Shura ya maimamu yakana kutoa waraka wa uchaguzi, yampongeza Rais Magufuli kwa kuitokomeza Corona

Kitendo cha mtu kuitwa gaidi au kutumiwa na beberu kinafanyika ili kuvunja nguvu msimamo ulio nao
 
Muhimu ujumbe umefka bwashee
View attachment 1504296

Amiri mkuu wa Shura ya maimamu Shehe Kundecha amekana Taasisi anayoiongoza kutoa waraka wowote unaohusu uchaguzi.

Kundecha amesema yeye kama kiongozi mkuu wa waislamu hana taarifa yoyote juu ya waraka unaosambazwa mitandaoni na kwamba waraka huo ni feki.

Shehe Kundecha amempongeza Rais Magufuli kwa namna anavyoongoza nchi kwa busara na hekima na hasa kwa namna alivyotuongoza katika kipindi kigumu cha Corona.

Kadhalika amemshukuru kwa kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo.

Source: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!

Zaidi, soma;

Uchaguzi 2020 - Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania
 
mh kuna usaliti humo .haiwekani katibu aseme hivi lakini siku kadhaaa mkiti naye aseme hivi. mwenye macho haambiwi tazama
 
Mmmmmmh wamesha ambiwa waukane hivyooo, ila ujumbe kwa walengwa umefika haswaaaah.
 
Back
Top Bottom