu BARUBARU, haiwezi kugawanywa kwa usawa kwn hugawanywa kutokana na uwiano sawa wa watu lakini pia hata kwny actle kumeeleza hvyo nadhani hoja ya msingi hapa hebu tujitengenezee tanganyika yetu na tuwaachie zbr yao kwn ht haya mambo ya bangi yangekuwa ya kwao. na cyo hayo tu kwn wanapewa misaada toka falme za kiarabu ila cyo kupitia bank na ndo maana inakuwa cyo rahisi BOT kujua.

Sasa maneno hayo jaribu kumuelimisha Nguruvi3, Chama na jasusi ambao wao wanataka kila nchi ichangie sawa katika Muungano bila kuangalia Misaada na Mikopo inagawanywa vipi baina ya nchi hizo huru.

Lakin na wewe ile misaada inayotoka Vatican na nnchi za Ulaya kupitia katika mashirika ya dini inaonekana?

Kinachotakiwa ni SERIKALI YA Jamhuri ya NCHI ZA TANZANIA na sio ilivyo sasa.

Pole sana
 
Mkuu Nguruvi3, Mtoto akifanya kosa la uharibifu wa mali, au trespass yoyote, anayewajibika kushitakiwa na kulipa fidia ni mzazi!.Vivyo hivyo mke, ambaye ni mama wa nyumbani, akifanya kosa, anayewajibika kulipa faini ni mumewe!.Zanzibar ni sehemu ya JMT, tumeungana kama mke na mume, yaani Tanganyika na Zanzibar zimeona na kuzaa Tanzania. Zanzibar ni "mke", mbele ya jicho la kimataifa, na Tanzania ndie "mume", hivyo kosa lolote la kimataifa "mke" huyu atakalotenda, anayewajibika ni "mume".Kwani OIC ilikuwaje?, acheni tuendelee kuwajibika, Zanzibar ni "mke" wetu, tumempenda wenyewe, lazima tumvumile na kwa vile tunampenda kwa dhati, talaka hatutoi ng'o!.Mpenda maendeleo yoyote, humsupport mkewe afanye biashara ndogo ndogo za "ubuyu", kuuza "asikirimu" juisi, visheti etc, na fedha zinazotokana na biashara hiyo, hujinunulia kanga, mitandio, wanja, udi, chetezo na nguo za kujisitiri, hivyo kujikuta anakupunguzia wewe matumizi ya kukidhi mahitaji ya nyumbani, na siku nyingine, fedha hizo hutumika hata kununulia vitafunio, mboga au hadi chakula!.Kwa biashara ndogo ndogo anayoifanya mkeo, hakukuondolei wewe mume, jukumu la kumlisha na kumvisha eti tuu kwa sababu anaingiza kipato!. Mwachieni mke wetu ile faini ni yake, mumu ataendelea kumlipia umeme, kugharimia gharama za safari zake za nje, kugharimia gharama za kuendesha muungano, kuendelea kuwahudumia ndugu wa mke wanaishi nyumbani kwako, kuendelea kuwatafutia kazi mashemeji kama kila kibarua cha wizara ya ulinzi, Afya, mambo ya nje, muungano, mabalozi etc. Hizi ndizo gharama za ndoa, ndizo gharama za kupenda na tunazilipa zote kwa roho kwatu "nyeupe" kwa sababu tumependa!.Sisi Watanzania tuko wengi wa aina tofauti na dini tofauti, kuna dini za wenzetu wanasema "mke kama hakutaki, mwache aende zake!". Au Mke kama umemchoka, mpe talaka yake!" hivyo wao wanataka "mke huyu" apewe talaka ende zake, kama ataolewa tena ni juu yake!.Mimi ni Mkristu Mkatoliki, ndo ni mpaka kifo kitutenganishe, hakuna talaka, hakuna kuachana wala kutengana!. Mke hata umchoke vipi, au akuchoke vipi, ndio itaendelea tuu kwa lazima!. Hata kama mapenzi ndani ya nyumba yamekwisha, utavumilia tuu, utaendelea kuubeba msalaba wako hadi mwisho wa safari!.Muungano wetu ni ndoa ya Kikristo!, hauna talaka!.Pasco.
Mkuu, hata ndoa ya kikatoliki kifo cha kiroho(dhambi) talaka ruksa!!
 
Si wanataka kujitenga na sisi tunawa ng'ang'ania?? Acha yatukute,CCM EEEH ZANZIBAR IACHENI IJITEGEMEE.
 
Ni kweli kabisa unayoyasema mkuu Nguruvi anajitoa ufahamu amesahau bangi iliyokamatwa
kwenye gari la polisi amesahau mfanyabiashara maarufu mwenye Home shopping center alivyo
mwagiwa tindikali au na hiyo ilikuwa ni Zanzibar Nguruvi fanya fear kwa wazanzibar.
Hii haiondoi ukweli kuhusu bangi iliyosafirishwa na SMZ kupitia ZMA na Philatex.
Tanganyika haisajili meli za ZNZ na wala haikujua kuna meli 400.
Tanganyika imekuwa inakamuliwa tu kulipia IMO kwa mzigo wa biashara wa bangi kutoka znz

Wewe na Takashi pamoja na waziri wenu hamna tofauti katika hoja zenu. Mnadhani bangi ikikantwa Dar basi linaiondoa znz katika kashfa hii!! hii ni kashfa ya kimataifa si ya mtaa.

Kitu cha muhimu sana ni ninyi kukumbuka kuwa znz inataka kushiriki OIC ambayo ni shirika la kiislam.
Je usafirishaji wa bangi unaipa nafasi gani katika hilo.
Pili, je hakuna unafiki kwa kusema asilimia 98 ya wananchi ni waislam huku kukiwa na biashara ya bangi? Hapo mnaitendea dini haki kweli. Niambieni taifa la kiislam linalojishughulisha na usambazaji wa bangi duniani, nitajieni taifa moja tu!

cc takashi GHIBUU Nonda
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3/

kama kawaida yangu naomba nikusaidie kitu fulani hapo katika maandiko yako.

Siku zote unapochambua jambo jiulize waliokamatwa kulikuwa na WaZnz pale?

Lakin ungeanzia Bangi hiyo wameipata wapi? Kwa kujiuliza je Znz kuna pahala wanalima Bangi kama inavyolimwa kule Tarime, matombo morogoro au songea na Iringa?

lakin kubwa je ni Taifa gani la Kikristu linalojishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya haswa ukizingatia ubalozi wa vatican upo nchini kwenu na mwakilishi wa papa yupo hapo tanganyika?

lakin huko nyuma nilikuuliza naona umekimbia. Nilikwambia wewe unataka mgawo sawa kwa sawa kuchangia muungano je na misaada na mikopo mnagawa sawasawa?
 
Nilikwambia wewe unataka mgawo sawa kwa sawa kuchangia muungano je na misaada na mikopo mnagawa sawasawa?
Mgao wa madeni ukoje?Ukijibu hili nitaendelea. Kama huongelei madeni ka kimya.

Barubaru
1. Umeme wa bure
2. Mihshara kutoka hazina
3. Wanafunzi 1000 kusomeshwa bure bila kurudisha hata senti tano
4. Umiliki wa ardhi usio na masharti
5. Ada za IMO bure
6. Ajira za upndeleo hata kama hakuna qualifications
7. Ulinzi na usalama bure
8. Pesa ziszo na audit bure
9. Huduma za viongozi wa SMZ kama usafiri bure(muulize mzee wa mkataba anatumia kubebea mkaa)
10. Mnapata 7% ya pato la taifa
11. Mnapata 4.5 % ya misaada
12. Wabunge wenu wanaokuja kujadili mambo ya Tanganyika wanalipwa na Tanganyika
13. wajumbe wa BLW wanoingia bungeni Dodoma buree
14. Wajumbe wa bodi mbal mbali kutoka znz buree
15. Tume ya warioba buree

Ongelea mgao sawa wa madeni na misaada kwa kuangalia hayo hapo juu kwanza halafu ujue gharama za madeni pia.

Huko nyuma umesema znz haiwezi kuchangia sawa ulinzi na usalama kwasababu ina watu 1.5
a) kwanini idadi sawa ya wajumbe ndani ya tume ya Warioba
b)Kwanini idai idadi sawa ya wajumbe wa bunge la katiba
c) Kwanini mbunge wa znz anyewakilisha watu 5,000 apewe hadhi sawa na mbunge wa Ubungo mwenye watu zaidi ya nchi nzima ya znz?
d) Kwanini utake mgao sawa wa misaada huku ukikimbia gharama za ulinzi na usalama kwa kigezo cha population
e) Kwanini utake mgao sawa huku ukikimbia gharama za kusomesha watoto wako.
f)kwanini utake urais wa kupokezana huku rais kutoka znz ataleta sura na si uchumi!
g)Kwanini utake mgawanyo wa madaraka sawa huku znz ikichangia sifuri na kuchukua zaidi kutoka shamba la bibi.

FYI, znz ilishindwa kununua kifaa cha umeme c fumbuni kwa gharama ya bilioni 5 hadi Nahodha alipokuja kuomba hazina kwa kulia lia. Leo unataka kusema kila kitu usawa, usawa gani usioweza kulipia kifaa cha umeme fumbuni achilia mbali kumulika usiku kucha kwa umeme usiojua gharama zake.

Nimekuambia ulinzi na usalama ni 1.5 Trilioni. Bajeti ya znz 2013 ni bilioni 700. Tukiweka usawa wa misaada wewe utachangia nini, wakati umeshakua 7% na 4.5% na bado hujafikia nusu. Lini znz iliwahi kujua gharama za ulinzi na usalama

Kumbuka katika 1.2 milioni ya wznz, laki 5 wanaishi Tanganyika, kupata huduma za afya Tanganyika ikiwa ni pamoja na elimu kuanzia msingi hadi chuo kikuu tena bureee bila kurudisha mkopo.

Kwa maneno mengine znz huwa na watu laki 5 halafu unataka ulete usawa upi? na kata ya mzimuni au!
Hakuna usawa mbunge akiwaklisha watu 2500 na mbunge mwenye nchi nzima ya ZNZ. Ilala ni zaidi na znz yote kwa kila kitu na ina mbunge mmoja

Una PhD, sasa mvuvi wa samaki ikoje ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom