Shura ya maimamu yakana kutoa waraka wa uchaguzi, yampongeza Rais Magufuli kwa kuitokomeza Corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,467
141,167

Amiri mkuu wa Shura ya maimamu Shehe Kundecha amekana Taasisi anayoiongoza kutoa waraka wowote unaohusu uchaguzi.

Kundecha amesema yeye kama kiongozi mkuu wa waislamu hana taarifa yoyote juu ya waraka unaosambazwa mitandaoni na kwamba waraka huo ni feki.

Shehe Kundecha amempongeza Rais Magufuli kwa namna anavyoongoza nchi kwa busara na hekima na hasa kwa namna alivyotuongoza katika kipindi kigumu cha Corona.

Kadhalika amemshukuru kwa kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo.

Source: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!

Zaidi, soma;

Uchaguzi 2020 - Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania
 
Nimependa sana hiyo mbinu ya Shura ya maimamu kurusha jiwe gizani, kisha ujumbe kufika vyema kwa umma, halafu wanakuja kukanusha wakati tayari ujumbe umefika kwa walengwa. Ningeshangaa sana kwa ukweli wa aina ule, serikali isiwafuate wahusika kimya kimya na kuomba po.
 
Vijisababu havijawahi kukukauka.
 
😂😂
Kwa hiyo huyo shekhe Ponda alijipinda kuundika yeye kama yeye siyo?
Mbona viongozi wa dini mnatufanyia hivi??
 
Back
Top Bottom