Sikia maajabu haya ya Mwalimu wa shule ya Kata

Sikia maajabu haya ya Mwalimu wa shule ya Kata

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,176
Reaction score
27,776
Leo nimetembelea shule moja ya Kata nikashuhudia kituko cha mwaka kutoka kwa mwalimu mmoja shuleni hapo.

Mwalimu huyo amehitimu Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni na akaajiriwa moja kwa moja kufundisha katika shule hiyo ya Kata.

Wakati akiendelea kufundisha nilimsikia akiwauliza wanafunzi swali hili: WHERE DOES IT LOCATED?

Inaonekana ni mwalimu wa somo la Jiografia, hivyo alikuwa akiwauliza wanafunzi wake wamtajie location ya kitu fulani kwenye ramani.

Jamani, hapa ndipo shule za kata zilipotufikisha. Ikiwa mhitimu wa Chuo Kikuu anaongea kiingereza kibovu kama hiki, tena mbele ya wanafunzi,mnategemea wanafunzi anaowafundisha watapata maarifa gani kutoka kwake?

Chukulia huyu ni mwalimu wa Kidato Cha Kwanza, wanafunzi wake wanaoambiwa kila siku "SPEAK ENGLISH" wataiga kiingereza gani kutoka kwake? Si ndio atawapoteza kabisa?

Ikiwa walimu hawajui kiingereza unategemea nini kutoka kwa wanafunzi wao? Haya ndio madhara ya serikali yetu kuchanganya elimu na siasa. Tumekwisha hasa!!
 
Wachina na wajerumani wenye maendeleo makubwa wanajua Kiingereza ?, pili ushasema ni mwl. wa Geography si kosa lake

Tatu ww kwa siku Kiswahili lugha yako unachapia mara ngapi ?

Nne ; watoto wenu mlokuwa mnawepeleka Kusoma Uganda na Kenya miaka michache ilopita mbona hamuwapeleki baada ya kuona watoto wanaendelea kuwa vilaza Tano Rekebisha ulitaka Mwl. aseme vp.
 
Elimu Ni Ujuzi Siyo Cheti
sasa Kuna mwenyewe Cheti Kizuri Mambo Hayawezi

Jamaa alishakuja hapa na story ya kwenda kumtembelea jamaa yake chuo kikuu akakuta watu wanaangalia porno akaponda eti badala ya kusoma wanaangalia mambo yetu.

Sasa na hii ya huyu ticha kisa amemaliza chuo kikuu kakosea ngeli jamaa anachonga.

Ninahisi jamaa kinamuuma sana kushindwa kwenda chuo kikuu ndo maana kila mara anakuwa anawatafutia kasoro watu qa chuo kikuu.

Hii lugha sio yetu, ukimsikiliza rais wa nchi mwenyewe gramar zinanchomoa pamoja na kuwa amesoma, amekaa wizara ya mambo ya nje, ulaya na US anaenda kama vile mimi navyoenda Ubungo Posta na ni Rais lakini bado ngeli ni shida.
 
Jamaa alishakuja hapa na story ya kwenda kumtembelea jamaa yake chuo kikuu akakuta watu wanaangalia porno akaponda eti badala ya kusoma wanaangalia mambo yetu.

Sasa na hii ya huyu ticha kisa amemaliza chuo kikuu kakosea ngeli jamaa anachonga.

Ninahisi jamaa kinamuuma sana kushindwa kwenda chuo kikuu ndo maana kila mara anakuwa anawatafutia kasoro watu qa chuo kikuu.

Hii lugha sio yetu, ukimsikiliza rais wa nchi mwenyewe gramar zinanchomoa pamoja na kuwa amesoma, amekaa wizara ya mambo ya nje, ulaya na US anaenda kama vile mimi navyoenda Ubungo Posta na ni Rais lakini bado ngeli ni shida.

Sio porno mkuu, alimkuta jamaa akicheza game kwenye laptop ikamuuma mbayaa, anataka jamaa wakamue kitabu 24/7 bila kupumzika. Inawezekana jamaa ana aleji na watu wa UDSM
 
Huna point. Yaani huyu mwalimu kuchanganya viashiria vya nyakati tu basi we tayari umeshahitimisha kuwa ni bomu na huyoooo mkuku kuja kumkandia hapa JF. Kuna makosa mengine ya hiyo lugha unayoiabudu alifanya au ni hili moja tu? Vipi ungemsikia akifundisha kwa Kiswahili na akawa amechanganya ngeli mf. Kisiwa iko wapi? Napo ungekuja hapa mbio mbio kumponda kuwa hajui Kiswahili?

Mbali na kwamba sera yetu ya lugha katika mfumo wetu wa elimu ni ya kutatanisha sana lakini kwa hili umemwonea huyu mwalimu na inavyoonekana una kasumba tena ya kushangaza. Kwako wewe mtu anayeongea Kiingereza fasaha basi huyo ni msomi wa kupigiwa mfano hata kama anachoongea ni pumba. Kwa mtazamo huu bado tuna safari ndefu sana kama taifa kwani hata watu wanaodhani kuwa wanajua sana ukiwaangalia vizuri kumbe ndiyo mbumbumbu wa kwanza. Na ni afadhali mtu asiyejua na hajui kuwa hajui mara mia kuliko jitu kengeufu lenye mitazamo potofu, jitu ambalo halijui kitu lakini lipo linajipiga kifua kuwa linajua mambo balaa. The former is a student and the latter is a FOOL !!!
 
Muhimu ni contents. Nafikiri kwa swali hili ilieleweka nini anamaanisha. Hilo ni kosa dogo ambalo halibadilishi maana mzima au kusudio husika. English sio lala mama kwa wengi wetu. Kama kiswahili kuna watu waliozaliwa na kuishi bongo na mpaka umri wao bado hawajui tofauti ya R na L sembuse "Kiinglish".

Ulisema somo la JIOGRAFIA, nafikiri amewasilisha lengo, Grama itakuwa kazi ya mwalimu wa Kiinglish
 
Unakosoa bila kuweka correction, nawe ndo walewale. Na uongo wako ni balaa, eti kamaliza UDSM juzi juzi na kuajiriwa moja kwa moja, je una mana gani? Serikali haijaaliz walimu ck za karibuni
 
Back
Top Bottom