kasyabone tall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2009
- 254
- 63
injinia japo bado ninaendelea na utafiti na mzee imbombongafu amesema anasubiri sasa inabini nifanye kazi kweli kweli japo ninakusanya data kwa njia ya interview sijafikia kwenye conlusion lakini nikapata wazo nafikiri ni la maana zaidi.Kaka Lole,
Mimi naweza kukusanya mtaa mzima kama hilo pambano litapangwa. Mtu lazima atolewe knock-out siku hiyo.
Hata mimi hawa wakubwa wamenichosha na hizi kelele zao kupitia magazetini. Wakipatanishwa wanashikana mikono, kesho yake wanaanza kugombana tena.
hio safi sana mzee. kunahabari nimezipata punde eti umefukuzwa Kyela sasa sijui kama ni uzushi au kuna ukweli ndani yake. naomba unihakikishie!!! na kuhusu laptop vipi eti wategemea kupewa na mwakalinga? mimi sijui huyo sikonge kakumbwa na nini maana hupo kimya sana. December lazima nione vituko mzee!!!Kasyabone,
Mheshimiwa Mwakyembe kaingia Kyela jana jioni na akaenda mpaka Ipinda, akakuta wale vijana wa kumshangilia hawapo tena. Baadhi ya vijana wakaanza kuimba mwogopeni huyo, ana mfupa wa Albino, kautoa Tabora.
Mkuu Sikonge, hatukutaki tena Kyela maana inaelekea huko Tabora kumbe mnaua Albino. Yaani siasa za Kyela ni usanii mkubwa. Watu tukacheka kidogo mbavu zipasuke.
Leo kuna mkutano muhimu sana wa vijana kule Ipinda. Lengo ni kupanga mikakati ya kuelemisha wananchi juu ya sifa za madiwani na wabunge kwa ajili ya 2010. Vijana wamepania kutokufanya makosa ya 2005.
Huyo diwani Makete hata kuandika kunampa shida. Ila jamaa ana wajibika mno. Pia sasa wamempa kuwa mwenyekiti wa Wazazi Kyela. Siku moja walishikana shati na mbunge kwenye mkutano. Mbunge kwa kujua Makete hajui kiingereza akaanza kumteta pale pale mbele yake kwa kuongea kiingereza na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya. Makete kumbe kuna maneno anajua bwana! Zogo lililotokea hapo ilikuwa balaa kabisa. Hawa ndio viongozi wetu, kazi kutetana kila sehemu, hayo maendeleo yatatoka wapi?
Mimi siasa siziwezi bwana! sina muda wa kuita mhogo eti karoti. Mtu mjinga mimi namwita mpumbavu, wananchi watanitupa baada ya wiki moja tu. Hata vijana hapa mimi nawatukana tu, walikuwa wanaona mimi najifanya babu kubwa kwasababu ni engineer, ila sasa wengi wamenielewa na tunaanza kuelewana. Tumewasaidia wengi waache kukaa vijiweni na walime kokoa. Tutaendelea kusaidiana kwa mbali lakini siasa sitaki kabisa.
Karibu Kyela, ila desemba naona hapa patajaa na hapatatosha maana Mwakyembe huwa anakuwepo xmas na sasa nimesikia Mwakalinga naye anakuja. Sisi wapambe tutashiba tu. Kulingana na mkwe Malafyale pikipiki yangu haitakosa mafuta. karibu sana Kyela.
hio safi sana mzee. kunahabari nimezipata punde eti umefukuzwa Kyela sasa sijui kama ni uzushi au kuna ukweli ndani yake. naomba unihakikishie!!! na kuhusu laptop vipi eti wategemea kupewa na mwakalinga? mimi sijui huyo sikonge kakumbwa na nini maana hupo kimya sana. December lazima nione vituko mzee!!! hivi wewe unamsapoti mtu yeyote au ni mwakalinga tu?Kasyabone,
Mheshimiwa Mwakyembe kaingia Kyela jana jioni na akaenda mpaka Ipinda, akakuta wale vijana wa kumshangilia hawapo tena. Baadhi ya vijana wakaanza kuimba mwogopeni huyo, ana mfupa wa Albino, kautoa Tabora.
Mkuu Sikonge, hatukutaki tena Kyela maana inaelekea huko Tabora kumbe mnaua Albino. Yaani siasa za Kyela ni usanii mkubwa. Watu tukacheka kidogo mbavu zipasuke.
Leo kuna mkutano muhimu sana wa vijana kule Ipinda. Lengo ni kupanga mikakati ya kuelemisha wananchi juu ya sifa za madiwani na wabunge kwa ajili ya 2010. Vijana wamepania kutokufanya makosa ya 2005.
Huyo diwani Makete hata kuandika kunampa shida. Ila jamaa ana wajibika mno. Pia sasa wamempa kuwa mwenyekiti wa Wazazi Kyela. Siku moja walishikana shati na mbunge kwenye mkutano. Mbunge kwa kujua Makete hajui kiingereza akaanza kumteta pale pale mbele yake kwa kuongea kiingereza na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya. Makete kumbe kuna maneno anajua bwana! Zogo lililotokea hapo ilikuwa balaa kabisa. Hawa ndio viongozi wetu, kazi kutetana kila sehemu, hayo maendeleo yatatoka wapi?
Mimi siasa siziwezi bwana! sina muda wa kuita mhogo eti karoti. Mtu mjinga mimi namwita mpumbavu, wananchi watanitupa baada ya wiki moja tu. Hata vijana hapa mimi nawatukana tu, walikuwa wanaona mimi najifanya babu kubwa kwasababu ni engineer, ila sasa wengi wamenielewa na tunaanza kuelewana. Tumewasaidia wengi waache kukaa vijiweni na walime kokoa. Tutaendelea kusaidiana kwa mbali lakini siasa sitaki kabisa.
Karibu Kyela, ila desemba naona hapa patajaa na hapatatosha maana Mwakyembe huwa anakuwepo xmas na sasa nimesikia Mwakalinga naye anakuja. Sisi wapambe tutashiba tu. Kulingana na mkwe Malafyale pikipiki yangu haitakosa mafuta. karibu sana Kyela.
Mapambano ya hwa jamaa kwenye vyombo vya habari inaeleka havina mshindi.
Mimi nataka kufadhili pambano la NDONDI KAVU KAVU kati ya Mwakyembe na Mwakipesile.
Sisi tunataka tujue nani zaidi.
Wengine kina Engineer na wapambe wa pande zote tafuteni washabiki ili mufurahishe roho zenu.
mwee tubhuke nkughala ubwalwa iwikiendi jifikile bha kana nongi
Mwakyembe awa mbogo
Atoboa siri ya ugomvi wake na Mwakipesile
Adai kiongozi huyo anafanya kazi ya mafisadi
Ataka atambue kwamba yeye ni RC na siyo MC
Na Gladness Mboma
MBUNGE wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tatizo analoliona kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. John Mwakipesile ni harakati zake za kutaka kumng'oa katika jimbo la Kyela, jambo ambalo hataweza.
Alisema kuwa kazi anayoifanya Bw. Mwakipesile katika jimbo lake ni sawa na kuuza kofia za polisi ambazo hazinunuliki na kwamba anajisumbua, anajidhalilisha na kujifedhehesha licha ya kutumwa na mafisadi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Dkt. Mwakyembe alitoa kauli hizo za kejeli alipozungumza na gazeti hili kujibu hoja za Bw. Mwakipesile kuwa mbunge huyo anapotoshwa na wapambe wake wanaompa taarifa za uongo na kwamba hajawahi kuwaomba wazee wa Mbeya ili wawapatanishe.
"Ni lazima Bw. Mwakipesile atambue kuwa yeye ni RC na siyo MC kwa maana ya msema chochote. Mkuu wa mkoa mmoja kati ya wakuu wa mikoa 21 kuzungumza magazetini kila siku akiwarukia wabunge wanaopambana na ufisadi ni dalili ya kuweweseka.
"Ninalazimika kusema kuwa mwenzetu anahitaji ushauri nasaha, waandishi mchunguzeni Bw. Mwakipesile ili kujua anapatana na mbunge gani mkoani Mbeya?" alisisitiza Dkt. Mwakyembe.
Dkt. Mwakyembe aliongeza kuwa, kila mtu anatambua kuwa Bw. Mwakipesile anashinda Kyela kufanya kampeni za kuhakikisha kuwa, anamuondoa mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu na kwamba Serikali inatambua jambo hilo.
"Hili tatizo halinipi tabu hata kidogo kwa sababu kazi anayofanya ni kama kuuza kofia za polisi mali ambazo hazinunuliki anajisumbua, anajidhalilisha na kujifedhehesha," alisema.
Dkt. Mwakyembe alisema kuwa alipata kura asilimia 93 katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, lakini anashangazwa na kauli aliyoitoa Bw. Mwakipesile katika gazeti hili kwamba wapambe ndio wanaompotosha na kumtaka atambue kuwa wapambe hao ni wananchi wote wa Kyela.
"Tatizo la Bw. Mwakipesile anadanganywa sana na mafisadi ambao wanamtumia kama wakala, hiyo kazi waliyompa kwa Kyela ni ngumu kwelikweli, ni sawa na kuuza kofia za polisi kwa wananchi hivyo ni lazima atambue kuwa mimi ni mti mkavu usiochimbwa dawa," alisisitiza Dkt. Mwakyembe.
Alisema kuwa yeye alikuwa nje ya nchi na amerudi juzi ndipo alipomkuta mwenzake akiongea hovyo katika vyombo vya habari huku akitoa malalamiko kwamba yeye ndiye anayekwamisha maendeleo ya Mkoa wa Mbeya.
Alipoulizwa kiini cha mgogoro kati yake na Bw. Mwakipesile unasababishwa na nini, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa yeye hana mgogoro wowote na mkuu huyo wa mkoa, bali yeye RC huyo anayekwamisha maendeleo ya mkoa huo kutokana na muda wote kukaa Kyela kwa lengo la kumwondoa mbunge mwaka 2010.
Akizungumzia madai ya kutaka kuuawa alisema kuwa huo ni uongo na kwamba anaokoteza maneno barabarani na kuyafanyia kazi.
hio safi sana mzee. kunahabari nimezipata punde eti umefukuzwa Kyela sasa sijui kama ni uzushi au kuna ukweli ndani yake. naomba unihakikishie!!! na kuhusu laptop vipi eti wategemea kupewa na mwakalinga? mimi sijui huyo sikonge kakumbwa na nini maana hupo kimya sana. December lazima nione vituko mzee!!! hivi wewe unamsapoti mtu yeyote au ni mwakalinga tu?
Nyani haoni kundule, kama Mwakipesile hapatikani na mbunge yeyote wa mkoa wa Mbeya, je yeye Dr. Mwakyembe mbona na yeye hapatani na diwani yeyote wa wilaya ya Kyela? Mbona hapatani na kiongozi yetyote wa CCM wa wilaya ya Kyela. Hawa jamaa wote wawili wanaturudisha nyuma shauri ya ujinga wao usio na mwisho.
Baada ya kuitangazia dunia yote kwamba alitaka kuuwa, sasa anaanza kuruka na kusema ni uwongo? Amejua polisi wamegundua nini na anaanza kujiandaa kabla ya report. Kama ni uongo kwanini alienda kununua kisu na kuwapa wapambe ili wakitumie kama ushahidi wa kutaka kuuwa kwa kisu? Mbona alitumia magazeti ya MENGI kuitangazia dunia nzima kwamba alitaka kuuwa?
Kasyabone,
Huyu Masanilo nuksi kabisa, mimi engineer mzima eti mpaka laptop nipewe na mtu?
Mimi nipo Kyela tena leo tumewalima wenyeviti watatu wa vijiji. Tulikuwa kuchuja majina ya wagombea wa serikali za mitaa. Hao wenyeviti wa kata za Ipinda na Ikolo wametupwa nje kwasababu waligawa kadi fake kwa wanachama ili wawapigie kura.
Ushahidi uliletwa na katibu wa wilaya akathibitisha ni kweli hizo kadi haziko kwenye daftari lake. Mheshimiwa akajaribu kuwatetea wapambe wake lakini ushahidi ulikuwa mzito, hata mwenyewe akaamua kuondoka na kwenye kikao.
Kasyabone, hata wewe unaweza kuja na sera zako na kama tutaona zinafaa, sisi vijana hatuna noma, tutakuunga mkono. Kwasasa ni wawili tu Mwakyembe vs Mwakalinga. Mimi mpaka sasa namuunga mkono Mwakalinga. Lakini sijawekeana naye mkataba, akija mwenye sera nzuri zaidi mimi nageuka kinoma. Hapendwi mtu mwaka huu, ni sera. Tunataka jogoo linalozalisha kuku, sio jogoo linalojua tu kupiga kokolikoooooooooooo!! asubuhi.
Ogah, kama unashangaa hiyo habari, basi njoo siku moja huku vijijini na umsikilize Dr wakati anahutubia, ukiwa na hasira utachukia na kuondoka, vingine utacheka mpaka mbavu zikupasuke.
Mbunge wa Kyela,Dk Harrison Mwakyembe, amedai vigogo wa CCM, wanaratibu mpango wa kumhujumu kisiasa kwa kutumia pesa za mafisadi.
*Chiligati asema watalijadili kwenye vikao vya chama
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe ameitupia kombora CCM kwamba, baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, wameamua kumhujumu kwa kupeleka fedha za rushwa katika jimbo lake ili kumng'oa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, Mwakyembe alisema viongozi hao wamekuwa wakishirikiana na jopo la mafisadi kusambaza fedha hizo kwa wananchi wa Kyela.
Alisema hivi karibuni wabaya wake hao waliingiza mamilioni ya fedha katika jimbo hilo, zilizopelekwa na kiongozi Mwandamizi wa CCM Mkoa wa Mbeya, lakini alipewa taarifa na kuwataka wazee wazipokee na kuzitumia kwa vile ni fedha zao zilizoibwa na mafisadi.
"Mimi nimewashauri wananchi wazipokee fedha hizo na wazitumie kwa sababu ni mali yao iliyoporwa na mafisadi," alisema.
Mwakyembe alisema anashangaa kuona kwamba rushwa inayopelekwa katika jimbo lake na kusambazwa na mafisadi inajulikana na viongozi wa serikali na CCM, lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa mpaka sasa.
"Serikali ina vyombo vya dola inaweza kuchunguza, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wahusika," alisema.
Alisema njama za watu hao zinafanywa zikiwashirikisha pia baadhi ya viongozi wa serikali waziwazi bila ya kificho, hali ambayo inamfanya aamini kuwa wabaya wake wana baraka na wanayoyafanya.
Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema kama taarifa hizo zipo zitazungumzwa kwenye kikao cha ndani cha chama na si nje.
''Kama hilo lipo tutalizungumza kwenye kikao chetu, siwezi kumwaga mchele kwenye kuku wengi, hivyo akiwasilisha madai yake tutayashughulikia,'' alisema Chiligati.
Mbunge huyo ambaye aliongoza kamati ya bunge ya kuchunguza kashfa ya Richmond alijifariji kwamba, atashinda mapambano hayo kwa sababu wananchi wa Kyela bado wana imani naye.
Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka Kyela, zinaeleza kuwa baadhi ya watu waliozipokea fedha hizo walimtaarifu mbunge wao na wakakubaliana kuwa wagawane na nyingine wakanunulia vinywaji.
Mwakyembe ambaye amekuwa katika ugomvi mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile kwa madai kuwa mkuu huyo wa mkoa anamhujumu akitaka kumng'oa katika jimbo hilo, alisema yote hayo anawaachia wananchi wa Kyela kuamua.
Hii ni mara ya kwanza kwa mbunge huyo ambaye yupo katika kundi la wabunge wanaopambana na ufisadi, kuwashutumu baadhi ya viongozi wa juu waandamizi wa CCM kuwa sasa wanashirikiana na wabaya wake kummaliza.
Akizungumzia uhusiano wake na Mwakipesile, mbunge huyo alisema walishasuluhishwa siku nyingi anashangaa kuona bado anaendelea kuzungumzia tofauti yao na akashauri kama hajaridhika ni vyema akalifikisha suala hilo katika ngazi ya CCM.
Hivi karibuni kumeibuka mgawanyiko wa wana CCM wanaopinga ufisadi na wana CCM ambao wako upande wa mafisadi , hali ambayo ina hatarisha uhai wa chama hicho.
Mgawanyiko huo ndani ya chama hicho ndio ambao ulikifanya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho mjini Dodoma kuunda kamati ya watu watatu wakiongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Abdulrahman Kinana kufuatilia uhasama uliopo kati ya wana CCM na wabunge wa chama hicho. Wakati akizungumza na wananchi kwa staili mpya ya kujibu maswali ya papo kwa hapo, Rais Jakaya Kikwete alisema CCM na serikali haijawafunga midomo wabunge wake kuikosoa serikali.