Waziri Jafo aridhishwa na ukarabati wa shule za Sekondari Ihungo na Rugambwa zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi

kichoroba89

Senior Member
Oct 3, 2019
197
57
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Selemani Jafo aridhishwa na utendaji kazi wa viongozi wa Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Waziri Jafo ameyasema hayo akiwa Mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba katika ziara ya siku moja Juni 5, 2020 wakati akitembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Shule za Sekondari za Rugambwa (wasichana) na shule ya Sekondari ya Ihungo (Wavulana) pia na mradi wa barabara za kilometa tano wenye gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.3.

Akiwa katika Shuleza Sekondari Ihungo na Rugambwa Waziri Jafo alisema kuwa ameridhishwa sana na ukarabati wa shule hizo kongwe ulivyofanyika na kuzifanya shule hizo kuwa mpya kabisa. Pia aliwashukuru wanafunzi wa kidato cha sita katika shule hizo kutii maelekezo ya Serikali baada ya janga la ugonjwa wa KORONA kwa kurudi shule kwa asilimia 99 kuendelea na masomo yao.

Waziri Jafo aliwapongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Ihungo kwa viwango vya hali ya juu sana ambapo alisema kuwa ubora wa majengo ya shule hiyo ni wa kwanza nchini na kutoa rai kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera kuacha ndoto za kugeuza shule hiyo kuwa Chuo Kikuu badala yake wanafunzi wasome katika mazingira bora zaidi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera akitoa taaarifa katika shule hizo alisema kuwa Mkoa wa Kagera unazo shule za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita 36 zenye wanafunzi wa kidato cha sita 3,590 na wanafunzi 3,393 tayari wameripoti katika shule hizo kuendelea na masomo yao ya kidato cha sita wanafunzi 197 asilimia 5 bado hawajaripoti.
 
Jafo hajatenda haki, hasira zake amezielekeza sehemu isiyo sahihi.

Ni wazi kwamba RC alikua akijua ujio wa Waziri kwakua RC wanaripoti kwa Rais kupitia ofisi ya Jafo kwahiyo Jafo ni bosi wa ma RCs kwa maana hiyo.

Kama RC alijua ,ni wazi DC na DeD alijua ujio wa Waziri.DeD kupitia kwa watendaji wa kata na mitaa kama kuna ulazima wa uwepo wa watu alipaswa kufanya kazi hiyo.

Meneja wa Tarura yeye anasimamia wafanyakazi wa ofisi yake na mitambo ya kujengea barabara, hana mamlaka na watu.Hana namna ya kuwaalika watu ambao wako chini ya DeD au DC.

Jiji la Arusha ,juzijuzi limekumbwa na tumbua tumbua,ina maana RC,DC na mkurugenzi wa Jiji bado wapya kabisa.

Hata hivyo,uzinduzi wa barabara hata watu wasiwepo si bado barabara itaonekana!? Kumekuwepo na matangazo mengi hata kwa vitu vidogo vidogo ambavyo havikupaswa kuzinduliwa na watu wenye vyeo vikubwa kabisa,lakini wanalazimika kizindua mbele ya kamera za wanahabari na maelfu ya wananchi.

Miradi mingine inazinduliwa mara mbili mbili, ili ijulikane imefanyika.

Inawezekana awamu zilizo pita zilifanya mambo mengi makubwa tofauti ipo kwenye matangazo, awamu hii wanapenda sana matangazo.TBC imekua kama vile ni mali ya serikali, kumbe ni mali ya umma,inafanya coverage za shughuli za serikali tu,hata siku moja hawawezi kufanya coverage za shughuli za ACT WAZALENDO au Shughuli za chadema au CUF.

Kwa ujumla amekosea sana.
 
Pole sana meneja wa tarura Arusha
 
Akumbukwe Eliakimu Maswi aliyekuwa naibu waziri TAMISEMI aliyebuni mradi wa maji katika shule hiyo katika ziara yake ya kushtukiza kulikuwa na tatizo sana la maji lililowatesa wanafunzi
Serikali msiboreshe majengo tu ya shule na hilo kanisa pamoja na msikiti pia yanawasadia wanafunzi kukua kiimani boresheni pia ni sehemu ya majengo ya shule
 
Back
Top Bottom