Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

wewe unajuaje kama natumika?
Mtu anayeamini kwamba binaadam wenzake hawastahili kuwa na HAKI, huyo ni mtu asiyetumika kwa lolote?
Tena unazidi kuonyesha ni jinsi gani ulivyo kikaratasi tu kinachotumiwa kufutia kila aina ya.uchafu
 
Mtu anayeamini kwamba binaadam wenzake hawastahili kuwa na HAKI, huyo ni mtu asiyetumika kwa lolote?
Tena unazidi kuonyesha ni jinsi gani ulivyo kikaratasi tu kinachotumiwa kufutia kila aina ya.uchafu
we bado mdogo sana kuelewa dunia inavoenda, nenda kamsome LUCIFER alafu uje na porojo zingine apa
 
your too young kuelewa dunia ikoje, kale mihogo ulale
"your too young...", what the heck is that!
Hiyo dunia ya kishetani ni nyinyi tu, genge la uovu mnao ijuwa. Usitake na wengine wawe na uovu kama mlionao nyinyi.
 
"your too young...", what the heck is that!
Hiyo dunia ya kishetani ni nyinyi tu, genge la uovu mnao ijuwa. Usitake na wengine wawe na uovu kama mlionao nyinyi.
umeibiwa mke nn mbna unaongea kwa uchungu sana, nyie kaeni pemben chama kikuu kingine kipatikane
 
Na mma yenu anajiita chura kiziwi lazima maji tuite mma safari hii,akimalizana na nyie anarudi kwao nchi ya kizimkazi kusubiri afe aende akaione pepo
 
Kama sauti zetu wenyewe Watanganyika hazitasilizwa na watawala ktk kurekebisha mambo yetu, basi Mungu atainua mawe au miti au hata punda au mbuzi na ng'ombe kupaza sauti kututetea dhidi ya uonevu wa watawala wetu wenyewe wanajisema kuwa waliwekwa na wananchi kwa sanduku la kura lakini ukweli ni kuwa walijiweka wenyewe kwa mabavu kwa wizi wa chaguzi/kura...

Wakenya, Bunge la Ulaya, Marekani na wengine huko duniani ni mawe na miti yanayosema kwa ajili ya Watanganyika...

Iko sawa kabisa. Na sisi raia wa Tanganyika, tuko tayari kuungana nao kuhakikisha madikteta wetu, weusi wenzetu wanajiita CCM wanatoweka mara Moja na kutuachia nchi yetu...!
Tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

Jamii inayo ongozwa kwa mfumo wa unyumbu wa kisiasa, unyumbu wa kisiasa ni mfumo unao ruhusu watu kurubuniwa Kwa hali na mali hatimaye hukengeuka kwa kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data tume kuahirisha kufikiri kizalendo


Silence surrenders public responsibilities
 
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuitwa kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamoja na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisumbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekima na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao na Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanzania wameshindwa kuungana katika sakata hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin. Kule Uganda.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Korongoni.

TUJIREKEBISHE!!
Uzi unafikirisha mno
 
Back
Top Bottom