Sikieni hoja za wazanzibar

Sikieni hoja za wazanzibar

wazanziabari wanaokufa Dafur DRC wale ni nani SMZ au JMT wacheni upumabvu
kama wenzenu wamekuzidini kete mlie tu
Hoja ya bandiko hujaijibu.
Lakini si huwa mnataka usawa wa kila jambo, kwanini mlalamike yakitokea ya Darfu? Si ndio usawa wa kugawana madaraka huo! au kugawana madaraka ni veyo?
 
Muungano upo kwa kuwa Tanganyika haikuwepo. Tufanye subira kidogo. Tanganyika inarudi, Muungano hautakuwepo na haya yoote yatatoweka.
 
Hatuna wivu wa biashara ya bangi inayofanywa na SMZ. Hatuna kabisa.

Waziri wa miundo mbinu keshaitetea sisi tunasema bendera yetu kufungia tani za bangi haifai!

Inachafua sura ya nchi na hata znz. Hivi OIC(Shirika la dini) wakisikia znz inafanya baiashara ya bangi watakuwa happy kweli,

Mkuu tuweke wazi,bendera yenu ipi uliokusudia?
 
Mkuu tuweke wazi,bendera yenu ipi uliokusudia?
Yetu ya Tanzania ambayo imetumika katika kufungia zigo la bangi lililopaswa kufungwa na bendera ya Zanzibar, au nimekosea?
Sheria ya usafiri wa majini ya mwaka 2003 znz ilijitoa na kuanzisha usafiri wa majini na bandari ya mwaka 2006.
Hadi hapo znz haikutaka kutumia bendera yetu bali bendera yake iliyoanzisha ZMA. Umeelewa.

Sisi tuliobaki kama Tanzania na sheria ya usafiri wa majini ya mwaka 2003 ndio wenye bendera ya JMT.
Usajili wa meli ulifanywa na Philatex kwa idhini ya ZMA ambayo ni taasisi ya SMZ iliyounda sheria ya 2006 na kujitoa JMT.

Tunapochafuliwa na mzigo wa Zanzibar uliofungwa na bendera yetu kama nilivyosema inakera.
 
Mkuu futa kauli yako sisi hatufanyi biashara ya bangi
Waziri wa miundo mbinu wa znz hakulaani wala kuonyesha kuchukizwa na meli iliyosajiliwa na ZMA taasisi ya SMZ.

Kilichomkera sana Mheshimiwa Seif Suleiman ni habari hizi kuandikwa na magazeti tena ya Bara kama wanavyosema. Habari zimeandikwa na vyombo vyote vikubwa duniani vikiwa na jina la Tanzania kwasababu ndio yenye bendera katika meli ya bangi ya zanzibar. Kwa kuonyesha jinsi BARA walivyo na wivu na wanavyozuia biashara za ZNZ waziri kaamua kuvinanga vyombo vya habari kisawa sawa! ala! kwanini waongelee biashara isiyowahusu!

Hapa anayesema bangi ni ya znz si mimi ni kutokana na waziri kuridhika na suala la bangi na kukasirishwa na kuandikwa kwa suala la bangi. Hakuna tatizo kama waziri alikuwa anasiamamia masilahi ya znz ambayo ni kazi yake lakini kutuhusisha na kutuchafua halikuwa jambo la kliungwana hata kidogo

Nadhani ungemshauri waziri afute kauli ya kushambulia vyombo vya habari vinavyosaidia mapambano dhidi ya mihadarati na badala yake aeleze umma nini ZMA, imesajiliwa na chombo gani duniani, Inalipa ada zake kutoka wapi. Pia aeleze uhusiano wa ZMA na Philatex ya dubai na JMT.
Kisha afafanue kuhusu mzigo wa bangi uliokutwa katika meli iliyosajiliwa na SMZ kupitia taasisi na wakala wake.

Ndugu yangu endapo waziri hawezi kulaani bangi tani 30 analaani wandishi na vyombo vyao wewe unaelewaje?
 
Ungejua ndugu yangu usingeandika hay6 maelezo yako.
CHAMVIGA kuna kitu kinaitwa vision. kama hunacho una tatizo kubwa sana. Naomba uachie hapo maana aliyelala usimwamshe, ukimwansha...... Tumekuelewa mkuu ila si kila mmoja atakuelewa. Matter of time
 
Last edited by a moderator:
Ulinzi na usalama pia. Mkatae muungano wa mkataba au serikali 3. Mkishindwa hayo mtakuwa chini ya JMT mtakae msitake.

Mkuu leo ndio umenifumbua macho kumbe wale wazungu kutoka uk nyinyi ndio mume watupia tindikali na nyinyi ndio manchoma makansa ndio njia yenu ya kuwafanya mabwana zenu wa ulaya wajue kuna nchi inaitwa zanzibar sisi tunategemea nguvu za Mwenyezi Mungu tu
 
Unafanya spinning ukwepa hoja ya bandiko. Huko unakotaka twende kwasababu una 'ujuzi' nako mimi siendi. Mada si matusi wala kashafa, ni juu ya waziri wa zanzibar kuwananga waandishi wa habari wa Tanzania kwa kuandika habari hizi na wala si wa duniani ambako meli imeonekana ikiungua moto na juu bendera ya JMT ipo.

Narudia waziri hakuona tatizo katika mzigo huo wa tani 30 zenye bilioni 125 thamani. Tatizo lake kubwa sana ni kwanini hanari hizi zimeandikwa! Hapo unaweza kuona jinsi ambavyo zigo la bangi ya Zanzibar lisivyousa hisia bali mashambulizi kwa waandishi wa Tanzania bara kwa kuandika.

Hoja ni kwanini SMZ yenye ZMA ambazo si sehemu ya JMT kwa makusudi kabisa wameamua kutumia bendera ya JMT kufunikia tani 30 za zigo la bangi. Hili ndilo lipo mbele yetu na linakera sana.
Hatuna kero na bilioni 125 za mapato, kero ni kutumia bendera yetu kufungia zigo la uhalifu na waziri wa SMZ kutoonekana hata kujali yarabi!

Waziri anaita waandishi wa habari kulaani waaandishi hao na si tani 30 za zigo la bangi, hii inaingia akilini kweli.
Kama inaingia kwanini tusidhani mzigo huo ni wa biashara na waziri alikuwa anatetea masilahi ya nchi, why?
 
Mi nlijua nyie wasomi kumbe wadanganyika! Umewahi kuona wap mume akibadilisha jina? Pili Nguruvi, soma ebu, bendera ya zanzibar haitambulikani kimataifa, kwaiyo meli yoyote iliyosajiliwa Zanzibar ama tanganyika lazima ipeperushe ya tanzania. Kisha tambua, hio ni ya tanzania sio ya tanganyika. Ebu leo tutizame, meli hiyo mmiliki nani? Usikute myanganyika mwenzenu. Lakini kwa nini ilaumiwe zanzibar kwa kosa hilo nakudai eti tunaichafua tanganyika? NI CHUKI ZENU TU. watanganyika wangapi wamekamatwa na unga na huandikwa tanzania? Mbona hamusemi hilo kuwa linatuchafulia na sisi?
 
nadhani itakuwa ya Kinana! Msomali
 
Kauli ya Waziri wa Mawasiliano na Miundo mbinu wa SMZ, Rashid Seif Suleiman ya kuvilaumu vyombo vya habari vya Tanzania BARA ilinishangaza sana.

Ni kweli kabisa kuna kitu viongozi wetu waasisi wa 'muungano' walikiona kama kilikuwa ni cha muhimu sana kuziunganisha nchi zetu, lakini vile vile makosa ya kutokuelimishwa na kutoshirikishwa kwa wananchi wengi katika kufikia uamuzi huo ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwa chanzo cha mitikisiko na utegemezi katika 'muungano'.

Imedhihirika kuwa viongozi wakuu waliokuja baada ya marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na pia Wazanzibari wengi hawakutaka kuendelea kuwepo muungano na kwa sababu hiyo ilibidi viongozi wetu wawabembeleze kihoja na ilipobidi pia yalitumika mabavu ili waendelee kuwepo mwenye 'muungano' . Hii ilipelekea wananchi wengi wa Zanzibar na pia wachache wa bara kuamini kama viongozi wakuu wa bara walikuwa na ajenda fulani za siri ambazo kuzitimiza ilibidi tuwaombe na kuwashinikiza Wazinzibari waendelee kuwepo kwenye 'Muungano'.

Fikra na mitazamo hii imekuja kujisimika zaidi pale badhi ya viongozi wakuu wa Zanzibar walipotiwa misukosuko pale walipohoji uwepo wa muungano na manufaa yake.

Kwa sasa wanafanya kila wanachotaka bila kujari mshikamano, sheria na taratibu za nchi wakidhani kuwa Tanganyika inawahitaji sana zaidi ya wao kuihitaji Tanganyika.

Hata kujitoa kwao katika sheria za Jamhuri ya muungano zinazohusu usafiri wa majini za mwaka 2003 na kuunda sheria zao za bahari na usafiri na kuwa chini ya Zanzibar Maritime authority((ZMA) mwaka 2006 ilikuwa ni katika mwendelezo wa fikra hizo.

Waswahili wanasema, mdharau mwiba mguu huota tende!.

Tumezidharau na wakati mwingine kuzipuuzua chokochoko za 'muungano' kwa muda mrefu huku tukiwadekeza Wazinzibari kwa kuwapa kila kile wanalichokuwa wanakitaka na matokeo yake kwa sasa tunayaona. Kwa sasa imekuwa chao ni chao lakini chetu pia ni chao na wakati mwingine wanataka wakichukue chote.

Tulianza muungano vibaya na inavyoonekana pia tutaachana nao vibaya, na kwa maana hii, dawa ya muungano kwa sasa siyo serikali tatu kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali ni kuachana kabisa na muungano ili pande zote zipate ukweli halisia kama kuna umuhimu katika muungano. Hatutakuwa wa kwanza wala wa mwisho katika kuvunja muungano kwa sababu kuna nchi zimevunja muungano na zikapiga hatua zaidi za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hata katika ndoa, watu wanapokinzana sana, huwa wanafikia maamuzi ya kuachana ili kujipima na kuona umuhimu wa wao wakiwa pamoja au wakiwa single (space) na wakipatwa na reality, wengi wao hurudiana tena.

Mkuu Ng'wamapalala nimekusoma vizuri sana. Hapa suala sio kuendelea kuukumbatia Muungano bali kila mtu achukue chake. Mpaka inatokea zanzibar inaamua kuanzisha chombo chake huru cha usafirishaji (ZMA) na huku Tanganyika au serikali ya muungano ndio inalipa huu ni udhaifu mkubwa ulionyeshwa na serikali tanganyika/muungano. Sijaona sababu ya kumlaumu zanzibar hao waliomruhusu kuanzisha ZMA ndio tunapaswa kuwahoji ni kwanini walimruhusu zanzibar kuwa ZMA? Walimuogopa nini mpaka kumpata chansi hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Unafanya spinning ukwepa hoja ya bandiko. Huko unakotaka twende kwasababu una 'ujuzi' nako mimi siendi. Mada si matusi wala kashafa, ni juu ya waziri wa zanzibar kuwananga waandishi wa habari wa Tanzania kwa kuandika habari hizi na wala si wa duniani ambako meli imeonekana ikiungua moto na juu bendera ya JMT ipo.

Narudia waziri hakuona tatizo katika mzigo huo wa tani 30 zenye bilioni 125 thamani. Tatizo lake kubwa sana ni kwanini hanari hizi zimeandikwa! Hapo unaweza kuona jinsi ambavyo zigo la bangi ya Zanzibar lisivyousa hisia bali mashambulizi kwa waandishi wa Tanzania bara kwa kuandika.

Hoja ni kwanini SMZ yenye ZMA ambazo si sehemu ya JMT kwa makusudi kabisa wameamua kutumia bendera ya JMT kufunikia tani 30 za zigo la bangi. Hili ndilo lipo mbele yetu na linakera sana.
Hatuna kero na bilioni 125 za mapato, kero ni kutumia bendera yetu kufungia zigo la uhalifu na waziri wa SMZ kutoonekana hata kujali yarabi!

Waziri anaita waandishi wa habari kulaani waaandishi hao na si tani 30 za zigo la bangi, hii inaingia akilini kweli.
Kama inaingia kwanini tusidhani mzigo huo ni wa biashara na waziri alikuwa anatetea masilahi ya nchi, why?

Mkuu zanzibar ni nchi ya kiislamu haiwezi kufanya biashara za haramu hata siku moja na meli kama imekamatwa na bangi sio kosa letu kwanini mnashikia bango sana mbona nyinyi serekali yenu inafanya ujambazi kila siku sisi tupo kimnya kwanini hili mmeshikia bango sana ?
 
Mkuu Nguruvi3 Hivi kama muungano usingekuwapo unadhani malalamishi ya kuchafuliwa kwa tanganyika na nchi ya zanzibar, na sio Tanzania kama unavyoandika ingetokea?
Nb tanzania ni pamoja na tanganyika na zanzibar yenyewe. Na kama jibu nila unadhani ni nani wa kulaumiwa? Walioasisi Muungano au wanaondeleza muungano?
 
Hapa kuna issue ya muungano watu wanachanganya. Hili si suala la muungano.
Hoja ni hii niweke kwa urahisi zaidi.

Mwaka 2003 Zanzibar wanajitoa katika usafiri wa majini wa JMT na kutokuwa sehemu ya JMT kwa suala hilo. Walifanya hivyo kupitia BLW bila kuishirikisha JMT na wala hawakuwa na mawasiliano zaidi ya kuondoka kama walivyofanya katika katiba mara nyingi.

Mwaka 2006 wakaanzisha chombo chao cha ZMA akinachosajili meli. Hadi sasa wanasajili meli 400 kupitia Philatec bila kushirikisha serikali ya JMT

June 2013 meli zilizosajiliwa na Zanzibar kupitia ZMA na Philatec zaonekane zikiisaidia IraN kinyume na vikwazo vya UN. JMT yapokea barua za onyo kutokana hjambo isilolijua.

Mwaka 2013 Sept meli yakamatwa ikiwa na bangi tani 30. Imesajiliwa na ZMA na Philatec kama taasisi za SMZ. Picha na habari za zagaa duniani kuhusu JMT.

Waziri wa miundo mbinu ajitokeza kulaumu vyombo vya habari vya Tanzania bara kuweka habari hii wazi kwa wananchi. Amezea kulaani au kueleza ushiriki wa znz katika zigo hili la aibu

Waziri Mwakyembe wa JMT aingilia kati kutoa ufafanunuzi wa jambo lisilo la JMT ambalo znz imeshajitoa.

Tangau mwaka 2003 ada za usafiri wa majini zinalipwa na JMT wakati znz imeshajitoa na kuwa na chombo chake bila kuishirikisha JMT. Udanganyifu wa juu kabisa.

Sasa tunataka tuelezwe uhusiano wa
1.Jumuiya ya kimataifa na JMT kuhusu zigo la bangi. Wapi na kwanini tuhusishwe
2. Kwanini znz itumie bendera ya JMT waliokataa kuwa sehemu yake mwaka 2003
3. Kwanini waziri wa JMT ashughulikie mambo yasiyo mhusu
4. Kwanini waziri alaani vyombo vya habari kwa habari za dunia na si bangi
5. Kuna uhusiano gani wa vyombo vya habari vya bara na zigo la bangi, kwanini isiwe vyombo vya habari vya Italia.
6. Kwanini JMT ilipe ada IMO kwa chombo ZMA kisicho na masilahi na JMT na ibebe lawama na kashfa zinazotokana na chombo kilichoikana JMT

Ukishaelewa hapo utaona suala la muungano halina mantiki zaidi ya mantiki ya ''hujuma'' kutojali na kushiriki kwa mgongo wa
 
Back
Top Bottom