Sikieni hoja za wazanzibar


Mkuu wewe ni muandishi wa habari?
 
Mkuu Nguruvi3 huwezi tenganisha hili la ZMA na muungano hata kidogo. Hiki chombo kimeanzishwa baada ya SMZ kutoridhika na mamlaka inayosimamia vyombo vya usafiri Bara. Kwa maana muungano ndio ulioleta manung'uniko yote hayo. Usingekuwapo muungano sidhani kama ingechafuliwa tanganyika kwa uovu wa nchi nyingine.
Ama kuhusu bandiko lako ulichokionyesha kwanza ni zanzibar kuinyonya tanganyika.
Mimi siamini kama eti sisi tanganyika tunawabeba wazanzibar. Kumbuka hata kabla ya muungano zanzibar ilikuwa inajiendesha na ilikuwa na kila kitu. Iweje leo ndio tuanze kulalamika eti watanganyika twanyonywa na wazanzibar kisa wana ZMA, au Upendeleo ktk nafasi za elimu n.k wakati sisi ndio tuliowaomba tuungane nao? Kifupi huu ni uzushi na hata bandiko lako linakosa natija ya kuwa SMZ inatunyonya labda useme tanganyika inajinyonya.
2. Pia mkuu kila nilipoona mamlaka kamili ya zanzibar inadaiwa au kutamkwa unasema 'usalama' pia wajitegemee. Yaani muungano wa mkataba pia uondolewa. Mimi kwa ufahamu wangu asilimia kubwa ya wazanzibar hawautaki muungano hata huo wa mkataba ila mamlaka kamili. Hapa unataka tuamini zanzibar itatetereka kiusalama endapo itajitenga na tanganyika. Si kweli hata kidogo mkuu, kila nchi inauwezo wa kujisimamia na kuwa na jeshi lake kamili. Kama ni kutetereka kwa zanzibar basi useme tu hata tanganyika.
Isitoshe, nje ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar zote kwa pamoja zitalazimika kubeba mzigo wa kugharamia ulinzi na usalama pamoja na uendeshaji wa Ofisi za Balozi nje ya nchi. Gharama hizi zikigawanywa kwa kila nchi kuendesha mambo haya yenyewe inawezekana kwa kila nchi. Kwasasa Usalama wa Zanzibar na Tanganyika unategemeana sana na Muungano ndio chombo kinachohakikisha usalama wa pande zote mbili. Hivyo, ustawi wa Zanzibar na Tanganyika unategemeana, wala sio kweli kuwa yuko mmoja anayembeba mwenzake au atakayekuwa salama zaidi nje ya Muungano. Tusiwe wenye kuzunguka kwenye ishu hii ya muungano bali kila mtanzania apaze sauti na kusema kila nchi ijitawale yenyewe. Otherwise kama unaupigania muungano utuambie wewe unafaidikaje binafsi wakati wenye nchi wameukataa. Mimi sitaki muungano.
 
Last edited by a moderator:
Mambo yao ya zanzibar waachieni wenyewe nyinyi hayakuhusuni mbona mnawabana kwenye mambo mengi sana

Hatuwabani. Wao ndio wanaofanya mambo ya ovyo na kutuweka sisi hatiani. Mapato wanayoyapata kwa kusajili hizo meli hayafiki JMT, lakini JMT ndio inalazimika kulipa ada IMO kila mwaka! Upo hapo? Sasa nani kabanwa?
 
Mkuu wewe ni muandishi wa habari?
La hasha! nathamini sana kazi yao.
Nachukia mtu anapokwepa ukweli na kuwasingizia wao kwa kufanya kazi yao kwa njia sahihi na zilizotukuka.

Waziri hana sababu ya kuwalaumu waandishi wa Tanzania bara wakati dunia nzima imeandika.
Alichotaka hapa ni ku insinuate suala la muungano ili kufunika uvundo wa bangi.
Waziri alipaswa kwanza kuonyesha masikitiko, pili kulaani na tatu kutoa ufafanuzi.

Hakukuwa na haja ya kuwananga na kuwadhalilisha waandishi wa habari kwa kutimiza wajibu wao.
Tatizo la meli ya bangi ilisajiliwa Zanzibar ndilo tatizo kubwa sio mtu aliyetueleza shehena hiyo ya biashara ilikamatwa wapi ikitokea wapi na mali ya jamii gani. Ni kuwaonea sana waandishi na inauma sana kwakweli.
 
Well, haikuridhika sijui kama inafanya kazi vema ukilinganisha na mamlaka waliyoikimbia. Wansajili meli mobovu sana duniani na kuua watu wao (juzi wameadhimisha kumbu kumbu). Wanasajili meli kwa wakala wasiyejua anabeba bidhaa gani kama hili la bangi tunaloliongelea. Zipo taarifa kutoka kwa wazanzibar kuwa ZMA na Philatec ni mradi wa watu serikali ni daraja, hilo sina uhakika nalo ninachojua lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Lakini muhimu hapa ni ukweli uliousema kuwa baada ya kutoridhika na mambo ya muungano wakaamua kujiondoa. Tunakubaliana wameshajiondoa na hawana uhusiano na muungano tena.Usisahau kuwa baada ya kutoridhika na mambo ya muungano na kuunda ZMA bado walikaa kimya katika kujiandikisha IMO na ada zao zililipwa na muungano ule ule mbaya.

Hakuna jaribio lolote lililofanywa la kujiunga huru! hakuna! na sababu kubwa ilikuwa ni kufanya shughuli kwa mgongo wa Tanzania a.k.a Tanganyika kwa kuvizia malipo. Huu kama si uhuni sijui tuuite nini. Hakuna suala la kama usingekuwepo muungano kwasababu tayari kujiondoa ni kuwa hawakuwa sehemu ya muungano Kuwataka kuungana sidhani kulimaanisha kuwa Tanganyika ina dhiki. Nikiweka sawa rekodi mara zote nimesema na leo nasema Zanzibar itabaki kuwa nchi nje ya muungano kama ilivyokuwa kabla

Kinachojitokeza kwasasa ni Zanzibar kuwa tegemezi kwa Tanganyika. Mathalan, kuna sababu gani mtu wa kidatu Morogoro alipe umeme na mzanzibar atumie au alipe kidogo. Kuna sababu gani SMZ hailipi umeme ikijua unazalishwa kwa gharama. Matokeo ya hilo ni bei kuongezwa kwa Mtanganyika ili kumfidia mzanzibar. Hapo hakuna kunyonyana kweli.

Mfano wa pili: Zanzibar wanasheria zinazobana ajira kwa Mtanganyika. Wakati huo huo wanaomba ajira asilimia 21 kutoka Tanganyika. Katika muungano huu wao wametoa ajira zipi kiasi cha kusema tunategemeana?
Mfano wa tatu: Elimu ya juu haipo katika mambo ya muungano, wao wamekubali kuingizwa kwasababu hiyo ni huduma. Ingekuwa ZMA wasingekubali kwasababu kuna mafao.

Watoto wao 1000 wanatengewa nafasi na malipo wasiotakiwa kurudisha mikopo kila mwaka.
Uwezo wao ni kudhamini watoto 800 kwa gharama za SMZ. Hakuna Mtanganyika anayefaidika na udhamini huo wa 800, isipokuwa mtanganyika analazimika kunyimwa fursa ili apate mznz kwasababu ni mzanzibar.
Wakati Mtanganyika analipa mkopo mzanzibar ana asilimia 21 za ajira. Kama si kunyonyana sijui tuseme ni nini.

Mfano wa nne: Kuna wabunge kutoka znz na wale wa baraza la wawakilishi.
Gharama zao Dodoma zinalipwa na JMT a.k.a Tanganyika sio BLW au SMZ. Kama si kunyonyana sijui ni nini.

Haya ni kwa uchache kuonyesha jinsi gani wenzetu wameweka mirija yao huku wakiwa wazuri sana wa kupiga mdomo wanaonewa. Anayeonewa ni mwananchi wa kidatu anayelipa umeme kumfidia mzanzibar asiyelipa serikali yake hailipi.
Nikuhakikishie znz itakuwa na jeshi lake hilo halina shaka. Ninachokataa ni kusema kuna usawa wa mambo ya ulinzi na usalama, hapa usijaribu kufananisha Tanganyika na Zanzibar hata kidogo. Ni hivi bajeti ya ulinzi na usalama ya JMT inayoshirikisha znz ni mara mbili ya bajeti ya znz. Bajeti ya znz kwa mwaka huu ni nbilioni 700. Bajeti ya wizara ya mambo ya ndani na wizara ya ulinzi ni zaidi ya 1.4 trilion. Kwa hesabu ni kuwa kama znz ikishiriki katika usawa wanaoutaka kama mbia basi haitabaki hata na senti tano ya kununua sindano.

Ulinzi na usalama ndio hoja ya sasa ya waznz. Wanasema rasimu iondoe kila kitu isipokuwa katiba na ulinzi na usalama.
Huu kama si upuuzi sijui tuite nini. Kwanini tuwe na muungano wa ulinzi na usalama peke yake na tusiwe na MoU tu.

Nchi gani duniani ina muungano au shirikisho la ulinzi na usalama tu.Hoja kubwa ya wznz ni kuelewa kuwa gharama za ulinzi na usalama ambazo hawana kwa nusu karne zinaweza kubebwa kwa njia kama ya umeme Kwanza kutegemeana sijui una maana gani, kigharama au kitishio?
Kigharama hakuna kutegemeana hata kidogo. Tanganyika itakuwa inakamua ng'ombe mgonjwa na hiyo ni dhambi kubwa.
Unategemeaje ZNZ kwa gharama kama hawawezi kulipa umeme?Kwa tishio nakubaliana nawe. Tuishie hapo.

Mbona tumepaza sana sauti kuwa znz watusaidie kuvunja muungano na hawataki? Tuliwaambia wasusie tume ya warioba wenzetu wakataka wajumbe sawa. Tukawaambi wazuie wabunge wenzetu wabunge wa CCM unawasikia. Tukawaambia wapeleke mswada BLW hakuna aliyethubutu n.k. kinyume chake wanataka muungano wa mkataba ambao hawawezi kuutetea ni kitu gani bali wamesikia tu mtu mmoja ana sharubu nyingi pengine akisema,au mzee mmoja akiongelea masikani n.k.

Tanganyika haiwezi kuvunja muungano kwasababu yenyewe ndio muungano. Kwa msingi huo sisi tunaongeza nguvu Tanganyika irudi kila nchi isimame kivyake. Tanganyika ikirudi mambo yatanyooka sana lakini nanyi wznz tusaidieni basi habari ya kutaka vyeo na makao makuu, muungano wa mkataba na vituko vingine muache. Ongozweni na weledi si jazba.
 


Nguruvi3 unataka tufahamu kuwa hao uliowaandika hapo ndio wa mrengo wako au ukimaanisha wao tu washiriki katika kuelimishana?
 
Ninyi si wazanzibar? Utanzania si mliukataa tena kwa katiba, leo unajiitaje Mtanzania.
Watanzania wanaokamatwa ni wale wanaoitambua JMT sijui kama wznz wanaitambua.

Alaa kumbe bendera haitambuliki kimataifa!!! sasa zile kelele za kutaka wimbo wa taifa na bendera ya znz zilikuwa za nini?
Vipi kama mngetangulia kwanza kujitoa halafu mkawa na bendera. Kwahiyo sasa hivi bendera ya znz ni sawa na ya Yanga au Simba! sijua hilo maana kelele zilikuwa nyingi sana kuhusu bendera.

Tatu sasa kama bendera ilikuwa ya JMT kulikuwa na haja gani ya kuanzisha ZMA?

Na mwisho ni kweli Watanazania wanakamatwa na madawa, hiyo ni tofauti na serikali ya nchi kushiriki katika biashara ya bangi.
Watu wanakamatwa duniani ni nadra sana kusikia serikali inashiriki biashara kama ya bangi,ni rare!!
 
Hakuna Tanzania Zanzibar, wznz walikataa kwa kutumia katiba yao neno Tanzania sasa wewe unatiwa kichefu chefu. Wazanzibar ni wazanzibar bwana, leo uwaite Watanzania, tafadhali ndugu yangu.

Meli haikuandikishwa na JMT, nionyeshe imeandikishwa vipi. Kinyume chake meli imesajiliwa na SMZ kupitia ZMA yenye wakala Philatec ya Dubai. Makubaliano hayajulikani na yoyote isipokuwa SMZ. Linapotokea kama hili la kubeba bangi na kuzunguka nayo duniani hilo halina mjadala.

Waandishi wa dunaiani wameadika sana kuhusu zigo la bangi ya zanzibar. Hakuna kiongozi aliyelaani hilo si SMZ ua Wapinzani . Kinyume chake waziri wa miundo mbinu 'anawavamia ' waandishi wa habari wa Tanzania bara kwa hoja kwanini wameandika mambo ya bangi la zanzibar. Kosa la waandishi ni nini?
Mtanganyika ni nani ndugu yangu? Kuna Mtanzania na Mzanzibari na ingekuwa busara kuuliza madhara kwa Mtanzania kama yanavyoletwa na mauwaji ya maalbino na usafirishaji wa madawa kupitia JNIA. Watanzania wote wanapata madhara kwa tendo lolote baya!
Madhara ya madawa yameathiri kila mahali na si Tanzania au Zanzibar tu, mataifa yote yameathirika. Tofauti ya madawa ya kulevya ya JNIA na bangi la meli ni kuwa kimoja kimefanywa na watu binafasi kingine kimefanywa na taasisi ya serikali. Ndugu yangu kashfa ya nchi ni tofauti na kashfa ya mtu kukaa utupuKumbuka hapo juu ulishasisitiza utengano wa SMZ na JMT lakini unapata karaha linapokuja suwala la mafao.
uliona kichefuchefu kwa kuharibiwa jina, aisee unahangaika, hutulii!
Karaha ya mapato si kwakuwa znz inafaidika na biashara hii ambayo haikubaliki katika imani za dini, karaha ni kuwa wanapata pesa za kutosha kwanini wasilipe ada zao hadi wasubiri kodi ya muuza mitumba na madafu wa Tanganyika?
yenye mzigo wa Bangi ya SMZ.Unaona jinsi chuki zako zinavyokupotowa? Eti ni mzigo wa bangi wa nani?
Hakuna chuki hapo jamani mbona hamuelewi? JMT haikujua hiyo meli na zingine 400 zilizosajiliwa na Zanzibar.

Waziri wa miundo mbinu wa SMZ akubali kuwa meli hiyo ya bangi imesajiliwa Zanzibar.
Akatoka mbio kwenda kuwashambulia waandishi wa Tanzania bara kwa kuandika habari ambazo zipo duniani.
Pengine waziri walikusudia kulifanya jambo hili siri. Hatujui ni siri ili tusijue kodi zetu zinalipia biashara ya mihadarati au alitaka lisisemwe ili zigo la kashfa ya bangi libebwe na Tanzania. Hilo sijui.

Waziri wa SMZ asingetumia muda kushambulia vyombo vya habari. Tena hakulaani tukio hilo la zigo la mhadarati tani 30 za bangi ya meli ya znz. Hivi mwenye akili timamu anahitaji maelezo gani zaidi!
 
kwa mara ya kwanza leo tuko pamoja lakini kwani ccm mna wangangania hawa znz haya yatakoma tukishakuwa na tanganyika yetu..

Tatizo lako unafikiri napigania maslahi binafsi !Mimi sitaki hata kuusikia sijawahi kuona faida yake zaidi ya watu kulia wanaonewa lakini hawataki kujiuondoa kwenye muungano; mimi ni CCM lakini siutaki hatuna shida ya muungano wa aina yoyote na hawa wabinafsi!
 
kwa hiyo msimamo wako ni upi gamba we? Serikali 2 au 3?

Kikaragosi wewe ni kipi usichonielewa? Narudia tu Tanganyika hatuhitaji muungano na mtu yoyote? watu milioni 45 tulioungana tunatosha!
 
Kuna mtu hapa anayo mikataba ya kuisajili Meli ? Isije kuwa mnazungumza msichokijua ?

Nimekukodisha gari (Rent car) ,kisha umeenda kuitumia kwa ujambazi,umekamatwa ,mimi niliekukodisha nitaingiaje kwenye kesi hiyo na kuwa mkosa ? Wacheni umbutwai !
 
Swali la msingi hapa ni kwamba Zanzibar ni nchi au si nchi... Hili swali hata mzee wa "wapingwe tu, kwani tumechoka" alishindwa kujibu pale bungeni...

Jibu ni rahisi! Zanzibar ni nchi ina serikali yake na katiba ambayo imefafanua wazi kuwa Zanzibar ni nchi na kueleza mipaka ya nchi hiyo yenye rais, bunge, wimbo wa taifa, bendera, jeshi,nk. ZANZIBAR NI NCHI SIO MKOA WALA JIMBO. La kusikitisha zaidi mpaka mtu ulie ni kuwa TANGANYIKA SIO NCHI! Na sio nchi kwasababu wenye nchi hawataki iwe nchi na viongozi wao hasa wa CCM wanaogopa TANGANYIKA kuwa nchi kama ukoma. Mzanzibari mmoja kachania hapa Jf aliyesema kila Mzanzibari ni Mtanzani lakini si kila mtanganyika ni Mzanzibari
 
kabla ya hao niliowataja nimeandika haya ''Hebu tuelimishane kwa pamoja wanajamvi wote'' nenda katika bandiko.
Ambayo ni usanii na unafiki mtupu.

Utasemaje tuelimishane wanajamvi wote halafu unatutajia majina ya wapenzi wako kumi?

Kama unadhani open forum modality haikidhi viwango vya mjadala wako basi waandikie pm hao wapenzi wako mkajadiliane pembeni huko! Mnataka kujifanya kama ma prima donna wa opinion leadership kumbe hakuna umakini wowote wa maana, mtu makini hawezi kualika watu mjadalani halafu akataja wapenzi wake watano anaowataka, unafiki mtupu.
 

Mkuu wewe lazima utakuwa muhariri wa gazeti la nipashe au umemaliza chuo juzi bado thinking capacity yako is too low kujua mambo ambayo yalokuwepo ndani ya muungano wote na kilicho tokea kwenye hiyo issue ya meli lakini very soon kila kitu kitakuwa sawa na kila mtu atapata anacho kihitaji katika maslahi ya nchi yake
 
Mkuu Pasco pamoja na kuufananisha muungano wetu na ndoa ya kikristo bado wakristo pia hupewa idhini ya muda ya kutengana iwapo ndoa ipo katika hali tete! Kwa hiyo mimi nilikuwa nadhani tutengane kwa muda!
 
kwa hiyo unapingana na msimomo wa chama chako, huogopi kufukuzwa kwenye chama kama alivyofanywa yule mzanzibar...
 
Nguruvi3, hivi waziri mwenye dhamana kwa Zenj ni chama gani?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…