Sikia maajabu haya ya Mwalimu wa shule ya Kata

Pole sana kaka UDSM ndo English imelala eee....Nimesoma hapo na hadi nahitimu nilikuwa nikicheka tu watu wanavyoongea vingereza...et UDSM
Nakubaliana na wewe elimu yetu imeshuka sana. Sio English tu hata Kiswahili kinawashinda wengi humu jamvini. Tunahataji total transformation ya leadership system in our country kama tuko serious ku rescue hii situation.
 
Hahahahahaha! Walimu wa shule hii wanatisha kwa kweli. Leo tena wameendeleza vituko vyao! Mwalimu mmoja kwenye shule hii alikuwa akifundisha somo la Jiografia kidato cha kwanza, kama sikosei. Akauliza wanafunzi wake: A line which DIVIDE Earth into two parts is called WHOM? Du, hii ni kali ya mwaka... A LINE CALLED WHOM? Haya sasa masikhara I see.

tpaul;
Wadhani mwalim ka huyu asikie wakizungumzia kuhusu kukizika kiingereza leo leo si atakuwa wa kwanza kusema na kife kabisa?? Ndg zangu, tusijilinganishe na wengine ati mbona wachina... ni ukichaa tz yangu kujilinganisha na super powers.
 
Ndo maajabu ayo? ? Kasentesi(Where does it located)aka tu ndo kamekuleta apa kuandika ushuzi huu? Achia io pumba musee
 
Wakuu, wale manaotetea uzembe kwa hali na mali hebu jioneeni jinsi uzembe wa walimu unavyoenea kutoka ngazi ya Kata hadi ngazi ya Taifa. Yafuatayo ni baadhi ya maswali yaliyochukuliwa kutoka paper ya mtihani wa chemistry (CSEE) wa mwaka 2016. Tazama jinsi mitihani inavyotungwa kwa kiingereza kibovu na cha kuungaunga. Inasikitisha sana paper moja tu, tena ya mtihani wa kitaifa, inakuwa na makosa mengi kiasi hiki! Prof Ndalichako huwa anajidai kuwa anajua saaana wakati wizara inamshinda kuendesha. Hv anakuwa wapi wakati watumishi hawa waliopo chini ya usimamizi wake wanapoandika kiingereza cha ovyo kama hiki huku akifahamu kwamba hii ni paper ya kitaifa?

Kwa sababu hii, nadhani kuna haja ya kuufanyia marejeo mfumo wetu wa elimu vinginevyo wimbi la vilaza (wanafunzi, walimu, wakufunzi, wahadhiri, nk) litaendelea kutamalaki katika nchi hii huku wakitetewa na vilaza wenzao (na wengine wamo humu JamiiForums kwa gharama ya upotofu wa kielimu kwa watoto wetu.
upload_2017-2-8_15-45-59.png

upload_2017-2-8_15-47-32.png
 
Leo nimetembelea shule moja ya Kata nikashuhudia kituko cha mwaka kutoka kwa mwalimu mmoja shuleni hapo.

Mwalimu huyo amehitimu Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni na akaajiriwa moja kwa moja kufundisha katika shule hiyo ya Kata.

Wakati akiendelea kufundisha nilimsikia akiwauliza wanafunzi swali hili: WHERE DOES IT LOCATED?

Inaonekana ni mwalimu wa somo la Jiographia, hivyo alikuwa akiwauliza wanafunzi wake wamtajie location ya kitu fulani kwenye ramani.

Jamani, hapa ndipo shule za kata zilipotufikisha. Ikiwa mhitimu wa Chuo Kikuu anaongea kiingereza kibovu kama hiki, tena mbele ya wanafunzi,mnategemea wanafunzi anaowafundisha watapata maarifa gani kutoka kwake?

Chukulia huyu ni mwalimu wa Kidato Cha Kwanza, wanafunzi wake wanaoambiwa kila siku "SPEAK ENGLISH" wataiga kiingereza gani kutoka kwake? Si ndio atawapoteza kabisa?

Ikiwa walimu hawajui kiingereza unategemea nini kutoka kwa wanafunzi wao? Haya ndio madhara ya serikali yetu kuchanganya elimu na siasa. Tumekwisha hasa!!
Mimi SUA pia nilisikia Kingereza cha ajabu namna hiyo.Inaelekea ndio hali halisi ya vyuo vyetu kwa sasa.Very pathetic indeed.
 
Wachina na wajerumani wenye maendeleo makubwa wanajua Kiingereza ?, pili ushasema ni mwl. wa Geography si kosa lake

Tatu ww kwa siku Kiswahili lugha yako unachapia mara ngapi ?

Nne ; watoto wenu mlokuwa mnawepeleka Kusoma Uganda na Kenya miaka michache ilopita mbona hamuwapeleki baada ya kuona watoto wanaendelea kuwa vilaza Tano Rekebisha ulitaka Mwl. aseme vp.
umemuelewesha vizuri.yy kwa ubongo wake robo gram anadhani kiingreza ndo elimu.yaani mwalimu akiongea kiingereza sn ndo kujua kufundisha.kiingereza ni lugha tu kama kigogo.
 
Duuh eti jamaa anasema kabisa ameona kituko cha mwaka!!!! We huna kazi za kufanya Mkuu acha kuleta story za kijinga. Na Trump alivyoshindwa kutaja neno Tanzania vip nae elimu yake ya UDSM?
 
waliomponda mleta mada naamini ni kati ya ambao kiingereza kinawakwaza. wanafunzi wa vyuo vikuu wana msingi dhaifu wa lugha hiyo. wanafunzi discusions zao wanafanya kwa kiswahili. kuna somo la kiingereza kwa chuo cha saut tabora. big up, itawasaidia wa aina ya mwalimu wa shule ya kata.
 
We shida yako tushaijua,ni kukidhalilisha chuo chetu kikuu kitakatifu cha UDSM,kwa kifupi wewe ni mchochezi
 
Tpaul una chuki na chuo kikuu cha Dar es salaam

Kama tuhuma zangu sio kweli sema chuo ulisoma wapi na kozi gani.

Je hukuwahi kuomba kusoma UDSM?

Bila shaka uliomba na hukupata, hii habari umeipika kwa lengo la kuonesha UDSM inatoa wahitimu wenye uwezo mdogo.

Pole mkuu hata huko Teofilo Kisanji ulikosoma wewe pia ni Chuo kikuu
 
umemuelewesha vizuri.yy kwa ubongo wake robo gram anadhani kiingreza ndo elimu.yaani mwalimu akiongea kiingereza sn ndo kujua kufundisha.kiingereza ni lugha tu kama kigogo.
Mkuu hakuna mtu anayekataa kwamba kiingereza sio lugha yetu lakini kwa msomi wa ngazi ya chuo kikuu kuongea kiingereza kibovu kama hicho inatia ukakasi.
 
waliomponda mleta mada naamini ni kati ya ambao kiingereza kinawakwaza. wanafunzi wa vyuo vikuu wana msingi dhaifu wa lugha hiyo. wanafunzi discusions zao wanafanya kwa kiswahili. kuna somo la kiingereza kwa chuo cha saut tabora. big up, itawasaidia wa aina ya mwalimu wa shule ya kata.
Asante sana kwa kunielewa mkuu maana kuna wengi ambao bado wanakodoa macho kodo kwa kunisakama badala ya kuchangia hoja maridhawa iliyo mezani.
 
Wakuu, wale manaotetea uzembe kwa hali na mali hebu jioneeni jinsi uzembe wa walimu unavyoenea kutoka ngazi ya Kata hadi ngazi ya Taifa. Yafuatayo ni baadhi ya maswali yaliyochukuliwa kutoka paper ya mtihani wa chemistry (CSEE) wa mwaka 2016. Tazama jinsi mitihani inavyotungwa kwa kiingereza kibovu na cha kuungaunga. Inasikitisha sana paper moja tu, tena ya mtihani wa kitaifa, inakuwa na makosa mengi kiasi hiki! Prof Ndalichako huwa anajidai kuwa anajua saaana wakati wizara inamshinda kuendesha. Hv anakuwa wapi wakati watumishi hawa waliopo chini ya usimamizi wake wanapoandika kiingereza cha ovyo kama hiki huku akifahamu kwamba hii ni paper ya kitaifa?

Kwa sababu hii, nadhani kuna haja ya kuufanyia marejeo mfumo wetu wa elimu vinginevyo wimbi la vilaza (wanafunzi, walimu, wakufunzi, wahadhiri, nk) litaendelea kutamalaki katika nchi hii huku wakitetewa na vilaza wenzao (na wengine wamo humu JamiiForums kwa gharama ya upotofu wa kielimu kwa watoto wetu.
View attachment 468495

View attachment 468497
wakuu nimewatolea mfano wa makosa yaliyomo kwenye paper hii hapa ya NECTA ili muone jinsi msingi mbovu wa kiingerereza kwenye ngazi ya chini kinavyoleta madhara hadi kwenye ngazi ya kitaifa. someni hayo makosa niliyopigia mstari halafu mje tujadiliane kwa ufasaha.
 
Leo nimetembelea shule moja ya Kata nikashuhudia kituko cha mwaka kutoka kwa mwalimu mmoja shuleni hapo.

Mwalimu huyo amehitimu Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni na akaajiriwa moja kwa moja kufundisha katika shule hiyo ya Kata.

Wakati akiendelea kufundisha nilimsikia akiwauliza wanafunzi swali hili: WHERE DOES IT LOCATED?

Inaonekana ni mwalimu wa somo la Jiographia, hivyo alikuwa akiwauliza wanafunzi wake wamtajie location ya kitu fulani kwenye ramani.

Jamani, hapa ndipo shule za kata zilipotufikisha. Ikiwa mhitimu wa Chuo Kikuu anaongea kiingereza kibovu kama hiki, tena mbele ya wanafunzi,mnategemea wanafunzi anaowafundisha watapata maarifa gani kutoka kwake?

Chukulia huyu ni mwalimu wa Kidato Cha Kwanza, wanafunzi wake wanaoambiwa kila siku "SPEAK ENGLISH" wataiga kiingereza gani kutoka kwake? Si ndio atawapoteza kabisa?

Ikiwa walimu hawajui kiingereza unategemea nini kutoka kwa wanafunzi wao? Haya ndio madhara ya serikali yetu kuchanganya elimu na siasa. Tumekwisha hasa!!
Inatisha.
 
Ufisadi wa CCM ndio umetufikisha hapa. Wanapenda sifa za kijinga pasipo kuboresha elimu ktk nchi hii. Mungu anawaona.
CCM ndiyo imewasomesha ma boss wako wa chadema, kumbuka hilo.
 
Back
Top Bottom