Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,620
Wanabodi
Shuhudia sensa live kupitia TBC, nimeshuhudia live, citizen No. 1, Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan akihesabiwa toka katika makazi yake rasmi ya kiserikali Ikulu ya Chamwino Dodoma!.

Saa hizi ameisha maliza kuhesabiwa.

Wana JF, let's share different experiences za sensa na muendelezo wa zoezi la Kuhesabiwa toka maeneo tofauti tofauti. Mimi niko home kwangu hapa maeneo ya Tandale kwa Mtogolo ambapo nimepanga ubazi mzima, nawasubiria kwa hamu na shauku kubwa makarani wa sensa wananifikie, na kwavile tuna taarifa ya ugeni huu, kama jadi ya Uafrika, tumewaandalia chai ya rangi na vitafunwa vya huku kwetu Uswazi, chai na chapati, vitumbua na maandazi. Chai ya maziwa na Vitafunwa vya mitaa ya kishua ni keki, sambusa, mkate wa siagi na mayai ya kukaanga.

Bado nawasubiria makarani wa sensa, vipi wewe mwenzagu?. Tuhabarishane na kupashana kuhusu zoezi hili.

Paskali
 
Rais Samia baada ya kuhesabiwa, amezungumza, na Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu Anne Makinda pia amezungumza, na kusema zoezi la sensa litadumu kwa siku 7, hivyo makarani wa sensa wasipopita kwako leo, watapita kesho au keshokutwa, acha majibu ya dodoso la sensa kisha endelea na shughuli zako.
P
 
😄😄😃
Nimedhani live ukiwa chamwino kumbe kwenye tv!!!

Ila mkuu P, siasa nenda nazo polepole.
Hazitaki haraka. One day yes.
Kuna wazee wanapata fursa baada ya kustaafu (60+yrs) so, kikubwa uzima!
Muhimu, epuka kusifiasifia hata visivyofaa kusifiwa! Kuwa ndani ya CCM au kumkubali kiongozi fulani, haimaanishi kuunga mkono kila kitu!
 
Pascal laiti kama usingekuwa mwenye njaa kali baas nazani ww ungekuwa mtu bora sana kwa nchi yetu..lakini njaa yako inakupotezea mengi sana. You have to stand on what you believe. Stop being dragged by dumbest politicians.
 
Back
Top Bottom