Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

Tatizo ni uongozi mbovu.
Watz wengi watamuunga mkono adui iwapo nchi itavamiwa, na hii imesababishwa na uongozi usiojali maisha ya watz wenzao.
Uongozi unaofurahia na kukutengeneza ama kulinda magenge ya kihalifu yanayoteka na kuua.
 
Hayo ni maneno ya busara! Tanzania ni yetu sisi watanzania bila kujali tunatofautiana katika lipi.
Serikali ambayo ina dhamana ya maisha ya Watanzania ichukue hatua zote kukomesha Uonevu,Utekaji,Kupoteza au Kuua watanzania wake,kufungulia watu kesi za Uongo ili tusiipoteze Amani yetu ambayo ni adimu katika baadhi ya mataifa.
Tanzania bado ni yetu tuilinde kwa gharama zo zote!
Naamini Amiri Mkuu wa Nchi yetu atalichukulia hili kwa uzito wote.
God keep blessing our country Tanzania.
 
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuita kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamija na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti za pembeni na kuungana dh8di ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisunbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekuoa na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao ma Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanza wameshindwa kuungana katika sakati hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Koringini.

TUJIREKEBISHE!!
Yeyote anayeijali na kuithamini Tanzania hawezi kupenda hiki kinachotokea. So sad!
 
Waambie mashoga zako waache kutegemea wazungu na kutukana ,kukejeli viongozi kwa mgongo wa haki za binadamu, utaiona Tanzania njema.
Hizi ndiyo akili halisi za Mtanzania kipenzi cha watawala wasiojali maslahi ya nchi.
Viongozi ambao walioamini kuwa nchi ipo vizuri mitandaoni ikiamini ikitokea vita ya mitandao hao machawa ndiyo watakuwa askari. Hawakutarajia wala kuwahi kufikiri kuwa vita ya mitandaoni itahusisha udukuzi na uvurugaji wa njia za mawasiliano kwa umma
 
Sikiliza we nyang'au wa kikenya, hii nchi yangu haiitwi tz ni Tanzania 🇹🇿 paka shume we!
Wakenya walikuwa wanatuonea wivu wamepata sababu sasa wanataka nchi yetu ivurugike...kwahili TL aende polepole maana anachokitengeneza kitakuja kumrudi yeye mwenyewe na tutakuwa tumepoteza Ile nchi yetu nzuri ambayo tuliona fahari kujitambulisha kokote duniani
 
Wakenya walikuwa wanatuonea wivu wamepata sababu sasa wanataka nchi yetu ivurugike...kwahili TL aende poleole maana anachokitenhemeza kitakuja kumrudi yeye mwenyewe na tutakuwa tumepoteza Ile nchi yetu nzuri ambayo tuliona fahari kujitambulisha kokote duniani
Dawa ni kufanya reforms za uchaguzi tu ili viongozi wapatikane kwa kura sahihi za raia walio wengi
 
Waambie mashoga zako waache kutegemea wazungu na kutukana ,kukejeli viongozi kwa mgongo wa haki za binadamu, utaiona Tanzania njema.
Ongea kama mtu mzima aisee nyie ndio mnaopeleka nchi pabaya kwa ubinafsi wenu lakini mambo yakiwa mabaya ukumbuke familia yako itaguswa tu acheni mihemko ya kipuuzi kwenye mambo nyeti watubtuna watoto wadogo tunaifikiria kesho yao wewe unaangalia tumbo lako kenge wewe
 
The government of the political party for the political party by the political party.Siku ikawa the government of the people for the people by the people mambo yatakua safi sana.
 
Unachezea uchawa wewe; Prof. Juma (jaji Mkuu wetu) jana alizima simu yake alivyoona call ya Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya. Yaani jamaa alimkimbia mate wake ili wasiongee achiliambali kukutana.
Inachekesha na kuuzunisha kwa pamoja, mate anamkimbia mgeni aliyekuja kusikiliza kesi mahakamani kwani alikuja kuongeza tu maarifa na kupata uzoefu.

Ccm acheni kudhalilisha viongozi wetu.
 
Consigliere wa familia gani ? Maana consigliere ni jina linatumika kwenye familia za "cosa nostra"
 
Hizi mdiyo akili halisi za Mtanzania kipenzi cha watawala wasiojali maslahi ya nchi.
Viongozi ambao walioamuni kuwa nchi ipo vizuri mitandaoni ikiamini ikitokea vita ya mitandao hao machawa ndiyo watakuwa askari. Hawakutarajia wala kuwahi kufikiri kuwa vita ya mitandaoni itahusisha udukuzi na uvurugaji wa njia za mawasiliano kwa umma
Andika kiswahili.
 
Tulipokuwa tunasem umoja wa kitaifa haupo maana kuna upande unaoonekana una kila kitu na unaweza fanya lolote.

Na upande unaoonekana ni wachache na hawana nguvu ya kufanya lolote.

Sasa mtu akitokea kuwasaidia hawa wanaoonewa bila shaka watamuunga mkono bila kipingamizi.

Naweza kukukumbusha tu mfano mdogo unakumbuka ile ajali ya wabunge waliyopata wakiwa wanaenda Kenya kwenye michezo ya mabunge ya Afrika Mashariki?

Wale wabunge hadi leo haijawahi kutajwa walikuwa ni kina nani kwa sababu ya maoni hasi katika mitandao yote ya kijamii hata humu post ile ipo.

Je siku kikitokea cha kutokea wamlaumu nani?

2021 tuliona serikali ilipopiga marufuku "sherehe "kabla Magufuli hajazikwa na hata wapo waliokamatwa sababu walikuwa wakisherekea ilitakiwa imkumbushe huyu mama chuki ilikuwa ya kiwango kikubwa sana ila yeye pia kaamua kupita njia ile ile.

Itachukua muda sana kuja nchi kutibiwa majeraha iliyopata kuanzia 2015 ndio maana hizi 4R tangu siku ya kwanza zimeanzishwa niliona ni utapeli kuna aina fulani ya maridhiano yangefanyika kwa wahanga wote wa utawala wa mtangulizi wake ningemuona ni mtu mwenye nia njema ila hakufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom