beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Shule hiyo iliathiriwa na tetemeko lililotokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kupelekea majengo mengi kuharibika ambapo Serikali iliagiza ijengwe upya. Mradi huo umegharamiwa na Serikali za Uingereza na Tanzania.
Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amesema Shule ya Wavulana ya Ihungo ambayo majengo yake yamezinduliwa leo ina uwezo wa kuchukua Wanafunzi 1,152 kutoka 640 ya awali.
Katika hafla ya uzinduzi, Dkt. Ndalichako amesema Mradi huo umehusisha miundombinu ya madarasa, mabweni 3, vyoo pamoja na nyumba za Walimu 30. Pia, baadhi ya majengo machache yaliyoweza kuhimili tetemeko yamefanyiwa ukarabati.