Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Naomba kuuliza kitu kwa watu wa Mbeya na wanaoijua Mbeya, hata kama hili suala limewahi ongelewa naomba kuuliza kwamba JE MH PROF. MWANDOSYA amefanya mambo gani Mbeya? maana anasifiwa sana na naomba kujua hao wabunge wengine MH Mwakyembe ambacho hawajafanya. Nimeuliza kutaka kujua tuu.
 
Lusajo Mkuu, mtu yeyote anayechaguliwa na watu ukiona watu wake wanamsifi ujue yuko karibu sana na watu wake wakati wa shida na raha; nakumbuka soko la Mwanjelwa lilpoungua Prof. Mwandosya nadhani alikuwa mbunge wa kwanza kwenda kuwafariji wafanyabiashara waliopotelewa mali zao na moto. Uongozi maana yake kuonesha njia na nadhani huyu bwana ndicho anachofanya huko Mbeya; tofauti na wabunge wengi wanaopoteza muda mwingi D'Salaam yeye mara kwa mara yuko huko kwao na wananchi.
 
Naomba kuuliza kitu kwa watu wa Mbeya na wanaoijua Mbeya, hata kama hili suala limewahi ongelewa naomba kuuliza kwamba JE MH PROF. MWANDOSYA amefanya mambo gani Mbeya? maana anasifiwa sana na naomba kujua hao wabunge wengine MH Mwakyembe ambacho hawajafanya. Nimeuliza kutaka kujua tuu.

Lusajo,

Prof. Mwandosya anajua grassroot politics, anajua shida za watu wa Mbeya na kikubwa anajua shida za watu wa jimbo lake. Hayo mambo hajaanza baada ya kuwa mbunge.

Mimi nilimfahamu huyu mheshimiwa wakati nikiwa mwanafunzi Rungwe secondary, alikuwa anapita sehemu mbali mbali akihimiza na kuchangia maendeleo ya shule. Wakati huo ilikuwa ni miaka ya mwanzoni mwa 80 na amekuja kugombea ubunge 2000 kwahiyo ni dhahiri hakutumwa na nia ya kutaka kuwa mbunge.

Nilipokuwa mlimani, kuna kipindi cha likizo tulikuwa tunaandaa mikutano ya kuwashawishi wanafunzi ambao walikuwa hawafanyi mazoezi ya vitendo wakati wa likizo, wale wanaotoka Mbeya ili wakasaidie kufundisha baadhi ya shule za private ambazo zilikuwa na hali mbaya ya kukosa walimu. Huyu mheshimiwa alikuwa anakuja kuhudhuria baadhi ya hiyo mikutano na kutoa ushauri wake. Kulikuwa na lecturers wengine toka Mbeya ambao wala hawakujali na hawakuwa na mpango.

Tukiacha hayo jamaa anahamasisha watu kule kwao ili wajiletee maendeleo, wakati wilaya zingine? sijui labda mimi sijui. Mfano mmoja ni wakati JK alipoenda juzi kutembelea Mbeya, wakati Rungwe wanafungua viwanda, Kyela, JK alifungua SACCOS iliyopewa mkopo na NBC wa milioni moja. Nilijiuliza hivi kweli mkopo wa milioni moja ndio hata wa kumsubiri rais aufungue? Kwa kifupi wilaya kama Kyela, Ileje na hata ule upande wa kwa prof. Mwakyusa, hakuna maendeleo ya maana yanayofanyika. Hawa waheshimiwa sio mawaziri lakini ukiwakuta kwenye wilaya zao, utakuwa na bahati sana. Wanashinda Dar, hapo ndipo mwenzao alipowazidi.

KIla siku hapa tunasikia maugomvi tu, umewahi hata siku mmoja kumsikia prof. Mwandosya akiongelea ugomvi Mbeya? Pamoja na yeye kuhusishwa na maugomvi yote hayo, yeye anachanganyikana na wote tu. Kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM mkoa, yeye alimwunga mkono huyo Mulla, pamoja na kujua kwamba anaunga mkono wapinzani wake. Alimuunga mkono kwasababu alikuwa bora kuliko hao wengine na sio kwa kufuata upande upi wa CCM.

Wabunge wetu, mnashinda kila siku na prof. Mwandosya kwanini hamjifunzi toka kwake?
 
Analysis yako naiunga mkono hasa. Ila pia kuna haja ya watu wa huko Mbeya kuwa na na tabia ya kujitolea. Ninaposema kujitolea nina maana kushirikia katika shughuli za maendeleo ya mkoa wao kama walivyo wengine hasa kaskazini na kule Kagera. Umeongelea kuhusu mikakati ya milimani enzi hizo kuwashawishi watu waende kufundisha shule lakini hawakujali. Ni kweli kabisa.

Ni muda muafaka kwa watu wa Mbeya kuanza kujitolea. Hasa kwenye michango. Mara nyingi sana ukienda kwenye Harambee za watu wa Mbeya, si ajabu kabisa kukuta mkutano wenye big names wakaibuka na mchango wa 150,000 tu! Mambo si hayo kwa wengine, hasa wa kaskazini. Wale wengine si wagumu sana na wanajitolea sana.

Kwa hiyo Mbeya pamoja na kuwa elite in terms of education (uki-compare na baadhi ya sehmu zingine), bado kuna safari ndefu sana ya maendeleo, ambayo mimi naamini watu wa huko wakigeuzwa mioyo na kuacha ugumu, inaweza kufanya kuwa fupi sana. Hii TABIA ya watu wa kule ya kusema mtu fulani hana MSAADA,, kwa kweli ni mbaya sana! Kwanini usaidiwe wakati mwenzako ana miguu, mikono na kila kitu kama wewe?!!! Inahitajika mabadiliko kwenda mbele.
 
Mwanjelwa mkuu. tunaposema hawatoi msaada kwa watu wanaotoka sehemu za kwao hatuna maana ya kuwa hawawagawii fedha hapana; tuna maana ya kuwa kwa vile wao ni viongozi ni jukumu lao kuwasaidia watu wa kwao kwa kuwaonyesha njia ambazo zitawaletea maendeleo na hiyo ndiyo kazi ya viongiozi. Nadhani uelewa wako ,ulidhani tunataka hawa jamaa wagawane ngawila zao na watu wa kwao sio hivyo!!
 
Tatizo la watu wa mkoa wa mbeya hasa wanyakyusa ni selfishness; hawa ni watu wabinafsi hasa viongozi wao.Huna haja ya kwenda mbali we waangalie hao wabunge wao maprofesa ni wanafiki wala hawana msaada kwa watu wanaotoka kwao ukiwafananisha na wenzao kutoka mikoa ya ziwa na kaskazini!! ....

Msaada upi unaoongelea hapa?! KIla mtu anatakiwa ajisaidie mwenyewe.
UBISHI HAUSADII HUO NI UKWELI
 
Mwanjelwa mkuu. tunaposema hawatoi msaada kwa watu wanaotoka sehemu za kwao hatuna maana ya kuwa hawawagawii fedha hapana; tuna maana ya kuwa kwa vile wao ni viongozi ni jukumu lao kuwasaidia watu wa kwao kwa kuwaonyesha njia ambazo zitawaletea maendeleo na hiyo ndiyo kazi ya viongiozi. Nadhani uelewa wako ,ulidhani tunataka hawa jamaa wagawane ngawila zao na watu wa kwao sio hivyo!!

Njia zipi ambazo mpaka leo watu wa mbeya hawazijui? Wewe niambie kwa jinsi unavyoona pilikapilika za wau wa kule, Mbeya, Tukuyu, Kyela na sehemu nyingine, kuna kitu ganikipya ambacho wewe kama kiongozi unaweza leta?
Hiyo habari ya msaada ni zaidi na hivyo unavyosema. Unaweza kukuta msaafu mwenye asili ya Mbeya anafuatilia cheque yake wizarani na pale wizarani kuna mtu wa Mbeya. Kama kuna ucheleweshaji au bureacracy yoyote,,, utasikia akilalamika kuwa,,,,, mnyakyusa mwenzangu yule lakini hana hata msaada!! Kuna mifano mingi sana nimeona hapo Tanzania ya lawana kama hizi za mtu fulani hana msaada,,,,,.! Tuachane na hizi na kujisaidia wenyewe kila mtu kivyakevyake. Ndiyo essence ya maendeleo hapa Scandinavia, kila mtu anafanya kazi kwa bidii na kivyakevyake bila kumwangalia mtu wa kumsaidia.
 
Mwanjelwa,

Nafikiri umeenda mbali kabisa na maana au dhana ya kuwaletea wananchi maendeleo ambayo wengine tunaongelea.

Hatuongelei kumsaidia mtu mmoja mmoja au kugawa pesa zako za mfukoni. Tunaongelea kuwasaidia wananchi kutumia resources mbalimbali kujiletea maendeleo. Kwa mfano kule Kyela, lini mara ya mwisho ulisikia watu wakiongelea kilimo bora cha kokoa, mpunga au migomba? Kwanini ukipita Rungwe uone migomba iliyostawi lakini ukiingia Kyela migomba 20 imelundikana pamoja na mazao yake hafifu? Hao viongozi wa Kyela kila siku wanapita hiyo wilaya ya Rungwe, je hawaoni hiyo tofauti?

Tatizo kubwa la wilaya za Tanzania ni capacity, uwezo wa watu uko chini sana na hapo ndipo uongozi bora unaweza kuleta mabadiliko kwa kuangalia resources zilizopo na kuchagua priorities kwa maendeleo ya wilaya.

Umeongelea Scandinavia kwamba kila mtu anafanya vyake vyake, labda hiyo Scandinavia huijui. Serikali ina mkono mkubwa sana Scandinavia labda kuliko hata nchi zingine za West. Huku West kuna wajinga wengi sana ila wana wenye akili wachache ambao wanajituma kuchapa kazi na kutengeneza mipango ya maana ya kuendeleza nchi zao.

Hata kwenye kusaidia watu, hivi huyo mzee mstaafu kwanini mpaka aende kuhangaika Dar kufuatilia mafao yake? Kwa Mbunge anayejua wajibu wake anatakiwa ayatatue matatizo kama hayo na kuwapunguzia watu gharama na usumbufu wa kwenda kuzunguka Dar kufuatilia mafao. Mambo mengi yanayowasumbua watu yanaweza kutatuliwa kwa muda mfupi kama kuna viongozi ambao wako tayari kuwasikiliza watu wanaowaongoza.

Ukienda kwenye zile shule mpya za secondary, hivi unategemea vijana watakaotoka kwenye hizo shule watakuwa na uwezo gani? Je Mbunge au viongozi wengine wa wilaya hawawezi ku influence ubora wa hizo shule? Kama hawawezi kwanini kwenye wilaya zingine ikiwemo Rungwe, shule ziwe bora zaidi kuliko wilaya zingine? Hiyo ndio dhana ya kuwaletea maendeleo wananchi ambayo wengine tunaongelea.

It takes two to tango, ni kweli ili maendeleo yaje lazima wananchi nao wawe tayari kushiriki kwenye shughuli za kujiletea maendeleo. Mimi nafikiri wananchi tayari wanashiriki ila uwezo wao wa kujiletea maendeleo ndio haba na hapo ndipo uongozi bora unakuwa muhimu.

Hapo ndipo tofauti kubwa kati ya Prof. Mwandosya na hao wengine inapoanzia. Prof. anajua matatizo ya Rungwe na muda wote anajaribu kuyatatua, wakati kwenye wilaya zingine sioni kama kuna juhudi kubwa kushughulikia umaskini wa watu wetu.
 
Mtanzania, partly nakubaliana na wewe partly not. Hivi unafahamu kubwa asilimia kubwa ya mji wa Mbeya umejengea na watu wa Kyela zaidi kuliko Rungwe na wilaya zingine? Zile mansions nyingi ni za watu wa kule. Usangu, na partly Chunya, asilimia kubwa ya wale ni wa "ntebhela". Sasa nikikubaliana na hoja yako kuhusu role ya viongozi, pia ninarudi kwenye individual problems. Watu wa kule pamoja na kuwa wengi ni wajanja, imani ndogo ndogo zinakwamisha sana maendeleo kule. Mvua ikinyesha nyingi na kuzoa zitu, zinaingia imani za hapa na pale na watu wanakimbia!. Si kweli kwamba Kyela watu wapo wapo tu. Ni tatizo la kiimani. Kwa kukubaliana nawe, ni kwamba viongozi wangetumia muda wao kuwezesha kuwabadilisha hawa tu wawekeze kwenye wilaya yao badala ya kukwepa imani za hapa na pale. Lakini siyo viongozi tu, hata wewe na mimi.
"
Kyela waweza fananisha na Wapemba. Kariakoo wana majumba makubwa sana na ya hali ya juu, lakini ukienda kule unaweza usiamini amini kumwona mwenye ghorofa Kariakoo anaingia kwenye kibanda kwamba ndiyo kwao! Sasa wanaishia kulalama kuwa siasa zimewaathiri! Is it true?!

Issue ya Rungwe si Mwandosya ndiyo ndiyo mwanzilishi. Rungwe was dynamic even before. Ila Mwandosya kaja ku-open na ku-speed up. Amewakuta watu wako dynamic na aka-takeover from there. Ingekuwa Kyela, niamini kabisa kuwa asingefana chochote kufananisha na kule Rungwe. Lakini Mwandosya ni wa Rungwe Mashariki, magharibi kuna Prof mwingine, huwa namwona kwenye TV tu!. Lakini kule jimboni wako speed kubwa sana. Na huyu si Mwandosya anayechagisha hapa. Ni kama nilivyosema, mindsets na dynamism
 
By Pendo Fundisha, Mbeya

Kyela MP Dr Harrison Mwakyembe has said that the only magic for leaders of Chama cha Mapinduzi to remain in power in the next election is through delivery to the public in the manner they want.

Dr. Mwakyembe made the remarks at the weekend when wrapping up his official tour in the constituency.

He said political leaders needed to be closer to their voters and be able to solve some of the critical social problems they faced.

``This is the only way that will make CCM to continue ruling the country,`` he said.

The lawmaker said that many people want to see the given promises practicaly fulfilled.

Dr Mwakyembe said the party wouldn\'t tolerate leaders who go against its laid down election manifesto geared to bring development to all people.

``Those who want go with the speed of the third-phase government should leave the post and clear the way for other people who are ready to deliver to the people,`` he said.

He said it was high time leaders seriously worked on people`s problems rather than sit on them.

``What people want is development, so as leaders we are supposed to assist them bring them about; too much politics cannot work under the current situation,`` he said.

Meanwhile, Lukwego and Lusungo villagers have hailed the efforts made by the government to put up a durable bridge along Lufilyo River.

They said for year`s the area had been experiencing serious communication problems.

SOURCE: Guardian
 
Easier said than done
 
Easier said than done
Lusajo,

Kwenye siasa siku hizi wanaita usanii. Unaweza kusema lolote hata yale ambayo huwezi kuyatenda au huyatendi. Nahisi kuna waheshimiwa wa huko wanafuatilia huu mjadala.

Kama kuna jambo watajifunza itakuwa afadhali, vinginevyo ndio yale yale.

Hivi inakuwaje mbunge unafanya ziara kwenye jimbo lako? Muda mwingine wote unakuwa wapi? Nilikuwa nategemea wakae kwenye majimbo yao hasa kwa wakati ambao sio wa bunge.
 
Unajua kabla sijajiunga JF nilikuwa nasoma tuu kwa pembeni na sikujua umuhimu wake na watu wanaoingia na kusoma humu. Lakini kuna mambo mengi nimeyasoma na kuyaangalia na yanayowekwa humu, inaonekana wanaochangia ni watu wenye akili zao, (Inafurahisha sana). Na kama waheshimiwa au wapambe wao wanasoma hii ni safi sana na naombea wajifunze na wafanye kimatendo na sio blah! blah! na wajifunze kwa wenzao wanaofanya kweli. Safi sanaa JF.
 
CHADEMA wamshukia Waziri Mwakyusa
• Wadai daktari wa Nyerere aliyekosa ujasiri

na Christopher Nyenyembe, Rungwe

MKURUGENZI wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema Jimbo la Rungwe Magharibi, linaongozwa na mbunge asiyefaa kuwapigania wananchi na kukemea maovu.

Mnyika, alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Rungwe katika ziara ya Operesheni Sangara mkoani hapa.

"Ndugu zangu mna mbunge mzuri (Profesa David Mwakyusa) aliyewahi kuwa Daktari wa Nyerere, lakini ni mpole mno, hana ujasiri wa kukemea maovu na hiyo sio sifa nzuri naona kwa sifa hizo hafai kuwa kiongozi wenu," alisema Mnyika.

Alisema Profesa Mwakyusa ambaye kwa sasa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alipokuwa daktari wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipaswa kujifunza kwa undani tabia za kiongozi huyo kutokana na ukaribu mkubwa aliokuwa nao; hakupaswa kuwa mwoga wa kukemea maovu yanayotokea ndani ya CCM na serikali yake.

"Najua fika kuwa Profesa Mwakyusa alikuwa karibu na Nyerere na kwa uzoefu wa kukaa nae alipaswa kuiga ujasiri wa Nyerere ambaye hakuwa na mzaha katika uongozi wake, hakuwa mtu mkimya, alipiga vita rushwa na tabia zote za ukandamizaji,Profesa wenu hayupo hivyo," alisisitiza Mkurugenzi huyo wa vijana.

Aidha, alisema Wilaya ya Rungwe ni moja ya wilaya zilizofanikiwa kuwa na wasomi na watu wenye msimamo kama walivyokuwa akina Elly Anangisye na Mwakitwange ambao walikuwa kitovu cha mabadiliko katika mkoa huo, lakini hivi sasa upo nyuma ikilinganishwa na mikoa ya Kaskazini.

Pia Mnyika, aliuponda uongozi wa Mkoa wa Mbeya kuwa haupo kwa ajili ya kuleta maendeleo isipokuwa ni kuendeleza migogoro ya kisiasa na chuki zisizokwisha ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya mkoa.

Alisema uongozi wa Mkoa wa Mbeya ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya mkoa huo na kwamba Rais Jakaya Kikwete alifanya makosa kumteua kiongozi ambaye ameshindwa kwenye kura za maoni za CCM mwaka 2005 na hakuchaguliwa na wananchi, lakini amempa ukuu wa mkoa.

"Mkoa wa Mbeya sio kitalu cha majaribio ya kuongoza, tabia hiyo pia ilifanyika kwa Basil Mramba, Nalaila Kiula, na sasa Mwakipesile watu wanaoangushwa kwenye ubunge kupewa ukuu wa mkoa kunazidisha mtafaruku kwenye chama hicho na hakuhamasishi maendeleo," alisema Mnyika.

Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu, Ali Chitanda, alisema umefika wakati kwa Watanzania kujitoa muhanga, ili kujenga chama cha upinzani chenye nguvu kitakachoweza kufichua maovu ya chama tawala na serikali yake.

Chitanda alisema serikali ya CCM hivi sasa inaandamwa na tuhuma nzito za ufisadi na tuhuma zote walizokuwa wakizipinga kutoka bungeni hivi sasa zinajidhihirisha mahakamani baada ya mawaziri na watendaji wakuu wa serikali kupandishwa kizimbani.

"CCM wizi mtupu! Wezi wa EPA wizi mtupu! Mikataba ya madini wizi mtupu! Umeme wa IPTL wizi mtupu! Mikataba ya Richmond nayo wizi mtupu! Kusainiwa kwa mkataba wa Buzwagi wizi mtupu! Sasa wananchi hapo mna imani gani na serikali ya CCM iliyojaa wizi mtupu?" Alihoji Chitanda huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Rungwe waliofika kwenye mkutano huo.

Akizungumza baada ya kuhutubia mkutano huo, Mnyika alisema huo si mwisho wa Operesheni Sangara kwani sasa inahamia Jimbo la Mbeya Vijijini ambako wameshaomba kibali cha kuendelea na ziara hiyo.
 
Back
Top Bottom