Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

Wakenya walikuwa wanatuonea wivu wamepata sababu sasa wanataka nchi yetu ivurugike...kwahili TL aende polepole maana anachokitengeneza kitakuja kumrudi yeye mwenyewe na tutakuwa tumepoteza Ile nchi yetu nzuri ambayo tuliona fahari kujitambulisha kokote duniani
MSISITIZO:
Tundu Lissu na CHADEMA ni LAZIMA wajitenge na kuonekana kuwa ni tegemezi kwa watu/makundi toka nje, kuja kuleta mabadiliko hapa. HiILO HALIWEZEKANI.
Hii kazi ya mabadilko hapa ni ya waTanzania wenyewe; na kwa kweli tayari waTanzania wanaitambua hivyo.
Hao watu/makundi toka nje, ni msaada tu kwa waTanzania, kutuwezesha sisi wenyewe kujitoa kwenye ukandamizi

Kwa hiyo, wajibu wa kwanza kabisa ni kwa Tundu Lissu na timu yake kuhakikisha kwamba ni waTanzania ndio wenye jukumu, na kuwapanga vizuri watimize jukumu lao hilo.

Kuhusisha hayo makundi toka nje, ni 'counterproductive'. WaTanzania hawatalielewa hilo.

Kwa mfano: Tanzania ilipokuwa ikisaidia katika maswala ya ukombozi Kusini mwa Bara hili; haikwenda yenyewe kama nchi kwenda kupigana na kuwakomboa wenzetu wa huko. Tulicho fanya, ni kutoa misaada tuliyoweza kutoa kusaidia hao wenzetu kujiondoa kwenye ukoloni.

Hali ni hiyo hiyo, hata katika maswala mengine, hata ya uchumi. Hatuwezi kutegemea watu waje hapa kutuletea maendeleo; hata kwa huo uwekezaji. Jukumu hilo ni la waTanzania wenyewe.
 
haiwezekan wao kuchukua the point ni chadema ni creator wa vurugu za apa na pale kwahio bada ya uchaguzi kitapatikana chama kipya cha upinzani si wamekataa kushiriki uchaguzi acha wengine wachukue nafasi then watanyooshwa vizuri wakiwa nje ya kivuli ya chama kikuu cha upinzan
Bado mnajiliwaza na mawazo hafifu ya aina hii kweli?

Yaani hata huna wakati wa kufikiri waTanzania wenyewe wapo wapi; unabaki tu na "vyama vya upinzani"?
 
mi ni non-partisan, comments zangu ni "my common sense". Kama unategemea maisha yako na familia yako yataboreshwa siasa za vyama, utapigwa stress na ku-commit suicide. 😀 hao wenyewe wana hustle wapate mkate.
EeeeeenHEEEeeeeee!
As "non-partisan" as they come.

Strangely enough, immediately after stating the non-partisan claim; only a few words in the same sentence proclaims the opposite!
 
Mtoa mada nakushukuru sana,kuna kitu muhimu umekisema ambacho ni cha msingi sana.
Hao wanaouawa wakati mwingine wana ndugu zao kwenye vikosi hivyo vinavyoua.
Siku wauaji wakikosea wakaua mke/mtoto wa muuaji mwenzao mfano wa akwilina
usitegemee huyo mwenzao baada ya msiba atakuwa kama jana yake.
Mambo haya ni ya kutazama kwa jicho la tatu.
 
Bado mnajiliwaza na mawazo hafifu ya aina hii kweli?

Yaani hata huna wakati wa kufikiri waTanzania wenyewe wapo wapi; unabaki tu na "vyama vya upinzani"?
Sikio la kufa halisikii dawa, Hoja kubwa hapa ni mauaji yanayoendelea
kuna siku ndugu yako au wewe utauwawa wakati hata ulikuwa huandamani,risasi itapoteza mwelekeo
 
Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.
Usishangae siku ukasikia wanataka Tanzania Kusini na Kaskazini
 
Kwa maana hiyo hiyo, nadhani itakuwa sahihi zaidi ukisikia Zanzibar (nchi kamili), inaungana na Pwani yote ya Tanganyika (pengine ukiiondoa Dar, kutokana na hali yake iliyo tofauti zaidi na mikoa mingine ya Pwani ya Tanganyika.). Lakini mikoa kama Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga wakiungana na Zanzibar hiyo labda (?) itaridhisha zaidi hamu ya wenye kupenda mwelekeo wa namna hiyo; ambao binafsi nadhani ni sehemu muhimu ya tatizo linalo chochea haya tunayo yashuhudia sasa hivi ndani ya CCM na serikali yake.
 
Kwa maana hiyo hiyo, nadhani itakuwa sahihi zaidi ukisikia Zanzibar (nchi kamili), inaungana na Pwani yote ya Tanganyika (pengine ukiiondoa Dar, kutokana na hali yake iliyo tofauti zaidi na mikoa mingine ya Pwani ya Tanganyika.). Lakini mikoa kama Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga wakiungana na Zanzibar hiyo labda (?) itaridhisha zaidi wenye kupenda mwelekeo wa hivyo; ambao binafsi nadhani ni sehemu ya tatizo linalo chochea haya tunayo yashuhudia sasa hivi ndani ya serikali ya CCM.
Nimekuelewa vilivyo
 
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuitwa kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamoja na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti za pembeni na kuungana dh8di ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisumbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekima na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao na Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanzania wameshindwa kuungana katika sakata hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin. Kule Uganda.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Korongoni.

TUJIREKEBISHE!!
Ndugu Mtanzania, you have said it ALL.
Tanzania kumeingia ugonjwa. Watawala wanafikiri wao ni kila kitu, wako juu ya Katiba na Sheria na wanaweza kufanya chochote kwa yeyote maadamu hakubaliani na mawazo yao.
Tanzania sasa kuwa Mwanasiasa lakini hauko CCM ni hatari. Wewe ni adui namba moja wacSerikali. Wewe ni mpinzani unaye ichukia Serikali, unaichukia CCM na unamchukia Mama.

Katiba yetu ni ya mfumo wa Vyama Vingi. Lakn hawa Watawala wanasahau kwamba tuko milioni 60+ na wote si wana CCM. Unaweza kukuta familia moja Baba ni CCM, Mama ni CHADEMA, Mtoto ni ACT au CUF. Sasa ukimkamata Mama au mtoto I,amtesa au kumpoteza, unafikiri huyo Baba au ni Mama ataipenda CCM tena???

Laxima Baba au Mtoto wataanza kutafuta namna za kulipiza kisasi huko huko ndani ya CCM kwa kutumia mbinu xoxote wabazoxijua. ,kuna wakti Rais Mdtaafu JK aliwai kusema Watz wameanza kuogopana wakiwa kwenye vikao ,mikutano au sherehe kwa hofu ya kutiliana sumu, kumwagiwa tindi kali au chochote,

Ni uadui usio na mwisho, Tunaenda kwenye uhasama na chuki za piga nikupige. Mwaga mboga sisi tunamwaga ugali. Tuombe Watz wasije wakafikia point of no return au enough is enough...wakaamua kuingia msituni!!

Polisi wanaojidai Wasiojulikana, Watz wanawajua, wanaonekana mtaani, tunaishi nao na tuna kula na mitaani. Siku wakiamua kulipiza kisasi sijui watakimbilia nchi gani. Maana hata majirani sasa wameanza kufurushwa kisa wamekuja kusikiliza kesi ya mpinzani aliyeonewa kwa kesi za kughushi..!!

Twendeni tu lakini muda utaongea!!
 
ngoja uchaguzi upite alafu chama kipya cha upinzan kipatikane kelele zote ztaisha
Cha ubwabwani unachekesha walionuna ,
Chama Gani nje ya chadema kwenye upinzani kinapata sapoti ya wanainch wengi ,
Hicho kingine hata kikiwa na wabunge 50 wa mchongo bado kwenye ground kitakua kama CUF tu ya lipumba ujue kumanipulate watu ilikuwa rahis huko nyuma tofauti na sasa technology iko juu niko kijijini huku lakini najua kuwa Mrema ni fala tu kama ww
 
unaonekana hujala leo, ebu pata kitu kwanza
 
Bado mnajiliwaza na mawazo hafifu ya aina hii kweli?

Yaani hata huna wakati wa kufikiri waTanzania wenyewe wapo wapi; unabaki tu na "vyama vya upinzani"?
tunajua kabisa lengo lenu ni kumpush mtu mje mpate vyeo ndo maaana amna anaehangaika na nyie
 
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuitwa kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamoja na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti za pembeni na kuungana dh8di ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisumbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekima na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao na Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanzania wameshindwa kuungana katika sakata hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin. Kule Uganda.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Korongoni.

TUJIREKEBISHE!!
Usiishie kulia lia tu, majinga yamekuwa mengi na yanajisifia kwa kuchoma nyumbani kwao yakasitiriwe barazani kwa jirani
 
Imekuwa ni nchi ya ovyo sana!

Back
Top Bottom