Tena Nina uhakika katika watumishi wa serikali wenye angalau kuelewa kiingereza ni walimu wa sekondari!! Njoo huku jeshini uone,njoo wizara ya kilimo ,afya ,mifugo uone
Wanajua kingereza cha kuandika. Unatakiwa utambue kingereza kina nguzo kuu nne.
1. Speaking skill
2. writing skill
3. listerning skill
4. Reading skill
Sasa mtaala wa Tanzania umeshindwa ku intergrate those skills.
Mtaala unazingatia writing skill na hizo zingine ni bla bla walau reading skill.
Dk 40 za kipindi cha kingereza TZ umfundishe mwanf.
Kusoma., kuandika, kusikiliza na kuongea. Atambue sauti za maneno, muundo wa neno, kuliambisha, kupata maneno mengine.
Alijue neno ktk tenses, asome sentense, aunde sentense, aigize sentese, asikilize.
Asome habari na kutambua matumizi ya vocabilary na maana zake.
Ajue part of speech, ajue kwa ujumla grammer yote.
Aweze kusikiliza habari kisha aifupishe, aitafsiri aisimulie nk.
Vipindi ni 192 au 194 humo kuna sikukuu, ugonjwa, ukaguzi, michezo, wageni, seminar, incompetency, uvivu na mambo mengi yasioeleweka.
Isitoshe mtoto wa miaka 7 drs la 3 asome masomo 6 nayo yana mlolongo wa vitu kibao kama hapo juu.
Ni mwalimu gani wa kayumba anaweza kumuwezesha mwanafunzi wa TZ awe fluent speaker.
NECTA wanapima skills kizamani sana, yani ni wasomi wasioenda na wakati au wanahofia upimaji wa kisasa unatumia gharama kubwa nao hawana zana bora za upimaji.
Wizara nayo imeshindwa kutekeleza mahitaji wa msingi ya utekelezaji wa kisasa wa mtaala hasa lugha.
Tukirudi kwenye hoja yako, kimsingi hizo sekta zingine training yao ni tofauti na walimu. Mwalimu wa sekondari comm skill ni jambo linalotiliwa mkazo na anafanya presentation nying chuoni na TP. Anatumia hio lugha kufundishia.
Shida inakuja je msingi wa huyo mwalimu upoje ? Ukizingatia katoka kayumba s/m.
Wapo walio vizuri na wasio vizuri.
TZ hakuna pa kuiongelea lugha ya kingereza hasa kama sio mwalimu au mkufunzi wa chuo. Hivyo si rahisi kuiongea.