Shule ya Wavulana ya Ihungo yazinduliwa rasmi, iliharibiwa na tetemeko la 2016

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,649
2,000
Shule hiyo iliathiriwa na tetemeko lililotokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kupelekea majengo mengi kuharibika ambapo Serikali iliagiza ijengwe upya. Mradi huo umegharamiwa na Serikali za Uingereza na Tanzania.

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amesema Shule ya Wavulana ya Ihungo ambayo majengo yake yamezinduliwa leo ina uwezo wa kuchukua Wanafunzi 1,152 kutoka 640 ya awali.

Katika hafla ya uzinduzi, Dkt. Ndalichako amesema Mradi huo umehusisha miundombinu ya madarasa, mabweni 3, vyoo pamoja na nyumba za Walimu 30. Pia, baadhi ya majengo machache yaliyoweza kuhimili tetemeko yamefanyiwa ukarabati.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,655
2,000
Shule hiyo iliathiriwa na tetemeko lililotokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kupelekea majengo mengi kuharibika ambapo Serikali iliagiza ijengwe upya. Mradi huo umegharamiwa na Serikali za Uingereza na Tanzania...
Shule hii CCM ilidai ni mali ya TAPA! CCM ilisema baada ya ukarabati itaiuzia serikali! Pesa ni msaada kwa serikali toka Uingereza, baada ya kuikarabati CCM inaiuzia serikali! Huu ni upigaji.
 

Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,782
2,000
Shule hii CCM ilidai ni mali ya TAPA! CCM ilisema baada ya ukarabati itaiuzia serikali! Pesa ni msaada kwa serikali toka Uingereza, baada ya kuikarabati CCM inaiuzia serikali! Huu ni upigaji.
Usichanganye mambo, hii shule haijawai kua ya ccm na ccm haijawai kudai ihungo ni shule yake.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,328
2,000
^Ni aibu kubwa ya kutisha & isiyovumilika kwa wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini sakafuni, katika karne hii ya 21 ya sayansi & teknolojia^ ~ JPM
 

SueIsmael

JF-Expert Member
Dec 11, 2013
806
1,000
Kumbukumbu kutoka Maktaba:

1610990746370.png


 

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
1,707
2,000
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar, katika ufunguzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ihungo, iliyopo Bukoba Mjini, yaliyokarabatiwa baada ya kuharibiwa na Tetemeko.

Screenshot_20210119_032215.jpg


Screenshot_20210119_032159.jpg


Screenshot_20210119_032242.jpg
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
42,059
2,000
Balozi mbona hajavaa mask?!! Halafu kesho watoe waraka kuhusu Corona Tanzania.
 

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,446
2,000
Kwa shule hii ilivyokua mwanzo na sasa..
Kwa wahusika(wanafunzi&watendaji) Heko kwa tetemeko
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom