Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

Kwanza pole
Pili niulize. Hili la kudukuliwa umelishuhudia? Umejaribu kuingia mfumo wa taasisi yoyote zilizotajwa ukakuta ukweli?
Tatu tuko kizazi cha watu wanaonunuliwa. Kutofautiana kupo maadam tuna akili timamu sio mazezeta, hata kuchapana sawa lkn Umoja wa Kitaifa ni nambari 1. Sasa kizazi cha kuuzika na kununua watu ikoshida kama mtu anahama lei chama hiki na kwenda kile tena alikokuwa anatukana huyo USd ataiacha, ikibidi kuleta vurugu ilimradi ale sijui 7K.
Nne uongozi unataka kila kitu iwe mimi sio yule, ubnafsi unatawala mioyo ya wengi
Mwisho bado tutasimama walaaaa hakuna kitu kitatingisha
 
EeeeeenHEEEeeeeee!
As "non-partisan" as they come.

Strangely enough, immediately after stating the non-partisan claim; only a few words in the same sentence proclaims the opposite!
I am free to vocalise anything against any body's views, niko huru siko allied na any political party, ni raha sana kuwa huru :FEMLY:
 
EeeeeenHEEEeeeeee!
As "non-partisan" as they come.

Strangely enough, immediately after stating the non-partisan claim; only a few words in the same sentence proclaims the opposite!
sio kila anaepinga chama chenu cha fujo yuko ccm. ata walioondoka wameenda vyama kama chauma
 
Wakenya walikuwa wanatuonea wivu wamepata sababu sasa wanataka nchi yetu ivurugike...kwahili TL aende polepole maana anachokitengeneza kitakuja kumrudi yeye mwenyewe na tutakuwa tumepoteza Ile nchi yetu nzuri ambayo tuliona fahari kujitambulisha kokote duniani
Kwanza niwaambie tuu wakenya wengi wameshahamia Tanganyika na ardhi washannua na kilimo wanafanya huku wakiongoza kuchoma mkaa ili nchi iwe jangwa
 
sio kila anaepinga chama chenu cha fujo yuko ccm. ata walioondoka wameenda vyama kama chauma
Kuwa partisan ni slavery to unknown masters, hawa politicians know each other deeply, and later on they will always forge alliances against u.
It's a circus, G55 mliowapigania sasa wako kwa "ubwabwa", (supposidy carefully orchestrated by u'r enemy (the GOLIATH/CCM)
You will never enjoy their secret political endeavours, mtakuwa loyal circus spectotors
 
Kuwa partisan ni slavery to unknown masters, hawa politicians know each other deeply, and later on they will always forge alliances against u.
It's a circus, G55 mliowapigania sasa wako kwa "ubwabwa", (supposidy carefully orchestrated by u'r enemy (the GOLIATH/CCM)
You will never enjoy their secret political endeavours, mtakuwa loyal circus spectotors
i dont even mind that, mm najiskia vibaya wanavowatumia vijana for their own agenda and some of them die! swala la nan kawa mbunge ama diwan dont matter that much
 
ngoja uchaguzi upite alafu chama kipya cha upinzan kipatikane kelele zote ztaisha
Zama zimeshabadilika, cdm imeshageuka imani, hata kufanyike chaguzi za maigizo vipi, cdm imeshateka kundi kubwa linalotaka mabadiliko, hivyo vyama vingine ikiwemo na ccm watafanya siasa za mazoea, huku cdm ikibaki na kundi kubwa linalotaka mabadiliko, na wataibuka washindi kwenye hili.
 
Waambie mashoga zako waache kutegemea wazungu na kutukana ,kukejeli viongozi kwa mgongo wa haki za binadamu, utaiona Tanzania njema.
Viongozi ama majiz ya kura? Zama zimeshabadilika,tegemea kuona nguvu ya mabadiliko.
 
Kama mama ana akili,ishu ya hacking na maudhui ya taarifa iliyotolewa Kwa umma kwa akaunti zile za .......! Anapaswa awaze upya juu ya maamuzi yake!!

Ajiulize kama serikali ikishavunjwa yeye atakuaje sio victim wa future hacking na maudhui yatakayotoka!!?

Siamini kama wakenya wame hack bila msaada wa watz!!!

Nawaza!!
 
Tulipokuwa tunasem umoja wa kitaifa haupo maana kuna upande unaoonekana una kila kitu na unaweza fanya lolote.

Na upande unaoonekana ni wachache na hawana nguvu ya kufanya lolote.

Sasa mtu akitokea kuwasaidia hawa wanaoonewa bila shaka watamuunga mkono bila kipingamizi.

Naweza kukukumbusha tu mfano mdogo unakumbuka ile ajali ya wabunge waliyopata wakiwa wanaenda Kenya kwenye michezo ya mabunge ya Afrika Mashariki?

Wale wabunge hadi leo haijawahi kutajwa walikuwa ni kina nani kwa sababu ya maoni hasi katika mitandao yote ya kijamii hata humu post ile ipo.

Je siku kikitokea cha kutokea wamlaumu nani?

2021 tuliona serikali ilipopiga marufuku "sherehe "kabla Magufuli hajazikwa na hata wapo waliokamatwa sababu walikuwa wakisherekea ilitakiwa imkumbushe huyu mama chuki ilikuwa ya kiwango kikubwa sana ila yeye pia kaamua kupita njia ile ile.

Itachukua muda sana kuja nchi kutibiwa majeraha iliyopata kuanzia 2015 ndio maana hizi 4R tangu siku ya kwanza zimeanzishwa niliona ni utapeli kuna aina fulani ya maridhiano yangefanyika kwa wahanga wote wa utawala wa mtangulizi wake ningemuona ni mtu mwenye nia njema ila hakufanya hivyo.
Umeongea ninachokiwaza daima , Mama alianza poa kwa lugha ya uungwana na kwa kweli kama angeendelea katika njia hiyo huyu ndiye alikuwa Rais ambaye vizazi vingemkumbuka kama mkombozi wa pili wa taifa letu.Ikumbukwe taifa letu likipata tu reforms bora za uchaguzi kisha katiba bora hawa Kenya tutawapita kiuchumi haraka , naamini tunaweza kuwa na taifa zuri na bora sana maana Mungu alitujalia rasilimali lukuki ambazo tukiwa na viongozi ambao watazilinda na kuzisimamia ipasavyo basi miaka 20 tu inatosha kutuweka top ten ya nchi tajiri za Africa kwa uhalisia kamili.
 
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuitwa kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamoja na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisumbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekima na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao na Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanzania wameshindwa kuungana katika sakata hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin. Kule Uganda.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Korongoni.

TUJIREKEBISHE!!
Tanzania sasa hivi ni nchi kipumbavu tunaichukia kama harufu ya mavi, Serikali inayofurahia vifo vya raia, kutekwa na kuteswa na kuuwawq tunawaombea wafe wote hata kwa ajali za ndege wafe wote na Mungu atawaua wote hao hakuna cha uzalendo tunawachukia
 
Yeyote anayeijali na kuithamini Tanzania hawezi kupenda hiki kinachotokea. So sad!
uipende Tanzania alafu badae wakuteke wakuue, wacha yatokee tu waone upumbavu wao
 
Back
Top Bottom